Extraseen
Senior Member
- Feb 18, 2017
- 141
- 140
Maumivu yangu katika maandishi
Unaweza zoea "ukiwa" katika maisha yako kiasi kwamba ukiona mtu anacheka unajiuliza hivi huyu yupo dunia ipi?
Guys, kuna maisha na kuna mapito. Kuna laana na kuna kuchukiwa. Siku zote usiombe Mungu akachukia familia yako wala asitie laana kwenye familia yako maana
Kuna kusaga meno na kuna kulia machozi ya damu
Kuna kudharauliwa na kutemwa mate
Kuna kushushwa kabla huja jishusha
Balaa zaidi nikukutana na watumishi fake wanao taka kutumia mateso yako kukutoa hela kwa kivuli cha mungu kawaagiza utoe sadaka flani ili akusamehe. Amini nakuambia usiombe usiombee!
Utashughudia hatua za maendeleo ya wenzako na wewe utakuwa ngazi ya kukanyagiwa wawo wafike juu. Ogopa sana hasira za Mungu. Ogopa sana maana hata usali na kutubu vipi kama asha piga muhuri wa mateso katika uzao wenu utaomba aridhi ipasuke.
Kuna wakati huwa najiuliza mara yangu ya mwisho kuwa na tabasamu la kweli usoni mwangu ni lini, wala sikumbuki nalitafuta sana jibu katika kipindi cha miaka mingi nyuma silioni, kile ninaweza kiona kwangu ni huzuni, ukiwa, maumivu ya moyo, maisha ya siyo na ladha, kutengwa, kufungiwa gereza kuu la ajira, mikono yangu kuwa locked na pingu isifanye biashara.
Mifuko yangu imetobolewa isikae na hela, hisia zangu zime kuwa diluted na chuki usipende wala kupendwa. Macho yangu yamekuzwa nishughudie maendeleo ya wengine na akili yangu imefungwa isifanye chochote katika dunia.
Kila nisalipo naona kabisa sala zangu hazina nguvu wala hazi mfikii muumba. Nikiwaza ukiwa wangu tangu nikiwa na miaka 3 mpaka nafikia utu uzima huu, najiuliza ikiwa tuna ambiwa mungu halali wala hafungi macho ilikuwaje mimi na ndugu zangu tukayapitia yote yale na mpaka sasa nayapitia haya yote?
Huwa najiuliza maswali ya wapi jicho lake lilipo kuwa hata mimi na ndugu zangu tuka yapitia yote haya? Najiuliza ule mpango wa wenye hila kutudhulumu haki yetu ya amani hapa duniani na kumuuwa baba na kaka yangu mkubwa, na bado wameendelea kuangamiza ukoo wa baba yangu, je! Mungu hakuona? Bila shaka aliona je! Ukimnya wake kwa miaka yote hii 30 ni kwamba haoini mateso yetu?
Je, yanayoendelea mpaka sasa hayaja mguswa kutoa adhabu yake kwa wahusika? Je, kama kuna kisasi cha Mungu cha adhabu kwetu, let' say kwamba mababu zetu wali muudhi akaachia laana ikaja kwetu sisi wa kizazi cha 4, je katika kulia kwetu na kuomboleza bado adhabu hizo za mababu hazi sameheki kwetu?
Je, hawa wanao tumia uchawi kutesa familia nzima na bado wana raha katika maisha yao na bila aibu wana jisema wazi wazi kuwa wata mmaliza yeyote atakaye inua mdomo kudai haki au kuulizia kifo cha baba mzazi, je hawa wame mpa nini mungu ata awafanye watabasamu na kuishi katika nyumba yetu?
Je, inatupasa tuishi kwa kulipiziana kisasi kwa kuwa haki kwa mungu haipatikani? Je, na mimi nikibuni mbinu yangu ya kuwaangamiza wale wanao wafanya ndugu zangu kuwa vichaa na kuuwa wengine, mungu ata nilinda kama anavyo walinda wale? Je huu uchawi unao tumika kuuwa wasio na hatia umepewa baraka na maandiko? Kama jibu ni hapana mbona maandiko yana sema usimuache mchawi aishi ila hawa wanaishi na kila mwaka wanauwa na kutesa watu kwa magonjwa, je hayo maandiko hayatendi kazi kwa ulimwengu wa sasa?
Kuna mengi sana nimejiuliza bila kupata majibu sana sana naogopa kuishia kumkufuru mungu wangu, ila naamini sistahili haya nipitiayo sasa, kwa kuwa nimeshughudia baadhi ya watu mbali mbali wakifanya kufuru na ushirikina mkubwa ambao mm sikusubutu hata kuya waza ila wao wana ishi kwa mafanikio na baraka za kila wafanyacho, ila uzao wa mama yangu umekuwa na mateso makali tangu utotoni mwao na bado wanataabika mpaka leo hii, na ukitafuta kikubwa walicho mkosea mungu hukioni.
Namuomba mungu sana kabla ya kufa kwangu angalao anifungulie kosa langu na ndugu zangu ni nini nipate amani maana nimetafuta tangu tukiwa na miaka mi3 ni mateso katika hii dunia, najaribu kuwaza ndugu zangu kwa mri ule walimkosea nini mungu hata aruhusu wawe mateka wa nguvu za giza, mateso yao kwa miaka yao yote mpaka sasa! Sina maana ya kupinga kazi ya mungu ila nautafuta ukweli wa fedhea hizi katika familia mauwaji, dhuluma na kusoma na kukosa kazi, biashara haziendi, kuchukiwa kwetu na kudharaulika.
Natamani siku moja niandike kitabu cha mapito yangu ya adhabu ya laana za mababu zinavyo ni andama mm wa kizazi cha 4.
Watu wajifunze kuwa hata ukiwa mwema kwa Mungu kama kuna muhuri wake ulifanyika juu ya kizazi chenu huta epuka muhuri huo.