Wema wanakufa. Wabaya wanakufa. Sasa niwe mwema ama m-baya ndani ya jamii?? Wema una faida gani??

Wema wanakufa. Wabaya wanakufa. Sasa niwe mwema ama m-baya ndani ya jamii?? Wema una faida gani??

Diego Santana

Senior Member
Joined
May 10, 2025
Posts
147
Reaction score
202
Wakuu, Kuna jamaa yangu anaitwa Michael amefariki jana na habari nimezipata leo kupitia accounts za washkaji zangu za Facebook pamoja na Instagram.

Sasa ninajiuliza, kuna faida gani ya kuwa mtu mwema kwa maana wema wanakufa na wabaya pia wanakufa.

At least labda ingekuwa wema wanaishi muda mrefu hapa duniani, lakini wanakufa tu kama wakufavyo watu waovu.

Kuna faida gani ya kuwa mtu mwema??
 
Watendee watu kadri uwezavyo
Ubaya utaomtendea mwenzako utakurudia wewe siku si nyingi
 
Kutenda wema sio kwa sababu ya kufa ama kuto kufa , ni sehemu ya ustaarabu wa binadamu na utimamu wa akili yake tu.
 
Wakuu, Kuna jamaa yangu anaitwa Michael amefariki jana na habari nimezipata leo kupitia accounts za washkaji zangu za Facebook pamoja na Instagram.

Sasa ninajiuliza, kuna faida gani ya kuwa mtu mwema kwa maana wema wanakufa na wabaya pia wanakufa.

At least labda ingekuwa wema wanaishi muda mrefu hapa duniani, lakini wanakufa tu kama wakufavyo watu waovu.

Kuna faida gani ya kuwa mtu mwema??
Pole kwa msiba wa rafiki yako.

Kuhusu swali lako. Mtu akikufanyia ubaya utafurahi?

Fikiria kwamba upo katika mfumo. Na katika mfumo huo unaweza kuongeza ubaya, wengine wakaona ubaya huo, ukawaambukiza kutenda ubaya, na wao wakafanya ubaya, ikawa dunia ya ubaya ubaya tu.

Au, upo katika mfumo, unaweza kuongeza wema, wengine wakaona wema huowema huo, ukawaambukiza kutenda wema, na wao wakafanya wema, ikawa dunia ya wema wema tu.

Hapo utaamua kufanya ubaya ama wema?

Nitakupa story ilimtokea rafiki yangu mmoja Toronto. Jamaa alikuwa hana tabia ya kutoa pesa kwa ombaomba. Ila siku moja alijisikia tu kutoa pesa, pesa ndogo tu. Sasa, katika purukushani za mjini, mara baada ya kutoa oesa tu ile wallet yake ikadondoka. Sasa kumbe kulikuwa kuna mtu alikuqa kaona kika kitu kuanzia jamaa anatoa pesa kwa ombaomba mpaka wallwt inaanguka. Akaiokota ile wallet, akaanza kumfuatikia rafiki yangu amoe ike wallet. Rafiki yangu alikuwa anatembea haraka huyo jamaa aliyemfuatikia hakuweza kumpata kirahisi. Lakini hatimaye alimpata, akamrudishia ile wallet. Akasema "A guy who gives to the poor should never have to lose his money".

Yule bwana aliyerudisha wallet aliguswa sana nankitendo cha rafiki yangu kumpa ombaomba pesa akasema mtu anayetoa pesa kwa ombaomba hatakiwi kupoteza pesa zake. Akamrudishia wallet.
 
Mti uliodanganyika kwamba mizizi yake inaelea tu hewani, kamwe katu hauwezi kujua umuhimu, faida na raha za msingi wake ardhini.
 
Kuna mtu mwema kuna faida gani ilhali siku moja atakufa tu kama ambavyo wabaya watakufa??
 
Faida ya kuwa mwema.

Inapunguza idadi ya watu wanaoweza kulawiti watoto wetu.
 
Wakuu, Kuna jamaa yangu anaitwa Michael amefariki jana na habari nimezipata leo kupitia accounts za washkaji zangu za Facebook pamoja na Instagram.

Sasa ninajiuliza, kuna faida gani ya kuwa mtu mwema kwa maana wema wanakufa na wabaya pia wanakufa.

At least labda ingekuwa wema wanaishi muda mrefu hapa duniani, lakini wanakufa tu kama wakufavyo watu waovu.

Kuna faida gani ya kuwa mtu mwema??
Wee mtegemee tu kipenzi chetu cha dhati mwamba mkombozi wa waislamu Imam Hussain ibn Ali AS aliyeuwawa kikatili kuutetea kuulinda na kuupigania uislamu dhidi ya dhulma ukandamizaji unyanyasaji na uonevu.

The road to Karbala, join the movement NOW!

Screenshot_2025-07-30-19-19-40-01_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg
 
Ukifa na ubaya kesho uko unaenda kufa tena na tena ila wema unauwezekano ukakuweka pazuri baada ya leo.
 
Back
Top Bottom