Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Msomali anampima mrembo or azalishiiiiiishiiiiiiii hahahah ila no hii mimba yake japo lolote laweza tokea
 
1. Dee atabakia na mama watoto wake
2. Sally Mimba ya msomali ila atabakia na Tonny
3. Msomali atarud na msomali mwenzie / atachukua loose ball moja shuhuli imeisha
Tonny gam imemshinda goma linarudi liliko toka mbona
 
Happiness is over rated!

Since i came back, mimi Dee nimefanya several attemps za kumpata Sally. Na mda woteee kikwazo kinakuwa kimoja tu, mke wangu Pendo na mwanangu. Kinaniumaaa sanaa hiki kitu, cause Mzee baba it is asituation i am in, and i cant do shit about it. Niko na mwanamke nisiempenda ila mwanangu nampenda, ni damu yanguuu. Sasa kumpenda mtoto bila mama ni uongo mtakatifu.

Why i dont love my wife, dont blame it on Sally, blame it on me. Ujue sisi wanaume mda mwingine badala ya kuoa mtu, tunaoa sababu. Sababu ndo inakushawishi uingie kwenye maisha na mtu, sasa kimbembe ni ile sababu inapokuja kuisha na lile jitu ndo umenasa nalo. Kama mimi sababu tu huyu mwanamle alinijali kipindi sina kitu ndo kuamia kuwa nae. Sasa sahivi nina vitu, na jinamke ndo ninaloooo, limenikamataa sijui nafanya vipiiii.

I cant tell her simpendi kwa maneno, cause it is inhuman and childish ila i am not sure my actions are not giving me out. Hii hali ni mbaya sanaaa, mnoo mnooo. Unakuta saa ingine kitu kidogooo navowakaaa na kumwaga povuuu utasema mtoto wa watu sijui kanikoseaaa nini. Alafu mnyenyekevu anaomba msamaha hata kama hana kosaaa.

You can take the girl out of the hood but you cant take the hood out of the girl. Mke wangu ni mchoyoooo sijapata kuonaa. Wakija ndugu zangu nishamjuliaaa nawaachia 20k kila siku wale wanachokipenda huko nje maana namjua ni mchoyo. Kuna siku alikuja uncle wangu akala maharage weeee, aligombwaaaa, akatukanwaaaa, na kama Mungu tu nilikuwa nimetoka nikarudi ghafla nasikia anawakaaa anawakaaa, ana mbwabwaja mpaka maneno yasiofaaa. Niakjua sijui kafanyaje. Pendo kuniona anazugaa zugaa hatoi maelekezo yalio nyooka. Analalamika hana adabu, hana adabu, kafanyaje? Hasemiii direct anazunguka tu.

Nikamuita house girl nikambana kumuuliza kwani Uncle kamfanya nini Aunt yake? Akasema, unclekala maharage yaliobakia jana. Mxiuuuuuu! Nikasikitika tu. Nikawa kila asubuhi nampa uncle 20k ale anachokipenda huko nje, na kumpooza kishkaji asiwaambie ndugu maana ni mambo ya aibuuu.

Siku nyingine mdogo wangu kabisaa kala sneakers chocolate hii, weeee hilo povu lake sio la nchi hii. Nikamjua tu ni mtu aliepata sana shidaa utotoni ya chakula kwa hio ameona chakula ni dili sanaaa. Ana thamini vitu vidogo vidogooo mpaka aibuuu. Kashindwa kuelewa sasa maisha yamebadilikaaa. Ukinunua kuku wa 3 atapika nusu na mko nyomiii humo ndani, bajetiii. Mi nachukiaa mwenzenuuu, bajeti ya nini mambo ya kisengery.

Nishazoea nikitaka kula chakula kizuriii naenda hotelini. Gari iko nje haendeshiiii mwanamke yule ana ubahili wa kikinga. Na hataki mtu aendesheee. Unaenda kupanda basiiii. Inshort mke wangu hajui maisha mazuriii. Haweziii kuishiiihaweziii. Ashazoea ku survive. Anaweza kununua chips kuku, watu wapo na akaingia kula chumbani ili wasimuombeee. Khaaaaa! Nishamkuta anakula vyumbani mara kibaooo. Acheni kufungia sukari, mchele, mafuta, unga wa ngano chumbani. Bajetiii. Yaani chumba kama stooo.

Ni mambo madogooo ila yananikeraaa mnoo mnooo. Yananichefuaaaa sanaaa. Kuna siku niko kwenye conference na maboss wenzangu, nikawaza hivi hawa watu wakijua kama nalala na unga chumbaniii, na mchele na mafutaa uvunguniii si watanidharauuu sanaaa. Nikajikuta tu nasonyaaa kimya kimyaaa.

Mwanangu sasa anabahiliwa mpaka pampers. Nikiwepo sababu nagomba atamvisha, nikigeuka tu anamvisha nepi. Jamaniiii. In short maisha ya ndani kwangu yalikiwa local local sanaa afu bila sababu za msingi. Ni mambo flani ya kibwegeee na kutia aibu. Asikwambie mtu nyumba ni mwanamke, ukishakosea hapo tuuuu baaaassss. Na mimi nishabugi hapo.

Siku hio nimeenda kwa Sally nikatamani maisha wanayoishi. Ndo maana msomali alingangania pale kama luba. Kwanza anaishi na Feisal na dada wa kazi, ambae ni professional cheff. Well not professional ila alifanya kazi kwa wazungu walivoondoka ndo sally kamdaka. Aubuhi jikoni kuna ubao wa kubandika note, unakula nini siku hio, na kama kuna wageni kama sisi tutakula nini. Unaandika unachojisikia kula, kama na matunda, au juice, au salad. Mpaka dessert. Nikakuta sally kabandika vyake, na Feissal kabandika, na rafiki zake Feissal, na kimoja kimeandikwa DR. Sikjelewa hii Dr vepeeee. Na mimi nikaa dika ili tu nijue huyu dr ni nani na kwanini yupo kwenye ratiba ya menu.

Friji limejaa smoothies, majuice, soda mizaga zaga. Counter imejaa vinywajii. Unaona kabisaa nyumba hii sio big deal chakula. Nilienda saa 4 kupeleka kitu, sasa kuona Dr. Nikaamua kuua ratibaa nikasema sibanduki hapaa. Mchana Feisal kaja na hao marafiki zake, kanikuta, aaah Bro Dee! Shwariii! Nilistukaa shikamoo inagombaa kisa kabalehe wakati anafanyiwa sunna namuonaa. Nikajibu Shwariiii!

Mpishi kawaletea chakulaaa, wale rafiki zake wanalalamika sijui walisema asiweke kitu gani mpishi kawekaa, wanafokaa. Nikaingilia na kumuuliza Kwenu kuna mpishi? Mnakula hivi? Kuwa na adabu! Ushasema kashakuelewa. Walinimind sema Feisal ashasikia nilikiwaga Pablo zamani. Akamwambia chunaaa.

Nikamuita Feisal counter, na kuanza kumchimbaa Dr ni nani kama ndugu yao au vipi? Na ana ishu gani. Mi namimina kilauriiii, nikamuuliza vipi haya mambo unatumiaaa? Akasema Hapanaaa, bro Dee haramu hioo. Nikamuuliza huyu Dr ni ndugu yenu yupi tenaa? Akasema sio ndugu bro Dee ni rafiki yake Da sally! Moyo ukastukaaaa. Akadakia pia ni daktari wakeee. Anamsaidia sanaaa.

Nikauliza Sally anaumwa nini? Feisal akashtukaa kidogo. Kwani hujui? Nikasema sijui. Akabadisha engine angani maana sio gia, mie pia sielewiii, labda umuulize mwenyewe, haniangalii usoni. Nikamwambia fesial this is man to man anaumwa nini?Feisal anajikuna nyweleee, Bro Dee bwana mi sielewi ila Dr. Anakuja saa 10 mda si mda labda umuulize yeye. Mi naenda kumalizia homework.

Nikabakia pale nakunywa taratibj. Kweli sa 10 na nusu Dr kaja, akanisalimia, nikaona kaingia chumbani, kabadilisha nguo, kavaa bukta na tshirt katokaa. Kumbe anaishi hapaaa. Nikazidi kushangaaa. Nikaanza kuhisi labda Sally anaumwa gonjwa kubwaa sanaa. Nikaogopaaa. Mpishi akamletea msosi wake, na Dr hajibani, kaagiza samaki changu mzima na salad.

Akaja sasa tufahamiane, akajitambulisha Dr. Levin, wanakuwaga na nyege hawa kutaja hio title. Mi nikamwambia mi Dee. Akatabasamu The Dee! Nikashangaa ina maana huyu boya ananijuaaa, basi mfugo mpya wa sally hamna mgonjwa wala nini. And mnanijuaaa i am rude, extremly rude kwa mifugo ya Sally.

Nikamwambia Sally kaniambia anaumwa, can i know more about situation yake, Dr. Ashaniambia ila ukiniambia kitaalamu zaidi itakuwa poa, ikizingatiwa mimi ni mtu close sana kwake. Dr. Akasema sio vizuri kuzjngumzia hali ya mtu. Kama kakwambia, alivokwambia ndo hivo hivo. Nikajifanya kuendelea kumchimba, its okay if you tell me, like i said we are close, closerthan you hav been told perharps. Akakomaa Dr, patient confidentiality inanibanaaa. Tukaanza kuongelea mpiraaa.

Jioni Sally karudiii, akanikutaaa. Akafurahii Dee, katukumbukaaa. Akamuita Feisal, zile hesabu uwe unampa kipanga Dee. Mi dada ako hamnazo. Nimekaa pale naona analetewa juice, mara snack, mara salad. Nikawa sielewiii. Akitaka kubeba kitu kizito Dr. Anamuwahiii. Akikaa anamuwekea mito. Nikawa nausoma mchezooo kimyaa kimyaaa. Bado sijaelewaaa. Akaaga kuingia chumbani, nikamfata huko huko.

Nikaenda kumuuliza Sally unaumwa unanifichaaa, unaumwa nini? Akasema Dee niacheee, ugonjwa ni siriii ya mtu. Ukiona sijakwambia ujue sitaki. Niachee bwanaaa. Akaja Dr. akasemaaa anatakiwa apumzikeee. Nikaaagaaaa kimya kimyaaa. Nikawa najua pale kuna kituu.

Nikampeleleza Lidya Sally anatibiwa wapi akawa very cold, bila sababu hataki tu kuzungumzia hill swalaaa. Nikawa sina jinsi zaidi ya kuwahi saa 10 usiku, nimvizie Dr nimfate nyuma nyuma mpaka hospital kwake. Na saa 12 akatoka pale, nikamfata nyuma nyumaaa. Nikaingia, nikatafu nesi, nikampa kilo 2 cash anilete file la sally! Aprint anileteee. The hustle is real, ndani ya nusu saa nikawa na copy nalo. Sikutaka papara. Nikaingia kwenye gari na kuanza kuisomaaa ripoti ya makanikaa.

Nikaona PREGNANCY! Whaaaaat! Nikaendelea kusomaaa. Nikaona ana mimba, ya miezi mi 2 na. Vovote iwavyo sio yangu, na huenda ya msomaliii. Tumbo likanikataaa. Kmaninaa kweli yule mngese kaondoka kaacha mbegu zake huku ziendelee kututibuliaaa. Na mitoto yake itakiwa misomali huwezi hata kujibambikaaa. Shenziiii wahid! Shubhamiit. Nikaendelea kusoma tenaaa. Mimba ina complications nyingi sanaa. Possibility ya miscarriage ni kubwaaa. Kizazi chake kiko wazi. Kwa hio imebidi ashonwe huko chiniii ili mimba isitokeee na atatakiwa kukaa bed rest mda woote wa ujauzito bila kufanya kazi ngumu.

Nikajikuta tu namuonea hurumaaa. Mbonaaa balaaa hilooo. Uzazi gani tena huu mgumu hiviii, maskiniii, na mume wa kumdekea hanaaa. Au ndo kaamua ampooze dr amuhudumie. Ila si kashonwa huko chini so Dr nae hapati kitu. Itakuwa yupo kwenye payroll. Sasa si gharama sanaaa. Nikajikuta tu namuhurumiaaaa. Nikarusha ile karatasi nyuma ya gari na kwenda kwenye deal zangu.

Jioni nikampitia kwake, na kumpelekea mto wa nyoka. Mke wangu alivokuwa mjamzito ulimsaidia sanaa. Akashangaa mto vipiii. Nikasema nimeona unaumwa mgongo nikuletee ukusaidie balance. Tukawa kimyaaa. Nikamwambia Sally pole sanaa. Akamkata jicho Dr. Dr akawa anatoa ishara yeye hausiki na usnitch huu. Akaniuliza who told you? Nikajibu no body. Akaanza tu kulia. Isingekiwa lile li Dr. ningembembelezaa na kumbusuu busu labdaaa. Ila ndo hivo tenaaa.

Tukiwa wote akaja Tonnh, mshikaji wa chriss. Kutukuta akastukaaa sanaaa, na hakuelewaa, ila akajikazaaa kukaa na sisi. Akauliza Sally unalia nini? Nikajibu mimi baba mwenye nyumba ninae kaimuuj, anaumwaaa. Anajitia oooh my god unaumwa nini? Jesus! Moyoni nikasema tuliaaa wewe boyaaa hata kwa kulogaa uchi hapo hupewi you dont have what it takes. Dr. akadakia nenda ukapumzike.

Mi nikaaga, naona Tonny kajibakizaaa, nikamwambia Tonny hujiii? Akataka kukataaa nikamwambia you should. Akaamua kuja. Ni washkaji ila sio kihivoo. Nikaingia nae kwenye gari, akauliza Sally alikuwa analia nini? Nikamwambia najua mzee baba pale u anyapia nyapiaaa ila inabidi ustop maana sio ishu kwa sasa. Sally anaumwa sanaa. Akaomaa anaumwa nini? Nikampa report ya Hospital, akauliza she gave you these? Nikamkata jicho la una akili timamu wewe?

Akasoma nikaona nae anaanza kuliaaa. Nikapaki bar, tukaanza kunywa, man to man. Nikamchokoza hivi na wewe boya ulizania kabisaa utapewaa pale. Akasema the child could be mine! Nikastukaaaa! What? How? Akasema alivoondoka msomali alipewaga friendly mechi moja kama bahati mbaya hiviii. Na ilikiwa kavuu kavuuu. Nuksiiiii. Ilinipenyaaaaa mpaka kwenye Tigo hio taarifa na uwezekano mimba ni ya huyu boya na sio msomaliii ikazidi kunimaliza nguvu.

ITAENDELEA SIJUI LINI, MAANA KESHO NITAKUWA TRANSIT NA KESHO KUTWA NDO NITAKIWA NAFIKA UGHAIBUNI. LABDA JMOSI INSHAALAH!
 
Back
Top Bottom