Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema "LIFE BEGINS AT 40". Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji... Uwe na familia yako tayari... Uwe na kwako tayari na sio umepanga bado... Uwe na usafiri binafsi... Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!!
View attachment 1049533
At 40 inabidi uwe unaishi. Sio ndio unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri. At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule katika dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje??? At 40 utakuwa bado unaomba nauli kwa baba na mama kwani???
Sasa hivi vitu haviji ukiwa upo upo tu, unashangaa shangaa hovyo magorofa Posta na Kariakoo. Hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti. Upo tu una "LIKE" kila kitu Facebook, Twitter, JamiiForums na Instagram. Unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana, unatuma za migomo ya madereva, mgomo ukiisha unatuma za mafuriko, kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa. Yaani umekuwa mtumwa wa simu.
Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabu ajabu tu. Havikufikishi popote na "UMRI UNAZIDI KWENDA", unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi.
Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula "LIKES" zako za Instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada shule na si "LIKES" zako za Facebook. Wanahitaji wewe kua mfano bora wa maendeleo katika maisha yao. Wanahitaji maisha bora. Wewe unasubiri maisha bora "CCM" au "CUF" ndio wakupe. Wasipokupa unataka "UKAWA" waje wakupe ukiwa umekaa Instagram una "LIKE" picha za Wema Sepetu. Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje??? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see???
Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa "KU-ENTERTAIN" brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.
Kwani wanasoka wangapi wako kama David Beckham na Zinedine Zidane. Wanamuziki wangapi wako kama Kirk Franklin. Wacheza Tennis wangapi wako kama Roger Federer??? Unadhani amekuwa champion akiwa amekaa na "TECNO" na "POWER BANK" chumbani ana comment kuhusu migomo au mafumanizi ya wanandoa??? No. Alikuwa anapambana, alikua ana hustle wakati wengine wako bussy wanachat.
Diamond unayemfollow anafanya kazi hivyo. Anatoka studio saa saba usiku, wewe uko kwenye page yake una "LIKE". Huwezi kuona kuwa uko tofauti??? Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu, wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo tu, na kutuma picha za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndo NIPASHE sasa hivi???
Kuwa serious na maisha yako, angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako. "Aise huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana". Au unadhani watazikuta hizo "COMMENTS" na "LIKES" zako??? No. Wanapaswa wakute Nyumba, Viwanja, Account za benki zinazopumua (sio Account zipo ICU au MORTUARY). Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu!!!! Wanatakiwa wakute assets za maana angalau. Siyo rundo la "CD" za bongo movie ambazo hazikusaidii wewe wala wao.
Siku zilizobaki kumaliza mwaka huu umeweka mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40???
Au bado unategemea mshahara wa laki 8 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako???
Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele???
Kua mwangalifu rafiki yangu, maisha yanakwenda mbele na kamwe hayaarudi nyuma.
"Kuzaliwa MASIKINI si kosa, ila kufa MASIKINI ni dhambi"
#UKUMBUSHO