wenyeji wa Tanga mpo...?

Ha!Ha!Ha!ha!ha!ha!....hapo Tanga hotel.....ni maarufu kwa vikao vya harusi, send off, ''chicken'' party etc! ....na ofcourse weekend kuna live band pale ndani......but si pazuri kwa kulala ati!

Tanga Hotel jamani acheni kabisa. Raha za Tanga Hotel hazikamiliki bila Mkongwe wao mzee Hiza (Fax Band). Kulikua na company nzuri sana za jamaa wa Tanga cement pamoja na wataalam wachache toka Bombo hospital. Wapi Bandari? (Palalalapalalala palalapalaa!!!) "Najuta,ni jina langu lenye rangi ya chungwa....nachoka kabisa!" till dawn,acha bana!
 
Kweli kuna watu wamevinjari TA vya kutosha. Vipi polisi wa pale Chumbageni walikua hawawapi taabu na kelele zenu za magitaa na ngoma till dawn aisee? Nilikua nakaa zangu nje tu nakula samaki na bia taratiiibu!, saa sita sharp nawahi zangu Nguvu Mali kusleep.
 
Wapeleke Maua Inn Hotel barabara ya Saba ni karibu na Travellers Hotel. Ukishindwa hapo Nenda maeneo ya Mkwakwani karibu na Stadium kuna hotel nzuri sana jina limenitoka kidogo.

NB
Husisahau kuwapeleka LaCassaChica wakaburudike na kila aina ya vivutio
 
nilichogundua ni kuwa weeengi kama sio wote sio wenyeji Tanga.

Mbu kama sijachelewa waambie waende Nyinda mpya ipo Bombo area sio Raskazone (inapakana) au Regal naivera ipo Bombo area.

Hizo hotel zipo safi sana. Mkonge ipo juu yao ila labda hizo huduma zilizolalamikiwa. Mengine wamesema na kutia chumvi.

Kujirusha mie sijui maana umri umeenda.
 
...hujachelewa FP, nipo bado katika kuchukua ushauri na kuufanyia kazi, mwishoni mwa mwezi ujao ndio wageni wangu wataingia 'waja leo warudi leo'...

Uzuri wenyewe, Next Level amegusia mpaka mahala pa nyama choma, na Bao3 kanielekeza Mitaa ya Posta kama kutakuwa na vifurushi vya kutuma.

Again, shukran mkuu kutumia muda wako kunisaidia mawazo.
 
Pia waweza fikiria sehem moja inaitwa Peponi. Nje kidogo ya jiji la Tanga,ukiwa unaelekea Pangani. Ukiwasiliana nao in advance wanaweza wakaorganize usafiri. Tel: +255 (0)784 202962 :: +255 (0)713 540139 :: E-Mail info@peponiresort.com
 
Back
Top Bottom