Wenye uzoefu na harusi msaada!!

We jamaa nakuhitaji
 
Usiache kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki..unaweza kusema unagharamia kila kitu mwenyewe mwisho wa siku ukumbini unajikuta wewe na familia yako tu..watu watasema ameona sisi ni masikini hatuwezi kuchangia ndo maana hakutuomba mchango, basi na hiyo sherehe ufanye mwenyewe... harusi ni suala la kijamii hivyo hata kama una uwezo ushirikishaji ni muhimu sana...over and out
 
Namba 4 na 5 nimecheka San daaah
 
Inategemea location ni jijini au kule kwetu sitimbi? Pia inategemea ukubwa na vikorombwezwe unavyo taka viwepo kwenye event yako. Mfano mie nikifanyia kijijini lakini sikujitwisha yote bado kwa kupata support kidogo lakini hata 3M haijafika.
Kwa hiyo angalia yafuatayo:
1. Idadi ya wahudhuriaji
2. Aina ya vyakula na vinywaji
3. Ukumbi, mavazi, muziki, MC, na mapambo.
Maana hivyo huwa ndo msingi wa sherehe yako japo sio vyote nimetaja vipo na vingine kulingana na mabadiliko ya kila siku.
Ila kujitwisha mzigo mzima ni nzuri japo kwa baadhi ya watu wako wa karibu wanaweza pata tafsiri mbaya kuwa umewadharau kuwa mchango wao si muhimu japo wengine ni sawa na kuvuja kwa pakacha......
Lakini pia shirikisha familia yako na yule unayemuoa mawazo yenu yatafikia mwafaka mzuri.
Angalizo langu; USIAMIN SANA AKILI YAKO PEKE YAKO KAMA UTAWEZA KUKAMILISHA KWA 100% wape ndugu na jamaa nafasi ya kutoa maoni na michango yao ya mawazo hata kama hawakwenda shule.
 
Wana JF habari!!
Nimekaa nikawaza kuhusu harusi bila kuchangiwa hata mia labda mawazo tyuu !!
Kiwango nilichopanga ni kuwa nacho ni million 6 je itaosha kumaliza mchato mzima!!
Wenye uzoefu na kamati za harusi hapa vipi mtakaa kikao!? Au niongeze!!
MTAFUTE LARRY KING MTANGAZAJI MSTAAFU WA CNN.
Aliwahi kuoa mara tisa.
 
Ushirikiano ninao hitaji ni nikulete kadi ya mwaliko tyuu hivyo vingine nimeshamaliza umaskini nitakuwa nimekusave saana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…