Weka wazo au kisa ambacho ungependa kiandikwe kama Riwaya au hadithi fupi?

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Habari, wapendwa. Uandishi wa riwaya na simulizi ni kazi ngumu na nyepesi kwa wakati mmoja! Ngumu kama mwandishi anatazamwaa na rundo la karatasi nyeupe huku akiwa na kalamu bila uhakika anaanzia wapi. Uandishi pia ni mwepesi kama mwandishi ana 'sense' ya angalau pointi A, B na C kabla hajaifikia Z. Ingawa hii sio kanuni kubwa sana. Wapo waandishi wakianza kuandika ndiyo wameenda hivyo. Na kwa bahati nzuri nimebarikiwa hicho kitu. Hata hivyo, fasihi ili iwe na ladha inahitaji uhalisia kidogo. Ndiyo maana mwandishi anatakiwa kusoma kila neno analoliona mbele yake. Na uhalisia unatokana na watu walio wa kweli na hai.

Basi ombi langu kwenu kama kuna mtu ana kisa, wazo au chochote ambacho angetamani ama kiwe riwaya au hadithi fupi anaweza kushea hapa kwenye replies. Mimi na waandishi wengine, ambao watapenda, tutajitahidi kuzifanyia kazi na kuzishea hapa. Itakuwa kama kichalenji kidogo. Sio kwaajili ya kushindana, ila kama mazoezi na kubadilishana hili na lile. Karibuni!
 
DARK WEBSITE

Njia yangu ya kuandika huwa ni ya ajabu kwangu.

Kila riwaya ambayo nimeandika ilikuwa ni ndoto ambayo niliona. Na kwa kawaida kila nikilala nikajikuta nimepata ndoto yenye kusisimua ninaamka na kuanza kuandika.

Mnamo mwaka 2009 nilianza kujifunza karate na kungfu .Lakini lengo langu halikuwa kutafuta nguvu wala ujuzi.

Nilijifunza kwa ajiri ya kujiandaa na kujiunga na jeshi ama usalama wa taifa.Mawazo hayo ya kutamani kuwa mwana usalama yalianza kuingia akilini kidogo kidogo kutokana na mzee wangu kuwa ananiletea vitabu vya riwaya za kijasusi za Ben Mtobwa.

Mwingine aendelee hapa.
 
Mnamo mwaka 2009 nilianza kujifunza karate na kungfu. Lakini lengo langu halikuwa kutafuta nguvu wala ujuzi.

Nilijifunza kwa ajili ya kujiandaa na kujiunga na jeshi ama usalama wa taifa. Mawazo hayo ya kutamani kuwa mwana usalama yalianza kuingia akilini kidogo kidogo kutokana na mzee wangu kuwa ananiletea vitabu vya riwaya za kijasusi za Ben Mtobwa.

Cont: Kusema kweli sikuwa nimeelewa maana ya baba kuniletea vile vitabu. Kuna muda nilijiuliza sana. Sikupata majibu. Nilikuja kugundua miaka saba baadae. Kumbe baba alikuwa ni shushushu na juhudi zake zote za kunifanya niuelewe uwanja wa majasusi, lengo ilikuwa ni siku moja nifanye kitu anachokifanya kwa mapenzi ya taifa na serikali yangu. Nasikitika nilipoingia dhani yangekuwa. Taarifa kuwa chombo cha usalama wa taifa kinatakiwa kutetea maslahi ya taifa ni kinyume chake. Kuna watu wanakitumia hiki chombo kwa maslahi yao na wapo kwenye mpango hatari wa kufanya jambo ambalo litaigharimu nchi yangu. Kwaajili ya baba, na tanzania itabidi nifanye jambo kuwazuia hata kama itatakiwa nife kwanza. Sitakuwa kama mashushu wengine ambao walipoona vitendo vibaya walivifumbia macho na kukimbilia nje na kugeuka kuwa wanaharakati wa mitandaoni. Mimi nitapigana mwanzo mwisho. Nimekwishamwaga damu, sitaogopa kumwaga jasho.... Nikimaliza misheni yangu nitakuja kueleza kila kitu.
 
Nickson Chabela
ANASIMLIA YALIYO MKUTA
Sikuwa nakumbuka tarehe wala siku nilizo kuwa nimeanza kuulizwa swali nisilo lifahamu.Ninacho kikumbuka hadi wakati huu ni ujumbe ambao nilitumiwa na mtu nisiye mfahamu kabisa.Maneno yake ya kejeli yangali yananitesa na kunifanya nilie hadi muda huu.

Kama utani nilianza kuvuliwa nguo zangu ambazo hazipaswi tena kuitwa nguo maana zilikwisha chakaa na kubaki matambala na rangi yake haikutambulika tena.Maana damu na jasho la mateso yalikwisha ibadilisha rangi yake ya asili.Mwili wangu hakika ulikuwa umebaki mifupa mitupu,hakuna tena cha kujivunia tena.Maana nilikwisha fanana na sanamu la kufukuza ndenge wala nafaka.

"Unajua tunakupenda sana ndiyo maana tubaendelea kukuacha hai hadi utupatie kitu hicho ambacho unakilinda bila kujua madhara yake.Kama ungelipewa nafasi kama tunayo kupa hii ya kukumbusha ungelipaswa kushukuru mno.Lakini kwa kuwa unajifanya kiburi acha tukupatie ukalimu wetu wa kila siku."

Nilivuliwa matambala yangu na kuingizwa katika chumba kingine ambacho tangia niingie kwenye mikono ya watu hawa sikuwahi kuingizwa kamwe.Sikuwa naogopa kifo tena kama hapo mwanzo kufikia sasa nilianza kutamani kufa maana mateso niliyo kuwa nimepatiwa yalikuwa ni ya kiwango cha juu sana. Kama ningeliyafananisha na elimu yetu nilikuwa tayari nimepata PHD kufikia sasa.

Mwili ulikuwa umejaa alama ya mishono na alama za mijeredi ya kiboko.Sikutazamika kwa sura nzuri tena maana nilikuwa nimekwisha badilika hadi rangi yangu ya ngozi na kuwa na rangi isiyo eleweka kabisa.

Katika chumba hiki hakukuwa na mambo mapya sana kwangu zaidi ya kuona pipa la plastiki litumikalo kubebea mafuta ya taa.Lakini hili niliona linao mchoro wa hatari.Nilipo endelea kuchunguza chumba hicho macho yangu yalitua kwenye vyuma vitumikavyo kubebea nyama kwenye mabucha.

Kulikuwepo pia meza iliyo kuwa na mapanga,visu vidogo visogo vitumikavyo kwenye oparesheni za upasuaji katika mahospitali,mikasi nyaya na madawa.

Chumba hicho kilikuwa na harufu ya kifo haswa ingawa sikufahamu harufu hiyo ndiyo kifo chenyewe ama woga wangu.Ndiyo nilikitamani kifo lakini siyo kifo kilicho kuwa mbele yangu maana kingelikuwa nimekufa kifo cha kijinga sana.Kufa na tai shingoni kama mwingereza,sikuwa nimeyazingatia maneno ya mtesaji huyu hadi pale nilipo shuhudia kwa macho yangu yanayo kuja kujili.

Zoezi la kuvuliwa nguo lilinikumbusha kitu muhimu ambacho nilipaswa sasa kukitumia kabla ya kufa kikondoo.Maana ni kama tukio hili liliwahi kutokea lakini nilifikilia ni ndoto za kawaida ambazo huwa naota kila nilalapo katika nyumba yangu ya mateso.Hivyo niliazimia kufanya jambo kabla ya kuzua hatima yangu ya mwisho.

"Hebu sogea hapa tuendelee na zoezi letu ama tupatie kitu chetu ubaki salama kwa leo."

Aliniamrisha mtesaji huyu ambaye huwa hana masihara mengi wala maswali mengi zaidi ya kinitumia kama kifaa chake cha mazoezi kila ajisikiapo kufanya hivyo.Kwa kawaida ilikwisha mzoea kwa tabia yake ya kuamlisha kisha ananifuata kwa mitindo yake ya pekee ya Karet na judo.Kisha unipatia nafasi chache ya kusikiliza mapigo yake kama yameniingia ama awndelee na mateso ya siku hiyo.

Lakini wakati huu hata nilipo kataa kutii hakunifuata kwa mateke bali alinyamaza kimya kana kwamba amenielewa sitaki kupata mateso ya siku.

Kumbe nilikuwa nimejidanganya sikuwa salama kama nilivyo fikilia hapo mwanzo.Maji yenye presha kali yalianza kunichapa haswaa wala sikuwa na pa kujitetea maana maji yalinipiga kila sehemu bila kujua wapi yalitokea.Maji haya kadili yalivyo nipiga nilihisi ni kama yananitoboa mwili maana maumivu niliyo kuwa nikiyahisi hayasimliki kwa maneno ya kawaida.

Nilojikuta napoteza fahamu na sikujua kilicho endelea zaidi.

JOHN TRUCK**
ANASIMLIA
Ahaaaaa!!! Nilipiga ukunga, wa maumivu makari baada ya kuwekewa pasi ya umeme wa A30. Sikuwa nikitambua kosa langu, wala sikutambua nilikuwa wapi.Walikuja wanajeshi wawili ambao walikuwa wamevalia sale ya jeshi la Uganda, na hilo likanipa jibu kuwa niko Uganda.

Washa tena, aliongea askari huyo huku akiwa ameshikiria pasi. "Utaongea" Aliongea mwanajeshi aliyeenda kuwasha umeme. Asira na nguvu zisizo na msaada vikanipanda na kujikuta nikipoka " Nijibu nini". Yule mwanajeshi aliyeshikilia pasi alinisogerea na kuzaba makofi mawili,
"Paaaaaa"
"PAAAAAAA"

Nilitulia kama mtu aliyekuwa ameondokewa na fahamu. Taa ndogo nyekundu ilikuwa kwenye pasi hiyo iliwaka, kisha yule mwanajeshi akanisogelea na kuitia tena kwenye mwili wangu. Ahaaaaaa! Hiiiiiiiiii! Hiiiiahaaaa!!!.
Akatoa kidogo,
Akarudisha,
Haaaaaaaa,
Akatoa.

Baada ya mateso makari wanajeshi wale walicheka sana. Kisha mmoja alisema: nilikuwa nafanana kama dreva wa pikipiki. Nilifikiri, hivi kama mmoja wao nikamunjesha kidogo si wanaweza kunambia ni nini wanataka? Ila kabla sijafanya lolote aliingia askari ambaye alikuwa na cheo cha chini.

Alisema: John Truck, anahitajika katika chumba namba 99. Nilifunguliwa minyororo ambayo nilikuwa nimefungwa kisha nikanyanyuliwa kutoka kwenye kiti kile. Na safari ikaanza. Tulitoka kwenye chumba kile na kutokea kweye korido ndefu yenye milango mingi sana na hiyo milango ilikuwa na namba.

Safari ilienelea,tulifika kwenye mlango ulioandikwa "no true no life" likimanisha "hakuna ukweli hakuna maisha" nilibaki nikilitiza neno lile huku mlango ukifunguliwa taratibu. Tuliingia ndani huku nikiwa na mawazo kulihusu neno lile.

Tulizidi kusonga mbele na ile korido ilikuwa ndefu sana, pia nayo ikiwa na milango mingi sana iliyo na namba. Yule askari alisimama kwenye mlango ambao haukuwa na namba wala andishi lolote. Aliufungua mlango ule.jambo la ajabu nililoona katika korido ile hakukuwa na milango mingi kama korido tulizopita apo nyuma.

Nilikuwa naenda huku naangaza angaza macho, atimaye ulionekana mlango japo tuliupita. Tulipokuwa tukiupita mlango ule nilintizama ma kuona namba iliyoondikwa kwa wino mwekundu na chini ya namba hiyo kulikuwa na mchoro wa fuvu. Namba hiyo ilikuwa namba 100.
"Ilinishutuwa kidogo"

Tuliendelea kusonga mbele bila kuona mlango mwingine wowote. Akuna aliyemuoji mwenzie huku nikihisi maumivu kidogo kwenye mwili wngu. Atimaye tulifika mwisho wa ile korido. Yule askari aliongea kwa kinhereza "inter" akimanisha ingia. Mi mwenyewe nilisukuma mlango ulikuwa na namba 99. Nikaingia na kukuta kunamo viumbe wanne walio na hali ya kuhurumiwa. Maana mmoja alikuwa amekatwa mkono, huku mwingine akiwa na mdomo chekacheka, pia mwingine akiwa amebakiza vidole viwili, nafikiri vingine vilikatwa. Na wa nneakiwa hana shati na katika tumbo lake kukionrkana mshono ulioshonwa kwa waya wa umeme.

Mimi sikuogopa mateso hayo bali nilitakujua wanataka kujua siri gani kutoka kwangu. "KOO KOO" nilisikia mtu akikohoa sauti iliyotoka nyuma yangu, ingali nilikuwa karibu na mlango. Niligeuza shingo langu taratibu. Hee! Nilishutuka kuona kiumbe kilichovalia vazi jeupe.
Alikuwa Dakitari.

Aliongea kwa kejri "sogea mbele" nilimtaza yule dakitari naye akanitaza.
Nikaona nisikimbize cd, nikaamua kusonga mbele atua kumi kisha nikamgeukia dakitari yule. Akanambia: na hawa wenzako walikuwa na kiburi kama wewe ila mafuta yamepunguzwa.

Sikufuatilia maneno yake bali nilifuatilia kiswahili chake na kutambua kuwa naye alikuwa akizungumza kiswahili cha uganda. Nikazidi kupata majibu zaidi kiwa apa nilipo ni uganda.

Sikuwa na fikira ya kifo maana nimeona walio nitangulia ni wazima na bado kuna dakitari. Ila niliogopa nilipokumbuka chumba 100. Hilo lilinitia kwenye mawazo mazito.

Mawazo yaliisha baada ya kuhisi mtikisiko wa ardhi. Nilijiambia kwa kimyakimya nikitumia lugha ya mtaani ya kitanzania "huu ni mkwala". Nilibaki nikiwa makini sana, mara niliona mlango uliofunguka kutoka chini. Nilijiambia "kuna andaki".

Nilisikia sauti kutika chini yaani ndani ya andaki "come in" mi nilitaka kusita ila ujasiri wangu ulivunjwa baada ya kuona yule aliyekuwa ameshonwa na waya akianza kulia kwa kwikwi.

Yule aliuekuwa amekatwa mkono alinitaza na kuangalia ukutani. Hapohapo niliyaelekeza macho yangu kwenye ule ukuta, nikaona mdomo wa bunduki inayolusha kisu. Nikatambua kuwa naye alikatwa kwa njia hii.
"Hacha nijinyenyekeze ili nione atima yao"
Nilijiambia.

Sote tulitelemka tukishuka nganzi ndefu huku yule aliyeshonwa akitokwa na machozi ya uchungu. Alinifanya niwe na wazo la kuwa huku chini kuna islaeri mtafuna nyama wa kibinadamu.

Tulifika chini. Sikuwa na cha kujitetea, nilianza kuisi harufu ila niliipuuza.
Nilijikuta nikiwa tayari nimefungwa kwenye kiti. Nilifiri "kumbe wanaujinga wa namna hii ati wanatumia..." Nilikatishwa baada ya kuona kiumbe kikubwa waswahili huviita miraba minne.

Nilibaki nikimtazama mtesaji yule. Alikuwa amejaa vya kutosha. Kisha yule dakitari naye alishuka kupitia ngazi ile baada ya kufika chini ngazi zilipanda na mlango wa juu ulijifunga, huku mwanga hafifu ukipenyeza.

Yule dakitari aliongea maneno yaliyozungumzwa na mtesaji wa mwanzo "utasema yote". Sikufikiria maneno yake. Nilisikia "muoneshe".

Kabla yule mtesaji ajaanza kuwatesa wale wanne, aliongea kwa sauti ambayo utadhani amepanga kokoto kwenye koho lake, maana aliongea utadhani ananalazimishwa huku ikikoroma.
Introduction...
"Ukiona ninawatesa hawa, kabla yako utsema"

Atimaye yule aliyekuwa ameshonwa waya, alitiwa waya za umeme, kisha wakawasha,
Haaahaaaaaaaa!!!
Akazima.
Akawasha,
Hiiiiihaaaaaaaaaaa!!!
Akazima.
Akawasha mazima,
Haaaaaaaaa!!!
Hiiiiiiiihaaaaaaaaaaaa!!
Mhmhmhnh!!
Akazima.

Kutokana na nguvu ya umeme zile waya zilikata ngozi kwa mara nyingine. Utumbo mwembamba na mpana ulitoka nje huku ukisindikizwa na tumbo pamoja jirani yake kongosho.
Ardhi ilitikisika kwa mara nyingine tena. Mlangi mwingine ukafunguka kutoka chini. Ndani ya mlingo ule palitokea dada wawili waliovalia sale za manesi. Wakiwa na kitanda kidogo, kisha wakambeba na kumtia kwenye kitanda kile kidogo.

Atimaye walimchukua kule chini huku wakifuatwa na yule dakitari. Mtesaji alisema "utasema. Kisha akanigeukia je, una la kusema?
Sikujibu lolote.
"Eti bado una kiburi"
Sikujibu lolote.

Gafra mlango mmoja kati ya milango iliyokuwa kwenye andaki ile ulifunguka. Akatoka simba dume mwenye njaa. Akalia,
"Krararaaruuuu".
"Nilihisi harufu ya kifo"

MSIMULIAJI
Uliwahi kuhisi harufu ya kifo!!!
Hivyo ndivyo majasusi wawili wasiojuana walivyohisi. Hakuna aliyependa kuishi maisha hayo, japo kila mmojs alijikuta katika maswali,mateso, mawazo yasiyokuwa na mwisho.

John Truck, huyu alikuwa jasusi ambaye alitumiwa katika kumtafuta dakitari ambaye alikuwa ametengeneza kirusi ambacho alitaka kukieneza katika jiji la kampala. Waganda walitambua kabisa kuwa John Truck ni jasusi, na walitambua jinsi ambavyo Jonh Truck anamjua dakitari huyo ambaye amedadisiwa na kutambua kuwa anaishi marekani.

JohnTruck ni ni mzaliwa wa Tanzania, mama yake ni mhindi na amekuwa akijishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Baba yake ni mtanzania mzaliwa wa bukoba kagera kashai na amekuwa akijishughulisha na wizi wa madini na kazi amemfundisha mwanae. Babu yake ni mzaliwa wa bukoba kashai huku bibi yake akiwa mzaliwa wa bukoba vijijini kule kasharu.

Pia, John truck alikuwa mrefu mithiri ya wanyarwanda na alifanikiwa kuibeba sura ya baba yake ambaye alikuwa na rangi ya kiafrika. Anapenda kuvaa suti nyeusi akibadili rangi ya shati na tai bluu na nyekundu. Ana mwili mkubwa ambao ulikuwa umejaa vya kutosha kutokana na mazoezi makari.

Kutokana kuwa baba yake John Truck amekuwa akifanya wizi wa madini, hilo lilimfanya anakuwa na pesa nyingi. Kutokana na kuwa na pesa nyingi sana hilo lilimsukuma kumsomesha mwanae wa kwanza aliyemwita John.

Truck hakumsomesho mwanae ali akapewe kazi selikarini, bali alimsomesha ili kufuta visingizio vya iwapo mwanae ataanza kazi ya ujasusi akikamatwa apate majibu rahisi na haraka. John amesoma vya kutosha japo hana faida na elimu yake maana anaitumia kama pambo la ndani. John hajawai kuwa na rafiki wala mpenzi, maana alipofikisha miaka 18 baba yake alimwelezea mambo kwa undani kuhusu kazi atakayoifanya hapo mbeleni. Kwaiyo Truck alimpa mwanae njia ya kufuta marafiki na wapenzi,
Kuanzisha visa visivyo na maana.

Kampala, Uganda
Huku John Truck akiwa amekaa kwenye kiti, simba yule alizidi kusogea kumwelekea mmoja kati ya wale watatu walobaki. Akailamba pua yake akitumia ulimi uliokuwa mrefu na mwembamba. Anapomaliza anakitisa kichwa chake huku akiupanua mdomo wake ulokuwa na meno manne makubwa na marefu na mazuri yalimaliza chuo kikuu cha ulaji wa nyama.

Simba yule alimsogelea aliyekuwa na vidole viwili. Akautoa ulimi wake na kuanza kuulamba mwili mateka yule. John Truck alikaa macho wacho wazi tena kwa umakini mkumba akitizama jinsi gani simba humtafuna binadamu. Macho yake yalitelemka na ulimi wa simba yule maana hakuwa kuona igizo kama lile.

Simba yule alizidi kuulamba mwili wa yule mateka. Akiwa makini alishtuka alianza kugeuza jicho lake moja kumwelekea mtesaji kama paka aliyekula panya aliyekufa kwa kusu. Akigundua mtesaji hayuko makini na igizo lile, bali yuko maini na hisia za John. Akaanza kulielewa igizo lile lililo chezwa tangu apo awali.

Gafra yule simba alimg'ata mgongo na kuanza kumburuza kuelekea kwenye mlango aliotokea simba yule. Na baada ya kuingia ndani mlango ulifuna wenyewe. John alifurahishwa na igizo hilo maana amefanikiwa kuuelewa mcheza kidogo. Sikutambua john alikuwa akiwaza nini.

Mtesaji akamuuliza John Truck: Jitetee, au bado utasema utakapofikiwa wewe. John Truck alimtama mtesaji yule kisha akamwambia: aka bado, maana bado sijaridhika na igizo ili na lililopita, ebu nipe linalofuata maana napenda nifike huko chini kwa dakitari. Mtesaji alikasirika sana kutaka kuutoa uhai wa John Truck. Sauti ilisikika "iwe sebo".
Alishusha pumzi.

Yule mesaji aliitoa simu yake, ngeli ya simu janja na kuanza kuandika ujumbe fulani, huku John akizidi kuendelea kumtazama mtesaji yule aliyekunja sura yake mithiri ya nguo za mitumba. Kisha aligeuza macho yake kwa yule aliyekatwa mdomo, alijikuta akizidisha tabasamu lake maana jamaa yule hawezi kununa.

Mlango wa juu ulifunguka. John Truck alifurahishwa na mtambo ule uliofunguliwa na vyuma vikubwa vyenye meno. Alijiwazia kichwani mwake"
 
MSIMULIAJI
Uliwahi kuhisi harufu ya kifo!!!
Hivyo ndivyo majasusi wawili wasiojuana walivyohisi. Hakuna aliyependa kuishi maisha hayo, japo kila mmojs alijikuta katika maswali,mateso, mawazo yasiyokuwa na mwisho.

John Truck, huyu alikuwa jasusi ambaye alitumiwa katika kumtafuta dakitari ambaye alikuwa ametengeneza kirusi ambacho alitaka kukieneza katika jiji la kampala. Waganda walitambua kabisa kuwa John Truck ni jasusi, na walitambua jinsi ambavyo Jonh Truck anamjua dakitari huyo ambaye amedadisiwa na kutambua kuwa anaishi marekani.

JohnTruck ni ni mzaliwa wa Tanzania, mama yake ni mhindi na amekuwa akijishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Baba yake ni mtanzania mzaliwa wa bukoba kagera kashai na amekuwa akijishughulisha na wizi wa madini na kazi amemfundisha mwanae. Babu yake ni mzaliwa wa bukoba kashai huku bibi yake akiwa mzaliwa wa bukoba vijijini kule kasharu.

Pia, John truck alikuwa mrefu mithiri ya wanyarwanda na alifanikiwa kuibeba sura ya baba yake ambaye alikuwa na rangi ya kiafrika. Anapenda kuvaa suti nyeusi akibadili rangi ya shati na tai bluu na nyekundu. Ana mwili mkubwa ambao ulikuwa umejaa vya kutosha kutokana na mazoezi makari.

Kutokana kuwa baba yake John Truck amekuwa akifanya wizi wa madini, hilo lilimfanya anakuwa na pesa nyingi. Kutokana na kuwa na pesa nyingi sana hilo lilimsukuma kumsomesha mwanae wa kwanza aliyemwita John.

Truck hakumsomesho mwanae ali akapewe kazi selikarini, bali alimsomesha ili kufuta visingizio vya iwapo mwanae ataanza kazi ya ujasusi akikamatwa apate majibu rahisi na haraka. John amesoma vya kutosha japo hana faida na elimu yake maana anaitumia kama pambo la ndani. John hajawai kuwa na rafiki wala mpenzi, maana alipofikisha miaka 18 baba yake alimwelezea mambo kwa undani kuhusu kazi atakayoifanya hapo mbeleni. Kwaiyo Truck alimpa mwanae njia ya kufuta marafiki na wapenzi,
Kuanzisha visa visivyo na maana.

Kampala, Uganda
Huku John Truck akiwa amekaa kwenye kiti, simba yule alizidi kusogea kumwelekea mmoja kati ya wale watatu walobaki. Akailamba pua yake akitumia ulimi uliokuwa mrefu na mwembamba. Anapomaliza anakitisa kichwa chake huku akiupanua mdomo wake ulokuwa na meno manne makubwa na marefu na mazuri yalimaliza chuo kikuu cha ulaji wa nyama.

Simba yule alimsogelea aliyekuwa na vidole viwili. Akautoa ulimi wake na kuanza kuulamba mwili mateka yule. John Truck alikaa macho wacho wazi tena kwa umakini mkumba akitizama jinsi gani simba humtafuna binadamu. Macho yake yalitelemka na ulimi wa simba yule maana hakuwa kuona igizo kama lile.

Simba yule alizidi kuulamba mwili wa yule mateka. Akiwa makini alishtuka alianza kugeuza jicho lake moja kumwelekea mtesaji kama paka aliyekula panya aliyekufa kwa kusu. Akigundua mtesaji hayuko makini na igizo lile, bali yuko maini na hisia za John. Akaanza kulielewa igizo lile lililo chezwa tangu apo awali.

Gafra yule simba alimg'ata mgongo na kuanza kumburuza kuelekea kwenye mlango aliotokea simba yule. Na baada ya kuingia ndani mlango ulifuna wenyewe. John alifurahishwa na igizo hilo maana amefanikiwa kuuelewa mcheza kidogo. Sikutambua john alikuwa akiwaza nini.

Mtesaji akamuuliza John Truck: Jitetee, au bado utasema utakapofikiwa wewe. John Truck alimtazama mtesaji yule kisha akamwambia: aka bado, maana bado sijaridhika na igizo ili na lililopita, ebu nipe linalofuata maana napenda nifike huko chini kwa dakitari. Mtesaji alikasirika sana kutaka kuutoa uhai wa John Truck. Sauti ilisikika "iwe sebo".
Alishusha pumzi.

Yule mtesaji aliitoa simu yake, ngeli ya simu janja na kuanza kuandika ujumbe fulani, huku John akizidi kuendelea kumtazama mtesaji yule aliyekunja sura yake mithiri ya nguo za mitumba. Kisha aligeuza macho yake kwa yule aliyekatwa mdomo, alijikuta akizidisha tabasamu lake maana jamaa yule hawezi kununa.

Mlango wa juu ulifunguka. John Truck alifurahishwa na mtambo ule uliofunguliwa na vyuma vikubwa vyenye meno. Akiangalia mtambo ule wenye meno kama picha ya programu ya simu ijulikanayo kwa jina la mipangilio (settings). John akajiambia "nimewaweza".

Ule mlango ilipofunguliwa ukatokea ngazi, kupitia zile ngazi akaonekana mwanajeshi akishuka akiwa amevalia sare ya jeshi la Uganda. Alipofika chini akasogelea mtesaji yule alikuwa mweusi sana hii ikizidi kumthibitisha kuwa huko uganda. Yule mwanajeshi akamtazama mtesaji yule pia naye akamtazama wanaongea kwa signo za uso. John aliwatizama tu akitaka kujua wanasema nini. Jambo hilo lilimwondoa uoga.

Walipomaliza kupeana alama hizo, yule mtesaji akaenda kwenye ukuta na katika ukuta huo kulikuwa na bayana zenye michoro ya vitufe. Akaenda na kubonyeza barani yenye kitufe cha mstari. Na hapo kamba zilikuwa zimetoka John Truck zikakimbia na kupotelea ardhini hivi kwamba visingeweza la kulikuwa na kamba kwenye kiti kile.

Yule mwanajeshi akamwambia John Truck: nifuate hewe mateka. John hakujibu jambo lolote,alichofanya aliamka na kuanza safari ya kumfuata mwanajeshi yule alionekana kukomaa zaidi ya yule mtesaji japo alikuwa na mwili mdogo, ila yeye hakuwa machachari, alikuwa ametulia na alionekana kuwa makini sana.

Walizopanda ngazi na wakatokea chumba cha juu. Wakafuata mlango waliutumia kuingia pale mwanzo. Wakatoka, safari ikaendelea na bado John Truck alizidi kuyatazama mazingira yale kwa umakini mkubwa. Akazidi kuyasoma na kuyakamilisha mazingira yale. Safari ukakolea kwenye chumba namba 100.

Yule mwanajeshi akamwonesha Johnstone John Truck ishara ya kuwa atangulie mbele. Huku mlango ulifunguliwa, huku moyo ukienda mbio maana mlango ule una mchoro wa kutisha karibu na ile namba 100. Akaingia ndani, akamtazama nyuma akamwonesha yule mwanajeshi alivyomtazama. Yule mwanajeshi alikuwa na kovu lilishindwa japo lilikuwa tayari limekauka.

Kiotomatiki mlango unajifungua . Bila kuchelewa John Truck aliligeuza shingo lake na kutazama mbele, tena makini mkubwa. Akajaribu kusogea ingawa bado hakuweza kuona kiumbe chochote kwenye kile chumba.

Chumba namba 100.
Chumba kile kilikuwa kikubwa sana kilichoonekana kuwa na madirisha ingawa yalikuwa yamefungwa. Kilionekana kuwa na mlango mmoja yaani wa kuingilia tu. Kilikuwa sakafu iliyoonekana kuchoka huku kuta zake zikiwa na plasta huku mwanga hafifu wa taa ndogo zilizojitupatupa kama nyota za hasubuhi.

John Truck alizidi kukichunguza huku akizidi kuangalia kama kutakuwa na kiumbe chochote katika chumba kile kinachoogopesha na kuzishutuwa hisia. Atimaye akafanikiwa kumuona kiti kilichokuwa na muundo wa kufungwa na kufunguliwa. Akakisogelea kiti kile akamtazama kwa makini akainama na kukichunguza chini naye akajiakikishia kuwa kiko salama, japo hakukikalia. Akautumia mda ule kukichunguza chumba kile kikubwa na chenye ukimya ka kilichotelekezwa.

Katika chunguza chunguza akagundua kuwa kuna kamera iliyolingana na sindano na yenye mwonekano Kawa sindano, ingawa haikuwa na sehemu ya kuchoma. Hapo ndo kulikuwa na kamera.

John alijifanya kama hajaiona. Akaingia na wazo maana alijuwa jinsi ambavyo wanaona vyote anavyofanya, akaamua kugeuza tabia yake na kujitoa katika hali ya ujasusi na kujifanya kama mtu aliyetoka kijijini akishangaa mataa ya mjini. Akaanza kujifanya anashangaa mwonekano wa zile taa na hapo ndo alitambua kuwa zile taa pia ni kamera. Hapo ndo alimweshimu mganda.

"Habari yako John Truck". Ni sauti ilitokea nyuma yake. John Truck jakugeuka haraka haraka, bali aligeuka polepole na kugundua kuwa sauti ile ile ilitokea kwenye spika iliyokuwa imeningizwa kwenye roof (paa). Akaitazama spika ile kwa sauti ya dharau "niwe na habari gani, badala ni nikuulize habari. John Truck aliamua kumfukuza adui wa wengi ambaye ni uoga na akayatamka maneno yale huku akiwa ameota zama spika ile.
Ukimya ukapita bila jibu lolote

ENDELEZA WAZO . ..... .................
 
Nimefurahi sana,

Je naweza endeleza?
 
Nitaendelea ingawa kwa sasa bando ndo tatizo.Najikuta natumia free basic SANA kuingia JF. Lakini nitaiandika niitupie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom