Gill knew life could be cruel but he didnt expect that sometimes it ha no limit. Kukweli kabisaa toka moyoni mwake yule ni mpwa wake. Sema alitaka kumrudishia Stacy ajue how it feels, kumpenda mtu mwingine asie na mda na wewe au anakupa priority number 2 kama alivokuwa anamfanyia kwa Gill. Lile wazo lilimjia tu ghafla kule shule, kuona Stacy kaumia kwamba yeye ana mtoto na anashoboka live live. Akajisikia tu kumkaanza bila chumvi, aki expect sooner or later ata come clean kwamba alimkaanga tu. Sasa in the longrun akajua tangu amwambie Stacy ana mke amekuwa na dabu sanaa na unyenyekevu and he can control her, akaamua to keep it going a little longer. Siku ila ya Gill he wanted to come clean so much, ila he didnt want to do it infront of Gill sababu angemchekaaa sanaa na kumtania na kumdhalilisha he has no balls to own a wife mpaka anafanya hoax, aka plan kuwa he will come clean latter. Latter ndo ikawa latter mpaka maisha yakajambaaa na kweli now it is suspicious.
Akaenda kwao kwa mjomba wake of which he neve likes to go of recent maana ananona kama wanamchoraa na umasikini wake. He could snse dharau za aunt yake zimeanza upyaaa wakati mda ule ana hela alibadilika kabisaaaa. Akawaza sometimes kuishiwa tu unakuwa unajihisi maybe anaonggea tu from normal context yeye anahisi ni shade. Akingia chumba chake ambacho uncle wake mwingine yumo humo, basi chumba lote kabandika mapicha ukutani, yaani vijana wana tabu sanaaa. Akaz uvunguni akatoa msanduku wake akachukua alichotaka, akaaga. Wakati anaondoka mjomba wake akamuita waongee chembaaa. Anamwambia basi inabidi urudi nyumbani tuangalia tujadiliane tunakabiliana hilo nalo vipi, usione aibu wala usijisiki vibaya ni maisha tu, wewe njoo hapa hatushindwiii. Hapa fo you it is home, nitampa mpangaji wa servant quater notice uje tu nyumbani. We love you ande we support you hata kama dunia nzima inakuchekaa. Akajitetea mjomba things are not that bad, usiwe na wasiwasi kuna mambo yangu nasikilizia.
Mjomba akamuuliza hivi umesikia anythinga about Imelda toka nimfukuzeee? Moyounaniuma sanaa nad i regret kicking her out. Sijui anaendeleaje na mjukuu wangu sijui kama yupo, uzazi ulivo mgumuuu, yaani ni kama wana ni windaa. Nishawaita wasichana zaidi ya 10 Imeldaaa mawazo najichanganya nawafananishaa. Aiseeeee. Ni balaaaaa. Kubwaaaaa. If i could take back my decision, ningeacha tu aisee ningekuwa hapa na mjukuu wangu tunakula bataaaa. Harry akakaa tu kimya juu ya hio topic.
Alivorudi kwa Stacy, akamkuta Imelda katoka shule akamuweka kikao, bwana nimetoka nyumbani Mzee anakuulizia sanaa, hasira zimeishaa, anakutafuta sanaaa mpaka huruma. Fanya uende nyumbaniii. Imelda anagomaaaa bado anaogopaa maana siku ya kutimuliw babaake alimbadilikia sura sio kidogo. Harry anamwambia sikiza nikwambie hapa tukiendlea kukaa wote atatuchokaaa. We rudi nyumbani wale ni wazazi wako hawawezi kukufanya kitu. Imelda hatakiiiii. Harry akaanza sasa kumfokeaaa na kutishia kumpigaaa. Imelda yuko tayari kupigwa ila sio kurudi kwao. Kipemba dada akaaga anaenda dukani kumbe kaenda kupiga simu kwa Stacy.
"Hallo!" Dada huku Imelda anataka kupigwaaa na mjomba wake, anamlazimisha arudi nyumbaniiii, Imelda hatakiii ndo anamfokea anatishia kumpigaaa." Stacy akashangaa akaona makubwaaa. Akwa convised more than ever yule ni mkewe. Akaanza kumuoogopa Harry he is such a monster, kwa hio plan kufeli ndo anamfukuza mwenzie. Mbona majangaa. Akaingiwa imani, akaamua akifika anatimua woteee.
Stacy karudi nyumbani hakumkuta Harry, akamkuta tu Imelda, akawa anaongea ongea nae pale kuhusu shule, akamuuliza hamna hostel huko za bei poa. Imelda akashukuru Mungu kweli maana mjomba wake alimletea mambo sio mchana, mambo ya kurudi home akadhalilike aaaah wapi. Akasema zipooo nyingi. Stacy akamuuliza bei, sio kubwaa 25000 kwa mwezi kama chumba tu. Akamwambia tafuta mi nitakulipia. Imelda akakubali bila kujivungaa. Akawa anamsisitiza tu asome sanaa wanaume ni wanyanyasaji sanaa, aki throw shade to Harry kwamba ni mnyanyasaji. Imlda anamkubalia dada kweli ni wanyanyasaji si uongo. Nimejioneaaa. Stacy anawaza maskiniiii.
Mda wa kulala akaingia chumbani na jeshi lake, akakuta Album. Akashtukaa, maana limewekwa ju ya kitanda meaning alione. Akaamua kulipitia, ni la Harry. Akakuta picha za Harry za utoto kabisaa tangu yuko kwa wazazi wake. Zingine ndo alivoamia kwa mjomba wake. Zingine kambeba Imelda tangu mchangaa. Imlda kafanana na mama mtu, shangazi yake Harry. Picha nyingi Imelda akiwa mdogo na Harry na familia yao. Akajiridhisha kweli yule ni mpwa wake. Ila bado akakasirika kwanini alimtia jamba jamb kubwa kama ile ya kuwa na mke. Jambo lile lilimuumiza sanaa, sanaa snaa afu kumbe uongo ndo maanake nini sasa. Akapanga kuendeleza mnunooo. Kesi tu imebadilka jina kutoka civil case mpaka ciminal case, manake mwanzo ilikuwa kesi ya kulalamika kwanini kaoaaa, sahivi ni kesi ya jinai on several grounds, Fraud and conspiracy to commit Fraud.
Wakiwa wamelala na wanae maana ishakuwa mazoea, akamsikia Harry karudi, dada akamuuliza nikupashie chakula akasema hapana, we kalale tu. Akaja huku anakuta jeshi limejaaa. Stacy akajikausha kimyaaaa, kama yupo usingizini, vitoo ndo balaaaa, viko mbingu ya 8. Harry akawa anaita Stacy, kimyaaa, Stacy mi nalala wapi? Stacy kimya akajua na lile album kumtimua itakuwa sio rahisi, na isitoshee akisema amruhusu ajibane pale atataka mzigo hivo hivo na watoto wako pale ndo mambo gani sasa? Akaamua kumwambia si unalalaga kwenye kochi wewe, hahaaaa akajikuta amecheka na Harry akachekaa. Aaaah wpi si kwa kujiridhisha huko na ushahidi usio tia shaka lolote. Stacy anamwambia sasa umechelewa pashajaa hapa. Ukitaka kulala hapa ndo uwe una wahi kurudiiii. Kwa leo nenda kweny kochi tu.
Harry akasema wewe wanao msinitanieeee kabisaaaa. Akavuta kitoto kimoja akakisogezea ukutani, kavuta na kingine akakibania ukutani, ikapatikana nafasi pembeni ya Stacy. Stacy anamwambia hawa hawawezi kulala hivi watalaliana mbona Harry mkrofii sanaa? Harry asikii la mhadhini wala manadi swala. Akajilaza pale pale pembeni. a kama Stacy alivojua akaanza kuchokoza mambo. Jamaniiiiiii! Mmmmmh! Basi anamuomba ampe kidogo tu, siku nyingi sanaa amemiss mambo. Stacy anamgomea watoto hawa. Nafanya taratibu, hawawezi kuamkaaa. Mmmmh! Stacy akawa ana hamu na mambo ila sasa watoto wale. Harry akamfanyia visaa mpaka akaubali mechi mojaa ya kimya kimyaaa. Ilinoga hatariiii. Akajua wamepunguza hamuuu watalala sasa. Mmmmh anamuona mwneia anawaza ananongonekaaa kujibana hata hamu haijamuishaaa. Mara kainuka kakabebaaa ka Stacy akaenda kumgongea mama yak, mzigo wako huu hapa, aha ule wewe tabu tupate sisi. Akambeba Prince akampeleka kwa dada, mwanao huyo.
Huku uwanja mambo yakawa coast is clear, uwanja mweupeee. Stacy akasikitika tuuu. Jinsi alivokosa uvumilivuuuu. Mchi ya marudiano ikapigwaaa, safi sanaa,mambo yakanogaa hatariii. Baada ya mechiwakawa wanaongea ongeaaa, Stacy kutaka kumu impress Harry na kumtia moyo kwamba yuko pamoja nae, akamwambia namtafutia Imelda hostel. Weee ikawa kosa la jinai. Harry kapanic vbayaa utasema katukanwaaa.
"Unamtafutia hostell kama nani? Kanini hujanishirikishaaa? Unafikiri sababu sahivi sina hela ndo unajiamuliaaa tu, unanicontrol mpaka kwenye familia yangu unafanya tu maamuzi, unanivua mpaka kwa mpwa wangu kwamba jomba lako senge tu sahivi halina hata 100, mimi ndo namuweka mjini nachoamua mimi ndo sheriaaa si ndio. Wewe tujadili yule tutafanya kumpa taarifa u, kwani atafanya nini?"
Stacy anajitahidi kujitete, "Sio hivo mi nimeona huku kwangu mbali na shule yake, atashindwa ku fous na masomo, na mda wote anaangalia mtoto hapati mda wa kusomaa. Nisamee basi kama nimekoseaaa nilikuwa na lengo zuri sanaaa tu, wala sipo katika hayo unayoniwazia"
Harry bado kapanic "Kwanini kabla hujamwambia hukuniuliza mimi? Umeanza dharauuuu eeeh, ushaanza kuniona me boyaa si ndiooo? Hata kuniuliza mambo madogo kama hayoo unaona shida kunishirikishaaa. We unamjua huyu Imeldaa? Unaujua umalaya wake kiwango chake kilivo kikubwa, unampeleka hostel akajiuzeee tu si ndio. Azae tena mtoto mwingineeee. Huyu haendi hostel anarudi nyumbaniii keshooo. Atake asitake. Ndo nishasemaaa. Na next time please keep your money off my family"
Stacy akapanga anyamaze yaishee ila akashindwaaa kabisaaa kufikiria kumrudisha Imelda nyumbani sio utu, yule kazaa tayari, nyumbani kutakuwa na stigma kubwaa sanaa. Sio wazo sahihi kumrudisha nyumbani na vile vijembe na nini ndo atazidi kuwa mnyongee. Akaamua liwalo na liwe ila anamtetea. Akaanza kiupole kabisaaa maana kumnyoso simba kunataka mahesabu makubwaa.
"Harry sikia sawa nilikosea kuongea nae bila kukushirikisha, lnamba msamaha baby wangu, nisamehe, ila naomba kushauri tu, huyu keshazaa, nyumbani kule kuna Stigma, lazima resentment itakuwpooo, na wata mnyanyas atakosa amani, na atashindwa shule......." Kabla hajamaliza akakatishwaa " We mwanamke una kiburiii sanaa, yaani ushaanza maamuzi yangu in less tha a minute, una challange authority yangu on what ahppens to my niece. Since when are you familly? Lini labda umejiunga na hii familia yetu? A man cant even make decision on his familly issues unataka uamue wewe? Haya ni mambo ya kifamilia and you are not familly, keep your money off my familly.
Akavaa nguo na kubamizaa mlango. Akaenda kugonga kwa Imeldaaa, mchukue Stacy na vitu vyake tunaondoka sasa hivi. Imelda akajua anapelekwa nyumbani tu akagomaaa. Akaanza kuita dada Stascy nisaidieeee sitaki kwenda nyumbaniii, Dada Stacy do something pleaseee dont let him take as away. Pleaseeee!" Stacy yuko chumbani anamsikiaaa lakini sasa atafanyajeee akaamua kujikaushaaa. Dada akatoka na Prince akawa wamestuka na ile mikelele saa 8 usiku.
Harry anamfokea Imelda "Yaani hata wewe sahivi unaniona mngese si ndio? you cant just do a simple thing nacho kwambia mpaka upokee oda kwa Stacy ya kuniheshimu mimi mjomba wako si ndio?" Akaingia ndani akazoa mabegi yao akayatoa njee. Mda Harry katoka nj, Imelda akaona sasa napelekwaaa akaenda kugonga kwa Stacy, nisaidie dada Stacy, anagonga mlangoo, nisaidie mwanamke mwenzioo. Stacy kabana ndani kimyaaaa. AKhaaaa! Akasikia Harry anamburuta Imelda, akamsikia dada wa kazi anasema utamuumizaaa. Akastukaaa, ukute Prince yuko nje anashuhudia hio cinemaaa. Akakurupuka akatokaaa.
Kweli Prince na Stacy wanashuhudia Harry anamburuta Imelda, pamgeuka Sobibor. Uvumilivu ukamshinda, akaamua kuingia front kupambana na Harry maana kidogo yeye ndo mkubwa wa kummudua. Akanza kumvuta Harry amuachie Imelda. Akasikia we malaya wewe nitakupigaaa, mbwa wewe. Alafu kuna watoto pale aiseeeee. Imelda akawa kachoropoka sasa. Harry akaanza kumkungutaaa Stacy. Stacy hajawahi kupigwa na mwanaume yoyote tangu azaliweee. Baba yake mzazi mwenyewe hakuwahi kumpigaaa hata siku moja.
Alivo mlaini mlaini ngumi zikawa zinamuingia si kidogooo, moja ikampata jichoniii sawiaa. Akahisi mkojo umepenya chupi, sasa kupigana hajui, kujizinga migumii isimuingie hajuiiii. Kipondo kikamkolea sio kidogoo. Anabakia kumwambia dada wtoe watoto, nenda nao nje wasione napigwaaaa. Imelda akapata nguvu za kuingiliaa sasa yeye akawa asha kasirika haogopi kitu akamkabili yeye mjomba wake, Nae kachezea kipondo toka kwa myweather. Kwa mwili gani alio nao kupambana na myweather. Sasa bahati yake Imelda wakati anachezea kipondo akawa anampa maneno ya shombooo, yakampenyaa rohoni Harry. Alimwambia "We mbwa tu sio mtu, dada wa watu katusaidia afu ndo umlipa hiviii, katupokea vizuriii tunasihi na vizuriii, kunisaidia mimi kakukosea nini kikubwa, umempiga nusu ya kumuua, kwa kitu gani kiaya alichokufanyia, and guess what yes ndio nakuona senge tuuu, tena senge baridiii nashangaa mwenyewe hujioni kama una mambo ya kingeseee" Harry yale maneno yalimuuma sanaaa.
Akaacha kutembeza kichapoooo, akatoka nje kwa Hasiraa, kufika nje, dada alikuwa amekaa AMEJIKUNYATA NA WATOTO na watoto kwenye ngazi anawaulia mbu wasiwangate, alivomuona Myweather anakuja upande wake akajua zamu yake sasa kuingia ulingoni na myweather, wacha atimue mbio kuelekea nyuma ya nyumba, watoto nao kutoa ukunga wanamkimbia wanakimbilia kwa dada yao. Akafungua geti akatoka nje kabisaaa. ya geti.
NDANI KOTE HALI IKAWA SIO SHWARIIII.
ITAENDELEA SAA 3 USIKU.TEAM FUDENGE DICLOPAR VIPIII, DOI ITAWATOSHA KWELI.