Nilishawahi kuomba kazi ya kuwa bodygurd ili nitimize ndoto yangu ya ku-date na Wema Sepetu

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
Lengo la kuandika uzi huu, naamini kabisa wanajamii forum mlio karibu na the Tanzania sweaty heart (Wema Sepetu) mumfikishie ujumbe huu baada ya juhudi zangu binafsi kugonga mwamba na kuona kabisa ndoto yangu ya kutuliza moyo/kudate na Wema inazimika Kama mshumaa uliowashwa katika wimbi la upepo mkubwa.

Ipo hivi, NALIA NGWENA nilianza kuvutiwa sana na huyu mwanadada kwa muda mrefu/toka kitambo lakini nafasi ya kua karibu nae ndiyo ilikua shughuli kubwa maana Mimi siyo msanii eitha bongo muvi, au bongo fleva sipo kabisa katika hizo talanta za kumfanya mtu awe maarufu.

Mwamba niliamini one day yes niliamini kabisa kuwa ipo siku Wema Sepetu atajaa kwenye mikono yangu na atakuwa mpenz wangu wa milele.

Baada ya kupata mafunzo ya maridhawa kabisa, niliona hakuna mtu wakunibabaisha na ndipo niliona nitumie hii nafasi ya kuanza kufatilia machimbo anayopatikana Wema Sepetu.

Nilianzia jimu moja maarufu ipo hapo Sinza alikua anapenda sana kwenda na Mimi militia miguu pale nililipia mwezi mmoja ili niwe nazuga na kupanga mikakati namna gani naweza pata angalau wasaa wa kuzungumza na mtoto mzuri.

Mwamba nikiwa pale gym nikajitengenezea ka umaarufu fulani baada ya kuwaambia vijana kuwa nitawafundisha karatee hapo ndipo nikawa napata info Wema muda wake wa kuja gym.

Kumbuka hapo mjuba nilishamtafuta sana instagram na kueleza hisia zangu meseji za hapa na pale lakini jibu lake lilikua ni Ok, na emoji za kucheka tu, kutokana na majibu hayo mwamba nilikua njia panda na mwisho wa siku nilikuja kukundua kafunga DM yake nafikiri hiyo ilikuja Baada ya kipindi fulani alikua anastres analia Lia kwenye mitandao na kusababisha kufunga Dm yake.

Sasa basi nikiwa pale gym nilikua napishana nae sana kila nikifika naambiwa katoka Sasa hivi, Mimi nikitoka kesho yake naambiwa alikuja bana, na Mimi sikutaka kuwaambiwa wajuba hisia zangu maana najua wangenicheka tu na kunivunja moyo.

Nakumbuka ilikua ni siku ya jumapili moja mwamba nikiwa mitaa ya pale gym ndipo nilipomuona mtoto huyu hapa, NALIA NGWENA kwa kujiamini kabisa Tena nikiwa na confidence ya hali ya juu nilimfuata walau nipate hata maneno mawili, alikua yupo na bodyguard wawili wameshiba ugali.

Niliita "madam" aligeuka akawa Kama anamshangao kuona MTU asiyenijua na akitazama sura yangu ni ngeni kabisa, wale bodyguards walitaka kunizuia lakini madam alisema muacheni.

Sauti yake nyororo NALIA NGWENA ilinifanya nikameza fundo la mate katika Koo langu huu mjulubengi/msonobali wangu uliona Kama unakata kiu ya muda mrefu ulianza kuvimba mdogo mdogo.

Mwamba nilisema "excuse me madam" naitwa NALIA NGWENA, natokea sehemu Fulani Nina mafunzo haya na haya.

Lakini natafuta kazi ya kuwa personal bodyguard wako Kama itakupendeza lakini samajani kwa usumbufu."

"Oh sorry huwa natumia bodyguard wa kampuni kam Hawa unaowaona hapa'

Nilipojibiwa hivyo niliishiwa pozi nakujibu tu "thank you madam"

Nilitaka walau niombe hata namba za simu lakini niliona ghafla sana basi Yule mtoto aliendelea na shughuli zake na kutokana na majukum yangu pia sikukutana nae Tena na niliona kabisa ndoto yangu inagonga mwamba.

Mpaka naandika Uzi huu bado sijakata tamaa ya kumpata Wema Sepetu, hao anaodate nao naimani kabisa NALIA NGWENA zamu yangu na Mimi utafika tu.

Mwenye namba ya Wema Sepetu nitafurahi sana akinipa huko PM na aliye karibu na Wema Sepetu amfikishie ujumbe wangu na amwambie namna gani NALIA NGWENA ninavyompenda mno Tena mno nasema maneno haya kwa moyo mkunjufu Tena yanatoka kwenye uvungu wa moyo wangu wa ndani kabisa.

Screenshot_20230508-123445.jpg
 
Kipendacho roho, mpaka umeanzisha Uzi umempenda kweli, angekuwa anaimba simple kumpata, ungetunga mistari ya uongo na kweli, ungeenda studio anayerekodia, Sasa bongo muvi kazi kweli.
 
Kapime Akili buroo,pili acha kuvuta bangi bila kula,mara paap umekua bodigadi wake,vp ungembaka?maana Kwa ulivyojielezea uko na pumbu zako tu na v*zi,mtoto anataka Hela,au akupende mwenyewe.
Hata ukiwa na hela kumpata mtu ni ngumu mpaka utengeneze connection
Hiyo ilikua ni tiketi tu ya kuwa nae karibu mbwa wewe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kipendacho roho, mpaka umeanzisha Uzi umempenda kweli, angekuwa anaimba simple kumpata, ungetunga mistari ya uongo na kweli, ungeenda studio anayerekodia, Sasa bongo muvi kazi kweli.
Ningejua hata mistari miwili ningezama studio ningemsifu sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom