Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 62,097
- 127,830
Heshima kwenu Great Thinkers
Mwenzenu nina jambo linanitatiza siku nyingi nimeshindwa kupata ufumbuzi.
Kwanza kabisa mimi sikulelewa na mama yangu, nilienda kuishi na sister nikiwa na miaka mitano na nimekulia huko mpaka nimekuwa mtu mzima najitegemea. Sio kwamba nilikuwa sionani na wazazu kabisa, karibu kila mwaka naonana nao na kukaa nao kwa kipindi fulani.
Kinachonitatiza ni mama yangu, huwa anahisi mimi simpendi wakati mimi nampenda kufa...najivunia yeye na najiona mwenye bahati kuwa na mama kama yeye. Yeye ndo malkia wangu wa nguvu,to me she is the best female on Earth ila sasa nashindwa nifanye nini ili aone nampenda kuliko kitu chochote duniani. Sina hela kwamba niwe namjaza mapene, na hata nikimpigia simu sinaga stori nyingi najikuta nimeishiwa ya kuzungumza tofauti na nikiongea na sister tunajikuta tunapiga stori hadi basi...huwa nadhani pengine ni kwa sababu mimi na yeye wote sio waongeaji wazuri lakini bado nahisi kuna kitu hakiko sawa.
Hebu nishaurini mwenzenu jambo hili linaninyima raha kabisa.