NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Hasa wanaume tunashindwa kusema ukweli kwamba tuna depression kwasababu tunaogopa kuonekana dhaifu kama wanawake, pia namna ambavyo jamii inamchukulia mwanaume inamuona kama kiumbe ambaye anatakiwa awe ngangali muda wote ila kiuhalisia depression haichagui mwanaume wala mwanamke.
Wengi sana tunapitia kwenye lindi la mawazo, stress na depression za kila namna kuanzia kudaiwa madeni, kufilisika, kukosa ajira, misuko suko ya ndoa, magoniwa, n.k.
Hivi ni vitu ambavyo ni ngumu sana kugawana na asiehusika lakini tunaweza kugawana comfort katika kufarijiana, kushauriana, kupeana moyo, n.k.
Kuongea huwa inasaidia kwa kiasi chake lakini sasa inafika kipindi unaona ni bora ukae kimya tu kulingana na uzoefu ulioupata katika maisha yako uliokufanya ujue maana halisi ya "kuwa uyaone" na "ukubwa dawa".
Unakuta una mtu wa karibu kabisa unaemwamini, anapoona una shida anaku hype kabisa "its okay unaweza kuongea na mimi, kuwa huru"
Baada ya muda unakuta mambo yako binafsi yameshasambaa mtaani, anaweza kuwa ni mzazi wako kabisa ama mwanafamilia lakini nae kwa lengo zuri la kupata ushauri wa zaidi akawaambia watu anaowaamini, matokeo yake hakuna siri tena, mtaani huko unaanza kujijua ushatangazwa "msimuone ana gari yule, pale alipo ana mawazo ya kurejesha deni", "msimuone ana mke mzuri vile, kagundulika ana kisukari shughuli hawezi", "msimuone vile anakwenda bar sana, kachapiwa mke yule", n.k. USHATANGAZWA!! hata kupita mitaa ya kati unaona noma.
Wengine unawaambia shida zako ila ndio wanafurahia mpaka wanaweza kukununulia chakula upate nguvu ya kuendelea kuwasimulia taabu zako, kwao ni kama kucheki tamthilia, kushuka kwako ama kuganda pale pale ndio furaha yao kubwa sana.