Wenyeviti wa Vijiji wanusurika kushambuliwa na wananchi Mtwara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,797
2,000
Jeshi la polisi wilaya ya Mtwara limeombwa kuongeza ushirikiano na viongozi wa vijiji katika kuimarisha ulinzi kufuatia wenyeviti wa vijiji viwili kunusurika kushambuliwa na wananchi likiwemo tukio la mwenyekiti wa kijiji cha Mtemba kubomolewa nyumba yake wakati akimwokoa mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika na kupotea kwa mtoto kwa njia ya ushirikina.

Wenyeviti wa vijiji vya Mtemba na Lilido Bw.Said Msoma na Bw.Said Salum wameyasema hayo kwenye kikao cha kutathimini utendaji wa kazi kwa Wenyeviti wa vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Alipotakiwa kuelezea kuhusu matukio hayo, Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Issack Mushi amewatoa wasiwasi wenyeviti hao kuwa, matukio ya uvunjifu wa amani vijiji vya Mtemba na Lilido, yamedhibitiwa, huku Mkuu wa wilaya Mtwara Bw.Dastan Kyobya akasisitiza kuimarishwa kwa ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.

ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom