Wema Sepetu apandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Mwanadada Wema Sepetu, leo amepandishwa Mahakama ya Kisutu kujibu kesi inayomkabili, ya matumizi ya mihadarati aina ya bangi.

Wema ameambatana na meneja wake, Martin Kadinda, mama yake mzazi, na wapambe kadhaa bila kusahau wale wadada wake wa kazi wawili aliokamatwa nao, tazama video
YouTube
 
Screen-Shot-2017-02-22-at-3.21.05-PM.png

Leo ilikua ni siku ya Mwigizaji Wema Sepetu kurudi Mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Kesi hiyo imeahirishwa leo baada ya upande wa Mashtaka kusema upelelezi kutokamilika hivyo kesi hiyo imepangwa tarehe 15 March 2017.
 
Back
Top Bottom