Weekend Story: You Can't Handle The Truth

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,160
Igwèeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!

Hivi kweli nyie watu wa kunidharau mimi na kuniita nimefulia sina jipya na story nilibahatisha? Kweliiii! Hahahaaaaaa! Eti kwenye fani ya story nabahatisha!!!? Sasa nimerudi kutoa story moja kaliiiii tuheshimiane humu ndani. Kama kawaida sibahatishi, sikurupuki, sijaribu nikifanya nafanyaaaaa kweli!

DUDE HILO SAA 5 KAMILI USIKU HUU INA PREMIER HAPA JF! Kama kawaida yangu sirudiii chochoteeee. Msikose na mpeane taarifa story addicts kuwa Igwe nisharudi kilingeni kufanya yangu.

SAA 5 USIKU.
 
Welcome back. Nilikumiss hadi naumwa. Nilitaka kulala muda huu nimeghairi. Hadi nisome stori.
 
1982 ARUSHA

Sikia mwanangu, nisikilize vizuri, mimi baba yako unanijua ni mlevi hapa kijijini sanaa, sina heshima yoyote zaidi ya kujulikana kama mlevi wa kijiji. Mimi sikuwa mlevi, wala pombe sikuwahi kuonja, ila walimwengu mwanangu ndo wamesababisha niwe hivi. We bado mdogo kuelewa kwa nini mimi ni mlevi, kwanini niko hivi, kwanini mke wangu mama yako yuko na mimi pamoja na yote nayomfanyia.

Nikilewa nasikia nakuwa sio mtu mzuri, nimempiga mke wangu na kumngoa meno yote ya mbele, nimemfanyia ukatili mkubwa sanaa, nikishapata nakuwa sijielewi nikizinduka nakujua niliofanya nashindwa kuvumilia nakimbilia kupata tena. Wewe mwanangu you saw me in action navompiga mama yako, navokupiga na wewe, navofanya fujo.

Nasikitika mwanangu umezaliwa katika kipindi cha my demise, na unafata mfano mbaya kutoka kwangu. Atleast mimi niliharibu maisha yangu mwenyewe ila wewe unaharibu maisha yako kuni impress baba yako. Juzi nilikuona unampiga yule msichana binti wa Masai ni aibu kwa mwanaume kumpiga mwanamke yoyote vile hususani ukiwa hujalewa. Pale ndipo nilipojua nimefanya makosa makubwaa sanaa kwenye malezi na nikizembea i will raise a monster.

Kabla hujaondoka nataka utambue baba yako ni mtu wa aina gani. Kalete mfuko mwekundu kwenye sanduku. Walter akaenda akiwaz njiani dingi aje mbona anazingua kaya, afu akakumbuka kabla hujaondoka akawaza hajaondoka kwenda wapi? Akawa haelewi. Huo mfuko anaujua una biblia so huwa hana mzuka nao sanaa. Akauchukua.

Mzee cha pombe akaufungua akatoa ile bible, kati kati akatoa picha 4. Moja yake akiwa kijana kavaa joho, ya pili akiwa kijana kavaa combat za jeshi, ya 3 ya harusi na ya 4 akiwa darasani anafundisha. Kama sio yeye. Akaelewa kwanini cha pombe akilewa anaongea English mwanzo mwisho. Akawa kazishika picha hizo bado anamsikiliza.

Walter ukiwa mkubwa kwa mda wako utatafuta nini kilinikuta baba yako mpaka nikawa mlevi, na kuja kuishi huku uswahilini. Mimi kama mimi nilitegemea nitapata nguvu za kukwambia ila nimekosa, lakini watu wapo wanaofahamu watakwambia tu. Sitaki uyatilie maanani sanaa haya ila pia si vema uyasahau. Picha hizo nakukabidhi , nasikitika sina vingi vya kukupa, ila unisikilize.

As a father i failed you my only son, i failed my wife, i failed myself, i am a failure. Baba yako ni failure. Sitaki uwe failure kama mimi, nasikitika nimekujengea msingi mbovu ila sijakukatia tamaa. Umefeli primary sina uwezo wa kukuendeleza ila sitaki uishi bila kusoma maana mimi wazazi wangu walinisomesha mpaka chuo, umeona ni graduate baba yako.

Mke wangu ana mdogo wake kule Dodoma ana vihela hela anafanya shughuli za Garage yule mjomba wako Jiles. Sasa yule hana mtoto mkewe hazai, wamehangaika sanaa, mjomba wako nae kahangaika kwingine nje ya ndoa ila hajapata kitu na anafadhaika sanaaa. Nimekaa nimetafakari nikaamua nikugawe uwe mtoto wake. Mwanzo alikataa, ila nimemuelwesha na amekubali.

Kikubwa usifikiri labda nimekugawa nipate hela ya pombe hataaaa, ila nimeona sina maisha ya kukupa, sina hata jina la kukupa, jina langu cha pombe, sifa zangu mbaya, katika maisha hutokuwa mtu wala hutofika mahali watakubagua mtoto wa mlevi mtoto wa mlevi sasa hili swala hata nilewe vipi bado linanisumbua kichwa.

Utapelekwa Dodoma na mjomba wako Wille, ukifika kule ndo kwenu, wale ndo baba zako, mama zako, jina watakubadilisha, chochote utachoambiwa fata, huku usirudi tenaa, rafiki zako utakao waaga waage jumlaaa. Sitaki mbeleni uje uhusishwe na maisha ya hapa kwa namna yoyote ile. Wewe utakuwa Walter Jiles, umezaliwa huko huko Dodoma, ni kwa manufaa yako. Ukiondoka usimuage mama yako, hatoweza kuvumilia. Mila zote tushamaliza, mbuzi kila kitu cha kukuuza ukoo kimekamilika. Haya kajiandae na safari mi naenda kilabuni.

Walter siku ikawa nzito sanaa, akajawa na mawazo mengi sanaa, hata michezo akawa hana hamu nayo. Akawa anakaa karibu na mama yake mda wote. Mama yake akamshangaaa sanaa. Jioni mjomba Wille akaja kweli mama mtu akawa hana hili wala lile. Usiku Wlater akapaki begi, wakalala sebuleni na mjomba Wille. Saa 10, baba yao akawaamsha wachimbe kimya kimya.

Wakaenda mjini wakazurura, Wille akanunu alivotaka kununua usiku wake sasa wakapanda treni kuelekea Dodoma sasa. Njiani Walter akamuuliza Uncle Wille kwanini baba yangu yuko vile? Wille akataka kusema kitu akaghairi njiani. Wlater akazidi kumuuliza. Wille akawa anapotezea hio mda juu kwa juu. Walter akachoka.

Wakafika Dodoma kumbe mjinii. Akapokelewa vizuri tu. Akakumbuka wosia wale ndo baba yake na mama yake. Akaanza kuwaita tu mama na baba from day 1. Kiukweli walikuwa watu wazuri sanaa sanaa tofauti na alivokuwa katarajia. Maisha mazuri anakula anachotaka, shangazi yake anampenda sanaaa, sanaaa. Anapendwa kama mtoto wa pale. Shangazi yake akamtafutia shule nzuriii sanaa ya kurudia la 6 ili afaulu sekondari. Hafanyi kazi yoyote. Mjomba wake akawa anamfundisha mambo ya Garage akiwa hana issue anayofanya. Kiukweli akayapenda maisha ya Dodoma kuliko kwao.

Akapata marafiki wapya wakamjua yeye Walter, mtoto wa kishua, mjomba wake ana magari, maisha bora. Ikawa akikumbuka kwao kunamnyima raha kabisaa, ila akawa anapakumbuka mara chache chache sanaa kadri siku zinavoenda. Akamaliza primary akapasi Sekondari boarding akawa anasoma Mazengo Secondary.

Tatizo la Wlater lilikuwa ni temper, hawezi kujizuia hasiraaa. Akikasirika anabutuaa mtu yoyote alie mbele zake, na anakuwa na nguvu za ajabu. Ashasimamishwa shule sanaaa, ashawekwa mpaka ndani kupiganaa na ugomvii. Yani shangazi yake alihangaika sanaa kumbadilisha kwenye hilo ikashindikanaaa. Akawa tu anamshauri Walter usiwe mgomvi, kuwa unaji control wapiiii.

Akiwa form 3 shangazi yake akabeba mimba. Basi anaogopa utasema sijui nini. Mungu mwema akajifungua mtoto wa kiume na yeye akamuita Wayne. Ila Walter akawa anampenda kama zamani. Sasa Wlater ashakuwa muhuniii, shule hapendi, vigenge vigenge, makundi makundi , kupiganaa ndo raha yake bila hata sababu. Akawa mbabe Dodoma nzimaaa.

Disco Walter akicheza marufuku kukanyaga kivuli chake. Yani mnacheza kwa uangalifu ukikanyaga kivuli cha Walter utakula ngumi mpaka utie akili. Akimtaka demu wako muachie, ama sivo mtapigwa wote. Akawa mkoraaa haina mfano. Mpaka watu wazima wanamuogopa Walter. Ashapiga watu mpaka wakalazwa. Polisi wenyewe wakija kumkamata wawe wengi lasivo anawapiga sio kidogo. Na akiwekwa ndani mjomba wake anaenda kumtoa siku hio hio. Watu wakawa wamemchoka.

Athari ingine ni ukatili wa kijinsia, akajikuta ni mtu wa kunyanyasa wanawake bila sababu. Asisikie mwanamke flani shule flani ni mzuri atamfata na kumuintimidate mpaka awe demu wake, na akiwa demu wake siku 2 atamchoka kitachofata ni kumtesaaa tu huyo dada mpaka atie akili. Na mwanamke akimzingua nae anakula kichapo. Akajikuta kamaliza mademu wote wa Dodoma wle wazuri wazuri.

Kuna siku kalala ndani akaja kuamshwa kuna demu mkali Disco, katoka Dsm yuko na mwarabu, demu nae kama mburushi hivi, kisuuuu cha hatariiii. Wlater akachanganyikiwa hata hajamuona huyo demu. Akatoka mkuku mpaka Disco. Kweli demu yupo, kumuona hivi moyo wake ukayeyukaa, ile hamu yake ikamjaa akajiapiza lazima ampate yule demu iwe isiwe.

Akanza kuleta ubabe watu walivomuona tu wakaja tayariiii. Dada wa kiburushi anacheza mwenyewe dancing floor, warabu wake wa 2 wamekaa wanakunywa. Walter akamfikia anafosi kudance nae. Demu akagoma. Wlater akamvuta kibabe sasa yeye si ndo Walter nani asiemjua mjini hapo.

Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Wale waarabu wakamuona, wakaja kumzunguka. Walter akaona rahisi sana kumbe hao waburushi ni wababe wa Iringa na Dar kina Cool 9 na kaka yake. Van Dame wa bongo hii, wanakipiga sio kidogooo. Walter alipigwaaa, kapigwaaaa, kapigwaaaa, mpaka mwenye ukumbi akaingilia akawaambia jamani BAAAAAAAAAAAAAAAAAASSS! Mwacheni. Wenzie kumpeleka kwao ikabidi kukimbizwa hospitali mbavu 2 zimeteguka akalazwa kama wiki 2.

Shangazi akamwambia Walter usipobadilika tena basiiii.

ITAENDELEA KESHO (INAENDELEA USIKU HUU MWENDO WA KOBE)
 
Back
Top Bottom