Weekend Story! Ugly Benny! (Get Rich Or Die Trying)

Weekend Story! Ugly Benny! (Get Rich Or Die Trying)

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,208
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Walamba Coni wa Azam wameikalisha Yanga leo kwa 2-2, hapo Simba akimchapa Azam anaenda kileleni, na wa kumkalisha labda Costal Union, manake Costal alishamlabua Azam FC na Yanga Mkwakwani na kama mjuavyo kumfunga Coastal kwenye uwanja wake sio rahisi, kachimbia vitu mulee mwenye ule uwanja na balaaa. Na kwa mpira wa ndumba costali hana mpinzani. Sema pia ni Simba 2, kama tawi la wekundu wa Msimbazi. Anyway matokeao leo sio mazuri sanaaa, mkiona story inaenda na kurudi mjue tu matokeo ya mpira ndo yamechangia.
UGLY BENNY, Get Rich Or Die Trying Saa 4 kamili.


Singida! Menge Secondary School 1996

"Irene utakuja maskani jmosi au sio? nitakuandalia mambo yako yooote unayoyapenda kuanzia kwiyooo, bila kusahau chips, fanta baridiii pembeni, sawa Kim, kila unachotaka mimi nitafanikishaaaa, ni promise tu kuwa utaibukaaaa" Irene akawazaaa kama dakika mbili hivi akamjibu."Well Benjamin i dont know! naweza kuja ndio lakini sina uhakika sanaaa, but you my good friend, nitajitahidi kuja, anyway, will do my best, you so nice to me and all, nitakujaaa. Nunua na bia, napendaga piaaa, sipendi sanaa sodaa." Benny hakuamini kabisaaa akawa anajisemea tu moyoni bia nitanunua creti zimaaa, akaachana na mrembo Irene, talk of the school, akitababasamu, tabasamu la ushindi. Akajiapiza mrembo Irene akiingia tu ghetto hafanyi ajiziiiiii, yaani hafanyi makosa kabisaaa.

Kumbe Muddy msela wake alikuwa anamcheki mda tu tangia anajiongeza kwa Irene. Akawa amemfata kwa nyuma na kumgutua, weweeee! Akastukaaaa! Vipi? Muddy akamwambia una wasiwasi kama unaogea nje! Hahahaaaaaaaaa! Wakacheka. Muddy akamwambia wewe ulikuwa unaongea nini na demu wa 2 Pac? Akazuga mimi? Saa ngapi? Muddy akamwambia wewe ndio, mda si mda, bishaa! Benny akaangaza angaza kulia na kushoto akamnongoneza kwa sauti ya chini Muddy anakuja weekend ghetto. Kausha lakini. Mmmmmmmhhh! Muddy akaguna. Akamuuliza "Hivi wewe una matatizo gani? if you are horny you wanna enjoy find a girl, nenda mtaani, au hata hapa skonga but dont defy another mans chick. Not to mention the man unaeingia anga zake ni yule 2Pac mtoto wa waziri. Unajue they dogs man! Huo moto wake sasaaaa, aaaah weka mbali na watoto. Si juzi tu walimfukia yule dogo kwenye shimo waliomchimbia kisa alichua demu wa mshikaji wake Pac? Sasa wewe ndo unataka kumchukua demu wa Pac. Hahahahaaaaaaa! Benjamini Peter umejichokaaa! Dogo aliefukiwa mpaka shule hataki tenaaa, shauri yako.

Benny akamwambia sikia Muddy, in this school there is only one beauty, Irene, all them other girls are either ugly or simply plain. And i happen to like Irene, so doeas 2Pack so what man? Why does 2Pack has to get the most beautiful girl in school and not me? What is wrong with me? Mi sio mwanaume Muddy? Si dindiii? Nina kasorooo ganiiii? I am going after her no matter what you say.

Muddy akamwambia Yes una kasorooo, kubwa tu, i mean no disrespect but man you ugly, broke and slow in class limiting you in all aspects to be noticed by people like Irene and the likes. Na kinachoniumaaa sanaa, Irene will only make fun of you with her friends, like all the other girls always do. Hivi hujichokii ukajihurumia Benny? Mpaka lini? It is so hard to be your friend cause unajitutumua afu ukiaibishwa washkaji zako ndo tunahadhirika na wewe. Ifike mahala ujitambue, ulivo na uwezo wako,

Benny akatafakari, akamwambia sikia Muddy amesema mwnyeweee, im good friend of hers, anakuja ghetto jmosiii. Naomba nipe mpaka jmosi ikiwa ndio sivo sitongozi tena mwanamke, nawaahidi, i know this is it, trust me, i can feel it. Muddy akasikitikaaa tu na kujua vovote itakavokuwa Irene hawezi kuwa kamuelewa Benny. Akajinyamazia aone mwisho wake.

Jmosi Benny kitaa alikopanga, kaamka saa 10, na dekio, kafuta bui bui, kabadilisha shuka, saa 1 kawaamsha wenzie excile. Chumba kimekodiwaaa. Akaa anasubiri. Ashaandaa hela ya chips na kwiyooo, na bia. Aliiyumbisha bajeti yake si kidogooo. Mpaka saa 11 jioni hakuan Irene wala kivuli chake. Saa 12 jioniii akasikia hodiiii, wacha ruke kwa bashashaaaa. Akaenda kufungua, Irene huyu hapa na kibegiii.

Akamwambia mi hata sikai, naomba tu unipelekee bag langu kwa mtu Kibaoni, pale kibaonii nyumba ya nne. Mmmmmhhh! Benny roho ikamsitaaa, akasema no sweat, mi nakungoja hapa hapaaa. Akachukua lile begi akaanza safari ya kibaoni, toka hapo alipopanga si mbaliii. Njiani roho ikamwambia fungua hilo begi mna nini? Roho ingine ikamwambia usifungueee. Akafika mbele akafungua, akakuta limejaa bangi mbichi. Akafunga, Akatetemeka, akakaaa chini. Akageukaaa. Kufika ghetto hakumkuta Irene wala nini.

Akasonga mpaka shuleni mwenge maana 2Pac na Irene wote walikuwa wankaa boarding. Akaanza kuwasakaaa. Akawakuta kwenye kona wanapigana mabusu. Akamuita Irene, wakastuka woteee na 2pack, akawarushia bag lao. 2 Pac akanza kugomba what the fack! Ulisema amekubali kukufanyia hii issue, what is this? Irene yupo baby! Baby! Benny akaishia zake kitaaa. Ile shock bado alikuwa nayo. Akawa yupo juu juu.

Jumapili akashinda tu ndaniii, jumatatu kuingia shule, kila mtu anamtolea macho huku wananongonaaa, hamna anemwambia kitu. Akajua tu kimenukaaa. Ila hakujua kimenukaa nini. Watu wanamwangalia tu kwa macho ya mashakaaa. Assembly akamuona mwalimu mkuu kaja jambo amabalo silo la kawaidaa. Tena kashika lile bag la bangi.! Akaitwa mbele, Benjamini Peter, wakaitwa na kina Irene Brown, Mohamed Ali au 2Pac. Mashtaka ni kukutwa na kiasi kikubwa cha Bangi.

Mwalimu mkuu akaeleza katika upelelezi ilionekana Benny ndo alikuja na begi hilo jumamosi jioni, na kuwaulizia wahusika kwa watu kadhaaa, kabla ya kwenda kuwatupia hilo bag, na mlinzi baada ya kumuona mtuhumiwa akiondoka, ndo akalihodhi hilo bag na kukuta hio bangi. Washtakiwa 2 na 3 wanadai Benny aliwatupia hio bangi wafukuzwe shule, kwa sababu Benny ni shogaaa na amemtaka 2Pac mara nyingi kimapenziii ambae ni mwanaume mwenzieee. Na kudhibitisha Benny ana tabia za kishoga watu kadhaa wamekuja mbele walishatongozwa na Benny mara kadhaa akiwemo best wa 2 Pack Mark na best wa Benny Muddy! Eeeeeeeeeeh!

Benny akawa ameshangazwa na kila kitu, akiwa bado na mstuko akasikia mwalimu akisema Ushoga na utumiaji wa madawa ya kulevya havitavumiliwa shuleni hapo kwa hio basi Benny amefukuzwa shule rasmi, na atarudishwa kwao, 2 Pack, Marry na Muddy wamepewa suspension ya miezi 2 warudi na wazazi wao. Akaondoka kikoraa mkuu wa shule. Watu wakabakia wananongonaaa. wananongonaaa. Mwalimu wa nidhamu akamwambia Benny twende ukachukue barua yako. Akachukua barua, akiwa bado hajitambui, akaondoka kimya kimya kurudi gheto!

Kesho akapanda basi la kurudi kwao Dareslaam. akiwa na mawazo mengi sanaaa. Haswaa kwanini Muddy alimsemea ubaya ule?

IMEENDELEA
 
KUBWA LA MAADUI!!!!!!!!!!! Dada la Dada sipati picha hilo muvi unavyolisuka kama [emoji3] [emoji3] [emoji3] watu usongo umewashika saa 4 utasababisha scrumble humu ndani.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Anyway ngoja tusubirie naenda kutafuta popcorn kabisa.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Duuuh ben kageuziwa case yote kisa mbunye mpya....yani kabeba msala kizembe
 
Lara Kaseja mambo gani tena! Yaan mpaka kesho,ebu achana na mitoko ya weekend, Tupe raha
 
lara 1 japo nna majukumu mengi kama unavyojua uchaguzi wa marudio ndio gumzo kwa sasa! ila bado sikosi muda wa kujiliwaza na simulizi zako maridadi......Huyo Binjamin atakua alikua na safari ngumu sana ukizingatia siku hizo hakukua na lami kuanzia Singida hadi Dodoma!!!!!!!
 
Hahahahahaaaaaaaa! nimejikuta nacheka sanaaaa
jama yakucheka tena haya. Yale ya yanga na simba alisema yamemshinda akadai nyingine ikianza tumstue..... sasa ile namna ya ku cc watu mi ndo hivo tena. Embu mlete tumwone tena na kwenye hii
 
Umesema kesho enhee hili movie tamu nmeanza kulielewa
 
Back
Top Bottom