Weekend Story! Ugly Benny! (Get Rich Or Die Trying)

Weekend Story! Ugly Benny! (Get Rich Or Die Trying)

Muddy!

Muddy asili yake ni mmakonde wale walichanganya na waarabu, na siku zote hakupenda kuwa wa 2 katika maisha yake. Siku zote shuleni alikuwa wa kwanza, nyumbani alikuwa kinara ukimlinganisha na ndugu zake, msikitini pia alikuwa moja ya vijana wanao heshimika sanaaa. All he wanted in this life is to be the winner of everything and win everything at any cost.

Huko kwao Mtwara aliahirisha kwenda kumzika baba yake mzazi ili tu akafanye mtihani wa darasa la saba, kupelekea maziko kuchelewa tofauti na dini ya Kiislamu inavoagiza, na alikuwa wa kwanza wilayani kwake na kimkoa. Mashindano ya Quoran siku zote alikuwa anakuwa wa kwanza kitaifa mpaka kupata mialiko Misri, Saudi, Oman, Yemen. Kiumri alikuwa mdogo ila alishatembea nchi nyingii mnooo.

His desire to win and conquer was unsurpassed. He just had to win in everything and anything. Hapo shuleni alimtaka Irene leo kesho, kesho kutwa sababu tu ndo alikuwa chaguo namba 1 kwa wanaume wote wa Mwenge Secondary School. Kwasababu yeye Muddy alikuwa namba moja kimasomo, na ndio kaka mkuu wa shule hio aliamini Irene alikuwa ni haki yake kabisaaa, na hakustahili awe na mbweha yoyote. Siku zote alimuhesabia 2 Pack ndo mpinzani wake mkuu kwenye suala la kumpa Irene, na 2Pac hakuwa mwepesi, hivo alihitaji akili nyingi kumfukuzisha shule 2Pac ili yeye Muddy apate chance la kuwa na Irene.

Na mpango wake aliusuka mda mrefu, kwa utaalamu wa hali ya juu, na kuhakikisha ungefanikiwa kumngoa 2 Pac kabisaaa. Akijua 2 Pac ni mtu wa matumizi makubwa ya pesaa, akampa dili la kusafirisha bangi hio mpaka kibaoni ambapo Muddy alishaenda kureport kituo cha polisi Kibaoni kuna mtandao wa kusafirisha bangi mbichi, na bangi mtuhumiwa anayo, anaenda kuiza Kibaoni nyumba ya 4. Akitumia mwavuli wake wa kaka mkuu,na dini kujifanya anawajali wanafunzi wenzie.

Kilichoharibu dili ni Irene kuingiwa na woga wa mpenziwe kuifanya hio kazi hatari, na ndipo Irene pasipo Muddy kujua, akamshauri 2 Pac kazi hio wambabatize Benny sababu ni mdhaifu kwa Irene. 2 Pac akaona sawa tu as long as he gets to keep the money. Muddy alivowaona Benny na Irene akawa anamtafutia dawa nyingine Benny maanake alikuwa kama kupe mvamizi wa ghafla ila hakutegemea vinaingiliana na mpango wake na 2 Pack.

Kimbembe begi lilivotaitiwa na mlinzi, ikabidi Muddy aje na huo mpango kabambeee wa kujiokoa yeye binafsi manake kesi ingeishia kwake, lazima 2Pack na Irene wangemtaja kwa vyovyote ikabidi ndo kuwashawishi kama vipi wampakazie Benny. Na sababu Benny kweli aliingia na bag hilo shule, akaonekana, na akawaulizia kina Irene kwa watu kadhaa haikuwa kesi, ila bado kesi ingepelekwa polisi, na majirani wa Ben wangetoa ushahidi kumuona Irene akiingia kwa Benny na bag hilo. Kuziima jitihada zozote za swala hili kupelekwa polisi akawapanga kina 2Pack wampakazie tuhuma za Ushoga, ambapo ingemlazimu mkuu wa shule kutatua ishu kimya kimya isifike gazetini, na hivo asingeweza kwenda polisi na ngepeleka kesi mpera mperaaaa kuzima scandal ya ushoga shuleni kwake.

Tofauti na matarajio yake kidogo ni wao kupewa hio suspension ya miezi miwili, na yeye kuvuliwa u head boy rasmi kwakushindwa kureport vitendo vya Benny kabla. Moyoni alikuwa hajakata tamaa juu ya kumpata mrembo Irene kwa gharama yoyote ile, ili aweze tu, kuituliza kiu yake ya ushindi. Akapanga akirejea shule tena atashindanaa kama kawaida na atatafuta plan jipya la kumtoa 2 Pac na kummiliki Irene yeye peke yake.


IRENE.
Irene alizaliwa kijini babati, akiwa na baba mgogo na mama muhehe wakijihusisha na biashara za maduka. Baba Irene alikuwa mtu wa kusafiri sanaa, na mtu wa ubusy mwingii, huku mkewe akiwa mtu wa kukaa nyumbani tu na kulea familia. Mzee brown alikuwa tayari ana wavulana wa 3, na hivo kupoteza matumaini kabisa ya kupata kijike.

Baadae mama Irene inavosemekana alianza habari za kushinda kanisani, na chini ya kapeti zikadai akapata padri wa kimbulu, akawa wanachepuka kiutu uzimaa, akapata mimba ya Irene. Mimba ikaleta sintofahamu kubwaa, huku mumewe akisubiri mtoto azaliwe ndo atoe maamuzi ya mwishooo, kama ana muacha mkewe au vipi.

Baada ya mkewe kujifungua, Dr akamuita chembaa, Bw. Brown kiukweli katoto umepata kakike, sio kako kabisaa kwa kukiangalia tu, ila ni mtoto mzuriiii, yaani mimi nazalisha hapa miaka 10, yule binti ni mzuriii, ni kamgodi kaleeee, kakikua ukakapeleka shule na nini, kanaweza kuwa ka Mary Nagu kenginee. Mimi ningekuwa ni wewe ningejikaushaa tu. Bw. Brown akaingia kukaona katoto. Akakubali kweli kazuri, akamwambia mkewe turudi nyumbaniii.

Kila mtu alikubali kale katoto ni kazuriii, dalili mbaya zilianzaa mapemaaa, akiwa darasa la 4, Mr. Brown alimfuma Irene akitongozwa na mwanaume mkulima tu wa hapo Babati, akampasua pua, na kumtukana yeye ni mbwa tu wa kijijini hapo Irene sio hadi yake kabisaaa. Tena akomeee, na awaambie mbwa wenzie, Irene ni special kwa watu wa darisalaamu.

Akiwa darasa la 5, Mr. Brown alimshikia mwalimu wa Hisabati Panga, almanusura kumchinja kama kuku, sababu alikuwa anatengeneza mazingira hatarishi kwa binti yake, na mbwa tu, mwalimu wa kijijini sio size ya Irene. Ana mipango mikubwaa na binti yake huyoo. Ikawa kesi nzito sanaaa kijijinii akatakiwa na mkuu wa shule amuombe radhi mwalimu huyo ili Irene aendelee na masomo. Kuonesha hana matani na msimamo wake akampeleka Irene Arusha mjini kumalizia elimu ya msingi kwa dada yake, alie olewa hapo mjini Arusha. Na akampiga marufuku Irene kurudi kijijini Babati kwa sababu yoyote ile.

Akiwa Arusha mpaka Mwenge Sekondari, she always got the best boys in school. Kila mtu alipenda kuwa rafiki yake, na maisha aliyapata kirahisiiii, alisaidiwa homework, alifundishwa extra hours buree, na karibia kila mtu alikuwa anamtaka kimapenzii. Si walimu, majirani, ndugu, marafiki, mpaka mchungaji wa kanisani kwao ashawahi kumtongozaa. Sababu watongozaji ni wengi, alikula vingi mnooo. Hakuwahi kupata shidaaa kabisaaa.

Hapo Mwenge, alivofikaa tu, aksikia 2 Pac, 2Pac, ndo sukari ya waremboo, amefanana na 2 Pack kabisaaa, anavaa na zile scarf za 2 Pack. They are rolling big! Hapendi mademu, yeye mtu wa bangi tu sanaa. Unaambiwa mpaka hio form 3 hanaa demu kabisaaa. Irene akawa kajiwazia tu okay yawezekanaaa.

Basi siku hio Mwenge Sekondari kulikuwa na mpiraaa. Kwenda kwa mara ya kwanza uwanjani akamuona Muddy, mwarabu wa kuibiaaa, akiwa anamshangaa Muddy akasikia 2 Pack yulee, mmemuona ndo yulee, oooh my! Form 1 wenzie wanachachawa na 2 Pack na crew yake. Akamuangalia 2Pack akajikuta amenasa kwanzaaa kwenye kumuangalia. Jamani 2 Pack alikuwa mtamuuuu. Ilimchukua daikka kadhaa kuacha kukodoa, na kuendelea na mambo mengine bado alikuwa anamuibia 2Pac jichooo.

Ofcourse Muddy alikuwa anacheza, na ndo captain wa timu yao, 2 Pack mpambe tu, anaangalia mpira busy being cool, na WALK MAN (Wazee wenzangu hiki kitu mtakikumbukaa) yake, listening to RNB and Shit. Irene akawa anakodoa tu macho, ule ugeni bado hawajamjua vizuri yeye nani na anatokea wapi. Mpira ukaisha wakarudi mabwenini.

Mda wa mercy akagongana na Muddy, Muddy akamwambi we ni form 1, mbona sijawahi kukuona? Irene akasema ndio mimi ni form 1, BTW nice ball you played back then. Basi Muddy misifa kibaooo. Aaah Kawaida tuuu. Irene akamwambia na mimi nacheza ujue, nacheza sanaa Netball na Volleyball actually since STD 5 lazima niwepo timu ya UMITASHUNTA (Hii mpaka uwe kizee ndo utaikumbuka ni ligi ya taifa ya shule za msingi ya michezo mbalimbali) and im looking to play in UMISETA if i get a chance to practice here. Muddy akazidi kuhamasika huyu njukaa. Akamwambia tu kiukweli timu ya hapa ya Netball wanacheza mishangingi iliokubuhuuu, wanvaa tu tight na top, na ilivo mibonge sasa, mijimama ya form 4 hukooo, sidhani kama utapata namba. Sitaki kukuvunja moyo maybe uanzishe volleyball manake hamna timu. Irene akajiambia moyoni lazima acheze hio hio netball na mishangingi. Wakaachana na Muddy akaendela na business zake.

Katika kuulizia namba kwenye netball akakosaa, kama alivoambiwa na Muddy, yako mi jimama, ndo inamiliki netball hapo Mwenge Sec. Hakutaka kushindwa akaenda kwa mwalimu, akamwambia alicheza UTASHUNTA sanaa, mwalimu akamwambia subiri ikitokea nafasi nitakujaribuuu, you will get one and only one chance to prove your self. Irene akawa wakifanya mazoezi nae anafanya jpo hana namba na kma hwamuoni hapo uwanjanii. Basi akiwa anakimbia kuzunguka uwanja, Muddy nae anakuja kukimbia nae, anaacha kukimbia na wenzie kule wanaume anakimbia na Irene.

Muddy akavunja ukimya kuwa anamtaka Irene kimapenziii, hataki baadae aje aambiwe nilijua rafiki yangu, sijui nini, yeye anamtaka Irene leo kesho ila kimapenzi awe mtu wake. Alikuwa na mtu hapo shuleni ila wamemwaganaa kwa sababu zao binafsi tangu mwaka jana kati kati. Irene akamwambia nitakujibu maana Muddy sio mbaya pia, ila hakutaka kukurupuka kabla hajausoma mchezo vizuriii.

Siku hio Mwenge wakawa wanacheza na sekondari nyingine, mwalimu kocha yupo makini, irene anazengea namba kwa karibuuu. Mwenge wanafungwaaa tuuu. Wanabugizwa magoliii tu. Mwalimu anawatukana matusi mazitoo, kazi yenu kujiuzaa tu, ona mnavyohema juu juu, hata pumzi hamnaa, mnakula sanaaa, mitusi ya nguoniiiii, juu ya mitusiiiii. Kichapo kinaendelaaa. Akamwambia Irene pasha kwanzaaa, akaenda kuvaa bukta nyeupeee, na tshirt yake maana ya shule bado hajapewa na raba zake, kila mtu anamwangalia yeyea anavopashaaa.

Baadae Ticha akaomba SubstitutioN, akamuuliza unacheza position gani? Shooter, Defence au Central? Akamwambia Shooter ya Pembeni, ndo position ya head girl. Aka msub head girl akamuingiza Irene. Weeeeee! Wacha awabaabtizeee, manake anacheza Netball Professional, Ticha mwenywe akakubali kweli alikuwepo UMITASHUNTA. Tactics zotee, akikabwa sanaaa anaweka mpira chini anaukanyaga. wakiuchukua foul! Anapewa yeye. Kurusha kipembe, wenzie wanashika mpira mikono miwili yeye mmoja tu, kuruka sasa, na kuputa ndo usisemeeeee. Yaani Uwanja ilirindimaa. Si kwa netball ileee. Ilikosekana CHANETA tu pale. Akabadilisha mchezo woteee, wakarudisha goli zote na kushindaa juuu.

Basi pale pale uwanjani mechi kuisha tu mwalamu akamwambia head girl vua hio captain band mpe Irene, ndo new Captain wa Netball team. HG na wenzie wakasusia timu ya Netball! Irene akamwambia Ticha kwanza wale washakuwa mbuzi wazee hawana staminaa, hawana pumzi, hafundishiki machejo mpya, waunde timu mpyaa ya netball. Walikuwa wanaendesha timu kiushosti sanaa, ndo maana ilikuwa kichwa cha mwendawazimu. Mwalimu akaunga mkono hojaaa akamuachia hio kazi ya kuunda timu mpya.

Kumbe wakati anacheza siku kwa mara ya kwanza 2Pac alimuonaa, akwa anawauliza watu yule demu anaecheza nani? Akaambiwa yule katokea Arusha ila Bro Muddy design kamuelewa anafanyaga nae mazoezi, nasikia keshatangaza nia kugombea hilo jimbo. Na design atalichukua hilo jimbo. Mwanangu wewe si mtu weed umemuelewa nini yule demu? Sijawahi ona ukimuulizia demu, mademu wanaojiongeza unawatosa ujue nakushangaaa leo design umefatia mechi mwanzo mwengaa, mwanangu ajeee? Akamwambia kashaaaa kaka usinikosanishe na Head Boy.

Ikawa Messi anawahi kufika 2 Pack anakaa mlangoni ili tu amuone Irene anavoingia, mapumziko anaenda form 1 kuzuga tu ili amuone Irene, mara kibao akamfuma Irene anamwangalia. Sema ujasiri wa kumwambia hanaa, afu akitoswa itakuwa aibu, afu Muddy nae anasarandia sanaa. Akawa anakula kwa macho tu, mtu akisema Irene hivi anasimama kila anachofanya kusikiliza.

Irene timu ikawa imekamilika kakosa defence mmoja tu, na ashamuona sasa huyo defence haongei na mtu kabisaaa. Watu wote shuleni hapo walimuita baunsa matiti, kutokana na kuwa na titi kubwa na kifua kipana, sifa ambazo ni muhimu kwa Defence yoyote. Irene ashajaribu kwenda kuongea nae hakujibiwa, akaambiwa alikuwa psychologically bullied na wenzie kwa hio amejitenga kabisaaa, na kila mtu shuleni hapo, yuko peke yake peke yake. Irene akawa anataka kum sign leo, kesho. Kuna mtu akamtania labda 2Pack akakuombee, sababu anampenda sanaa Pac atakubali chochote Pac atachomwambia.

Irene akakata shauri amuombe tu 2Pac, akamvizia njiani, akamuanza, mambo kaka? 2Pack akstukaaa! Poa! Anamuangalia kicaxx kama kawaida si gangstar. Irene akaanza kujielezea nina shidaa, naomba ukaniombee kwa Florah, aje ajinunge na timu mpya ya netball! 2Pac akamuuliza Flora yupi? Mbona simjui. Irene akamwambia mnamuita baunsa matiti mimi sipendi kumuita mtu jina la ajabu. Mmmmh! Pac akagunaa! Mimi na yeye wapi na wapi? Akamwambia tu wewe muombe akikataa basi. 2Pack kutaka urafiki akasema poa. Kwa sifa zake saa 4 baada ya break watu wamejaa darasani kwa baunsa matiti akamfata, Mambo Flora! Akastukaaaa! Poa 2Pac! Hajaamini kama Pac kamuita Flora sio baunsa matiti, na kamsemesha akahisi anaota. Pac akamwambia yeye ndo meneja wa kusajili timu mpya na netball, ndo mshauri wa timu, na maeona Florah atafaa kucheza Defence, na akikubali yeye Pac atafurahi sanaa. Florah yupo sawaaa, haina shidaaa Pac. Akamwambia uje mazoezini. Flora yupo sawaa, sawaa.

Siku hio Pac nae akenda mazoezini kabisaa na track, kashajipa umeneja wa timu tena, akamkuta Irene anapasha, akajiunga jogging kuzunguka uwanjaaa, huku anampa Feedback za Florah kakubali. Nusu uwanja tu Pac hoi bin taabani, ikabidi asimamaem ghaflaa ainame kwanza kuvuta pumzi. Irene anamuuliza vipi? Pumzika youa re not in shape, nor active, yuko hamna shida tuendeleee, Ile wanakaribia goli linalofuata 2 Pack chaliii, akanyoosha miguu na mikonoooo. Irene akazunguka mara 3. Akaja kumuamsha mazoezi yameishaa. Ikawa Florah akigongana na 2Pack anasalimiwa, na watu wengine wakaacha kumuita baunsa matiti wakawa wanamuita Florah tena, wanaongea nae. Hivo she got her social life back.

Ikachezwa mechi ya kwanza, ilikuwa balaaaaa, Florah anakabaaa, afu ana miguvuuuuu, huku foward iko nzuri, mashooter wako poaa, Ticha mwenywe akawa anakubali pale sasa ana timu ya kujiamini hata kupeleka wachezaji watu wanne timu ya mkoa UMISETA. Kila mtu alikubali Irene jembeeee. 2 Pack akawa anaendelea kuja mazoezini kama kawaida Irene akikimbia 3 yeye 1 ya kusua sua. Wakazoeana kabisaa kabisaaa, messi wanakaa wote, break lazima aende kule kwa kina Irene. Prep lazima akae nae jiraniii, amsindikize bwenini waongeee, very closeee.

Watu kikawa kinawaumaaa, wao wapo siku zote afu kaja boya Irene kamchukua 2Pac sio ishu kabisaaa. Watu wakaanza wana date wana date, wengine marafiki tuuu, Hawaja doo bado (enzi zetu kutoka na mtu mpaka mpigane miti kwanza ndo iwe official). Sasa Irene akawa ashamuelewa 2Pack sio kidogooo ila kikawa kinamuuma mbona hamwambiii, anampenda, makiss, hata mambo na alivyo yamiss sasa? Manake ashayaanza likizo ya STD 7, na mkaka wa Form 4 huko Arushaaa. 2Pack anaongea mambo mengine tu yasiyokuwa na tijaaa. Mmmmh! Irene akjua tu yule domo zege, mambo ya yeye kwena kuazima jamvi apigishwe story aje mtu mwingine kuchukua hilo jamvi hataaaa. Atamfanyia dawaaa, yeye ndo Irene Brown!

Siku hio akamwambia Pac nisindikize chooni, Pac akakubali, walivotoka Irene akamwambia njoo tuongee hapa kwenye kigizaaa. Basi Irene anamuuliza hivi nini kinaendelea baina yetu, 2 Pac anajibu we friends, Irene anamtega only friends? Pac maneno yanakwamaaaa. enzi hizo google bado haijafika bongo. Irene akamsogelea akampa mateeee! Weeeeeee! Pac akalegeaaaa! Basi kuona tutam, ndo hataki kumuachia dada wa watu. Ikawa sasa wakiona kichaka, mavi yanawabanaaa. wasione kigizaa mateee tu. Irene akawa anawaza mbona haniambii kuhusu sex, afu mwenyewe nina hamu nayooo. SUBIRI NAMTAFUTIA SIKU.

Siku ya kufunga trem ya kwanza, wamekaa woote mpaka saa 5, Irene akamwambia twende wote Arusha, afu tulale wote ndo uende Dar, usipitie Dodoma. Pac kwa Irene kama uji kwa mgonjwa, akakubali. Wameshuka mjini, wakachukua guest house. Kungia Irene kavua nguo zotee, kaingia bafuni, anamuuliza wewe vipi huogi? Pac anangaa sharbu tu. Katoka bafuni mtupuuuu, anamuuliza vipi unaumwa? mbona umepoa ghafla?

Ikabidi tu Pac awe muwazi, kiukweli Irene mimi siwahi lala na mwanamke ni bikra wa kiume!

ITAENDELEA KESHO JIONI.
 
At last umeanza nyingine... Nikiri pamoja na kuwa mshabiki wa yanga na story zako pia, ile story ilinikata stimu kwenye episode 1 tu.....
 
Wakiona kichaka mavi yanawabana= irene akiona soseji hotelin njaa inamuuma. Haya lara leta utamu
 
naona umefika Babati, tadhali chonde chonde usije kufika mpaka mbulu
 
Basi Irene akamwambia najuaa sanaaa, sio kwa udomo zege uleee. Nilishajua kitambooo, ila sio kesiii nitakufundisha mwenyeweeee a,b,c,d. Pac kama mtoto akawa anangaa sharubuuu. (Kutokana na Kwaresma afu leo jpili details hazitokuwepo) Mechi ikapigwaaa fresh. Asubuhi 2 Pac akaenda zake dsm, jioni saa 11 Irene akaenda kwao kwa shangazi yake. Basi likizo hio ni barua juu ya baruaa. Ikakubaliwa wawahi kwenda Singida ili wapige mechi vizuriiii.

Kufika Singida wakaa motel, wiki nzimaa miti tu, mpaka siku ya kurepor wakarudi shule. Ndo ikawa washaona kabisaaaa. Kufika kina Muddy na Pac Form 4, Irene form 2 ndo likatokea sakata la Ben sasa, wote wakapewa suspension. Kiukweli ilimuuma roho, ila alikuwa tu anamuokoa Pac, roho ilimkataa kabisaaa Pac asiende. Sema Pac hana akili kubwa kujua Muddy anamtaka yeye afu ampe dili kama lile si balaaa. Baadae mambo yakawa mazitooo.

Akiwa nyumbani anatumikia adhabu, keshavuliwa u captain, wanawasiliana na Pac lakini, akaletewa barua na EMS anatakiwa haraka shuleni akajiunge na UMISETA. Adhabu yake imefutwa na amesamehewa makosa yoteee. Mchango wake kwa shule yake na moa wake kwenye UMISETA ni muhimu sanaa. Akajibu barua hawezi kurudi shule mpaka wasemehewe wote walio husika na sakata hilo mpaka Ben. Mmmmmmh! Baada ya siku 5 mkuu wa shule akaja kwao na mwalimu wa netball, akambembelezaa kuwa uongozi wa chaneta umekuja pale, umesikia kuhusu Irene ni muhimu sanaa aende UMISETA ili wampime uwezo wake asajiliwe kwenye kikosi cha taifa cha netball mwaka huo. Basi mkuu wa shule anajieleza ni muhimu Irene akaiwakilishe shule na yeye kama mkuu wa shule Irene akichezea timu ya taifa hatosahaulika kwenye kupandishwa kuwa afisa elimu mkoa au vyeo vingine, amesubiria chansi hili kwa miaka 13, hawezi kuliacha lipotee bureee, na kawadanganya Irene a lifiwa ndo maana hayupo shuleni. Kwa hio basi kesi imeishaa rasmi, amesha waandikia wote barua waliobaki warudi manake Muddy alisharudi manake nae anaenda kucheza mpira timu ya mkoa UMISETA,Pac na Ben wametumiwa barua warudiii shule, na kawapiga marufuku wanafunzi kukumbushia sakata lile. Hapo aingie kwenye gari la shule mguu kwa mguu mpaka shule Singidaaa.

Irene akarudi, wakawa yeye, Muddy, Florah wanajiandaa na UMISETA. Irene akakutana na uongozi wa CHANETA, Muddy akakutanishwa na uongozi wa Msimbazi na Makongo Sekondari juu ya future yake katika mpiraaa. 2 Pac akawa hataki Irene aende UMISETA basi tu kwasababu Muddy nae anaenda, afu yeye haendi. Benny hakurudi shule. Wakawa hawajui kwa nini. Wakiwa katika mabishano Irene anamueleza 2 Pac wote wamerudishwa shule sababu hio hio ya UMISETA. 2Pac kujitia kidume alivoona hasikilizwi akanza kutembea na mdada mwingineee.

Irene akawa anadhalilika, basi wanafanya nikomesheee. Irene akaawa na mawazooo, mpaka UMISETA inafika wakaondoka kwenda kambini, Muddy, Florah na Irene. Wakiwa kambini Muddy akajisogeza close na Irene, sasa Irene ana stress na mawazoo, Muddy akatake advantage ya situation, kumcomfort, kumpa moyoo na nini, akatengeneza mazingiraaa. Irene akanza kumuona Muddy mtu mzurii kwake, yupo mda wote akihitajikaaa. Akaanza kujihisi vitu juu ya Muddy ukizingatia 2 Pac ana mdada mwingineee. Kambini wakawa bega kwa begaaaa.

Kule kwnye UMISETA kutokana na stress zake Irene aka under perform vibaya mnooo, wakati Florah na Muddy wakangaa hatariii. Mpaka mwisho wa michezoo, CHANETA wakam saini Flora tu, kwenye Jeshi Stars atapomaliza form 4, ili aweze kuchezea taifaa, na Muddy akapata ofa za timu za Majeshi 3, Makongo Sekondari, na Simba Sports Club. Siku ya kurudi toka kambini Irene aka do na Muddy, kujipooza na machungu na kujiandaa na STIGMA inayo mngoja huko mbeleee.

Irene akarudi shule hana lolote hana chochoteee. Florah akawa captain wa timu ya netball, Irene akaacha tu mazoezi na kucheza, hata kupita uwanjani tu akawa hapitiiii, akastaafu rasmiii. Mkuu wa shule yupo bega kwa bega na Florah na Muddy, Irene akasahaulika kabisaaaaa.

Ila Irene akawa anatoka na Muddy kwa hiki kipindi walichorudi shule, 2 Pack akawa busy na mdada wakeeee hana mda ano. Ikawa ushindani couple gani kali Irene na Muddy au 2 Pac na mdada wake. Baadae kina Muddy wakamaliza shule na 2 Pack, Florah akawa form 4. Mwalimu mkuu akapanda cheo akawa afisa elimu mkoa. Mwalimu wa michezo kuona Flora atamalizaa soon, akaanza kumchachafya Irene acheze tena mpiraaa. Irene akagoma na kudai maisha yake ya kimichezoo yameishia kwenye UMISETA. Mwalimu anambembelezaa ajaribu tenaa, wapiiii. Hata uwanjani akawa hawezi kukatiza kati kati ya ile mistari, anapita tu pembeni. Florah akamalizaa na yeye akajiunga na Jeshi Stars, Irene akwa anamsikiliza redioni akichezea Jeshi stars, na mpaka taifa alichezaaa. Muddy akaenda Makongo kwa scholarship, akawa anamuandikia barua Irene kwa miaka yote miwili iliyokuwa Mwenge Sekondariii baada ya Muddy kumaliza, ila kama mjuavyo penzi la mbali halinogiii.

Irene akamaliza shule, akarudi Arusha, na kama ilivotarajiwa akawa hakufaulu vizurii, hivo kupangiwa Ualimu Korogwee, ambapo hakwenda akawa katafutiwa tempo shirika la bima la Taifa kama karani tu, Daresalaam..


BENNY!
Benny safari ya kurudi kwao ilikuwa nzito sanaaa, hakujua ataanzaje kumuelezea mzazi wake ambae ni muuz sokoni, na mama yake alihangaika sanaa Ben asome, kwenda kukopa pesa kwa ndugu zake. Pia kilichomuuma zaidi ni kwamba hakufanya lolote baya, na kilichomtoa roho bora hata angemuonja japo kijuu juu huyo Irene. Njia nzima akawa hana hamuuuuuuu.

Kufika nyumbani akawaambia tu wazee wake, nimefukuzwa shule kwa kosa la kupiganaa, barua hii hapa, uzuri walikuwa hawajui kusoma wala kuandikaaa. Baba yake alivua mkanda akamtandikaaa, ikabidi mama yake amkinge mikwaju ile imuingie yeye. Mama yake akwa kakosa raha kabisaaa. Benny nae anajifungia ndani siku nzimaa, analala tu.

Mama yake anamwambia basi nikakope tena uende hata private, mi sitaki uje uishi kama sisi kwa kubangaizaa. Benny akamwambia mama mimi shule basiiii. Mama ake akimuona anavoshinda ndani hana amaniiii, anakosa raha kabisaa, ikabidi amuombe mjomba wake anae uza sokoni Kariakoo, awe anaenda kushindaa nae, walau asaidie saidie apate nae hela za kupunguza makali pale nyumbani.

Ikawa Ben katafutiwa kibarua cha kubeba mizigo kwa wahindi kariakoo. Sasa siku ya kwanza kuingia kazini akaja mzungu, ben akaongea nae kingereza, Mzungu akanunua vitu vingiii, muhindi mwenyewe anajua kihindi na kwisahili tu, akamuambia Ben veve sasa nauza dukani,hapana beba zigo wakati iko jua English, nakwenda shule, nauza dukani na fanyia mimi hesabu. Tikeeeee! Benny akajibu Tikeeeee! Akaanza kukaa ndani dukani na mzee Hamadi.

Jioni Mzee Hamadi kamgea elfu 2 njiani, na kumwambia Ponjoro ana roho mbayaa sanaa, tunamuibia sio kidogooo. Ukikaa kimya na kujiunga na sisi, wote tuna nyumba Manzese wenzio. Mie na nyumba 3 kwa kazi hii ya kwa Ponjorooo. Sheria za pale Benny, usibadili nguo, hizi hizi ulizoanza nazo kazi, hamna kupendeza paleee, kiatu hiki hiki hata miaka 10, ukingaa tu ponjoro ataona wamuibiaaaa. Hivi hivi sis watu wa kunyongeaa, aaha ila tunajua tunaenda nae vipi huyu ponjoro.

Benny akarudi nyumbani na mchele, nyamaa, na nazi, Mama yake akafurahii akaona kweli kidogo maisha yatachia. Ikawa kila siku anakuja na vitu akitoka kazini, ila nguo ndo anavaa 2 tu kila siku. Akamshauri muhindi waende kutafuta tenda za vijuisi kwenye maduka yaliyopo shule za msingi sio kungojea waje dukani. Muhindi akamwambia Benny veve tafta, kama iko pata tenda mimi iko supply hapana shida kabisaa. Benny akaenda Olympio, Azania, Zanaki, Mzizima, Forodhani, Kisutu na Obay shule kuwaonesha biscuit, juisi, wafer, pipi zao wenye maduka, na kwamba bei rahisi akawapa maelekezo waende dukani kwao Kariakoo. Akarudi kazini kuwa anakaa dukani. Baada ya siku mbili wakaanza kuja kuchukua mzigo jumla, jumlaa, mzigo ukaishaaa. Muhindi kadataaa. Akamuongeza Ben mshahara, na hapo mambo ya na kina Mzee Hamad yakazidi mara dufuu, manake hela nyingiii, hata wakiiba nyingi muhindi astuki. Wkaka kikao na mzee Hamad wamshauri muhindi bidhaa wawe wanawapelekea shuleni, wawe na godown na Benny aongeze shule, duka halina maslahi. Muhindi akakubali, wakaungana na kaka zake wakaleta mzigo mwingii sanaa. Mzee Hamad store, Ben masoko. Kwanza mzee Hamad lazimaazidishe catoni hata 10 anavowapakilia, na kule Ben lazima azidishe bei kila caton. Sasa wakawa wanakoga helaaa.

Nadni ya miaka 2, Benny akawa ashajenga nyumba kubwa tu ya vyumba 10, magomeni. Siku ya siku mzee Hamad akamuuliza Benny wewe starehe yako nini? Pombe hunywii, wanawake hutaki, sigara huvutiii. Benny akamwambia mimi wanwake nawaogopa sanaa, nishakutwana tukio sina hamuu. Mzee Hamad akawambia basi leo tuongozane nikakuoneshe wanawake wasiotishaa, hawa hutowaogopaaa. Jioni wakaenda Msasani kwa malaya wanajiuzaa. Ben akanunua mmoja. Basi alivomalizana nae akamlipaaa. Ikawa sasa ndo tabia yake kila akitoka kazini lazima anunue Malaya. Na kwao ikawa ashahama anaishi kwake na wapangaji wake.

Akawajengea na wazazi wake nyumba, huko kigogo wakaacha kupanga. Ila kila akitaka kumtongoza mwanamke wa kueleweka haweziiii. Anakubwa na jinamiziii. Mzee Hamad akawambia Benny malaya watakuua na ukimwi, mi nilikupeleka kule utoe tu wogaaa, sio ndo ufanye tabiaa. Kama vipi nikuolee mke kijijini kwetu Tanga wanawake wana shidaa. Binti mzurii tu, ukimuelekeza elekezaaa mbona mnaenda sawaaa. Benny akasema hapanaa, ila nitaacha kunua Malaya.

ITAENDELEA SAA 4 USIKU
 
Back
Top Bottom