Wenzetu huko zimefika bar ngapi?

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,503
Sisi hapa Mwanza sidhani hata kama zimefika bar 7. Maana ikifika asubuhi tu wamekata na kuurudisha ni mpaka saa kumi na mbili jioni. Nasikia Dar zimefika bar 52, hivi ni kweli? Maana bwana .....Dar ndiyo kilakitu. Isije ikawa kelele zimepungua kwasababu Dar zimefika bar 52, kumbe sisi huku 'mikoani' bado tunaumia. Naomba tujulishane......hapo ulipo zimefika bar ngapi. Ili nijifariji na kauli ya wahenga "kifo cha wengi harusi".
 
MW,bar hayo hayana tofauti na haya mkurabita,mkukuta,tasaf ni njia za kutafuna hela hakuna kitu hapo..
 
Bibi wa Msimbati alisema haitoki,ikifika bar52 ukiwasha mashine inarudi bar 3
 
Hali kama hii wala hakuna mtu atakaejiuzulu .
Waziri mkuu wa japani alijiuzulu kwa kwa uchumi kukua 6% wakati yeye aliahidi 7%.
Tanesco wanadai kua uzalishaji umeshuka kwa 81% Kwa sababu mabwawa hayana maji ya kutosha.
hali hii ingeeleweka iwapo kumetokea ajali na mitambo kulipuka lkn inanipa uchungu sana kwa vile sababu zinazofanya umeme ukosekane leo zina historia ya zaidi ya miaka 20! Na hela nyingi za umma zimetumika kukabiliana na tatizo hili katika njia ambayo tatizo limebakia palepale! Siyo tatizo la dharura hili ni tatizo linalojulikana walau kwa miaka 20! Kwani binaadamu anaishi miaka ningapi hadi tuone kua miaka 20 ya kukosa umeme wa uhakika ni michache? Ni lini hasa tutakuja kufaidi maisha?
 
Wangejenga mitambo Mtwara na umeme ukaletwa Dar na nyaya.
Kama wa kuwasha majenereta unashindikana hiyo gesi ya kupeleka viwandani wataitoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…