Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 14,624
- 18,454
mkuu baada ya kuona kuna nyaka ndani Baba mwenye hekima aliamua kujenga nyumba nyingine na kisha kuwahamasisha wanae kuwa kutokana na nyumba hii kuwa na nyoka basi hamieni nyumba mpya niliyo wajengea ili msipatwe na madhara. Lakini kwa kuwa baba yeye ni mwenye uhuru hawezi mladhimisha mwanae kuwa toka humo ndani kwa lazima badala yake kajenga nyumba nyingine na kuwambia wanae wahaimie huma lakini kawe hawezi walazimisha kuhamia nyumba mpya.Umejenga nyumba,
Hapo ndani kwako anaingia nyoka,
unawaambia wanao kuna nyoka humu msimsogelee kaeni mbali atawauma,
nyoka anawauma wanao mmoja mmoja,
nyoka uwezo wa kumwondoa unao ila humwui unasubiri siku ya mwisho uchome wote wanao waliumwa na nyoka kwa kosa la kuruhusu nyoka awaume na nyoka mwenyewe.
Hizi hadithi za wachungaji kuna mambo hayapo sawa.
MUNGU yupo ila nina wasiwasi na haya mahubiri tunayohubiriwa.
Kuna uwezekano huyu MUNGU si huyu wanayemuhubiri.
mkuu kama ni propaganda za watu weupe kwa nini na wao wanaamini hivyo?Ukifa habari inaishia hapo mzee, hakuna maisha baada ya kifo, hizo mi propaganda za watu weupe na waarabu ili tuwe na tumaini.
Wengine hatuna tu option kulingana na vitisho tulivyopandizwa tangu utotoni ila huyu Mungu hatumpendi haswa
Katuondolea vipenzi vyeti ametuacha na majonzi yasiyoisha
Hatuna tu option tuna muabudu kwa sababu ya ubabe wake ila binafsi simpendi
Sikushauri uendelee kutokumpenda Mungu lakini angalau nafurahi kujua kuwa humpendi Mungu na unakiri kuwa humpendi. Hii ni hatua moja nzuri sana kwako kwa sababu Mungu kawaida huwa hapendi watu wanafiki, wenye sura mbili. Ninavyoona mimi, wewe una uafadhali mara mia zaidi kuliko yule ambaye ni mnafiki, anajifanya kumpenda Mungu wakati kumbe siyo.Wengine hatuna tu option kulingana na vitisho tulivyopandizwa tangu utotoni ila huyu Mungu hatumpendi haswa
Kwani wewe ulikutana nae wapi Hadi ukamchukia?Wengine hatuna tu option kulingana na vitisho tulivyopandizwa tangu utotoni ila huyu Mungu hatumpendi haswa
Usilainishe lainishe uhalisia wenye walakini kwa kuusifia kama raia na serikali zetu za duniani, huko ni kuwa mnafiki kwa MUNGU wako...mkuu baada ya kuona kuna nyaka ndani Baba mwenye hekima aliamua kujenga nyumba nyingine na kisha kuwahamasisha wanae kuwa kutokana na nyumba hii kuwa na nyoka basi hamieni nyumba mpya niliyo wajengea ili msipatwe na madhara. Lakini kwa kuwa baba yeye ni mwenye uhuru hawezi mladhimisha mwanae kuwa toka humo ndani kwa lazima badala yake kajenga nyumba nyingine na kuwambia wanae wahaimie huma lakini kawe hawezi walazimisha kuhamia nyumba mpya.
Baada ya mwanadamu kuanguka dhambini Mungu hakuishia kumtazama mwandamu ateketee badala yake aliandaa mpango wa ukombozi. Na ametupatia uhuru wa kuchagua sisi wenyewe either tukombolewe(kuhamia nyumba mpya) au kuendelea kubaki dhambini(Kubaki kwenye nyumba ya zamani yenye nyoka).
kazi yake hainaga makosa,Katuondolea vipenzi vyeti ametuacha na majonzi yasiyoisha.
Mungu hamchukii mwenye dhambi lakini anaichukia dhambi hiyo ndio sababu lazima aiteketeze dhambi.Swali: kwanini kuchoma watoto wako moto?
Shetani madai yake toka kule mbinguni ni kuwa Mungu ni dikteta. na hivyo basi Mungu angeweza muangamiza moja kwa moja baada ya kuasi kwake lakini jee wale malaika wengine si wangeamini madai ya shetani ni sahihi. Badala yake Mungu kamwacha kwanza ili kila mmoja ajionee matokeo ya kile alichokifanya shetani ili pale atakapo kwenda kutoa hukumu basi kila kiumbe aseme kuwa hukumu zake ni za kweli na haki.Swali: Hawezi ondolewa?
mkuu kumbuka wakati Mungu anamuumba mwadamu haikuwa lengo lake mwanadamu kufa ila alimwambia utakapo kula mtu huo ni hakika utakufa.
Na mimi na wewe tunajua kabisa kuwa shetani ndio sababu ya mwanadamu kula lile tunda kwa maana yeye ndie alie washawishi hivyo ni Lucifer anapaswa kulaumiwa juu ya vifo vya wanadamu.
Ukikutana na mzazi asiyependa kinyesi na anaua mtoto anayejinyea sababu ana kinyesi utamsifia kuwa hapendi uchafu?Mungu hamchukii mwenye dhambi lakini anaichukia dhambi hiyo ndio sababu lazima aiteketeze
Cha muhimu tumuombee sana ndugu yetu, kafika katika situation ngumu sana
Mungu ampe wepesi
Hakika mkuu na pia ni watu wengi wanasema wanampenda Mungu lakin kiuhalisia wengi hawana Upendo huo,ukitaka ujue uhalisi wa mtu ni akiwa nyumbani kwake ndio utajua kuwa huyu anampenda Mungu au launadhani hata ana shida!!!
yeye mwenyewe katika maagizo yake anasema huwezi kunipenda mimi kama jirani yako unayemwona humpendi,so kama unampenda jirani imetosha.
Huyu akiona maswali magumu anayakwepa. Kuna swali nimemuuliza juu hakulijibu. Ukifuatilia maneno ya kwenye vitabu vya hizi dini halafu ukifanya reasoning unaona kabisa kuna shida mahali.Kwani yeye si mungu alipaswa kujua mbeleni mwanadamu atakuja kosea. Kwanini aliendelea kumuumba. Na kama alikuwa hataki mwanadamu apotee kwanini amruhusu shetani kumshawishi mwanadamu. Na kipindi shetani anamlaghai mwanadamu yeye mungu alikuwa wapi? Kuna maswali bado hayajibiki
Unaposema Mungu hajawahi kutuacha una maana gani mkuu?Na pia mkuu Mungu hajawahi kutuacha bali ni sisi tunaomuacha Mungu
Huyu akiona maswali magumu anayakwepa. Kuna swali nimemuuliza juu hakulijibu. Ukifuatilia maneno ya kwenye vitabu vya hizi dini halafu ukifanya reasoning unaona kabisa kuna shida mahali.