ni kweli kuwa maisha ya kila mmoja yanategemea juhudi ya mhusika mwenyewe ambayo kwangu mimi nadhani inachangia kama 25% katika mafanikio na asilimia 75% ni mchango wa jamii kwa maana kama jamii haijajenga shule je mmoja mmoja juhudi zake zitamsaidia nini? kama jamii haina hospitali juhudi za mmoja mmoja zitafanya nini? kama jamii haijajenga barabara je juhudi za mmoja mmoja zitafanya nini? kama jamii haina uwezo wa kutumia huduma zako au kununua bidhaa zako je unadhani mtu atauza nini?
hapo utagundua mtu mmoja mmoja hawezi kufanya lolote peke yake bali jamii nzima kuweka nguvu ya pamoja ili kutengeneza fursa na hapo ndipo wananchi mmoja mmoja anapotumia fursa kujiendeleza.
jamii zimeweka mifumo ya kuwaongoza kufanya mambo yao kwa ushirikiano na hapo tunaongelea utawala wa nchi.
viongozi wa nchi ndio wenye wajibu wa kuisimamia jamii katika hayo kwa maana kuhakikisha wanajamii wenyewe wanajenga miundombinu ya kurahisisha maisha yao wachangie fedha zao kupitia kodi au kuuza mali zao walizokubaliana zimilikiwe na jamii kwa pamoja kama madini na gesi, wajiwekee taratibu na kanuni za kustawisha maisha yao.
hii ndio dhana ya kuchagua viongozi na hapo ndipo mwananchi anapobeba dhamana ya maendeleo yake kwa asilimia 100.
maana yake ni kuwa kama unalima nyanya unatakiwa kuhakikisha kabla ya kulima uchague kiongozi ambaye unaona anaenda kusimamia fedha za jamii zitumike kutekeleza asilimia 75 inayochangiwa na jamii ili wewe ukiweka juhudi zako upate maendeleo.
uchague kiongozi ambaye ataweka kanuni za kulinda soko la ndani ili wewe uuuze kwanza na bidhaa kutoka nje zije tu pale ambapo nyinyi ndani mmeshindwa kutosheleza mahitaji.
uchague kiongozi ambaye ataweka mifumo inayowaelekeza wananchi wake wazalishe nini kutokana na soko na sio umekwisha zalisha ndio unagundua soko hakuna.
uchague kiongozi ambaye atawajengea wananchi wake uwezo ili wazalishe
lakini kama wewe mwenyewe umegeuza uchaguzi wa kuchagua viongozi bora wa kuchangia maendeleo yako kuwa kamali unachukua rushwa za kijinga kama vyakula, nguo, pombe na vitu vingine vidogo na kuchagua wahuni au wezi ambao hawatumii fedha zenu kuwajengea mazingira, au unashabikia rangi za mavazi na bendera za vyama, majina au umaarufu wa wagombea na sio kusikiliza mipango ya maendeleo na kupima uwezo wa kutekeleza ukachagua nani alaumiwe pale unaposhindwa kupata fursa?
maisha yetu yanaanzia kwenye kulipa kodi ili serikali ituhudumie hivyo kama hauko tayari kuchangia ujue huwezi kupata maendeleo kwa maana maendeleo yetu tunayachangia sisi wenyewe,
yanafuataia kuchagua viongozi bora ili wasimamie fedha zetu na rasilimali zetu zitumike kuweka miundombinu, mifumo, sheria na kila kitu cha kurahisisha maendeleo yetu wote tukipewa fursa kwa usawa.
na hatua ya tatu ni kila mmoja kutumia fursa anayoitaka kujiletea maendeleo yake mwenyewe na huku akiendelea kujenga uwezo wa kuchangia zaidi katika jamii ili tupate huduma zaidi.
kama tunadhani hatustahili kuwa hapa tulipo tutafakari katika hayo matatu tumekosea wapi ili tupate jinsi ya kwenda mbele.
25 ina
Point tupu.
Sasa ili kusaidia zaidi hebu please weka na fursa. Yaani mawazo kama ukifuga kuku wa kienyeji soko lake wapi, ukifuga mbuzi unapelekaje comoro au uarabuni, ng'ombe utauzia wapi, mayai je ya kienyeji soko likwapi, je ni wapi pa kununua mazao kwa sasa na wapi pa kuyauza? kama kuwekeza kwenye soko la hisa mtu afanyeje?
Nasema hivi kwasababu moja kuu mkuu, Hapa nchini kila mtu analalamika kama wewe kuanzia wazazi hadi viongozi wa kitaifan lakini hawawapi vijana njia iliyonyooka ya kutafuta au namna ya kutoka.
Wazazi wengi wanawalalamikia watoto lakini hawaelewi miaka ya 1950 au 60 na sasa ni tofauti. Sasa watu wanahitaji capital na soko na vyote hivyo ni shida kuvipata kwasababu viongozi wetu hawajawa makini kuwekeza kwa vijana.
Mfano, mtu analima mpunga ila akivuna tu anakuta sokoni kuna mchele toka Thailand.... je huyo ana kosa gani?????? Mtu anafuga kuku wa kienyeji akitaka kuuza mayai mara tayari Wakenya wameshaingiza yakwao sokoni.. je huyo ana kosa gani???? hiyo ni mifano michache inayoonyesha kuwa uvivu wa asilimia 25 ya vijana wa sasa umesababishwa na mazingira zaidi kuliko wao wenyewe. Hao wengine 75% ni uvivu wao wa kujitakia.
Na ndio maana huwa nawaambia vijana wenzangu, usikurupuke tu kupigia mtu kura kisa umekunywa bia zake kadhaa. Jiulize, huyu mtu ataangalia maslahi ya vijana, ni mtu anayeyeweza na anayejua kuwaunganisha vijana na kuzungumza nao kuhusu maendeleo?????? Ni mtu mwenye mlengo wa maendeleo ya jamii kwa ujumla au tumbo lake????? je kama alikuwa bungeni, kwa kipindi hicho amewafanyia nini wanajimbo
wake??????
Kwahiyo maendeleo ni njia mbili. Kijana awe na mawazo ya kufanya kitu fulani na Serikali iwe imeshamwandalia mazingira mazuri ya kuuza hiyo bidhaa.