Wengi hawajui kwanini tunasema 'Life begins at 40'

Wengi hawajui kwanini tunasema 'Life begins at 40'

Monjo1

New Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
0
Reaction score
60
Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40.

Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.Uwe na usafiri binafsi.Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!

At 40 inabidi uwe unaishi. Siyo ndo unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.

At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?

At 40 utakuwa bado unaomba nauli kwa baba na mama kwani?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu.

Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi.

Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe inasubiri maisha bora CCM ndo wakupe.

Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram una LIKE picha za Wema Sepetu. Umeshajua Wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see?

Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.

Kwani wanasoka wangapi wako kama Beckham
Wanamuziki wangapi wako kama Kirk Franklin
Wacheza Tennis wangapu wako kama Roger Federer? Unadhani amekuwa champion akiwa amekaa na TECNO chumbani ana comment kuhusu migomo? No. Alikuwa ana-hussle wakati wengine wanachat.

Seriously. Diamond unayemfollow anafanya kazi hivyo. Anatoka studio saa saba usiku������ wewe uko kwenye page yake una LIKE. Huwezi kuona kuwa uko tofauti.

Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo tu na kutuma picha za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndio NIPASHE sasa hivi?

Anyway. Kuwa serious na maisha yako angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako. Aise huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana. Au unadhani watazikuta hizo comments na LIKES ������ zako? No. Wanapaswa wakute nyumba, viwanja, account za benki zinazopumua.

Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu! ������ Wanatakiwa wakute assets za maana angalau. Siyo rundo la CD za bongo movie ambazo hazikusaidii wewe wala wao.

Miezi hii 6 iliyobaki kumaliza mwaka huu 2015 umeweka mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40?

Au bado unategemea mshahara wa laki 8 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako).

Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele?

Be careful my friend

Natafuta watu ambao wako tayari kupunguza kuchat na kutuma picha za vichekesho na waanze kufanya vitu serious kwa ajili ya future. Natafuta watu ambao wako tayari kujifunza na kufundishika na kuweka bidii katika kujiletea maisha bora badala ya kuyasubiria yaletwe na UKAWA au Lowassa.

Haya sasa wamemkata jina.Utagoma kula au? Yaani mi huwa nawashangaa watu. Kabisa unadhani kuna mtu atakupa maisha ya ndoto zako?

Ukweli ni kwamba maisha ni ya kwako na ni wewe utakayeyabadilisha. Bill Gates huyo huyo anasema

"KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SI KOSA LAKO LAKINI UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO"
 
Upo sahihi mkuu lkn kwa maisha yetu ya kibongo na kiafrika kutimiza yote hayo ni ngumu japo pia kuna mantiki kubwa kwa hayo uyasemayo,kubwa ni kufanyakazi kwa bidii ili kutimiza malengo yk na kumwomba sana mungu akusimamie
 
Kwa nchi zilizoendelea ni kweli inawezekana lakini huku kwetu Africa ni wachache wanaweza hiyo formula yako ya maisha.
 
jopaboy

Point tupu.

Sasa ili kusaidia zaidi hebu please weka na fursa. Yaani mawazo kama ukifuga kuku wa kienyeji soko lake wapi, ukifuga mbuzi unapelekaje comoro au uarabuni, ng'ombe utauzia wapi, mayai je ya kienyeji soko likwapi, je ni wapi pa kununua mazao kwa sasa na wapi pa kuyauza? kama kuwekeza kwenye soko la hisa mtu afanyeje?

Nasema hivi kwasababu moja kuu mkuu, Hapa nchini kila mtu analalamika kama wewe kuanzia wazazi hadi viongozi wa kitaifan lakini hawawapi vijana njia iliyonyooka ya kutafuta au namna ya kutoka.

Wazazi wengi wanawalalamikia watoto lakini hawaelewi miaka ya 1950 au 60 na sasa ni tofauti. Sasa watu wanahitaji capital na soko na vyote hivyo ni shida kuvipata kwasababu viongozi wetu hawajawa makini kuwekeza kwa vijana.

Mfano, mtu analima mpunga ila akivuna tu anakuta sokoni kuna mchele toka Thailand.... je huyo ana kosa gani?

Mtu anafuga kuku wa kienyeji akitaka kuuza mayai mara tayari Wakenya wameshaingiza yakwao sokoni.. je huyo ana kosa gani???? hiyo ni mifano michache inayoonyesha kuwa uvivu wa asilimia 25 ya vijana wa sasa umesababishwa na mazingira zaidi kuliko wao wenyewe. Hao wengine 75% ni uvivu wao wa kujitakia.

Na ndio maana huwa nawaambia vijana wenzangu, usikurupuke tu kupigia mtu kura kisa umekunywa bia zake kadhaa. Jiulize, huyu mtu ataangalia maslahi ya vijana, ni mtu anayeyeweza na anayejua kuwaunganisha vijana na kuzungumza nao kuhusu maendeleo?????? Ni mtu mwenye mlengo wa maendeleo ya jamii kwa ujumla au tumbo lake?je kama alikuwa bungeni, kwa kipindi hicho amewafanyia nini wanajimbo
wake?

Kwahiyo maendeleo ni njia mbili. Kijana awe na mawazo ya kufanya kitu fulani na Serikali iwe imeshamwandalia mazingira mazuri ya kuuza hiyo bidhaa.
 
Last edited by a moderator:
jopaboy

We we kichwa!! You r a real great thinker.
 
Last edited by a moderator:
rr3

Umenena ukweli mtupu!
You are wide and tough minded,Vijana inapaswa tuwaze hivyo!
 
Last edited by a moderator:
Hapa najifunza kitu, vijana wengi tumekuwa tukishabikia hoja bila kui analyse, mkuu angesema na alternative ingekuwa bora zaid

Ndo hapa naona udhaifu wa vijana si kila kitu cha kuambiwa fursa unaiona mwenyewe kulingana na maisha unayoishi,kulingana na upana wako wa kufikiri na motivations ndani yako.

Fursa si za kufundishwa ndo maana tunaishia kuigana Fulani kalima ngoja na Mimi nikalime mwisho wa siku unajikuta umeanguka.

Tengeneza fursa kulingana na wewe mwenyewe.
 
We we kichwa!! You r a real great thinker.

Great thinker sio huyu, GT ni yule aliyeandika hii meseji, huyu kafanya kuileta tu hapa JF because wengine tumeshaipata through our mobile phone, tumesoma na kujua kwanini maisha ni at 40 lkn kwa Tanzania yetu hii mmh! labda uwe unatoka familia za kishua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom