Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Daaaaaah!! @Lara1 umetisha aisee, maana umeifanya jmosi hii nishinde ndani the whole day tangu naamka hadi muda huu, bonge la Story yani. Big up sana...
yaani simu ilikata moto nikaamua kuwasha na PC ili mradi tu hii story iishe kabla ya kurudi kwa kauli mbiu yetu sie watumshi wa umma...😉😉😉
 
Nilitaraji kujua baba mzazi wa Walter na connection yake na victims wengine kwenye huu mkasa!
Nilitamani kujua sababu ya baba mlezi wa Walter (Chapombe) ilikuwaje akawa ndani ya Gwanda za kijeshi wakati hakuna mahali mbeleni penye ufafanuzi!
Nilitamani kujua destiny ya Walter na kazi yake na maisha yalivyoendelea akiwa na chaukorofi wake Inspector Janeth
Nilitamani kujua hatma ya Muddy na Grace...
Nilitamani kujua destiny ya Fahad
Nilitamani kujua life after fujo za ujanani kwa Carina na training alompa mama yake ilihali Mzee Mujungu ndo basi tena
Kwanini Carina alielewana haraka na Fahad kwenye ile birthday,kwanini alimwonea huruma sana Iqra wakati Collins alipotaka kumtoa sill? Palikuwa na chemistry gani kubwa namna hivyo in between!
You're a good reader...
 
Ila kwenye kuagiza castle lite... Hapo umetukamata.. Hiyo miaka ya late 90s castle Lite ilikuwaga bado sanaaa
 
mamaeeee mpka van damme unamjua huyo uliyemtaja wewe nimaster wakinongmdoni mkwajuni
kunaile chafu namba nimyingine dame wa sinza huyo ndo alikiwa nishida mkora hatariii
 
Akiwa dirishani anachungulia nje, akasikia anaitwa Sabraaa!akasikia mbona nakuita mda mrefu huitiki au hili jina la Sabra sio jina lako? Akadakia mama yako kina mselemu, usiwe mkali sanaa kwake, jina lake ni Iqra sema maisha tu yupo hapo kama hivo unavomuona yupo kama hayupo. Unavoumona hivo ni kama yatimaaaa, na siku si nyigi anaozeshwa kwa mwanaume asiemtaka, atafanayaje wakati yatima hadeki?

Yule mwanamke wa kiarabu akampandisha na kumshusha Iqra, akatikisa kichwa. Haya mwali wangu njoo nikuchore hinaa, mi nishalipwaa, pole mwanangu, hata mimi niliozeshwa mdogo walau wewe una miaka 20, mie nilikuwa na miaka 15 nikaozeshwa kwa mwanaume simpendiii, yeye ndo alinipenda akaniposaa, zamani zile maisha yalikuwa magumu sanaaa.

Kanioa Oman, siku ya harusi nimetandikiwa shuka nyeupeee, kanivurugaaa, nilumiaaa mwanangu usisikie, ukubwa jalala. Kesho tena shurba ile ile. Baada ya siku 3 tukaja huku Manchester, tukafikia kwa dada yake. Naumiaa sio kidogo, mwanangu giza likitaka kuzama naanza kuliaaa utadhani nalilia lisizame. Manchester tukafikia kwa dada ake, siku ya kuondoka kwenda kwangu namlilia wifi namlia wifi eti mimi niachwe kwa wifi hahaaaa! Mxiuuuuuuuu! Ila sahivi alhamdullilah nimezoea tena kuolewa ni jambo la kujivuniaaa, mbeleni hao wanaume wanatafutwa hawapatikani.

Mwali wangu safari hapo ndo kwanzaaaaa inaanza kweupeeee. Yaani kaza moyo tena ukaze sawa sawa. Njoo nikuchore hina mimi, nishalipwaaa, nitakuchora maua mazuriiiiiiiiiiiii, utapendezaaaa, afu umebahatika umepata kijana mzuri tu. Said kijana wa kileo, hana hata dini sanaaa, mtu wa kujienjoy, hata ukiwa mke wake hutopata shida sanaaa. Sijui kwanini humtaki Saidi, hata muonekano mbona handsome tu. Wasichana wa sahivi mnajielewa wenyewe, we ungepewa mume wangu alivo mfupi vile si ungekunywa sumu, hahahaaaaaaaa!

Mke wa Nassor akamwambia embu bwana usimtishe mtoto wa watu, mwaya Sabra ndo ni kitu kizuri sanaa, utaenjoy kwa mumeo, utakuwa hunifanyii mimi kazi tena, unaamka unavotaka kwako na kula unachotaka na kulala unavotaka, sasa kwanini usiolewe eti Iqra? Aya njoo uchore hina, akija uncle wako Nassor akakukuta hujachora itakuwa ugomvi mkubwa na siunajua tangia afilisike sio mtu mzuri kumchokozaa, ashapokea posa, na wewe huna baba sahivi, Nassor ndo baba yako, Bibi angekuwepo angemuweka Nassor mahali pake nae ndo hayupoo, na mimi ndo nipo kama sipo siwezi sema lolote, ndugu zako wa Oman washakubali uolewe. Na kama unavojua babu wa Manchester kaahidi ukiolewa tu na mwanae Said anampa mkopo na kushirikiana nae kibiashara we unafikiri ataacha suiolewe? Olewa tu it is not that bad, haya njoo uchore hina.

Iqra akajibu SIOLWEIII na hina SICHORI. Wakamuangalia wote kwa mkupuo na kuangaliana kisha yule mama mchora hina akaaaga na kuondoka zake. Mke wa Nassor akaondoka zake, akabakia Iqra peke yake chumbani. Akawa anawaza mambo yote yaliyotokeaaa mpaka kumfikisha hapo.

Akakumbuka alivokwenda kwao na kumkuta Uncle wake Nassor nyumbani ghaflaaa, akamwambia baba yake yuko Somalia kapata matatizo wanatakiwa waende mara moja, dakika hiohio. Wakaondoka na wasomali wa pale DSM hio ni baada ya Uncle wake kuuza kila kitu chao na kubeba pesa zote. Alivomuuliza kwanini anauza akasema kwa ajili ya Fahad na kutatua matatizo ya baba yake huko Somalia.

Akakumbuka kusimamishwa Namanga na askari kumhoji huku uncle wake akimuangalia kwa jicho la tahadhariii ile wako useme kitu, akasingizia yuko mwenywe anaenda Somalia kumtafuta baba yake, askari akamuonea huruma na kumsaidia kuvuka border la huko Somalia.

Kufika Somalia Nassor akambadilikia baba yake yupo UK, kaagiza Iqra apelekwe UK, kupitia Somalia, ionekane ni Msomali na ni mkimbizi wa kivita. Atengenezewe karatasi za Somalia kabisaa ili kupata uraia wa kule usisumbue. Kwa hio wako Somalia kwa ajili ya kutengeneza karatasi hizo na kutafuta namna ya kuingia Iqra UK kama mkimbizi. Waktoa hela UN, akapatiwa karatasi na akaingia UK, ila kwa majina tofauti sio Iqra Idriss Mselem tenaa, bali Sabra Yunus Ali.

Kufika UK, akamkuta bibi, kumbe bibi ndo aliagiza afwatwe kwa gharama yoyote na bibi ndo kumtaarifu kuwa baba yao amefariki dunia huko Dubai. Na Nassor ndo alimpeleka Oman akazikwa na ndugu wa huko huko Oman. Iqra aliliaaa aliliaaaa, akajiona mpwekeee sanaa. Bibi akamuondoa shaka Nassor atawatunza na Fahad na kuedeleza mali za baba yao. Basi Nassor kulalamika kila siku Fahad anamfilisi, anatumia hela zake nyingi, ni gharama sanaa kumlea Fahad sijui nini. Bibi lile sikitiko jinsi Nassor alivobadilika likammaliza. Ndani ya mwaka tu akawa anajiuguliaa huku anasikitikaaa, mpaka siku ya umauti akamwambia Iqra msamehe Nassor na umtafute Fahad usimuamini Nassor. Nassor ni mwanangu ila na mashaka nae.

Baada ya bibi kufariki, hali ikawa ngumu sanaa, sanaaa. Iqra akimuuliza Nassor Fahad alipo hamwambiii. Nassor akaenda kuomba apewe posa ya Iqra kwa babu wa Manchester aliekubali haraka sanaa. Iqra alivojua akataka kutorokaa, Nassor akamwambia ukitoroka kaa ukijua hutokaa ujue Fahad alipo. Iqra ikabidi abakie akashindwa kutorokaaa tena maana ilimlazimu kujua Fahad alipo, na anapo pajua ni Nassor peke yake.

Akakutanishwa na huyo mchumba Siad, amabe ni check bob sanaa, akamkumbusha sanaa kuhusu Wlater, mambo yake mambo yake yalivo alivo mwingi wa habari na anasa. Na Siad kiukweli kwa Iqra siku zote alikuwa mkarimu wa nafsiii sanaa, na mwenye upendo mwingi. Iqra akamuomba asome kwanza kabla ya ndoa na Said akamkubalia ni jambo jema. Japo watu wengi walipinga hilo swala ila Siad akalikomalia kama bwana harusi kakubali Mkewe mtarajiwa asome mpaka aridhike. Na shule ndo imeisha mwezi huo, uncle wake Nassor anamngangania aolewe ahraka iwezekanvyo ili apewe yeye mkopo.

Iqra akawa anamtafuta mwenyewe Fahad kisiri siri sasa tatizo hakuwa na pesa, na kwa jina hilo la Sabra hakuwa na udugu na Fahad kabisaaa. Aliekuwa na udugu na Fahad mwenye kuweza kufanya chochote ni Nassor basi ndo alikuwa na karatasi na nyaraka zinazoweza ku link na Fahad. Iqra akawa anawazaa kila siku juu Fahad yuko wapi na anafanya nini mda huo.

Akamkumbuka na Collins akajiambia atakuwa alishaoaaa. Chuki ilishamuisha yakabakia masikitiko tu ya nafsi. Afanyajeee. Akaikumbuka sanaa zile siku zao 2. Akatafakari akajiona hana thamani kabisaa duniani. Akajiona asie na bahati kabisaa tajiri wa mikosiii maskini wa bahati. Akatafakari akaona maisha hayana tena thamani kwake. Akachukua pen akaandika barua ndefu kwa Fahad. Akawa amepanga kesho yake anywe asprini kama 10 akakutane na ndugu zake wengine kama bibi, baba, na mama yake ambae hakuwai kumuona akiwa na akili.

Alipotoka akampa ile barua mke wa Nassor, akamwambia naomba uitunzee hii barua, hili ndo ombi langu la mwisho kwako, itunze ikitokea siku ukimuona Fahad mgaie barua mwambie Iqra alikupenda sanaaa. Dunia hii si ya watu wote. Ni dunia ya wachache. Mke wa Nassor akapokea ile barua, akatafakariii akajua kuwa huyu bwanaa huyu ashafanya maamuzi magumu. Na mtu akishaamua hivo ni mambo ya wakati tu. Akamuonea imani familia ilivoishaaa vibayaaa. Akakaa akafikiriaa, akakumbuka kuna file la Nassor kabatini. Akaenda kulipekuaaa.

Akabahatisha risiti ya ada shule aliolipiwa Fahad enzi hizo Nassor ndo alitumwa na baba yao kina Iqra. Akatoka chumbani akamfata Iqra akampa ile risiti. Akamwambia kwanini usiende kumtafuta ndugu yako? Una zaidi ya miaka 18, Nassor hawezi kukufanya kitu chochote, we nenda Londo anzia hapo shuleni utampata tu Fahad. Iqra akatabasamu, matumaini yakamjia upyaaa. Mke wa Nassor akamwambia chukua na hili kopo langu la dhahabu, sina pesa ya kukupa kubwa ila hizi dhahabu najua za thamani sanaaa, zitawasaidieni kuanza maisha na Fahad. Ukiondoka wala usirudi tena hapaaa, uncle wako sio mtu mzuri kabisaa. Baba yenu alikuwa mtu mzuri sanaa. Ondoka sasa hivi kabla hajarudi. Usikate tamaa Iqra jitahidi wewe ndo baba ndo mama yake Fahad.

Iqra akachukua vile vitu, akamshukuru mke wa Nassor akaondokaa zake mda ule ule. Alikuwa an akiba kidogo maana kuna summer job aliifanyaga akaenda London jioni hio hio. Akapanga ki hostel na kuanza kumtafuta Fahad. Akaenda shule ya kina Fahad akaambiwa tu alihamishwa mwaka ule ule baba yao alivofariki kwenda kwenye goverment program maana ada haikulipwa.

Akaenda government program wakamulekeza mji alipo Fahad na kumtaarifu tu kuwa Fahad hakuwa anapata msaada wowote, popote pale. Mda wote huo tangia baba yao afariki alikuwa anaishi kwa shidaaa kwa msaada wa serikali na hapo alipo inaonekana hana ndugu wala jamaa yoyote UK. Iqra akaamini kweli Nassor mshenziii sio kidogo. Akaaondoka london kwenda huo mji aliopo Fahad.

Akafika alipoelekezwa, akaelekzwa alipo Fahad na mda gani wa kumuona. Akaambiwa asivuruge ratiba ya Fahad ni muhimu sanaa aendelee kuishi kwa ratiba yake ilio pangwa. Iqra akaenda kumsubiria mgahawani anapokulaga. Iqra ahawakumzuia kama Collins kwasabu ni mwanamke, wakajua tu Fahad leo kapata mchumba mbonaaa.

Fahad kumuon Iqra akamjuaa. Wakafurahiiii kuonanaa, mda wa kuondoka wakaondoka wote mpaka anaposhi Fahad. Iqra akawa hataki hata kutoa machoni hata mara 1. Wkapiga story haooo, alimmiss sanaaaa. Sasa baadae akamuona Fahad kavaa locket yake aliompa Carrina akastukaa akataka kumvuaa. Fahad akakataa aksema Collins. Iqra akamuuliza Collins alikuja kukuona huku? Fahad akawa anamjaribu kumsimulia alikuja sio huku nyumbani bali mgahawani. Iqra akachoka nafsi.

Usiku wakalala Iqra anaikodolea ile simu macho. Kila akitaka kupiga anasitaa. Akaamua kupiga namba ya kina Carrina ya nyumbanii. Ikaitaa haikupokelewa. Akapiga tenaa Haloo, nilikuwa nimetokaa mwanamke anaonge akwa bashasha, akauliza Carrina yupo? Akamwambia hayupo yupo kwa mumewe, andika namba yao, akamtajia Iqra akaiandikaa pembeni. Mimi mama yake Koku. Nani kwani wewe? Iqra akamwambia mi rafiki yake wa zamaniii. Akamuulizia Collins yupo? Koku akasema Collins hayupo anakaa kwake sahivi mpigie namba hii akampa namba. Wamekua wamenikimbia wameniacha na kizee chao. Hahaaaa. Iqra akamuaga koku akapumzika kwanzaa.

Asubuhi Fahad akaenda kazini kama ratiba yake inavotakaa, akabakia Iqra akawazaa na kuwazuaaa, akachukua ile simu na kupiga namba ya Collins. Ikapokelewa Haloo! Iqra nguvu zikamuisha a kabisaa, zikapita kama dakika 5 haongei kitu afu akakata simu. Akaa kwanza ajipange upya aanzie wapi na kumaliza wapi. Maana angeanza kusmeaje sasa.

Akapiga tenaaa, ikapokelewa Haloo! Iqra akajikusanya kusanya na kusema Mi Iqra! Ukapita ukimyaa mrefuuu bila upande wowote kuongea baina yao. Iqra akakata simu Akajilaumu kwa kupiga, akawaza ukute Collins alishaoa ana watoto kahaaa. It was a bad idea to call him after alla these years. Mara awaze angemshukuru kwa kuja kumuona Fahad akawa tu anababaika.

Baada ya siku hio akaamua kuanza maisha mengine na Fahad akaanza kutafuta kazi wasaidiane na Fahad maisha, waone itakuwaje . Akawa anajilazimisha kutokumfikiria Collins kabisaa. Anajiambia miaka imepita mingi snaaa jamani, hata hanikumbukiaa. Mara ajilaani kwa kuwa tajiri wa mikosi na maskini wa bahati. Yaani siku 2 hizo zilikuwa ngumu sanaa kwake. Akawaza mabo mengi sanaa. Lile wazo la kujiua likaanza kurudi upyaa. Akaanza kujipa moyo kwanza Fahad anaendelea vizuri on his own, akimuona yeye Iqra amevurugika nae atavurugika bora yeye atangulie tu kujipumzishaa mbele za haki, Fahad ataendelea tu vizuriii.

Siku ya 3 akiwa bado depressed akawa anawaza mambo mengi sanaa snaaa, ila kila jambo akifikiria juu yake binafsi linamkatisha tamaa kabisaaa na kumuhuzunishaa. Akawa amefanya usafi nyumba nzimaa kupunguza stress moyoni anawaza huenda huu ukawa usafi wa mwisho mimi kukufanyia mdogo wangu Fahad. Akaoga akapanga vitu vyake vizuriiii kabisaaa, na kutafakari atimize lengo lake la kujamaliza au afanyaje. Akawa anaiangalia picha yake na Carrina sisters for life akatabasamu.

Akasikia Fahad karudi anaongea ongea na mtu kama sauti anaijua akashuka chini fastaa ndo kumkuta Collins. Kumbe mda wote anaongea na Collins. Wakabakia wanaangaliana tu wafanyaje. Iqra akakaa pale pale kwenye ngazi. Ukaingia usiku hamna anemsemesha mwenzie. Kila mtu anaongea na Fahad tu hawasemeshani direct.

Mda wa kuondoka Collins akamwambia Iqra nisindikize. Iqra akakubali nje akaita tax, Iqra akataka kugeuza, Collins akamwambia nina maongezi na wewe hotelini. Iqra akaingia kwenye tax. Njiai akamuuliza mbona ulipoteaaa? Iqra akamsimulia ilivokuwa mpaka mwisho. Collins akamwambia na yeye alivomtafutaaa miaka yote bila kusahau kumtaarifu kuwa Walter ameoa siku nyingi sanaa na ana mtoto mkubwa tu. Hahahaa!

Wkabakia tena kimya, useme nini sasa. Hotelini kuingia na kuingia Collins akamdaka Iqra juu juu. Akaanza kumkiss, na alivokuwa na ugwadu sio kidogo. Hahahaa! Ikawa mechi ya kimya kimyaa haianmaneno wala nini. Asubuhi Iqra akamwambia mi naenda kwa Fahad, Collina akagomaaa kabisaa. Akamwambia yaani hapa sikutoi machoniii kwangu. Naongea na balozi tukufanyie mpango wa visa, yaani ni mguu kwa mguu mpaka bongo. Nimekutafutaaa, nimekutafutaaaaa siwezi kukutoa mahoni hata dakika 2.

Iqra akabakia kimya manake maisha yashamchosha kuongea sanaaa, ya kazi gani, akabakia mtazamaji tu. Wakaka pale hotelini wiki nzimaa, wakitoka ni wotee tena anamshika mkono kama atamkimbia vile. Ubalozini wako woteee mda wote. Balozi akawap karatasi zote. Wakaenda kumuag Fahad. Fahad hata haelewi anajionea sawa tuuu. Na kurudi wote Bongo.

Kufika Bongo akafikia kwa Collins. Sasa Collins anaenda kazini kwa mashaka kwamba akirudi anaweza asimkute au vipi basi akajiri mlinzi ili hata akitoka amwambie. Mwenyewe akawa hatoki wala nini. Ashajichokea maishaa, anaangalia tu mambo yanavoendaa. Collins akaenda kumwambia Carina nimempata huwezi amini. Carrina akaja na mwanae kumsalimia. Kidogo Iqra kumuona Carina akachangamkaaa na kufurahi.

Carrin akaanza kumkeep busy Iqra ndo akaanza kuchangamka na kuongea ongea upyaa kama zamani, wakaweza hata ku communicate na Collins, na akawa ana furaha tenaa. Siku hio wamekaa na Carrina Iqra akanza kutapikaa, Carina akamwambia una mimba wewe sio buree. Kweli alikuwa na mimba. Akawa anaishi pale pale kwa Collins mpaka kajifungua kabisaa mtoto wa kike. Wakawa wanapendana sanaa sanaa na Collins.

Mtoto wao akiwa na mwaka wakawa wametoka out, wasikutane na Walter na Jane na yule mtoto wao uso kwa uso. Walter roho ikafanya paaah. Wkasalimiana fresh tu na kuongea kinafiki, wakaka meza moja kama ndugu vilee. Walter macho yote kwa Iqra mda wote mpaka mkewe anamkanyaga miguuni.

Walivoondoka Walter akajiambia moyoni, Iqra nimekuona tena na najua pa kukupata sitaka niache kukufatilia, Collins kukuzalisha sio mwisho. Just because i cant be with you it doesnt mean i love you. I am comming for you Iqra.

Collins akaurdi na kumita Walter pembeni na kumuuliza we are just happy as we are, it is fate things turned this way. I guess you are okay with me kuwa na Iqra? Hahahaaaaaaaaaaaa! Damn Collins he jsut had to ask that question on his face.

Walter akatabasamu tu na kumwambia YOU WANT THE TRUTH? YOU CANT HANDLE THE TRUTH! Akarudi kwa mkewe akimuacha Collins akiwaza THE QUEST FOR IQRA BTN THEM HAS JUST BEGAN.

************************THE END**********************************
Finally The End Pheeeewww
Cc. Lara1 ww ni mkali kweli. Vipi mwaka huu je hujatoa any more stories?
 
Back
Top Bottom