Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Sio kila kisichokuimpress wewe basi ndio kisimipress nwingine. Where is your impressive story?? Duh! Kweli nimeamini kuna negative people. Ila watu kama nyinyi lazima muwepo aaargh... Story za lara 1 zote yaani ni level zingine,keep it up.
Chochea karama yako Lara 1 utafika mbali
Katika Maisha ya kila siku watu kama Hawa wapo, na ndo wanaotufanya tuwe strong
 
Hii story nahisi itaishia njiani kama zilivyoishia nyingine maana sio kwa ukimya huu.
 
kwani hata ingekuwepo ingekusaidia nini kwa sasa au ndio kukosoa kipaji cha mtu ......fanya uende kwa shigongo ukamkosoe maana yule kila gazeti lazima utoe hela sio huku hadithi bure bado na masharti juu Eminentia
 
1989 DARESALAAM

Idriss inabidi uoe mwanangu, mda umepita sanaa, afu bado kijana unadhani hawa watoto utawaleaje, mimi mwenyewe mama yako nishaisha warranty, siku yoyote narudisha kadi kwa Mungu. Hawa watoto peke yako hutawawezaaa nakambia. Unajua huyu mdogo hana akili, akili zake zipo slow sanaaa, alizaliwa kwa shida sanaa, ndo asha affectika. Ni mtoto anaehitaji malezi maalumu, pengine siombei lakini siku sipo hutoweza kuoa mke haraka afu akawaweza hawa watoto. Na peke yako hutowaweza.

Nashukuru huyu Iqra ana akili sanaa darasani, sanaaa. Huyu ndio wa kumtegemea amuangalie huyu mdogo wake. Kila siku darasani wa 1, walimu wenyewe wamekubali Iqra ni kiboko kabisaaaa. Kimbiza vidume wote mjukuu wangu. Nasikitika tu sababu mtoto wa kike ataolewa na akili zake zitaishia kwa mumewe. Fahad ndo kila siku anakuwa wa mwisho mjukuu wangu. Tution kila kitu hakisaidiii. Hapa imebidi mwaka ukiisha naenda shule kuomba ombaaa, nawapigia magoti, wananionea aibu mimi mtu mzimaaa, wanamsogeza tuuu, sasa sijajua mpaka lini itakuwa hivo.

Mama mimi kuoa badooo. Bado sanaaa, sijapata mtu wa kumuoa, afu naona wanangu wadogo, vile mama yao hayupo nikioa mambo ya dunia naweza nisiwaangalie vizuri, wakakosa kote kote. Maadamu mke wangu Mnyazi Mungu kamchukua mimi ngoja niwapende hawa watoto na kuwaangalia inavotakiwa . Sitaki distraction kwenye kuwalea hawaaa. Kama unavoona Fahad ndo hivo, nataka ni focus na kutuliza akili chochote nachofanya hawa wapo akilini mwangu.

Idriss nakuelewa sanaa ila sasa unachoshindwa kuelewa mimi kaka zako, wadogo zako huko Oman, London, USA, Morroco wananihitaji nikakae nao, nikakae na familia zao, sasa siwezi nashindwaaa kukuacha hapa na hawa watoto, na wale wajukuu zangu wengine wananikosa kwenye maisha yao . Watu wamekuvumilia miaka 6 sasa ila hujipangiii. Nassor keshapata karatasi za ukimbizi London, kaniita niende nikaone wajukuu, mke wake kazaa watoto 2 bado sijawaona na kuwabarikia. Hatuwezi kuendela hivi, mimi siwezi kusema niende nikuache na hawa watoto na biashara itashindikana, na mimi umri umeshasong mda wowote narudisha namba kwa Mungu afu wewe hujiandaiiii ndo tatizo langu.

Idriss akabakia anawazaaa tu atafanyaje na wale watoto kuoa hapana, na kweli mama yake umri umesongaaa mtu mzimaa kweliii. Akakosa kabisaa pozi la kufanyaaa. Na kweli Nassor anamsumbua kweli amruhusu mama yao aende London akaone tu wajukuu, Nassor atagharamia kila kitu. Amamzungusha ila imeshondikana ikawa ishaanza kuwa kama ugomvi.

Mama basi mi naona uende tu kwa Nassor na watoto wakifunga shule. Bibi akagunaaa. Akamuuliza kwa hio shule ikifunguliwa itakuwaje? Idriss akajibu tutajua huko huko. Ila kwa sasa jiandae kwa safari na hawa watoto mimi nitawaanda kwa safari, nitawatengenezea passport. Bibi akawa kanyamaza tu hajaridhia hilo swala ila sasa atafanyaje maana kwa Nassor lazima aende.

Baba yao akawatengeniezea pasport, kawaandalia mabegi vizuri kabisaa, akawaambia mtaenda na bibi kwa uncle Nassor London, kuzuri sanaa. Iqra anauliza kuna nini Baba? Baba ikabidi acheke, mwanangu baba yako hajawahi kufika London ila anaona tu post cards ni pazuri sanaa, wewe na Fahad mkifika London uangalie kila kitu kwa makini ili uje unambie baba yenu. Umuangalie na Fahad si unajua bibi mzee na kule nyie ni ugenini. Fahad anashangaa tu, haelewi.

Siku ya kuondoka Fahad kuona baba yake anabaki wacha afanye fujo na kupiga kelele za nguvu airport. Kumtuliza ikawa shida sanaa. Iqra nae aliumia roho sema akawa anajikaza maana hawajawahi kukaa mbali na baba yao hata siku moja. Siku zote wamezoea baba yao yupo. Ila sababu wako na bibi wakaona sawa tu. Wakapanda mpaka Nairobi, Nairobi ndo wakaunganisha ndege ingine.

Iqra anaangalia tu mambo anarecord ili aje kumsimulia baba yake. Kufika London, ndo akazidi kushangaaa mambo kule yalivoooo. Akaja uncle Nassor kuwapokea na bibi. Basi wakafika nyumbani akafurahi kuwaona wane maana alikuwa bado hajawaona tangu zaliwa, na akafurahi zaidi kumuona bibi. Nassor ana watoto wawili wa kiume rika la Iqra kabisaa. Bibi akamuuliza Nassor unafanya kazi gani huku? Nassor akamwambia mimi nafagai kanisa na kufanya uasfi kwenye kanisa nimeajiriwa vizuri. Bibi akanuna na kuanza kumfokea kiarabu Nassor.

Nassor anajieleza bibi huku maisha magumu, kazi hazipatikaniiii, hio kazi ya kanisa nzuriii, na wananilipa vizuri sanaaa, sizwezi kuiacha, na tangu hapo wananionea huruma mkimbizi wa vita, nimewadanganya natokea Algeria. Wananipa misaada, wananisomeshaa yani wananisaidia kujijenga upya mimi na familia yangu. Watu wazuri makafiri sio kama tunavowafikiria.

Bibi akasusaaa akawa ahataki tena mjadalaa. Akaalaani kama angejua Nassor anafanya kazi kwa makafiri nisingehangaika kujaaa. Anamkejeli kwa hio na nguruwe unakula si ndio na pombe wanywa ushakuwa kafiri wewe. Nassor analalamika mama mimi hunipendiii tokea zamanii sijui kwa nini, unampenda Idriss,Mselem na Yunus na binti yako Kauthar mimi hunipendi kabisaaa. Bibi hapo kavimba kama chatuuu.

Mke wa Nassor mtu mbayaa, Iqra alivomuona tu akajua sio mtu mzuri kama bibi yao. Jikoni kawawekea chakula, sasa Fahad anamwaga mwaga basi anamfokeaaa, ana panic kabisaa kwanini Fahad ana anamwaga chakula. Basi Iqra anamwambia usimfokee he is slow. Yani ndo anasonyaaaa, anatukana kiarabuuu. Wale wanae wanamcheka Fahad. Fahad yuko slow akawa anaogopa sasa kachanganyikiwa. Iqra akapata akili akanyanyuka na kwenda kumlisha mdogo wake ili asifokewe zaidi. Basi Fahad akaawa amenyongeaaa, na Iqra nae kanyongea akamkumbuka kweli baba yao. Mke wa Nassor analalamika mimi siwezi hii kazi, siwezi kabisaa, kama vipi warudi Tanzania kwao, mslaba ule na yeye hauwezi kabisaa. Iqra anamuelewa anavoongea maana bibi yake si anamfundishaga kiarabu. Akaona maisha magumu sanaa.

Wametoka jikoni bibi akauliza mbona kama Fahad alikuwa analia? Iqra akamuangalia mke wa Nassor akakutana na jicho kali sanaa akaamua kukaa kimya. Usiku bibi yake akamuuliza Mama Yunus alimfanya nini Fahad mbona likuwa analia, Iqra akawa anafichaa. Bibi akamkomalia nilikwambiaje kunificha jambooo? Iqra akamsimulia, bibi akasema nilihisi sasa nitamnyoosha. Wakalala. Asubuhi wakasikia kelele kumbe Fahad kakojoa kitandani, alikuwa hajakizoea choo akaogopa kuuliza akajikojolea. Basi mke wa Nassor ndo kufokaa fokaaa. Bibi hakumkopeshaa akaanza kumnyambuaaa hana roho nzuri, sio mkarimuuu. Sababu yule mkwe akanywea. Bibi akamwambia Fahad tutalala nae na Iqra chumbani kwetu. Nassor akagoma mtoto wa kiume atalalaje na wanawake. Bibi akasema niachieni mjukuu wangu, mimi mzee naweza kulala na mtu yoyote. Ndo ikawa salama ya Fahad.

Yunus na Mselem wote roho zao kama mama yao, vile Fahad alivo slow basi wanamtania huyu tahiraaa, toinyaa hiliii, chizi halina akili vizuri, basi Iqra anachukiaaa, akatokea kuwachukia ndugu zake hao mpaka basi. Akaamua kuwakomesha. Siku akaja babu yao wana undugu huko Oman aktokea Manchester, kaja kumuona bibi Iqra. Wakaitwa wasome Quran babu anasikilizaa. Yunus na Mselem wakaitwa wasome, wanachosoma hakielewekiii.

Iqra akamuuliza babu nisome mimi? Babu akamwambia soma. Iqra akasomaaa vizuriiiiii, babu akamuuliza una miak mingapi tena mjukuu wangu akajibu 7. Babu akawa amazed. Basi mke wa Nassor roho ikamuuma vile wanae wameaibishaaa, babu akadta na Iqra mpaka akamgea Pound 50 anunue anachokitaka london. Akamuahidi Manchester kuna mkutano wa waarabu kama wiki 3 zijazo watasoma Quran pale vijana kadhaa, hamna msichana ila nataka Iqra akasome ashindane nao, akishinda anapata pound 1000. Bibi akasitaaa kama Iqra ataweza kweli. Ila akikumbuka hela zilizotajwa anakubali. Iqra akaulizwa utaweza kusoma? Akasema naweza ila Fahad lazima awepo.

Bibi akaondoka na yule mzee kesho yake wakaenda Westham kwenye kikao cha waarabu wa huko, kulikuwa na msiba wa ndugu yao huko Westham. Iqra na Fahad wakabakia na Mke wa Nassor. Iqra hakulala usiku ili amuamshe Fahad akakojoeeee. Siku hio mchana kina Yunus wametokaa si wenyweji wakaacha mlango wazi Fahad akatoka. Iqra akajua wameenda nae, wamerudi anawauliza Fahad yuko wapi wanasema hawajaenda nae. Iqra akachanganyikiwaa, akatoka nje kumtafuta yeye mwenyewe mgenii. Anauliza wazungu hawamuelewii.

Akawa anahangaika mwenyewe anaita tu Fahad, Fahad! Hamuoniii. Ikafika mahala akakaa chini na kuanza kuliaaa. Akapita mkaka black tu, akamuuliza why you crying young lady? Basi anamuelezea i lost my brother he is slow, ametoka nje, anakoroga koroga lugha. Akamuuliza you speak Swahili, akasema yeah you know Swahili? Akamjibu tu kidogoo. I came from Tanzania. Akaanza sasa kumuelezea kiswahi. Akamwambia kwa hapa ltumtafute hizi njia 3 lazima tutampata. Wakaanza kumtafuta njia ya kwanza wakamkosa, ya pili wakamuona yupo kwenye gari ice cream analilia sasa wanamsemesha kingreza nae ndo hakijui vizuri.

Iqra kujisachi akakuta hana hela ila akakumbuka ana ile pound 50 aliopewa na babu yake akajua itatosha ice cream. Yule kaka akamnunulia ice cream Fahad na Iqra. Basi akawa anawarudisha akamwambia Iqra i want to work on my Swahili, how come uwe unanifundisha kidogo kodogo. Iqra akamwambia asante sanaa sina cha kukushukuru kumpata Fahad. Walivofika yule kaka akataka kuaga, Iqra akamwambia subiriii. Akaingia ndani akatoka na zile pound 50, akataka kumpa, yule kaka akakataa akasema kamsaidia tu sababu she ws a young girl frustrated and crying alone in the streets, ni wajibu wake kumsaidia akiwa kama coloured mwenzie kwenye nchi ya watu, na Mungu alivo mwema kumbe wanatoka nchi mojaa.

Basi kabla yule kaka hajaondoka akamuuliza jina lako nani? Iqra akamtajia. Yule kaka akamwambia naitwa Collins. akaondoka. Kesho yake Iqra anaangalia mda Collins atakuja saa ngapi? Jioni kweli akaja wakaenda park na Fahad wakwa wanaonge Kiswahili anaoksea, Iqra na Fahad wanamcheka. Basi ikawa good time. Wakazoeana sanaa tu. Baadae akamwambia kuanzia kesho usije bibi anarudi. Akasema sawa, akampa adress ya kwao akamwambia usiondoke bila kuniaga.

Mda ukawa umeend ainatakiwa waende Manchester kwenye hio competition, afu waondoke kurudi Bongo kupitia Oman kwanza lakini. Siku kama kesho wanaondoka akamuomba Yunus ampeleke kwene hio adress na asimwambie bibi, Yunus akagomaaa. Iqra ndo akampa ile pound 50 akakubali. Wakamsindikiza na Mselem. Basi akawakaribisha ndani kwao, wakamkuta na Carina. Carina anawauliza tu maswali. Akamwambia kesho naenda Manchester jumamosi kuna competition ya Muslims Society nitashiriki. Nikitoka hapo narudi Bongo. Wakapiga story kibao akamwambia anasoma Agakhan na kukaa Kariakoo. Wakarudi kwao na kesho kwenda Manchester.

Collins kwa mara ya kwanza akampoke baba yake kwa bashasha nyingi sanaa, na kumuomba kwa mara ya kwanza katika miaka mingi ampeleke Manchester weekend. Baba mtu akawa exited akajua anataka kucheki mpira maana kulikuwa na mechi akamuahidi atajitahidi wapate tiketi. Akamwambia siendi kwenye mechi naenda kwenye mashindano ya dini ya waislaam. Baba yake akawa disapointed but since ndo kitu cha kwanza Collins kumuomba akakubali yaishe. Wakaondoka Ijumaa ili amzungushe na mjini, mama yake akawa haelewi hio safari ya Manchester na walikubaliana asiambiwe it is a man thing kati yao. Wakawa wanamzingua tuuu.

Jumamosi Iqra akawa anasoma ile Quran kwa ufasahaaa afu msichana peke yakeee. Watu wooote wakakubali Iqra ni kibokoooooo kabisaa na bila ushindi alikuwa anashinda, miwhsoni mwishoni Collins si akaita Iqraaa kushangilia. Watu wote wakawashangaa baba yake anamwambia easy Son! Iqra sauti anaijuaa, akawa kapoteza concentration na kuharibu kidogoo mwishoni akiwaza Collins amekujaje paleee. Matokeo kutoa Iqra mshindi wa 2 akapata Pound 800. Wakafurahiiii familia nzima ila babu akawa dispointed alitaka ashinde. Akamuuliza nani alikuita? Iqra kadanganya sijuii maybe mshabiki tu.

Mpaka wanaondoka ikashindikana kuonana na Collin, wakapungiana kwa mbali tu, Collins akaondoka na baba yake, kina Iqra wakaenda kwa babu yao, kesho wakaondoka kwenda Oman na kurudi Bongo.

ITAENDELEA










My
 
Penzi jipya limechanua apo sasa nani ata kana dini yake amfate mwenzie!!!!
 
Hah

Hahahaaaaaaa! Wabongo na nyie toka lini penzi likachanua kati ya 15years old boy na 7 years girl?
Kijana alie kua ajawai mwamba chochote baba ake na alikua ampend leo kajishusha kumwomba apelekwe Manchester iyo tunaita power of love
Kaweza mficha adi swaiba ake mkuu(mama ake ) wanapo enda weeee ss watu wazima tunasema kaisha kamatika
 
Kama huto badili gia angan kijana lazima akomae likizo kuja bongo

Mshaanza story leading na utabiri utabiri, matokeo yake muendelezo ukiwekwa mnaanza kuniona mimi mbaya na mchakachuaji.
 
aya mama ngoja ntulie mie niendelee kufaidi utam Wa adisi
 
Hahahaaa! KUMBUKENI YOU CANT HANDLE THE TRUTH! CAN YOU?

Kwa experience yangu story zikifikamwisho panachimbikaga naonekana nimekula rushwa.
Dalili huwa zinaonesha hivyo, this time ukichoka kuandika nialike nitaandika mimi wewe unazungumza tu
 
Back
Top Bottom