Olaigwanani lang
JF-Expert Member
- Apr 26, 2012
- 541
- 175
Ndugu wana jf ni siku za karibuni tuu wananchi wa Loliondo ngorongoro wameondolewa kwenye maeneo yao ya asili...na sasa zoezi hilo limeshaanza wilaya ya Longido ambapo vijiji zaidi ya 30 vya mlima wa Ketumbeine na Gelai wameambiwa waondoke haraka kwenye maeneo yao ambayo wameishi kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika...Cha ajabu zaidi mbunge wa huku bwana Kiruswa hata hana muda wa kuwasemea wananchi wake na wamebakia na sintofahamu kwani wamenyimwa hata kulima mazao na hiki ndio kipindi cha kilimo kwa vijiji vya maeneo hayo ...
Ndugu wananchi tunaomba sauti ipazwe kwani jamii yetu imekuwa kama Wakimbizi katika nchi yao na hatuna haki na maisha kila mahali tunapoishi tumegeuka kama wanyama wa mwituni....
Huu ni uonevu na uvunjwaji wa hali hususan katika jamii yetu hii...
Mheshimiwa Rais tunaomba msaada wako haraka iwezekanavyo.