Weka siasa pembeni, tafakari "credibility" ya Mamlaka za Serikali katika sakata la CHADEMA

Imekuaje raia wa TANZANIAA wanaishi kama wageni kwenye Taifa Lao? Maana hawajali lolote wala chochote kuhusu serikali na mambo yanayofanyika ndani ya serikali, ili mradi maisha Yao yanasonga mbele kwa kupata ubwabwa na mboga wanaona ni Sawa tu.

Ukimya wao unaweza Sema Wana Taifa lingine tofauti na hili, Kwamba hapa wamekuja kutafuta tu na hawana haja ya Kutengeneza mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tume fika pahala raia wa Tanzania bila aibu anasema yeye siasa haimuhusu kwasababu sio mwana siasa! Anyway hapo utasema labda walinyimwa elimu ndio maana wanatoa kauli kama hizo.

Tuzidi kuwaombea hawa raia.
Umeongea kizalendo haswaaa.Nchi hii inahitaji sana watu kama wewe
 
Basi waanzishe chama chao kisichofuata utaratibu maana hawawezi kujiamulia wao kwa mwamvuli wa chama cha siasa wakati wameanua wenyewe kwa sababu zao wenyewe.
Kabisa wakianzisha chama chao hapo ndo watakuwa wameonesha kwamba wao ni watu huru ndani ya taifa huru kama wanavyojinasibu na kwamba wana uwezo wa kujiamulia wakitakacho wakati wowote bila kubughudhiwa na yeyote.
 
Kama kuna kitu kimekuwa constant kwenye awamu ya Tano ni impunity.

Wanaongoza nchi kwa mtazamo wa "Watatufanya nini?" Jeshi ni letu, mahakama ni zetu na bunge ni letu; mtafanya nini?

Kama kweli tume imefuata utaratibu katika kuteua hawa wabunge, na ingekuwa inajiheshimu, ingetoa tamko haraka sana kutaka vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa haraka. Maana kuna mawili, tume imepewa forged document, kitu ambacho ni jinai au CHADEMA inadanganya umma, kitu ambacho pia ni jinai.

Lakini wanaongozwa na impunity, hata kama tukifanya kinyume na taratibu, Watanzania watafanya nini?
Hili linawafanya wajiamini zaidi
 
Usirushe mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo siku akina mama wakiamua kujibu sinema za CDM zinavyotengenezwa akutokalika au wakiamua kumu expose Lissu for what he is.

Mwisho wa siku wao ndio wako mstari wa mbele kupokea virungu na kulala jela. Fatma Karume, Kigogo na Maria Sarungi wao wako Twitter waingie ulingoni kama wenzao halafu ndio waongee.

Alichokifanya Mdee na makamanda wenzake wao ndio wanajua uchungu wa sauti zao kuminywa sio nyie keyboard warriors.
Hao Unaowaita keyboard warriors ndiyo Wanao Wanyima Usingizi kila kukicha,Ungelijua Dunia kwa Sasa inaogapa keyboard warriors zaidi ya hao warafi wa Madaraka.

Ukiona leo CCM anamsifia na kumpongeza Mdee jifunze kwa mtini,toka lini FISI akawa muuza Nyama buchani??? Eti leo Mdee anakuja na Hoja ya MFUMO DUME😅,Ms Theodosia Usaliti haujawahi muacha mtu salama
 
Ukweli ni kwamba Yote haya yameanzia kwenye siasa za majintaka Sasa hivi siasa hizi za.majibtaka zinaathiri taswira ya nchi yetu. Haiingii akilini kuona mihimili ya nchi Bunge, Mahakama na Serikali kupitia NEC na Vyombo Mbalimbali vya Dola vikiingiza Nchi yetu katika Kashfa nzito za kimaadili na utovu wa nidhamu.

Inawezekanaje Spika mwenye washauri na Watendaji wa Kila Aina kujiingiza katika mchezo huu wa kihuni? Hivi kweli Tanzania ya Mwl. Nyerere imefikia mahala pa kuwa na Spika anayefanya mambo kihuni na bila kuheshimu Taratibu, Sheria na Katiba kiasi hiki?

Haiingii Akilini kwa Mhimili wa Mahakama kujiingiza katika Kashfa ya Kimaadili Kama hii. Hivi wananchi waiamini taasisi ipo nyingine Kupata Haki zao Kama chombo cha kutoa haki nacho kinaminya haki?

Wapo wapi wazee wa taifa hili?? Tunahitaji Sana busara na Ushauri wenu. Pamoja na ukweli kwamba mnaona Bora mkae kimya ili muishi vzr, lakini heshima yenu ni muhimu zaidi. Mambo haya kutokea mbele yenu na mkawa kimya, yanafikirisha Sana watu waliowaamini ndani na nje ya nchi yetu.
Wana msemo wao "Kwa maslahi mapana ya taifa"
 
Usirushe mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo siku akina mama wakiamua kujibu sinema za CDM zinavyotengenezwa akutokalika au wakiamua kumu expose Lissu for what he is.

Mwisho wa siku wao ndio wako mstari wa mbele kupokea virungu na kulala jela. Fatma Karume, Kigogo na Maria Sarungi wao wako Twitter waingie ulingoni kama wenzao halafu ndio waongee.

Alichokifanya Mdee na makamanda wenzake wao ndio wanajua uchungu wa sauti zao kuminywa sio nyie keyboard warriors.

Haya ndio malipo yao kwa kupigwa virungu, kulazwa jela, na sauti zao kuminywa? Hawakuwa wakosaji kustahili hizo adhabu? Iwekwe wazi basi.
 
Mnyika anasema...

Uhakika nilio nao, hao 19 walioenda kuapa, walishirikiana na ofisi za NEC, pamoja na Bunge kughushi nyaraka za chama, kujiteua bila kikao na kujipeleka kwenda kuapa. Huu ni USALITI mkubwa. Wote 19 wanafahamu orodha haiwezi kwenda NEC bila kupitishwa na Kamati Kuu ikiwa na saini ya Katibu Mkuu na mihuri ya chama. Na mimi sijasaini wala Manaibu wangu. Sasa NEC watueleze hiyo orodha waliyopewa ina saini ya nani?

Kughushi ni jinai. Na ni jambo la aibu kama Ofisi ya Bunge na Tume ya Uchaguzi wanaweza kushirikiana na watu wachache ndani ya chama kufanya jinai ya kughushi kwa maslahi yao wenyewe. Naomba wanachama wa CHADEMA, mtoe maoni yenu ni hatua gani zichukuliwe dhidi ya akina Halima Mdee na wenzake. Maoni hayo yawasilishwe kabla ya kikao cha kamati kuu Novemba 27.

Ieleweke hawa sio wabunge wa CHADEMA. Ni wanachama wa CHADEMA walioamua kutumia mwavuli wa Chama kunajisi heshima zao na heshima ya chama chao. CHADEMA hatuwatambui. Ni wabunge wa Viti Maalum kwa matakwa ya CCM, ni Wabunge wa NEC na ni Wabunge wa Spika Ndugai. Kwa ujumla CCM imeamua kujiundia kambi yake ya upinzani Bungeni ili kuokoa Trilioni 2 za wafadhili zisipotee."

Moja ya mambo ya msingi katika nchi huru kujenga taasisi imara ambazo hazitegemei mtu bali mifumo imara itakayofanya taasisi isimame hata asipokuwepo fulani.

NEC, DPP, Bunge n.k wanahusishwa katika jinai. Tafakari kama Tanzania ina taasisi na mifumo au kitu gani?

All Governments in the world are dirty and violent.
 
Kwanza, wote tunajua hapa hakuna kitu kama taasisi huru (autonomous institutions). Amri ya mwisho kwa taasisi zote hutoka kwenye mamlaka moja tu.

Pili, inashangaza sana hadi sasa media zinadai kuwa Mkurugenzi wa NEC hapatikani tangu kuapishwa hao wabunge kutoa ufafanuzi jinsi majina yao yalivyomfikia.

Kwa mwenendo huu wa Bunge na NEC zikiwa taasisi muhimu za utawala nchini na kampeni inayoendelea mitandaoni kuishinikiza CHADEMA “isiwasumbue” hao wabunge, NI DHAHIRI kuwa kuna mkakati mzito wa kuiua CHADEMA kwa kuiondolea nguvu ya imani ya wananchi (moral support), uongozi imara (leadership credibility) na uwezo wa kujikimu (material/financial wherewithal).

Leo tutajua hatma ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom