Wengi hawajui Nguvu ya Maaskofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi hawajui Nguvu ya Maaskofu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anold, Jan 10, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180

  Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!

  Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.

  Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?

  Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.

  Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  Haihitaji akili nyingi kujua umuhimu wa kanisa hapa tanzania, ni wale tyu wenye pepo wachafu na ambao vurugu za arusha wamezianzisha kwa makusudi na kwa maslahi yao binafsi kama akina kikwete na makamba...hakika hawa hawatataka kusikia matamko ya maaskofu kwani wanaharibu kitumbua chao kiliichojaa damu za wasio na hatiwa wale walioandamana kwa amani ili kushinikiza haki kutendeka........
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa siasa wanapaswa na kuzingatia KUWAHESHIMU VIONGOZI WA DINI,
  Viongozi wa dini wanayo nguvu kuliko dola, binafsi sielewi hizi kauli za Makamba kuwakejeli hawa spiritual leaders.
   
 4. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Anold, umenikumbusha kitu muhimu sana kuhusu kazi za Kanisa na uhusiano na uchumi wa eneo. Miaka ya 1970 na 1980, Padri mmoja mzee kule Maua Moshi alianza kuona chemichemi alimokuwa ametegeshia pump za maji kwa ajili ya shule ya seminari na majirani zilikuwa zinaanza kukaukia. Akagundua tatizo ni ukataji wa misitu millimani ambako ndiyo chanzo cha maji. Basi akaamua kuanza kuotesha msitu na amini usiamini kwa kushirikiana na wanafunzi na watu wachache walioajiriwa na kanisa aliotesha msitu wa zaidi ya kilomita mraba 6. Msitu ukakua na vyanzo vya maji vikawa vimeanza kushiba maji.

  Mwaka 2004, akiwa anatembea kwenye tafakari maeneo ya seminari yake, aliona malori makubwa makubwa yamebeba miti. Kumbe Afisa Msitu alitoa kibali cha kuvunwa ule msitu aliootesha yule Mzee. Alikimbiza magari yale kwa miguu na kupayuka, akitaka kujua imekuwaje wanavuna msitu! Alikwenda Idara ya Msitu, na wale watendaji wakamshangaa, kwanza yeye ni mzungu halafu anazungumzia uvunaji wa raslimali za kikwetu. Baadaye ilijulikana kuwa ni viongozi wa serikali za mtaa kwa kushirikiana na watendaji waliridhiana kuvuna ule msitu. Katika hali hii kweli watu wa Kanisa au Msikiti wasijali aina ya uongozi tunaokuwa nao kwa manufaa yao na wananchi wao.

  Bila shaka kauli za Katibu wa CCM Mkoa Arusha zimejikita zaidi kwenye ubinafsi kwani yeye ndiye kitovu cha vurugu zote za Arusha.
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Anold big up kwa kuwafumbua macho ya kiakili mambumbumbu. Huo ndo ukweli na siongezi zaidi ingawaje yapo. Ila tabia ya kupinga kila kitu hata kama ni chema wanachoongea maaskofu kisa umetega kitu fulani kwa serikali ili iwape favour ni UTUMWA NA FIKRA. NA kama viongozi wenye mentality za namna hiyo ni wa dini basi wana mushkeli katika imani yao labda wawe wanamwabudu Mungu ambaye si muumba wa Mbingu na nchi. Ninavyojua hakuna dini inasema waumini wapingane na kila kitu ndo waonekane wana msimamo au ndo liitwe tamko. Sidhani kama dini nyingine ikitoa msimamo wao mzuri kuhusu jambo fulani maaskofu watawapinga tu kwa sababu ni dini tofauti bali wata support ya maana hata kama ni dini tofauti.
   
 6. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  well Chitanda alisema wajihusishe na kukemea maovu TUUUUUUUUUUU! Hivi unajiuliza, uuaji wa raia namna ya Arusha si uovu huo? Na viongozi wasikemee hilo pia?
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa dini nyingine hawakuwa na ruksa ya kuwashambulia maaskofu kwa msimamo wao eti kwa kuwafundisha cha kuongea nani kawapa mamlaka hiyo?. Wao walitakiwa watoe tamko lao bila kuujilinganisha na maaskofu kwani walitaka maaskofu wajiunge nao kivipi wakati kila mtu ana haki kimtazamo kutoa msimamo wake na siyo kuukosoa msimamo wa dini nyingine.
   
 8. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Walichokisema maaskofu halina udini hata kidogo, ila kuna watu wachache ambao kwa maslahi binafsi au hongo wanayopewa wamesahau hata wajibu wao kwa mungu.

  Nakumbuka Askofu moja aliwahi kusema JK ni chaguo la mungu, hakuna askofu hata moja aliyetia neno na ni kutokana na kupata asilimia 80. Leo hii JK kageuke na kuagiza watu kupigwa risasi hadi kufa, wengine kujeruhiwa maskofu wanamwonya eti kuna wendawazimu wanasema wanamwonea kwa kuwa yeye ni muislamu hii inatoka wapi? Hivi mungu anapenda binadamu wauwane, au mnataka na katika hili maaskofu waseme ameagizwa na mungu kufanya hivyo.

  Ukweli uko wazi kama kuna kiongozi a dini awe mkristu au muislamu anataka watu wauawe huyo katumwa na shetani kabisa. Katika hili mimi sikubaliani na mtu anayeamini kuwa JK hahusiki. Tena kama ni mtuhumiwa JK ni namba moja maana hata hao polisi na CCM yote iko chini yake na ndio wanaoivuruga inchi hii ndio maana hatupigi hatua katika maendeleo.

  Peoples Power.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  VIONGOZI WAOOTE WA CCM VILAZA SIJUI PEPO GANI LIMEWAPITIa
   
 10. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtizamo wangu maaskofu wako sawa kabisa! Yaliyotokea Arusha ni uchafu wa watu wachache tu.
  Ebu niambie siku ya Leo kama CCM tunajiridhisha kuwa uchaguzi ulikuwa halali na tuna haki ya kushinda tuna hofu gani ya kurudia uchaguzi kwani wapiga kura ni wale wale, si waurudie tu tuwape raha Watanzania? Hiza Unapaswa kujua kuwa chama chetu CCM kinauwezo mkubwa na wananchi wanakipenda sana, hivyo mwambie Lyimo ajiuzulu na turudie uchaguzi, hatuhitaji Muafaka na CHADEMA ila uchaguzi urudiwe na CHADEMA WAJUE KUWA hapakuwa na njama/hila zozote. Watu
  Ubishi wa nini? mimi ninaamini kuwa CCM tunauwezo wakushinda huo uchaguzi nami nashauri turudie tu. Mungu Ibariki CCM, Mungu Ibariki Arusha, Mungu bariki Tanzania!
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Wako na Sheikh wao...........
   
 12. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Huyu mama aliwaambia Maaskofu wavue majiho wabaki vipi sijui. Ngoja kama hajaenda kuwapigia magoti .
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza BIG up ANOLD kwa kuleta hii thread kwanza nasikitika kwa kauli za mzee makamba na viongozi wengine wa CCM....Hawajali utut na damu ya binadamu iliyomwagika kwa sababu tu ya uchu wa madaraka mimi nawashauri kama siasa imewashinda waache tuu maana kuna siku wataburuzwa barabarani kama SAMUEL DO wa LIBERIA
   
 14. h

  hamida ally Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siasa ni ya wote mtu asijidai kujiita ye mwanasiasa,basi kura wangepiga wenyewe,maaskofu na viongozi wa deni wote wanapiga kura na ndo wanasababisha siasa kuwepo hapo bila wapiga kura kungekuwa na siasa?waacheni waongee wanahaki kuzungumzia madaraka waliowapa watu,  mbona kwenye kupiga kura hamuwaambie wenyewe ni kukemea maovu na sio kupiga kura?
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mfamaji, japo nina uchungu na huzuni kubwa kwa yaliyotokea nyumbani kwangu, lakini imebidi nicheke tena kwa hii quote.
  Tuendelee kufarijiana na kupeana moyo katika kipindi hiki cha majaribio yanayoongozwa na shetani.
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Asante kwa post nzuri,ukweli ni kuwa viongozi wetu wamelewa madaraka na kwa vile hawawajibishwi kwa yale wanayoongea,wana kiburi cha kusema wayatakayo.Hakuna mtu ana nguvu kama kiongozi wa dini kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni waumini wazuri wa dini yao...Kwenye imani ndiko tunakotafuta majibu ya masuala magumu kwenye maisha yetu including haya maisha magumu nchini kwetu,hatutegemei majibu kutoka kwa wanasiasa bali kwa Mungu.Na mtumishi wa Mungu ana heshima ya kipekee na nguvu kubwa na imani ya wale anaowangoza,kwa hiyo ni kosa kubwa kudharau Maaskofu na ni kukosa pia busara.Maaskofu wana uwezo wa kuleta vita na serikali na kuepusha vita na serikali?Kwa kuwa ndio wanaolea watu kiroho,hakuna kosa kwenda kuzungumza roho zinazolia kila siku kwa yale serikali inayofanya.CCM Arusha walikosea sana,na itachukua muda kumaliza hiyo chuki walioijenga si tu na viongozi wa dini bali na waumini wao,kwa kuwa ukimdharau askofu haiwezekani unaniheshimu muumini.
   
 17. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inaelekea Chitanda hajui definition ya maovu!!!!!!!!!!!!!
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inabidi wananchi waelimishwe ili wajue nguvu ya uma ilivyo
   
 19. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umesema vizuri sana. Kwani huyo Chitanda ni dhehebu gani? Na kwanini yeye na familia yake wasitengwe na kanisa kwa kukosa adabu hadi hapo atakapo tubu dhambi zake?
   
 20. c

  crown Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Biblia inasema kila neno mwanadamu anenalo atatoa hesabu yake siku ya kufa kwake.Yeye alitaka watu kanisa likae kimya tu kama waumini wao wameuawa na polisi?. Vilevile huwezi kutenganisha mambo ya kiroho na kimwili ndio maan watu wanapoapa huwa wanatumia vitabu vya dini.Mimi nafikiri huyu Chitenda ni mpagani na hiyo damu ya watu wasio na hatia itakuwa juu yake na familia yake asipotubu.Kama ni muumini wa dini yoyote huyu anapaswa atengwe kabisa.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...