Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,878
- 1,849
Habari, wapendwa. Uandishi wa riwaya na simulizi ni kazi ngumu na nyepesi kwa wakati mmoja! Ngumu kama mwandishi anatazamwaa na rundo la karatasi nyeupe huku akiwa na kalamu bila uhakika anaanzia wapi. Uandishi pia ni mwepesi kama mwandishi ana 'sense' ya angalau pointi A, B na C kabla hajaifikia Z. Ingawa hii sio kanuni kubwa sana. Wapo waandishi wakianza kuandika ndiyo wameenda hivyo. Na kwa bahati nzuri nimebarikiwa hicho kitu. Hata hivyo, fasihi ili iwe na ladha inahitaji uhalisia kidogo. Ndiyo maana mwandishi anatakiwa kusoma kila neno analoliona mbele yake. Na uhalisia unatokana na watu walio wa kweli na hai.
Basi ombi langu kwenu kama kuna mtu ana kisa, wazo au chochote ambacho angetamani ama kiwe riwaya au hadithi fupi anaweza kushea hapa kwenye replies. Mimi na waandishi wengine, ambao watapenda, tutajitahidi kuzifanyia kazi na kuzishea hapa. Itakuwa kama kichalenji kidogo. Sio kwaajili ya kushindana, ila kama mazoezi na kubadilishana hili na lile. Karibuni!