Miaka 20-40: Ramani ya Uzeeni au?

Miaka 20-40: Ramani ya Uzeeni au?

Dr Arshavin

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
26
Reaction score
75
Kama Umri Wako Unasoma Miaka 20 – 40, Uko Kwenye Daraja Hatari Zaidi.

Hapa Ndipo Unapochora Ramani Ya Uzeeni Kwako, Au Unapochimba Kaburi La Majuto Yako.

Kabla 50 Haijakugonga Ukaanza Kuilaumu Dunia; Shika Hizi Kanuni. Na Zikukae Kichwani Mpaka Unazeeka↓

Kwanza kabisa, jifunze kuamsha mwili wako.

Sikuambii uende ukawe na sixpack za kuonyesha Instagram au ushinde gym ukibeba vyuma vizito utafikiri unagombea ubingwa. Hapana. Nataka tu ufanye mwili wako uwe na mazoea ya kusonga. Tembea, kimbia, toa jasho. Unaposogeza mwili wako mfululizo, akili inafunguka. Unaanza kulala vizuri, na stress hazikubutui ovyo. Huna haja ya kadi ya Gym, anza tu hapo hapo ulipo. Na ukisimama, anza tena.

Pili, acha mdomo wako uwe na breki.

Mwanangu, sio kila unachoweza kusema lazima ukiseme. Kuna nguvu kubwa sana kwenye ukimya. Sio kila ukweli unapaswa kutapikwa muda huo huo, na kuwa mkweli haimaanishi uropoke kila kinachopita kichwani mwako. Jifunze kufunga mdomo wako.

Tatu, acha kujibebesha matatizo ya dunia.

Sio kila jambo likiharibika ni kosa lako. Ukiwa na tabia ya kufikiria kila kitu kinakuhusu, unajigeuza kuwa adui kwenye stori ambazo hata hausiki. Mambo mengine yanatokea kwa sababu watu wanapigana vita vyao wenyewe huko ndani. Jifunze kujiuliza kwa ujasiri: "Hili jambo linanihusu kweli, au najipa tu presha kwa sababu naogopa kukaa na kutokujua nini kinaendelea?"

Nne, kuwa bosi wa hisia zako.

Hisia zako hazipaswi kukuendesha kama gari bovu lisilo na usukani. Hizo ni waalimu wako. Wivu unakuonyesha kile unachotamani kwenye maisha; hasira inakuonyesha pale watu wanapovuka mipaka yako; huzuni inakukumbusha kile ulichokithamini; na presha (anxiety) inakuonyesha kile unachoogopa kupoteza. Zipe majina hisia zako. Zisikilize, ishi nazo, lakini usikubali zikuteke.

Tano, ukiumia, kubali kuumia.

Acha hii tabia ya kukimbia maumivu kwa kujifanya uko busy na mishe. Kukaa chini ukiwa na majonzi, kukataliwa, au ukiwa na hofu ni moja ya vitu vigumu sana kufanya lakini ni cha lazima! Jipe ruhusa ya kuvunjika moyo, lia bila sababu, na uwe na huzuni bila kukimbilia kutafuta suluhisho la haraka. Huwezi kuponya kidonda ambacho unakataa kukubali kwamba kipo. Jifunze kuhisi hisia zako.

Sita, kuwa na amani na upweke wako.

Acha kutibu maumivu ya mahusiano yaliyovunjika kwa kurukia mahusiano mapya. Acha kudandia situationships eti tu kwa sababu unaogopa ukimya wa chumba chako. Kaa na wewe mwenyewe. Mjue huyo mtu aliye ndani yako nje ya matarajio ya watu wengine. Tafuta kujua ni nini kinakufurahisha ukiwa peke yako. Huwezi kujenga mahusiano yenye afya na mtu yeyote, kama wewe mwenyewe huwezi kuvumilia kukaa na wewe.

Saba, itumie HAPANA kama silaha.

Vijana wengi wanasema Ndiyo kwenye mambo yanayowaumiza eti kwa sababu wanaogopa watu watawaonaje. Unajikandamiza ili tu kuwafurahisha wengine, ukisahau kwamba binadamu haridhiki kamwe, hata umpe roho yako. Mwambie HAPANA mshikaji anayekutaka mtoke wakati huna mood. Mwambie HAPANA yule ndugu aliyefanya mshahara wako kuwa bajeti yake ya kila siku. Jifunze kukataa.

Nane, amini maamuzi yako.

Wewe ndiye staa wa sinema ya maisha yako, sasa anza kuishi hivyo! Haiingii akilini uwe unakimbilia kwa watu kuomba ushauri hata kwa maamuzi madogo ya maisha yako. Fanya maamuzi, subiri matokeo, na ujifunze kutokana nayo. Sio lazima uwe sahihi kila mara. Unaanza kujiamini pale unapojifunza kujifanyia maamuzi mwenyewe.

Tisa, jenga nidhamu ya mwili wako na ngono.

Sikiliza kwa makini hapa. Ngono ni moja ya nguvu kubwa sana ndani yako. Lakini mwili wako sio biashara, na sio kitu cha kugawa gawa eti tu kwa sababu muda ulihusu, au kwa sababu ulisikia upweke, au ulitaka kumfurahisha mtu. Acha kutumia ngono kufunika mashimo kwenye nafsi yako ambayo ngono haiwezi kuyafukia. Kuwa na tamaa ni ubinadamu; lakini hekima ni kujua unazitumiaje hizo tamaa. Mwili wako una thamani.

Na mwisho kabisa, jipende jinsi ulivyo.

Zawadi kubwa kuliko zote unayoweza kujipa ni upendo wako mwenyewe. Kujipenda sio tu kwenda spa kufanyiwa masaji au kupiga picha ukinywa kahawa ya bei mbaya. Hapana. Kujipenda ni kujisamehe pale unapoteleza na kushindwa kuwa yule mtu uliyetaka kuwa. Ni kujipa pole unapojikatisha tamaa. Kadiri unavyojipa muda wa kujijua, ndivyo inavyokuwa rahisi kujikubali. Kumbuka, wewe ndiye mtu pekee ambaye utaishi naye mpaka siku yako ya mwisho. Hakikisha hiyo kampani ni nzuri na inafaa kuishi nayo.

Shika haya maneno, nenda kayaishi.
 
Huwa napenda sana mtu anayesisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi,hilo pamoja na mengine yote yamekaa sawa ni sisi wasomaji sasa kuona namna tutakavyoyatekeleza.
Kula vizuri shiba ota kitambi ukifa uwasumbue watakao kubeba kwa uzito wako watese hadi makaburini jamaa vipi!!?😂😂😂😂😂😂😂
 
Asante sana Dr Arshavin kwa ujumbe huu mzito na wenye hekima kubwa! Umeeleza ukweli mtupu kabisa kuhusu umri huu wa miaka 20-40, ni kweli ni kipindi muhimu sana cha kujenga au kubomoa.

Kila moja ya kanuni ulizotoa ni muhimu sana, lakini ile ya 'acha mdomo wako uwe na breki' na 'kuwa bosi wa hisia zako' zimenigusa sana. Ni kweli, kujizuia kusema kila kitu na kujifunza kuzielewa hisia zetu badala ya kuziruhusu zitutawale ni nguzo muhimu sana za amani na mafanikio. Ni changamoto kubwa lakini ni muhimu kujifunza.

Asante kwa kutukumbusha misingi hii muhimu ambayo mara nyingi tunaisahau katika harakati za maisha. Hizi ni kama ramani halisi ya maisha bora. Tujitahidi kuzifuata!
 
Kama Umri Wako Unasoma Miaka 20 – 40, Uko Kwenye Daraja Hatari Zaidi.

Hapa Ndipo Unapochora Ramani Ya Uzeeni Kwako, Au Unapochimba Kaburi La Majuto Yako.

Kabla 50 Haijakugonga Ukaanza Kuilaumu Dunia; Shika Hizi Kanuni. Na Zikukae Kichwani Mpaka Unazeeka↓

Kwanza kabisa, jifunze kuamsha mwili wako.

Sikuambii uende ukawe na sixpack za kuonyesha Instagram au ushinde gym ukibeba vyuma vizito utafikiri unagombea ubingwa. Hapana. Nataka tu ufanye mwili wako uwe na mazoea ya kusonga. Tembea, kimbia, toa jasho. Unaposogeza mwili wako mfululizo, akili inafunguka. Unaanza kulala vizuri, na stress hazikubutui ovyo. Huna haja ya kadi ya Gym, anza tu hapo hapo ulipo. Na ukisimama, anza tena.

Pili, acha mdomo wako uwe na breki.

Mwanangu, sio kila unachoweza kusema lazima ukiseme. Kuna nguvu kubwa sana kwenye ukimya. Sio kila ukweli unapaswa kutapikwa muda huo huo, na kuwa mkweli haimaanishi uropoke kila kinachopita kichwani mwako. Jifunze kufunga mdomo wako.

Tatu, acha kujibebesha matatizo ya dunia.

Sio kila jambo likiharibika ni kosa lako. Ukiwa na tabia ya kufikiria kila kitu kinakuhusu, unajigeuza kuwa adui kwenye stori ambazo hata hausiki. Mambo mengine yanatokea kwa sababu watu wanapigana vita vyao wenyewe huko ndani. Jifunze kujiuliza kwa ujasiri: "Hili jambo linanihusu kweli, au najipa tu presha kwa sababu naogopa kukaa na kutokujua nini kinaendelea?"

Nne, kuwa bosi wa hisia zako.

Hisia zako hazipaswi kukuendesha kama gari bovu lisilo na usukani. Hizo ni waalimu wako. Wivu unakuonyesha kile unachotamani kwenye maisha; hasira inakuonyesha pale watu wanapovuka mipaka yako; huzuni inakukumbusha kile ulichokithamini; na presha (anxiety) inakuonyesha kile unachoogopa kupoteza. Zipe majina hisia zako. Zisikilize, ishi nazo, lakini usikubali zikuteke.

Tano, ukiumia, kubali kuumia.

Acha hii tabia ya kukimbia maumivu kwa kujifanya uko busy na mishe. Kukaa chini ukiwa na majonzi, kukataliwa, au ukiwa na hofu ni moja ya vitu vigumu sana kufanya lakini ni cha lazima! Jipe ruhusa ya kuvunjika moyo, lia bila sababu, na uwe na huzuni bila kukimbilia kutafuta suluhisho la haraka. Huwezi kuponya kidonda ambacho unakataa kukubali kwamba kipo. Jifunze kuhisi hisia zako.

Sita, kuwa na amani na upweke wako.

Acha kutibu maumivu ya mahusiano yaliyovunjika kwa kurukia mahusiano mapya. Acha kudandia situationships eti tu kwa sababu unaogopa ukimya wa chumba chako. Kaa na wewe mwenyewe. Mjue huyo mtu aliye ndani yako nje ya matarajio ya watu wengine. Tafuta kujua ni nini kinakufurahisha ukiwa peke yako. Huwezi kujenga mahusiano yenye afya na mtu yeyote, kama wewe mwenyewe huwezi kuvumilia kukaa na wewe.

Saba, itumie HAPANA kama silaha.

Vijana wengi wanasema Ndiyo kwenye mambo yanayowaumiza eti kwa sababu wanaogopa watu watawaonaje. Unajikandamiza ili tu kuwafurahisha wengine, ukisahau kwamba binadamu haridhiki kamwe, hata umpe roho yako. Mwambie HAPANA mshikaji anayekutaka mtoke wakati huna mood. Mwambie HAPANA yule ndugu aliyefanya mshahara wako kuwa bajeti yake ya kila siku. Jifunze kukataa.

Nane, amini maamuzi yako.

Wewe ndiye staa wa sinema ya maisha yako, sasa anza kuishi hivyo! Haiingii akilini uwe unakimbilia kwa watu kuomba ushauri hata kwa maamuzi madogo ya maisha yako. Fanya maamuzi, subiri matokeo, na ujifunze kutokana nayo. Sio lazima uwe sahihi kila mara. Unaanza kujiamini pale unapojifunza kujifanyia maamuzi mwenyewe.

Tisa, jenga nidhamu ya mwili wako na ngono.

Sikiliza kwa makini hapa. Ngono ni moja ya nguvu kubwa sana ndani yako. Lakini mwili wako sio biashara, na sio kitu cha kugawa gawa eti tu kwa sababu muda ulihusu, au kwa sababu ulisikia upweke, au ulitaka kumfurahisha mtu. Acha kutumia ngono kufunika mashimo kwenye nafsi yako ambayo ngono haiwezi kuyafukia. Kuwa na tamaa ni ubinadamu; lakini hekima ni kujua unazitumiaje hizo tamaa. Mwili wako una thamani.

Na mwisho kabisa, jipende jinsi ulivyo.

Zawadi kubwa kuliko zote unayoweza kujipa ni upendo wako mwenyewe. Kujipenda sio tu kwenda spa kufanyiwa masaji au kupiga picha ukinywa kahawa ya bei mbaya. Hapana. Kujipenda ni kujisamehe pale unapoteleza na kushindwa kuwa yule mtu uliyetaka kuwa. Ni kujipa pole unapojikatisha tamaa. Kadiri unavyojipa muda wa kujijua, ndivyo inavyokuwa rahisi kujikubali. Kumbuka, wewe ndiye mtu pekee ambaye utaishi naye mpaka siku yako ya mwisho. Hakikisha hiyo kampani ni nzuri na inafaa kuishi nayo.

Shika haya maneno, nenda kayaishi.

Mkuu uzi wako ni kama synchronicity ya kile nimekuwa nikiwaza my whole life.
Asante Kwa bandiko zuri hasa kwa genz sisi Mababu Wacha tujikumbushe tuu maana hakuna mkamilifuu
 
Ila pia tusi negagate kuwa umri fulani ndo kipimo cha mafanikio.
KFC alitoboa at 62, Mc Donald's 50, Nelson Mandela 76, Harriet Tubman 70.

So umri nao is just a number. Sijasema mtoa mada asizingatiwe, in fact katoa mpk mwongozo wa namna ya kukua ili kujitambua na kufikia malengo.
 
Tufuate kanuni,taratibu na miongozo.Hilo halina ubishi kiviilee.Lakini, nyakati zingine maisha ni kama mtego tu.Unaweza kufyatuka muda wowote aidha ukakutega au ukakutegea/ukatega windo/tarajio lako.
 
Back
Top Bottom