Elections 2010 Wengi hawajui Nguvu ya Maaskofu

Status
Not open for further replies.

Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!

Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.

Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?

Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.

Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!

This is incredibly shallow. Gospel teaches you to cater for the poor and provide them a social service. ie shule na hospitali. U do that because those are the teachings of Yesu, irrespective to the current political situation. Kama Meya akiwa wa Chadema, CUF, CCM--it doesn't matter to you koz you are doing the work of GOD. Kama ukiacha kufuata mafundisho ya Yesu kwa sababu meya wa Arusha ni CCM na kapitwa kwa wizi, siku ya Qiyama utaulizwa na Mola, wewe ishu ya Meya inakuhusu nini? Na mafundisho yangu si unayajua?

In short bwana Anold, your whole argument above is flawed. But u wouldn't know that; would you? Uko Jamii Forum.

Hawa Maaskofu kuingia kwenye siasa demonstrate gross irresponsibility on their part, thinking they are influential than they really are. You see, matamko yao has created rifts in our society as it should because some of us do not really care what Maaskofu do. And now ndio tunainuka na kuwasoma mwenendo wao. Obviously, our social institutions are strong enough to allow any maaskofu or mashehe to use dini as wedge to divide us. We are not going to fight. Ila ya Kaisari muachieni Kaisari.
 
sishangazwi za comments zako! ila kama huna kitu cha kuchangia hata kukaa kimya ni mchango wa maana. shida yenu ni kuwa tamko hilo lilitolewa na wakristo ambao dini yako haiwapendi japo wao wanawapenda! mambo kama hayo ndiyo yanayowafanya muone mapungufu ya dini zingine bila kujua shida yenu ambayo naamini ni kubwa si kwa mipaka ya tanzania tu bali dunia nzima kwa ujumla. Tambua wazi kilicholalamikiwa na maaskofu ni utaratibu usio sawa wa kumpata meya kitu kilichokuwa kinaashiria uvunjifu wa amani. Ila kwa kuwa meya ni wa chama tawala ambacho uongozi wake wa juu umeundwa na safu ya watu wa dini yako ndiyo maana wewe pamoja na wanzako mnadhani kumpinga meya ambaye ametoka chama cha ccm ni chuki dhidi ya viongozi wa ccm ambo wewe pamoja na wenzako hamuawaangalii katika jicho la viongozi wa kitaifa bali kama wenzenu katika dini yenu hilo ndiyo tatizo!!!
 
This is incredibly shallow. Gospel teaches you to cater for the poor and provide them a social service. ie shule na hospitali. U do that because those are the teachings of Yesu, irrespective to the current political situation. Kama Meya akiwa wa Chadema, CUF, CCM--it doesn't matter to you koz you are doing the work of GOD. Kama ukiacha kufuata mafundisho ya Yesu kwa sababu meya wa Arusha ni CCM na kapitwa kwa wizi, siku ya Qiyama utaulizwa na Mola, wewe ishu ya Meya inakuhusu nini? Na mafundisho yangu si unayajua?

In short bwana Anold, your whole argument above is flawed. But u wouldn't know that; would you? Uko Jamii Forum.

Hawa Maaskofu kuingia kwenye siasa demonstrate gross irresponsibility on their part, thinking they are influential than they really are. You see, matamko yao has created rifts in our society as it should because some of us do not really care what Maaskofu do. And now ndio tunainuka na kuwasoma mwenendo wao. Obviously, our social institutions are strong enough to allow any maaskofu or mashehe to use dini as wedge to divide us. We are not going to fight. Ila ya Kaisari muachieni Kaisari.

what a crap!! maaskofu walilalamikia namna uchaguzi wa meya ulivyoondeshwa na kusababisha hali tete ya amani na usalama na hata umwagaji damu.

Tatizo lenu waislamu hamumwoni kikwete na ccm (yenye viongozi zaidi ya 75% waislamu) kama rais wa nchi na ccm kuwa chama cha kitaifa bali mnamwona kama vile ni rais wa waislamu na ccm ni ya waislamu na akitokea askofu au mkristo ye yote anamkosoa kikwete au anaikosoa ccm mnaona kama vile anaingiza nguruwe msikitini.
 
huo udini wenu ndio unaoendelea kuwatafuna na bado...! mambo yamebadilika nyinyi mnataka kuishi kama zamani kudadadeeki!

Hasswaaaaaaaaa! Wamepata mshituko. Ushauri wa bure ni kwamba wawe na subira watazoea tu maana mambo ndiyo kwanza yameanza na yapo njia moja.
 
Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!

Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.

Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?

Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.

Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!

jamani lazima tuelewe kuwa misaada isitufanye kuwa kondoo wa kukubali kila kitu mtoa misaada anachotaka.

pamoja na misaada waliotoa maaskofu huko Arusha lakini wao wanatakiwa waijue nafasi yao katika jamii ni kuhubiri amani na upendo na si vinginevyo. Hawaruhisiwi hata kidogo kuingilia mtu aliyechaguliwa kwa mujibu wa sheria kuongoza wao waseme wanampinga. kwani sheria zetu zipo wazi kabisa KUWA KAMA KUN MTU ANA MALALAMIKO KUHUSU KUCHAGULIWA MEYA WA ARUSHA BASI AFUATE UTARATIBU WA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE NA SI KULETA VURUGU.

KIFUPI HAPA MAASKOFU WAMEUDHIRISHIA UMMA WOOOOOTE WA TANZANIA KUWA WAPO PAMOJA NA PADRE SLAA HIVYO CHADEMA NI CHAMA CHA MAASKOFU HAO .

POLENI SANA
 
Kwa wanaojua position ya maaskofu katika harakati za ukombozi south africa na U.S.A na kwingineko hawawezi kamwe kushabikia uj..n wa akina fulani
 
what a crap!! Maaskofu walilalamikia namna uchaguzi wa meya ulivyoondeshwa na kusababisha hali tete ya amani na usalama na hata umwagaji damu.

Tatizo lenu waislamu hamumwoni kikwete na ccm (yenye viongozi zaidi ya 75% waislamu) kama rais wa nchi na ccm kuwa chama cha kitaifa bali mnamwona kama vile ni rais wa waislamu na ccm ni ya waislamu na akitokea askofu au mkristo ye yote anamkosoa kikwete au anaikosoa ccm mnaona kama vile anaingiza nguruwe msikitini.

kama kweli maaskofu sio wanafiki kwanini wasitoe tamko la kumkataa rais wa nchi kwani kulikuwa na mizengwe mingi katika kura zake. Kwa taarifa mpaka leo tume ya uchaguzi haina hesabu ya uhakika kusema alishinda kwa kura ngapi.

Wangekuwa wakweli si wanafiki wangemkana raisi lakini si meya.

Acheni unafiki
 
Umasikini wa mawazo ni mbaya zaidi kuliko umasikini wa kipato. Nini kiini cha mgawanyiko wa manajamii? Wanaotuwakilisha wanatoa wapi nguvu hiyo?
 
Hapa umekwishaingia udini ndani ya wachangiaji badala ya kujadili hoja ya msingi ambayo ililetwa hapa,unajadiliwa idini na umimi CCM,CHADEMA.
Kwa anayependa maendeleo ya Arusha basi tuajadili kwa kina na kwa kutumia vigezo muhimu kwa ajili ya kujenga si si kubomoa.
 
Shukrani kwa mchango wako, yani tukishindwa kuona tatizo hilo basi tunaelekea kuchinjana.. If great thinkers cannot see this obvious problem, imagine hao wananchi wa kawaida.. Ignorance will kill us.....Maaskofu wamevuka mpaka kama vile waliposema Kikwete ni chaguo la mungu..

Unaweza ku'define' mipaka yao bila kuwa'domesticate'? Maana kama wanapokemea maovu wanavuka mipaka basi hakuna haja ya hiyo mipaka kuwepo. Binafsi naona masheikh ndio wanaovuka mipaka kwa vile kila mara wanakuja na hoja za kulalamikalalamika na kuwatungia maaskofu uongo. Mfano, wamesema eti Kanisa Katoliki lina jeshi linaloitwa 'Commission of Armed Forces' na wanatafsiri Tume ya Jeshi na wameiomba serikali kuondoa hilo jeshi! Kweli hawa wanajua wanachokiongea au wanaongea tu? Kwangu mimi kama kuna kuvuka mipaka huko ndiko kuvuka hiyo mipaka. Kwa nini wasiseme jeshi hilo liko wapi na maofisa wao wako wapi pia ili tuwafahamu? Hii tabia ya majungu majungu ni hatari sana!
 
kama kweli maaskofu sio wanafiki kwanini wasitoe tamko la kumkataa rais wa nchi kwani kulikuwa na mizengwe mingi katika kura zake. Kwa taarifa mpaka leo tume ya uchaguzi haina hesabu ya uhakika kusema alishinda kwa kura ngapi.

Wangekuwa wakweli si wanafiki wangemkana raisi lakini si meya.

Acheni unafiki

Poor reasoning! Kwa nini uwachagulie wa kumkataa? Mbona wewe hujamkataa?
 
jamani lazima tuelewe kuwa misaada isitufanye kuwa kondoo wa kukubali kila kitu mtoa misaada anachotaka.

pamoja na misaada waliotoa maaskofu huko Arusha lakini wao wanatakiwa waijue nafasi yao katika jamii ni kuhubiri amani na upendo na si vinginevyo. Hawaruhisiwi hata kidogo kuingilia mtu aliyechaguliwa kwa mujibu wa sheria kuongoza wao waseme wanampinga. kwani sheria zetu zipo wazi kabisa KUWA KAMA KUN MTU ANA MALALAMIKO KUHUSU KUCHAGULIWA MEYA WA ARUSHA BASI AFUATE UTARATIBU WA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE NA SI KULETA VURUGU.

KIFUPI HAPA MAASKOFU WAMEUDHIRISHIA UMMA WOOOOOTE WA TANZANIA KUWA WAPO PAMOJA NA PADRE SLAA HIVYO CHADEMA NI CHAMA CHA MAASKOFU HAO .

POLENI SANA

Hiyo ni tafsiri yako tu! By the way, kwa mantiki hiyohiyo masheikh wameudhihiria umma kwamba wako pamoja na CCM na huenda ni kwa sababu ya kuahidiwa Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC! Kwa sababu hiyo hawataku ku'antagonise' serikali ya CCM na CCM yenyewe!
 
sizunguki kama unavyofanya. hao mashehe wametumwa na 'wanasiasa' waliotangulia kulalama eti kuna udini hapa nchini. ukweli ni kwamba huyo bwana alikuwa anaanda watu wa dini yake ili kutishia amani.
 
Hiyo ni tafsiri yako tu! By the way, kwa mantiki hiyohiyo masheikh wameudhihiria umma kwamba wako pamoja na CCM na huenda ni kwa sababu ya kuahidiwa Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC! Kwa sababu hiyo hawataku ku'antagonise' serikali ya CCM na CCM yenyewe!

Kelele za mlango hizo ambazo si tishio kwa mwenye nyumba na kumkosesha usingizi.
 
Salaam

Nimekuwa nikisita sana kutoa maoni yangu katika mjjadala wa aina hii kutokana na kutambua kuwa wengi wetu humu na kwenye majukwaa mengine tumekuwa tukiongozwa na emmotions na ushabiki zaidi kuliko common sense. Lakini leo naomba nijitoe muhanga kusema kile ambacho naamini kinapaswa kusemwa kabla ya kuikuta kuwa tumefikia mahala pabaya zaidi kusipokuwa na kurudi nyuma.

Ni kweli kabisa viongozi wa dini, wawe Mashehe, Maulamaa, Maaskofu, Mapadre na Wachungaji wana haki na wajibu wa kukemea maovu yote bila ya kuchagua wakiwa kama wanadamu na pia raia wa nchi yetu.

Ni kweli kabisa kuwa katika historia ya nchi yetu, wakati wote viongozi wa dini wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kisiasa kwa njia moja ama nyingine, iwe kushutumu ama kupigia debe kundi kundi ama suala moja na lingine.

Ni kweli kabisa viongozi wa kijamii wana umuhimu mkubwa katika kusaidiana na wae wa siasa katika kuendeleza jamii kwenye neema zaidi na kuepusha kwenye majanga yawe ya kisiasa, kijamii ama kiuchumi.

Hata hivyo ni muhimu sana kutambua kuwa haki na wajibu huu ni lazima utambue UHALISIA wa mazingira tuliyonayo kama jamii. Ni wajibu wa viongozi kuangalia hali halisi haswa ya mahusiano ya kijamii ili kuiga faida na hasara za kutekeleza haki na wajibu wao.

Tanzania yetu ni Tanzania tunayoamini katika umoja na amani. Hii ni nyenzo muhimu katika kufanikisha dira ya maendeleo ya nchi yetu. Watanzania kama jamii ama taifa tunaamini kuwa tunapendana na kuheshimiana. Lakini hilo halina maana kuwa watanzania wote tunaaminina, kupendana ama kuheshimiana kama tunavyopenda kuamini na kujigamba mbele ya wengine.

Ni ukweli ambao wengi tunajaribu kuukataa kuwa watanzania hatuaminiani. na kutokuaminiana huko kupo katika misingi ya kisiasa, kimapato, kiasili, kikabila na hata kidini.

Miaka ya zamani ilikuwa sio kitu cha kawaida kusikia mtu akisema hawezi kumuamini mchaga. Lakini sasa hilo ni neno la kawaida kusemwa tena bila ya kificho wala haya. Miaka ya zamani ilikuwa sio kawaida kusikia muislamu akisema hamuamini mkristo ama mkristo kusema kuwa hamuamini muislamu, lakini sasa hilo ni neno la kawaida kusemwa tena bila hata kificho.

Yapo mengi yanayodaiwa kuwa chanzo cha hali hii ya kutokuaminiana tuliyonayo sasa. Wapo wanaoamini ni kutokana na umaskini, wapo wanaoamini ni kutokana na ujinga, wapo wanaoamini ni kutokana na siasa za ushindani usio na kifani, wapo wanaoamini kuwa ni kutokana na historia, wapo wanaoamini ni kutokana na siasa za kidunia hasa siasa za marekani na ulaya katika kupambana na kile kinachotabulika kama ugaidi wa kiislamu na wapo wanaoamini yote kwa pamoja ama sababu nyingine tofauti.

Zote zaweza kuwa ni sababu lakini cha muhimu ni kuwa uhalisia unaonyesha kuwa watanzania hatuaminiani. Na mbaya zaidi ni kuwa kutokuaminiana katika misingi ya kikabila na kidini kumekuwa kunakuwa ama kukuzwa zaidi kuliko kushughulikia kwa nia ya kupunguzwa kama sio kuondolewa kabisa.

Katika moja ya hotuba zake, Mwalimu Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa ingawa nchi yetu inajengwa katika misingi ya kutokuwa na ukabila, udini ama ubaguzi wa aina yeyote ile, si kweli kuwa watanzania sio wabaguzi. Aliendelea kudai kuwa utakuta wengie tunajigamba kuwa tunachukia udini ama ukabila lakini tukiminya kidogo tunatoka mapovu ya udini na ukabila. Na ndio maana UTANZANIA wetu ukajengwa kwa misingi ya kupiga vita ubaguzi wa aina yoyote ile kwa sababu uo na ni hatari kwa taifa.

Mtizamo huu unasisitiza ule mtizamo ambao yawezekana hakuandikwa katika sheria zetu lakini ulikuwepo miongoni mwa fikira za utanzania wetu kuwa si BUSARA kuchanganya dini na siasa. Hii ni busara ambayo inatambua haki na wajibu wa viongozi wa dini zetu kushiriki katika kupiga vita maovu ya aina zote lakini pia inatambua umuhimu wa kuepuka athari za kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya jamii yetu.

Wote tunakumbuka ni jinsi gani viongozi wa kisiasa na kidini walivyokuwa mstari wa mbele kusisitiza BUSARA hii katika miaka ya tisini ambako kulikuwa na vuguvugu kubwa la viongozi wa dini ya kiislamu kutoa matamko ya kisiasa. Wengine ambao leo hii tunajaribu kuhalalisha hilo ndio tuliokuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya mashehe hao wakati ule.

Wapo ambao wanatumia matamshi ama uungwaji mkono wa wazi wa Askofu Kilaini katika ugombea wa Rais Kikwete mwaka 2005. Lakini wanaacha kusema ni jinsi gani viongozi wenzake wengineo ambao walilaani kitendo chake hicho na kumpelekea kupunguziwa madaraka yake kama ilivyo sasa.

Moja ambalo wengi wanashindwa kung'amua ni kutambua mchango mkubwa wa kujenga maelewano na kupunguza kutoakuaminiana kulikowahi kufanywa na kiongozi huyo miaka ile. Wengi tunashindwa kufikiria tamko lake lile katika upana wake na ni jinsi gani tamko kama lile kutoka kwa kiongozi mkubwa wa kanisa la katoliki kumpigia debe mgomba urais muislamu linavyoweza kujenga na sio kubomoa kama endapo lingekuwa ni tofauti na lile.

Wengi hawajui ama wameshasahau nini kilichowapata baadhi ya mashehe ambao wamekuwa mstari wa mbele kusifia uongozi wa Mwalimu Nyerere ambaye kwa baadhi ya waislamu yeye anawakilisha chanzo kikuu cha madhila yote ambayo wanaamini wanayapata kutokana tu kuwa wao waislamu. Lakini wengine tunatambua umuhimu wa mitazamo chanya ya baadhi ya viongozi wa kiislamu kwa Baba wa Tafa sio tu kwa kuendeleza misingi aliyotuachia lakini hata kupunguza hali ya kutokuaminiana miongoni mwa wanajamii wa dini zetu mbili kubwa.

Wakati wengi wa waislamu wakitambua mapungufu mengi yaliyopoa katika serikali ya rais Kikwete na chama chake ni uweli usiofichika kuwa kuna mtazamo unaolingana miongoni mwa waislamu walio wengi kuhusiana na matamshi ama makaripio yasiyoisha kutoka kwa viongozi wa dini ya kikristo. Mtizamo huo ni ule wa kutokuamini nia ya dhati ya makaripio hayo. Ni ukweli ambao wengi tunapaswa kuutambua kuwa mtizamo kama huo hapo mwanzo ulikuwa miongoni mwa wale ambao wengi tungependa kuwatambua kama SIASA KALI/ EXTREMISTS ambao wapo katika pando zote za dini zetu, hivi sasa ni mtazamo wa wengi ama MAINSTREAM feelings. Huo ni ukweli ambao wanaoshabikia hali iliyojijenga katika miaka karibia minne iliyopita wanapaswa kutambua na kupima kama ni busara viongozi wa dini wawe waislamu ama wakristo wanapaswa kuendelea kuachwa ama hata kushabikiwa pale wanapotoa matamshi yenye kuonekana kama yana malengo ya kisiasa.

Yawezekana kabisa hali hii ya viongozi wa kidini kuwa mstari wa mbele kutoa matamko ya kisiasa yakawa yanaendana kabisa na matakwa na nia njema kabisa miongoni mwa watanzania kuona kuwa taifa letu linaepushwa na wingi zito za madhila ya ufisadi linalotanda, lakini pia kama raia makini ni muhimu kupima kama msaada huo unazidi umuhimu wa BUSARA ya viongozi wa kidini kutofanya hivyo.

Naamini kuwa wanasiasa na wanaharakati kama watakuwa tayari kuwajibika zaidi na kwa umakini zaidi wanaweza kabisa kufanikisha kile ambacho viongozi wa kidini wanachojaribu kukifanikisha ama kuzuia. Ni wazi kuwa kukaa pembeni kwa viongozi wa kidini kutotumia haki yao ama kutotekeleza wajibu wao wa kukemea maovu kwa style ya makaripio ya wazi ama matamshi ya majukwaani, kutaweza kujenga zaidi kuliko kubomoa kama mbavyo hali inavyoelekea hivi sasa.

Wanasiasa, wanaharakati na raia makini wana wajibu wa kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu wa kidini wanatilia maanani uhalisia wa mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyonayo kama taifa ambayo ukweli yanataka yanataka subira zaidi, busara zaidi na uvumilivu wa hali ya juu kuliko hali ilivyo sasa.

Omarilyas
 
Hivi huu wimbo wetu wa taifa hauchanganyi dini na siasa unaposema "Mungu ibariki Tanzania"?.
 
:clap2::clap2::clap2::clap2: well said!

Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!

Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.

Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?

Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.

Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!
 
Omariylas said:
Salaam

Nimekuwa nikisita sana kutoa maoni yangu katika mjjadala wa aina hii kutokana na kutambua kuwa wengi wetu humu na kwenye majukwaa mengine tumekuwa tukiongozwa na emmotions na ushabiki zaidi kuliko common sense. Lakini leo naomba nijitoe muhanga kusema kile ambacho naamini kinapaswa kusemwa kabla ya kuikuta kuwa tumefikia mahala pabaya zaidi kusipokuwa na kurudi nyuma.

Ni kweli kabisa viongozi wa dini, wawe Mashehe, Maulamaa, Maaskofu, Mapadre na Wachungaji wana haki na wajibu wa kukemea maovu yote bila ya kuchagua wakiwa kama wanadamu na pia raia wa nchi yetu.

Ni kweli kabisa kuwa katika historia ya nchi yetu, wakati wote viongozi wa dini wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kisiasa kwa njia moja ama nyingine, iwe kushutumu ama kupigia debe kundi kundi ama suala moja na lingine.

Ni kweli kabisa viongozi wa kijamii wana umuhimu mkubwa katika kusaidiana na wae wa siasa katika kuendeleza jamii kwenye neema zaidi na kuepusha kwenye majanga yawe ya kisiasa, kijamii ama kiuchumi.

Hata hivyo ni muhimu sana kutambua kuwa haki na wajibu huu ni lazima utambue UHALISIA wa mazingira tuliyonayo kama jamii. Ni wajibu wa viongozi kuangalia hali halisi haswa ya mahusiano ya kijamii ili kuiga faida na hasara za kutekeleza haki na wajibu wao.

Tanzania yetu ni Tanzania tunayoamini katika umoja na amani. Hii ni nyenzo muhimu katika kufanikisha dira ya maendeleo ya nchi yetu. Watanzania kama jamii ama taifa tunaamini kuwa tunapendana na kuheshimiana. Lakini hilo halina maana kuwa watanzania wote tunaaminina, kupendana ama kuheshimiana kama tunavyopenda kuamini na kujigamba mbele ya wengine.

Ni ukweli ambao wengi tunajaribu kuukataa kuwa watanzania hatuaminiani. na kutokuaminiana huko kupo katika misingi ya kisiasa, kimapato, kiasili, kikabila na hata kidini.

Miaka ya zamani ilikuwa sio kitu cha kawaida kusikia mtu akisema hawezi kumuamini mchaga. Lakini sasa hilo ni neno la kawaida kusemwa tena bila ya kificho wala haya. Miaka ya zamani ilikuwa sio kawaida kusikia muislamu akisema hamuamini mkristo ama mkristo kusema kuwa hamuamini muislamu, lakini sasa hilo ni neno la kawaida kusemwa tena bila hata kificho.

Yapo mengi yanayodaiwa kuwa chanzo cha hali hii ya kutokuaminiana tuliyonayo sasa. Wapo wanaoamini ni kutokana na umaskini, wapo wanaoamini ni kutokana na ujinga, wapo wanaoamini ni kutokana na siasa za ushindani usio na kifani, wapo wanaoamini kuwa ni kutokana na historia, wapo wanaoamini ni kutokana na siasa za kidunia hasa siasa za marekani na ulaya katika kupambana na kile kinachotabulika kama ugaidi wa kiislamu na wapo wanaoamini yote kwa pamoja ama sababu nyingine tofauti.

Zote zaweza kuwa ni sababu lakini cha muhimu ni kuwa uhalisia unaonyesha kuwa watanzania hatuaminiani. Na mbaya zaidi ni kuwa kutokuaminiana katika misingi ya kikabila na kidini kumekuwa kunakuwa ama kukuzwa zaidi kuliko kushughulikia kwa nia ya kupunguzwa kama sio kuondolewa kabisa.

Katika moja ya hotuba zake, Mwalimu Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa ingawa nchi yetu inajengwa katika misingi ya kutokuwa na ukabila, udini ama ubaguzi wa aina yeyote ile, si kweli kuwa watanzania sio wabaguzi. Aliendelea kudai kuwa utakuta wengie tunajigamba kuwa tunachukia udini ama ukabila lakini tukiminya kidogo tunatoka mapovu ya udini na ukabila. Na ndio maana UTANZANIA wetu ukajengwa kwa misingi ya kupiga vita ubaguzi wa aina yoyote ile kwa sababu uo na ni hatari kwa taifa.

Mtizamo huu unasisitiza ule mtizamo ambao yawezekana hakuandikwa katika sheria zetu lakini ulikuwepo miongoni mwa fikira za utanzania wetu kuwa si BUSARA kuchanganya dini na siasa. Hii ni busara ambayo inatambua haki na wajibu wa viongozi wa dini zetu kushiriki katika kupiga vita maovu ya aina zote lakini pia inatambua umuhimu wa kuepuka athari za kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya jamii yetu.

Wote tunakumbuka ni jinsi gani viongozi wa kisiasa na kidini walivyokuwa mstari wa mbele kusisitiza BUSARA hii katika miaka ya tisini ambako kulikuwa na vuguvugu kubwa la viongozi wa dini ya kiislamu kutoa matamko ya kisiasa. Wengine ambao leo hii tunajaribu kuhalalisha hilo ndio tuliokuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya mashehe hao wakati ule.

Wapo ambao wanatumia matamshi ama uungwaji mkono wa wazi wa Askofu Kilaini katika ugombea wa Rais Kikwete mwaka 2005. Lakini wanaacha kusema ni jinsi gani viongozi wenzake wengineo ambao walilaani kitendo chake hicho na kumpelekea kupunguziwa madaraka yake kama ilivyo sasa.

Moja ambalo wengi wanashindwa kung'amua ni kutambua mchango mkubwa wa kujenga maelewano na kupunguza kutoakuaminiana kulikowahi kufanywa na kiongozi huyo miaka ile. Wengi tunashindwa kufikiria tamko lake lile katika upana wake na ni jinsi gani tamko kama lile kutoka kwa kiongozi mkubwa wa kanisa la katoliki kumpigia debe mgomba urais muislamu linavyoweza kujenga na sio kubomoa kama endapo lingekuwa ni tofauti na lile.

Wengi hawajui ama wameshasahau nini kilichowapata baadhi ya mashehe ambao wamekuwa mstari wa mbele kusifia uongozi wa Mwalimu Nyerere ambaye kwa baadhi ya waislamu yeye anawakilisha chanzo kikuu cha madhila yote ambayo wanaamini wanayapata kutokana tu kuwa wao waislamu. Lakini wengine tunatambua umuhimu wa mitazamo chanya ya baadhi ya viongozi wa kiislamu kwa Baba wa Tafa sio tu kwa kuendeleza misingi aliyotuachia lakini hata kupunguza hali ya kutokuaminiana miongoni mwa wanajamii wa dini zetu mbili kubwa.

Wakati wengi wa waislamu wakitambua mapungufu mengi yaliyopoa katika serikali ya rais Kikwete na chama chake ni uweli usiofichika kuwa kuna mtazamo unaolingana miongoni mwa waislamu walio wengi kuhusiana na matamshi ama makaripio yasiyoisha kutoka kwa viongozi wa dini ya kikristo. Mtizamo huo ni ule wa kutokuamini nia ya dhati ya makaripio hayo. Ni ukweli ambao wengi tunapaswa kuutambua kuwa mtizamo kama huo hapo mwanzo ulikuwa miongoni mwa wale ambao wengi tungependa kuwatambua kama SIASA KALI/ EXTREMISTS ambao wapo katika pando zote za dini zetu, hivi sasa ni mtazamo wa wengi ama MAINSTREAM feelings. Huo ni ukweli ambao wanaoshabikia hali iliyojijenga katika miaka karibia minne iliyopita wanapaswa kutambua na kupima kama ni busara viongozi wa dini wawe waislamu ama wakristo wanapaswa kuendelea kuachwa ama hata kushabikiwa pale wanapotoa matamshi yenye kuonekana kama yana malengo ya kisiasa.

Yawezekana kabisa hali hii ya viongozi wa kidini kuwa mstari wa mbele kutoa matamko ya kisiasa yakawa yanaendana kabisa na matakwa na nia njema kabisa miongoni mwa watanzania kuona kuwa taifa letu linaepushwa na wingi zito za madhila ya ufisadi linalotanda, lakini pia kama raia makini ni muhimu kupima kama msaada huo unazidi umuhimu wa BUSARA ya viongozi wa kidini kutofanya hivyo.

Naamini kuwa wanasiasa na wanaharakati kama watakuwa tayari kuwajibika zaidi na kwa umakini zaidi wanaweza kabisa kufanikisha kile ambacho viongozi wa kidini wanachojaribu kukifanikisha ama kuzuia. Ni wazi kuwa kukaa pembeni kwa viongozi wa kidini kutotumia haki yao ama kutotekeleza wajibu wao wa kukemea maovu kwa style ya makaripio ya wazi ama matamshi ya majukwaani, kutaweza kujenga zaidi kuliko kubomoa kama mbavyo hali inavyoelekea hivi sasa.

Wanasiasa, wanaharakati na raia makini wana wajibu wa kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu wa kidini wanatilia maanani uhalisia wa mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyonayo kama taifa ambayo ukweli yanataka yanataka subira zaidi, busara zaidi na uvumilivu wa hali ya juu kuliko hali ilivyo sasa.

Omarilyas
Pasipo na IMANI kuna Uovu, Pasipo na MISINGI kuna Ufedhuli, Pasipo na ITIKADI kuna Ujanjaujanja...Yote haya ni mazalia ya UFISADI

Omariylas,

..kama nimekuelewa hoja yako ni kwamba wa-Tanzania hatuaminiani kidini na kikabila.

..pia umeelekeza kwamba, pamoja na nia njema ya viongozi wa dini kuikosoa serikali hapa na pale, nia hiyo njema inapotoshwa kutokana na ukweli kwamba wa-Tanzania HATUAMINIANI.

..mapendekezo yako, kama nimekuelewa, ni kwamba ili kuliokoa taifa, na kuondoa hiki kiwingu cha udini ktk siasa zetu, ingefaa viongozi wa kidini wakaji-excuse kutoa matamshi yoyote yale yenye mwelekeo wa kisiasa.

..maoni yako yanaweza kuwa ya msaada ktk kuepusha haya malumbano ya kidini.

..pamoja na kukuunga mkono, naomba niongeze mambo machache hapa.

..kwa mtizamo wangu itafutwe namna[[mbinu] ya kushughulika na viongozi wa kidini wanaopandikiza mbegu ya kutokuaminiana miongoni mwa wa-Tanzania.

..binafsi naamini viongozi wa kidini ni very intolerant kwa watu wa imani tofauti na za kwao. sasa hawa wanapaswa kueleweshwa kwamba nchi hii ni yetu sote na kuna misingi inayopaswa kufuatwa ili tuweze kuishi kwa amani na maelewano.

..labda Mashekhe,Maimamu,Wachungaji,Mapadre,...waelekezwe kwamba kuna mambo mengi sana yanayowaathiri waumini wao bila kubagua na ingepaswa wayashughulikie hayo kuliko kuendeleza malumbano yasiyo na tija.

..Maaskofu/Mashekhe waache kuvizia wakisubiri Mashekhe/Maaskofu watoe tamko ndipo waibuke na kupinga. vilevile Maaskofu/Mashehe wajiepushe na matamshi yenye kushambulia dini na viongozi wa imani nyingine.

..kuna umuhimu wa Mashekhe na Maaskofu kukaa pamoja na kujadili jinsi gani watatekeleza wajibu wao bila kuifarakanisha jamii ya wa-Tanzania.
 
Vile vile ungeliongezea kuwa viongozi wa dini wangelijiepusha kuonyesha wanakubaliana na viongozi wa chama fulani au itikadi ya chama fulani, kwani waumini wao ni wafuasi wa vyama vyote Tanzania. Hivyo basi lingejenga mazingira ya kuaminiana zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom