Weekend Story: You Can't Handle The Truth

1982 DARESALAAM!

Hongeraaaaaaaaaaa! Hongera sanaa mzee Idriss. Mzee Idriss akawa amekaa standby aambiwe mtoto gani watu hawamwambii wanazuga zuga tu. Akauliza mtoto gani jamani tumejaaliwa na Mnyazi Mungu. Watu wote wakapoa ghafla. Akamuuliza Dr. wewe mwanaume mwenzangu nambie maana hawa kina mama wenzetu dhaifu sanaaa. Dr. akatabasamu umepata mama mzee Idriss, wakike mzurii kama mama yake. Mzee Idriss akanuna.

Wakaruhusiwa wakatoka hospitali, mkewe anajihami mume wangu watoto anatoa Mungu, najua unataka mtoto wa kiume lakini tumuombe Mungu na kusubiri maana huyu ndo kwanza wa kwanza. Akasikia Keleleeeeeeeeeee! Upumbavi anaoufanya Ibtysum mke wa kaka yangu wa Oman na wewe umeuanza si ndio? Unatakaa kunizalia malaya wa 5? Tulikubaliana nini? Sikukupeleka kwa Dr mashuhuri akuundishe calendar na mbinu za kupata mtoto wa kiume? Kwanini umeniangusha? Sio mimi mume wangu, Mungu mwenyewe ndo kapanga mume wangu. Mzee Idriss akaondoka. Mkewe akabakia kanyongeaaaa. Hana amani, anajilaumu na kumlaumu mungu kwanini kaanza uzazi na mtoto wa kike.

Ikawa mzee Idriss hamshiki mtoto, wala kama hamuoni kabisaaa. Hana mda nae, na mapenzi akapunguza asilimia 70 anashinda dukani mpaka usiku wa manane. Akaja mama mtu kutoka Oman, mkwe wa mke wa Idriss. Basi ndo kumjaza mwanae ujinga, si nilikwambia hawa watwana hawana maaana. La msingi nikuletee mke toka Oman, mtoto wa asili yetuuu. Mbishiiiii. Mzee Idriss anajitetea ujue mama huyu mke nilipewa na Mzee Justin, nilipokuja huku kutafuta alinifaa sana mambo mengi kibiashara, na nilipomuomba huyu bintie japo wakristu wale akakubali kunipa mwanae, na amekubali nimbadili dini. Sasa tukimtesa sanaa akaenda kumwambia baba yake, atamwambia arudi kwao. Hii jamba jamba nayompa hataorudia makosaa.

Yule bibi akawa anamlea mjukuu wake vizuri sanaa, akakuta mama mtu na mumewe wamempa jina la Sabra akalikataa bayaaa na kumpa yeye jina lake Iqra. Wakaridhia wote aitwe Iqra. Ndo kumfundisha sasa taratibu na swala zote za kiislamu. Malezi ya kiislam. Akibadilisha shuka, afanye vipi, asubuhi afanye vipi, darsa tosha. Sababu na yeye alikuwa anampenda mumewe kwa dhati akawa anakubali.

Mama Iqra alichelewa kuolewa, wadogo zake wakaolewa, akawa kakata tamaa kabisaa ya kuolewa. Sema alikuwa mtulivu sanaa nyumbani, baada ya kufikisha miaka 28 hajaolewa baba yao Mzee Lyamuya akaamua kumpeleka dukani Kariakoo kwenye maduka yake maana alisoma kidogo tu. Akawa anakaa dukani. Ndo kukutana na Idriss sasa akiwa anaenda kwa Lyamuya dukan. Idriss akawa anamuangalia yule binti akawa kamuelewa. Akawauliza watu wake wa karibu akaambiwa yule kafiri mchaga wa nini bwana, cha kufanya hapa wewe tukutafutie mke waarabu wa hapa hapa kariakoo, watoto wadogo yule kazeeka. Ikawa roho yake bado iko kule kule akampelelza mpaka akamjua katulia sanaa.

Basi akamwambia siku hio mi nataka kukuoa, sina mke nina miaka 33. Eliza akacheka sanaaa akajua Idriss anamzingua maana mwarabu handsome kama yule haiwezekani hana mke. Akamjoke tu mimi niko tayari kwa ndoa. Hahahaaa! Idriss akamfata Lyamuya kwa heshima na tadhima ana nia ya dhati kumuoa yule binti yake wa dukani. Lyamuya akamwambia ongea nae mwenyewe kama mkikubaliana sina shida. Idriss akamfata tena Eliza niko serious nataka kukuoa. Eliza akaendelea kukubali maana kweli shida ya mume anayo mnooo mnooo.

Lyamuya akaongea na padri ambae ni mdogo wake akamwambia usimpe mwarabu mke, toka lini wachaga wakaoana na waraabu? Kwanza wabaguzi afu wanyanyasaji wanawake na watambadilisha dini, usikubali. Akawa kapanga kwenda kumkatalia Idriss japo roho inamuuma maana Eliza angeolewa kule ingemfaa kibiashara, Idriss angemsamehe madeni yote, na mizigo angekuwa hanunui jumla anamuagiza Dubai moja kwa moja. Kikawa kinamsumbua kichwa akasema amwambie mkewe. Weeeeeeeeeee! Mkewe akaja juu Eliza kapata mume afu ananjishauri anachojishauri kitu gani? Weeeeeeeeeeeeeeee! Mama akasema ndoa itafungwa iwe isiwe. Lyamuya anadai dini mke wangu, mkewe anawasuta yule dada yenu mbona kaolewa na muislam? Ikawa mvutano mkali kati mke wa lyamuya na Padri. Lyamuya kati kati na intrest zake za kibiashara. Mwishowe ikaamuliwa ifungwe bomani

Mwarabu nae kufunga bomani ikatokea mvutano mkubwa sanaaa upande wake, kwamba itakuwaje mfungo. Funga yake itakuwa si halali na atakuwa anazini tu. Akaamua amuoe bomani hivo hivo potelea pote. Harusi ikafungwa ila ndugu zake wa Oman wakaisusia sababu anaoa mtwana afu kafiri. Maisha ya ndoa yakaanza bila kuzoeana, maana hawakudate hata. Eliza akaona Idriss ananyanyasika sababu yeye hajaslimu anakosa amani inabidi kila mda atumie nguvu na wajengezi wenzie waarabu wa kariakoo wakawa wanamtenga.

Akamwambia Idriss mi nimekubali kuslim, nifunge ndoa ya kiislamu na wewe, sababu sipo tena nyumbani hakuna wa kunizuia. Ndo akaitwa shehe wakamslimisha rasmi. Akaja Mzee Lyamuya kutoa mkono wa ndoa na kuwa karidhia mwanae aolewa , ubani ukachomwa pale wakaondoka nae. Akatiwa maji upyaaa, na kuwa mke rasmiii sasa.

Kimbembe dini haijui, na mambo mengi akawa mtu wa kushinda ndani kwake mda wote, mumewe akirudi ndo anapata nafuuu sasa na mtu wa kuongea. Akapata msichana wa kazi Zena, ndo anamfundisha dini kidogo kidogo. Kumfurahishs mumewe akawa anavaa majuba, nikabu, abaya, dash dash bila hata kuambiwa. Kiukweli mumewe alikuwa mtu mzuri sanaa. Wala hakuwahi kumnyanyasa chochote. Hela anachukua anavotaka. Akaboreka kukaa ndani akamwambia mumewe, mumewe akamwambia basi njoo dukani tukae wote.

Mwanzo akawa anavaa hijab tu, na abaya kubwaa, kubwaa, sasa mremboo sanaaa, afu mzuriii, wakija wateja wanadata nae, mda wmingine wanashoboka mbele hata mwarabu si hawajui kama mkewe. Mwarabu roho ikawa inamuuma wivu, Eliza mwenyewe akaanza kuvaa Nikab ya Ninja. Bado sauti na macho, mikono laioni ndo vikazidi kuwachanganya wateja wakawa wanataka kumuona sura sasa. Kuna siku mwarabu yuko upande wa pili, muhindi huku kapanda dau anatoa hela yoyote Eliza avue nikab. Mmmmh! Wale wauzaji wakawa wanamfuka kimya kimya ili bosi wao asijue. Mwarabu akajua akauliza mbona mnamfukuza mteja wakawa wanangaliana hawasemi, Eliza hasemi. Muhindi akasema mimi penda sanaaa Eliza, nakuja hapa taka sanaa ona Eliza naambia Eliza tampa pesa aoneshe sura yake, fanyakazi timua mimi. Wakaangaliana. Mwarabu akamuuliza wewe Eliza hujawahi kumuona umempendea nini? Muhindi anasema Eliza iko karimu sanaa, hudumia mimi zuri kabisaa, iko na sauti zuri, kono yake iko laini sanaa, hapana taka chezea Eliza, mimi taka oa Eliza. Akaona mwarabu kawa mwekundu muhindi akaondoka mwenyewe. Mwarabu siku nzima kanuna

Kesho Eliza kampikia chai mumewe, hajiandai, mwarabu akamuuliza huendi leo? Akasema naumwa. Hivo hivo zikapita wiki 2 kila siku anaumwa, baadae akamwambia nimeamua kupumzika Dukani niwe nakaa tu hapa nyumbani wateja wakorofi wanakuuzi nakugombanisha na wateja na kukufukuzia biashara. Basi mwarabu akafurahi manake kweli ilikuwa inamuuma ila akawa ahataki kumuuzi mkewe, na kingine bora akae ndani afikirie jinsi ya kupata mtoto. Basi siku zikawa zinaenda wale wajengezi wenzie wakamuona hana neno, wakaanza kumzoea.

Akawa hashiki mimba, ikabidi na mumewe waende kwa Dr. Basi Idriss akaingizia hilo la mtoto wa kiume. Dr akawapima akawaambia wote wako okay. Sasa Idriss kadri siku zinavoenda ndo anazidisha wivu anakuwa kama mjinga sasa. Akawa anakuwa mkali bila sababu. Kitu kidogo anagombaaa sanaa. Anamfokeaaa. Anahisi hisi Eliza anachepuka ila ndo haelewi kivipi na nani. Wivuuu. Ndo akaona awe mkali ili kumtishaa kama ana mpango huo.

Eliza akaamua maisha yale hayawezi, kama vipi arudi kwao. Akawa anajiandaa kumuomba talaka zake arudi kwao. Kila akisema anamuomba leo ana ahirisha, akirudi hamuombi ila ndo hana amani wala raha. Siku hio akajikaza kisabuni akamwambia Idriss, mi naona siku hizi umekuwa mkali sanaa,unanigomba gomba, upendo sio kama zamani. Kabla hajamaliza Idriss akamshushua acha mambo ya kipuuzi kwa hio ulitaka ukikosea nisikuulize? Acha kudeka wewe.

Eliza akawa kashaamua leo ndo leo, akamwambia sawa, nimeona hio yote labda kwa vile sizai ndo maana, mimi naomba talaka zangu nirudi nyumbani, uoe mwanamke mwingine anae zaa. Idriss akastukaa kwanza hakutegemea hilo swalaa. Akapanic sanaa. Akaanza kumtisha sasa, sikia mimi najua kuoa tu sijui kuacha, talaka sikupi wala nini, tena usijaribu kunitoroka, nitakutafuta nakuua afu na mimi najiua. Akaonge mambo mengi sanaa yasiyo na tija na mengi ni vitisho kwa Eliza. Eliza akaanza kuiona ndoa chungu.

Ikawa Idriss akamstopisha mdada wa kazi kesho yake asije tenaa, na akawa akiondoka anafunga mlango kwa nje, anamfungia Eliza ndani kama mfungwa akaiweka na komeo kabisaa. Majirani wakimuuliza anasema mke wangu ana mashetani siwezi kumuacha hivi hivi atawasumbueni mkimsikia anapiga kelele achaneni nae au niiteni dukani. Cha ajabu Eliza hakuwahi kupiga kelele wala kuita.

Chakula nguo, mafuta kila kitu anamleta ndani humo humo, mwenyewe. Ila nae Idriss akawa hana amani kabisaaa kama kitu kimemkaba kooni anampenda mkewe sanaa, na hawezi kufikiria akiondoka itakuwaje ila sasa wivuuu na ukorofi hawezi kujizuia. Hali ya ndoa yake ilikuwa sio nzuri maana mkewe ikawa miezi kama 2 kamuweka mateka. Siku hio akatafakariii akaamua kama vipi bora amuche aende kwao, ikiwa anampenda basi arudi mwenyewe na akaamua atakuwa mpole kwa mkewe.

Akarudi siku hio akayatupa yale makufuli, akamwambia mimi nimeona niruhusu tu kama umeamua kuondoka uende tu, ila mimi mumeo nakupenda sanaa. Kuanzia kesho sikufungiii tena nje. Kesho yake akawahi kufungua duka akaja kubana chini ya ghorofa ili amuone mkewe atakavokuwa anaondoka kwenda kwao. Mpaka jioni hajashuka, akaenda kufunga akarudi akajua kaghairi kuondoka. Akafurahiii.

Kesho kaenda kazini na amani zote, saa 4 ikaletwa funguo na kijana jirani yao, Eliza kaondoka roho ikamfanya paaaah! Akachanganyikiwa. Kurudi ndani pakubwaa. Akadataaaa. Akawa kakaa analia tu. Huku Eliza kafika mpaka kwao Ubungo anaiona nyumba yao ile roho ikawa nzitooo. Akajitafakari hivi kweli nimeondoka kwa mume wangu? Akaa kaa kwanza bar, watu wanamshangaa na majuba yake. Akakaa mpaka ikafika saa 1 usiku. Nguvu ya kuingia kwao akaikosaa. Akaamua kugeuza kariakoo saa 2 hio kwa mumewe.

Kafika saa 2 ile na begi lake akakuta mlango wazi, akaingia ndani na kumkuta mume analia, baba zima. Akakohoa. Mumewe kumuona karudi akajikausha machozi kimyaa kama si yeye. Akaingiza begi lake ndani, katundika nguo zake kabatini, akaanza kupika. Wakawa wanakula kimya kimya hamna anaesema neno. Idriss akashindwa kuvumilia akamuuliza kwa hio huondiki tena au? Eliza akamjibu itategemea, ukianza kuninyanyasa tena naondoka. Wakacheka wote na the ice was broken.

Asubuhi akamwambia Eliza jiandae, Eliza akauliza kwenda wapi? Idriss akamwambia dukani. Eliza akamjoke kwa hio una mashaka nikibakia hutonikuta au? Idriss akamwambia ndiooo. Sahivi mguu kwa mguu. Wakacheka. Akajiandaa, akapelekwa duka lingine la jumla, Idriss akamwambia nakuamini Eliza sahivi utakuwa huku mimi kule kuonana mara chache chache. Eliza akacheka manake anamjua Idriss kwa wivu sio kidogo. Saa 4 mbali Idriss huyu hapa tukanywe chai. Saa 7 huyu hapa tukale cha mchana. Yani akawa hatulii dukani kwake. Ndo ikawa maisha ya kila siku.

Eliza akanenepa na kuwa mvivuuu. Siku hio mdada wa dukani akamwambia Eliza una mimba kubwaaa! Eliza akamwambia mwenyewe nahisi ila naogopa kumwambia Idriss kama sio je? Siku Eliza akanguka dukani wakamkimbiza hospitali ndo kuonekana ana mimba kubwa afu hana damu. Wacha Idriss afurahi. Akawa anakaa nyumbani akatafuta na nesi wa kumuangalia. Maongezi yote mtoto wa kumee mtoto wa kiumee. Akamnunulia kila kitu si ndo akatoka wa kike balaaaa!

Mama mkwe kuja akamletea Eliza mwalimu wa madrassa nyumbani ajifunze dini, na hilo jina la Eliza akawa hataki mtu amuite hivo anataka jina la kiislamu Samiah alilopewa alipo slimu. Mtoto ana miezi tu akawa ana mimba ingine tayari. Mama mkwe akaanza kupata shaka uzazi unaweza kuwa mgumu maana afya ahajairudisha vizuriii. Wakawa wanasikilizia na kumuweka chini ya uangalizi.

Siku ya kujifngua uzazi ukawa mgumu ikatokea comlication, mama akawa hana nguvu za kusukuma ikabidi wamvute mtoto na zibulio. Mama akapoteza damu nyingi hali yake ikawa mbaya sanaa, mtoto alikuwa wa kiume. Baada ya siku mbili Eliza akafariki. Akaacha watoto wa 2 wadogo sanaa. Mmoja hajafunga mwaka, mwingine ana siku kadhaa. Ikawa mziba mzitooo. Mwarabu akachanganyikiwa. Akajuuta kumsakama mkewe na mtoto wa kiume. Matokeo yake kampa ila mke ndo basi tenaa. Mama mtu pia akachanganyikiwa.

ITAENDELEA!!!!
 
Duuu aya hongera Lara moko story tamu nataman uendelee tu japo naisi ako katoto ka kike ka Eliza ndo kalisababisha Jana mtu kutenguliwa mbavu mbili
 
1982 London!

Mumyyyy! My Son! Wakakumbatianaaa. Koku jinsi unavomlea huyu collins mi sipendi kabisaaaa. Toka lini mtoto wa kiume akalelewa kama mtoto wa mama. Mi sipendi ujueeee sipendi kabisaaa.

Mjungu acha stress bwanaa, huyu mtoto tu, huu upendo kwa mama yake utaisha akikua, mbona Carina anakupenda sanaa baba yake husemiii. Hawa watoto usisiwafikirie mbali. Wakikua hapa wakatukimbia tutabakia mimi na wewe tu tumedodaaa. Wakachekaaa.

Collins anampenda mama yake mda wote yuko na mama yake tu. Unashinda nae jikoni kupika, na kuosha vyombo. Usafi ndani anamsaidia. Mda unaobakia anajisomea vitabu au kutazama tv. Ni mtu mwenye aibu sanaaa

Carina dada yake ni binti mjanja mjanja, social, itokee party gani hapo london za wazungu ila Carina anaalikwa. Shule wanamjua Carina ni nani. Haogopiii ana confidence. Anajiaminii. Very social. Mda wa kufanya chochote ndani hanaaa. Anamtegemea Collins amfanyie. Na Collins anampenda sanaa mdogo wake basi anamfanyia tu.

Koku akashukuru kweli kuwa na mtoto kama Collins manake akawa hachoki kabisaa, na akaweza kufanya kazi 2. Manake Collins akitoka shule anafanya kila kitu mpaka unashangaa kama kweli ndo kwanza ana miaka 9. Sio mzito, sio jeuri mpaka unamwambia Collins pumzikaaa.

Shule napo anajitahidi, anafauluuu sanaaa, mpaka walimu wanampenda, anapataga awards nyingi sanaa. Pia shule ni mwana michezo mzuri sanaaa. Yupo kwenye riadha, football, swimming. Inshort alikuwa very active uwanjani.

Pia anasali sanaa, mtu wa ibada sanaa, anaimba kwaya. Yani mama mtu alikuwa anajivunia kuwa na mtoto kama Collins kwakweli. Hakuona sehemu yoyote anayomuangusha labda aibu zake na kuogopa watu.

Mpaka akichelewa anakuta kapika. Sio wa kumwambia Collins fanyaa hivi, anafanya mwenyewe. Na anafanya mpaka unaridhikaaa. Inafika mahali unamuamuru nimesema pumzikaaa utajiumiza sasa.

Kilichomsumbua ni upendo wake wa kupitiliza akawa ana mashaka kama ata cope kweli kdunia hii iliojaa watu wabaya, viumbe wazitooo. Maana Carina mwenyewe anamuendeshaa sio kidogo. Collin ni wajibu wake kumfanyia kila kitu mpaka home work mda mwingine.

Shuleni wakaanza kumbully mamas boy, manake mchana hataki kutoka ile kwenda kuhanga out na wenzie wa darasani kwenye makundi makundi anakaa tu kwao akifanya kazi za ndani. Na mda mwingi ukimuona katoka iwe for shopping au kanisani basi yupo na mama yake pembeni.

Collins anashangaa kwanini wanaona kuwa close na mama kitu cha ajabu wakati yeye anampenda mama yake to bits. Anaona sifa kwanza kuwa na mama yake. Akawa anapuuzia tu. Wale watukutu kila wakitaka kumvuta kwenye makundi yao Collins anagomaaa. Yeye shule, Mungu na mama yake baasi.

Wakawa hawaelewani kabisaa na baba yake, Mzee Mjungu mkorofi sanaa, afu muhuni basi wakigombana na mama yao, anakimbilia kumpigaa, Collins anaingia kumgombelezea mama yake kitendo kinachomkeraaa sanaa baba yake. Na kufanya amchukie tu huyu mtoto bila sababu.

Kuna siku Collins akamwambia mwalimu wao kuwa baba yao anawapigaga sanaa yeye na mama yake, mwalaimu akareport social workers wakawajia nyumbani na polisi. Ikabidi mama mtu akatae kata kata kuwa sio kweli na wao ni one big happy family sema Collins ni muongo. Wakamuuliza Carina, mama yake akawa kamkonyeza akawaambia sio kweli na Collins ni muongo na delusional. Polisi wakamuamini Carina ila mwalimu hakuwa convised.

Polisi walivoondoka Mjungu akavua mkanda akata kumtandika Collins, Collins akamwambia ukinipiga naenda polis tena. I am not afraid of you anamuangalia machoni. I aint scared of you at all. You can bully mom because she loves she wont report you, touch me and ill see you are depirted, i know the laws of this country. Mama yake anamnyamazishaa Collins, Mzee Mjungu akatoka nje kwa hasira hakurudi siki 3. Mzee Mjungu akazidi kumchukia Collins.

Mama yake akaanza kumlaumu Collins kwanini hana heshima, pamoja na yote yule ni baba yao anatakiwa amuheshimu no matter what. Anamueleza they should be glad they have a father providing for them, hata kama he is not perfect atleast he is there for them, analipa ada, anahakikisha wanakaa neighbour hood nzuri, wana mahitaji yote. Watu wengine wametlekezwa Tanzania na baba zao. Wengine hawana baba wanalelewa na single mothers. Even if he is violent inachotakiwa amuombee Mungu abadilike.

As years went by they grew apart more and more. Mjungu hampendi Collins, Collins hampendi baba yake. Hata baba yake akijitahidi kuwafanyia kitu kizuri walaaa hajamshawishi. Ikafika stage baba yake akawa anampenda Carina tu. Atamlipia camping sijui nini bila kumuomba Collins atamwambia mama yake, Mjungu atasema akitaka aniombe mwenyewe. Collins haombi ngooo na Mjungu hampi hio hela.

Anamwambia mama yake when i grow up i will take you away from this monster. Mama yake anamwambia careful what you call your father son. Moyoni akawa anajisemea i have no father. Never had one.

The more anavokua the more he despised his father na kujiapisha kuwa tofauti kabisaaa na yule mzee wa msoma. Yani just because baba yake anapenda kucheza darts, horse race, chase, na michezo kama hio akaichukia tuuu moja kwa moja simply becuase baba yake anaipenda.

Sometimes mzee mjungu anatamani waelewane na mwanae anajitahidi kuimprove relations anamwambia son can i come to watch you play ball this weekend, Collins atamjibu tu i wont be playing. Kuna siku akaenda bila kumtaarifu alivomuona akajifanya kateguka mguu ili awe substituted basi tu mzee wake asimuone akicheza.

Siku ingine mzee anamwambia son i hear you will be singing lead on Sunday i will be there to support you and all, as your pops it is my duty, dont let me down boy, commin with with my friends to show them my boy, proud pops. Jumapili akajifanya anaharisha mradi tu asiende kuimbaa kanisani. Baba yake akamwambia tu Why do you hate me so much son? I am trying you know?

Mjungu akajitahidi kuwaenroll yeye na Collins kwenye councelling akitegemea itasaidia wapiiii.Akachoka akajionea kuwa mwanae hampendiiii. Koku kajitahidii kuwasuluhisha kashindwaaa. Maana Collin akianza kuamini Mjungu kabadilika hakawii kuwa mkorofi na kumpiga na akishampiga Collins baaaas anajua hajabadilika chohote.

Collins akawa anajitahidi kuwa close na mama yake kumfariji akiamini kuwa ile gap ya baba mtu ataiziba yeye, hata akishindwa kuiziba yote walau kwa uwezo wake.

ITAENDELEA SAA 4 NA NUSU USIKU.
 
Back
Top Bottom