Gramu 8.42 za Bangi zamponza, apandishwa kizimbani Kisutu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,538
8,549
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani Salum Hamad (65) kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 8.42.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Judith Kyamba alidai kuwa Julai 30, 2023 maeneo ya Mbagala Rangi Tatu mshtakiwa alikutwa na dawa ya kulevya yenye Uzito wa gramu 8.42 kinyume na sheria.

"Maeneo ya Mbagala Rangi Tatu mshtakiwa alikutwa akimiliki dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 8.42 na upelelezi wake umekamilika tunaomba mahakama tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali," amedai Kyamba.

Hakimu Msumi alisema dhamana ipo wazi hivyo mshatakiwa anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh200,000.

Hata hivyo mshatakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa mashatri ya dhamana na shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 14, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
 
Serikali za madhalimu,waonezi,wakandamizaji,wababe,wanyonyaji inatutesa kila siku....

Bangi sio madawa ya kulevya jamani muelewe
 
Back
Top Bottom