London 1989
Son you finally like some girls, isnt she too young for you maybe? I am just saying you know. Collins akachekaaa, it is not like that, she is just my friend, like a little sister. She grew up without a mom you know, and she wished her mom was here. Baba mtu akampa ile sneaky face look ya kuwa you cant fool me son. Huku akimwambia, i get it, absoulutelyyyy, i understand complately. Wakajikuta tu wote wanacheka baba na mtoto. Collins anamsisitiza dont tell mom about this. Baba mtu akawa anachekaa, absolutely, this is between us.
Kidogo baada ya siku hio wakaanza kuwa close kimtindooo. Wakarudi London maisha yakaendelea. Wakiwa wamerudi tu London, hapo hawana hili wala lile, Collins ashaanza kuwa mvulana, aibu aibu na ndoto ndto zinamsumbuaaa. Carina ndo anamshauri kama vipi ni ku hook up na dada wa flani, au dada wa flani you guys will look amazing together. Collins anasita, sita, anakubalian na Carinaa kabisaa dakika za majeruhi ana ghairi. Aibu ndo ikawa inamponza ile kuwa social kujichanganya na mademuuu, hawezi kabisaaa.
Mademu wakawa wanamuelewa sanaaaa, yeye tu kujiongeza ndo anakuwa mzito sanaaa. Akiwa bado hajajiamini kuna demu kwenye kwaya ikawa kamzoea zoea huku na huku akamualika kwao weekend. Kufika kule demu akamuomba mambo akawa anasita, demu anamjia juu acha ushamba bwanaa, hivi vitu watu wote age yetu waeanza kufanya tangia 14 years. Anapewa mate, ndo kuona kumbe tutamuuu. Anaelekezwa fanya hivii, hiviii bwanaa, wewe vipiiii. Mipapaso kadhaa wazungu haooooo. Demu hakubaliii akasema zoezi linaanza upyaaaa. Mpaka kikaelewekaaa.
Akafika nyumbani akajisikia vibayaaaa, siku hio kwa yalio tokea, it was just gross. Afu akifikiria yeye mtu wa dini ndo anazidi kukosa amani akajiambia hafanyi tenaaa. Akawa anamkwpa yule demu. Anamshawishi you will feel much better the next tiem, Collins hataki kabisaa hayo mambo.
Carina akawa anakula favor za wadada akiwazuga atawahook up na kaka mtu. Kweli alikuwa anafanikisha kuonana sasa wakishaonana Collins mzito kwenda na mahitaji ya soko.Wadada wanangangania baadae wanaona hamna progress kwa hio wanajikata tu wenywe juu kwa juu.
Siku hio hawana hili wala lile, wamekaa na mama yao mzee hajarudi wakajua ni kawaida tu. Usiku mzee akarud wakamsikia anagomba sanaaa, anafokaa mnooo. Wakajua kishanukaa ila hawakujua ni nini haswaa wakajua maugomvi yao ya kila siku.
Asubuhi wakamkuta mama yao macho yamevimba, Collins anapanic kumuuliza amekupigaaa? Amekupigaaa? Mama akasema hapa hajanipiga kuna taarifa sio nzuri hata kidogo, baba yenu ametumiwa barua ya kuitwa nchini akalitumikie jeshi ila kwa Tanzania sasa. Si mnajua kuna serikali mpya ya Mwinyi, sasa siasa zimebadilika, watu wa Musoma sio wazito sanaa jeshini tena. Kwa hio tunatakiwa nchini awe amereport ndani ya miezi 3.
Sasa analalamika hajatendewa haki, haiwezekani yeye kurudishwa ni mistake, yeye anatakiwa alitumikie jeshi la JWATZ ila kwa upande wa UK. Hapo anahangaika kuongea na balozi kucheki uwezekano wa kufanya chochote kitu tubakie huku, ila dalili zote zinaonesha safari ya Bongo imewadia. Bora mawazo yenu myatune kurudi nyumbani Tanzania.
Nasikitika sanaa hamjazoea kule kabisaaa, things are so bda, worse infact, the education is terrible, health terrible, transport terrible, yani sijui tutamanage vipi sijuiiii. Na mimi kazi niliokuwa nafanya nishaachaga sasa sijui nitafanyaje kwa kweli kumanage maana mambo ni magumu sanaaa
Baba yenu asingekuwa kichwa ngumu , na analiabudu jeshi ningemshauri tutafute namna ya kubakia huku, ila damu yake ni jeshi, bila jeshi hajaishi badooo. Hata akipelekwa jangwani maadamu awe na cheo chake hicho hicho na ni mtumishi wa jeshi basi roho yake imeridhia kabisaaa.
Carina analia, i dont want to go back. I want to stay here. My friends cant be visiting me in Africa. Mom our home is here. anajilizaaa hatai. Collins anashangaa shangaa tu. Kiukweli alitishika sanaa maana mambo anayosikia ya Africa sio mazuri hata kidogo. Ila Grace alimwambia Tanzania mambo poa tu mbonaa, sanaa, hamna la ajabu. Akawa njia panda hajui huku Tanzania kuna nini haswaa kinaendelea.