Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

B alikuwa kaenda kwenye kazi yake ya ulinzi huko Arusha, ashanizoesha michezo michafu ya kufanyana fanyana mpaka basi. Kutwa mara 5 hadi 10 nilishaacha kuhesabu, tulikuwa hatujibaniiiii. Afu ndo kaondokaaa jamaniii, jamaniii. Na alivo mshenzi anaweza kupika skype video call saa 10 nilitaka kujua kama umelala peka yako. Haniaminiii, yaaani haniamini kabisaaa hata kwa kunitaniaaaa. Ni ile abiria chunga mzigo wako.

Na hivi security expart sijui ana ni truck sio kidogo. Akija mwenzenu atakagua millage za gari, moyoni nasema si nakodi bajaji tu au boda boda, atamuuliza dada, kaweka na mlinzi ambae anamuendesa yeye anavotakaaa kumpa habari zangu, nani kaja nani katoka, simu ndo kaifanyia sijui madudu gani anaona kila kitu. Sema niliwahi kustuka nikaanza kutumia simu ya dada.

Na ishu ni kwamba Dee anaumwa, sanaaaa, wanasema TB, wengine wanasema gonjwa kubwa, wengine kalogwa, hata haielewekiii kabisaaa. Mkitaka kujua anaumwa haswaa haswaaa karudi kuishi kwa Pendo. Kuhangaika kooooote karudi alipoanziaaa, ama kweli dunia duara, lazima urudi mwanzo. In short kila mtu anaongea lake. Mimi kilichonitisha what if Jolline was telling the truth kama kweli kawaambukiza gonjwa kubwa?

Nikataka kupiga na simu hii, namjua Dee angeweza kuanza kuongea upumbavuuu afu akaniaharibia, nikachukua simu ya dada na kumpigia. Haikupokelewa. Nikatuma sms mi Sally. Nikapiga tena akapokea kwa udhoofu mkubwa Hello! Nikamuuliza kwema, nasikia unamwa? Akajibu naumwa sanaaa Sally, naumwa sanaaa, niombee kwa Mungu tu, siku yoyote utasikia ya kusikia. Nikamwambia pole, nitakuja kukuona.

Sasa B namwambiajeee naenda kumuona Dee? Weeeeeeeeee! B ni mtataaaaa! B ni mtataaaa msisikieee. Mi sikuwa namjua sanaa mpaka majuzi tumeanza kuishi nae. Ilianza gari yangu kusumbua. Inakata tu moto paaah! Afu benz zile mafundi umeme wa magari sio wengi. Kuna fundi wangu akawa anakuja nampa 50, laki anashika shika natembea siku 2, umeme unakata tena, nampa tena, natembea wiki 3 au 3 kitu paaah. B akawa anaangalia tu.

Siku hio fundi akaja, sina hili wala lile, akasema fundi kwanini unamuibia mke wangu? Nikashangaa yamekuwa hayo? It was rude mjueee. Nikaamua kukaa kimya maana ashavurugwa. Akamwambia sasa basi chukua hii gari, nenda nayo kaa nayo kama wiki au mwezi au mwaka utajua mwenyewe ila ikirudi hapaaaa, sitaki kuona inapata tatizo hilo tenaaa. ikikata moto nakuamisha huu mji, hakiiiii vile nakuapiaaaa.

Fundi chupi ilimbana akiliangalia jitu lenyewe miraba nane, maana sio mi nne, mi tatooo kibao, baunsaaa. Akaona atahamishwa mji kweli. Akachukua akarudisha jioni, nawaaambia haikukata moto tenaaaa. Natumia kwa raha zangu sin wasi wasi. B kulitest kama limepona kaenda nalo Arusha jamaniii, anamwambia fundi uwe kwenye Dar express likata moto njiani utatafuta Helicopter kuja kulitengenezaaa. Kaenda karudi badi zimaaa. Nikaliuza na niliemuuzia hakulalamika kabisaa.

Ikaja gari yake sasa ikasumbua, akamuita fundi huyu huyu. Akamwambia tengeneza, fundi akasema vifaa kaweka vya elfu 70, mi niliona pesa ndogo. Akasema hapanaaa! Wakaanza kubishana. Nikasikia ngoaaa ngoaaa vifaa vyote ulivowekaaa usinilletee umaku. Si ukingoa hivo vifaaa gari halita tembeaaa? Ngoaaaa vyoteeeee!, tulipakiii hapo, nitaita break down. Fundi akawa mpolee oooh nipe hata 20,000 mi namuchia Mungu, akasema sinaaa, we ngoaaa. Fundi akasema mi namuachia Mungu ndo atanilipia. Tukaondokaaa. hahahaaaaa! Tukaenda kwa fundi mwingine, akamwambia tatizo ni betri afu anatumia sanaa radio siku nzimaa, fu, aache kutumia hivo vitu aone. Na haikusumbua tenaaaa. Ndo nilipojua B ni mtata. He is only sweet to me!

Kwenda kumuona Dee ni lazima na huku ulinzi ni mkaliii. Nikamchukua Hudda na kwenda nae, anapenda kwenda kumuona kaka yake wa hiari sanaaaa. Nikamkuta Pendo kavaa glopes na mask. Nikasema hii labda TB kweli. Nikamuuliza vipi hali? Yupo hali si hali, roho inaniuma sanaa Sally, raha tule wengi, afu zigo nibebe mwenyewe. She threw me a shade. Nikaipotezeaaa, na kuuliza anaumwa nini?

Anachoumwa hakijulkani, Ukimwi wanasema hana, ila nachukua tahadhari vile vile, labda carrier wale akipimwa hauonekani, ila anao, kama vipimo vyotee ni negative nimemuita mpaka mdogo wangu kabisaa asingeweza kunidanganya kasema he is negative wakati dalili zote anazo. Nikamuuliza TB je? Akasema nayo hanaa japo ukimtizama anayo. Nikamwambia kwani India walisemaje, akasema walimrudisha tu maana hakuna wanachokiona. Ndo anataka kwenda ujerumaniii. Ila roho inaniumaaa sanaaa, kahangaikaa kayakumba huko ndo anarudi hapa, na anajua sababu nyumba yake siwezi kumfukuza wala kuondoka, nakwambia Sally nisipomuwekea sumu sijuiiii, hilo wazo linanijia kila dakika. Jicho lilinitoka kama mjusi kabanwa na mlango.

Akanipa Mask na Glopes, sikuvivaaa, akaniambia shaui yako, una mtoto wewe, jitie unajua kupenda hapa maisha yashakunya. Nikaingia ndani, kweli hali sio nzuriii kabisaaa, kabisaaa. Na mgonjwa nae hivi aliwaza nini kurudi kwa Pendo mkinga amtunze? Matunzo pia hayakuwa mazuri. Chakula kiko hapo hakijafunikwaaa, nzi wamejaaaa. Duniani tunapita Dee alikuwa anatia huruma. Ujanja wote kwishaaa, body kwishaaa, kabakia mbavu tupu. Nguvu za kukaa hana. Simu kuishika anapepesuka.

Hamu ya story hamnaaaa! Namuuliza unamwa nini? Akasema amerogwa na mpemba! Waligombana na mpemba kuhusu mwanamke akasema nitakukomeshaa. Nikasema huyu virusi vimekula mpaka akili. Ila nikawa namuitikia tu kweli kabisaa. Basi ananielezea kisa cha mpemba kumloga hata hakieleweki. Pendo alikuwepo hapo hapo. Dee akikohoa Pendo anavaa mask vizuri, mkinga hana masihara na afya yake.

Pendo akatoka, akaanza kuniomba ahamie kwangu nimuuguze. Jamani life is really a bich, kukataa siwezi maana yeye aliniuguza nilivojifungua. Kukubali siwezi maana B ataninyonyoaaa au ataondoka bila kuaga wakati ndo roho yangu. Ni kweli pale hata lishe ilikuwa ya wasi wasi, compassion pia ya wasi wasi, na ashasema atamuwekea sumu hali ilikuwa si hali. Nikamuuliza kwani wale wadogo zako wa kike vipi? Akaonesha tu sura ya kukata tamaa, ofcourse waume zao hawawezi kukubali hili zigo. Nikamwambia tu i will find a solution. Basi ndo kunisistiza Sally usinitupeee, i have no one, alijua kutia huruma nyieee, mpaka nikasikitika.

Nikatoka na kuongea na Pendo kidogo, walau nimsaidie kumpikia Dee japo siku hio moja. Pendo curved me the entire day ananipa vijembe. Bora wanawake wa Dee tungekuwa tnapeana zamu kama tulivokuwa tunapasishiana dude lake kama mbio za vijiti mbona kumtunza sio ishu. Bado Jolline, yule mtu mzima kileja mwenye mume, lile shangingi la hotel na wengineo. Ngoja niwatumie sms kwamba zamu zao huku nawaambia kabisaa mimi nishamaliza ngwe yangu, Sally ndo kaanza, na wao wajiandae.

Namwambia Pendo i am sorry i tokk Dee from you ambae hata wewe ulinikuta kwake vile vile. I am sorry, maisha yashanifila kwa niaba yako kwa kosa hilo vya kutoshaa na ulisherekea mpaka basi, so now give me a break! Akachekaaa na yalijua kukufila bila mate wala KY. Nikachukua kuku mzima, na kumbanikaa, akastukaa unataka kumbanika wooote? Nikasema Pendo acha ubahili na kujibanaa wewe, wote ndio. Akaguna tu, hajaacha uchoyo.

Basi nampa story, mwenzio siku hizi nina bwanaaa shoga angu! Akadakia haya umempora nani mume safari hii? Maana tangu uporwe msomali unapora mji mzima mabwana, utaemkuta njiani ahalali yako. Pendo was still carving me for taking Dee back from her. Nikawa tu muelewa. Nikamwambia sio mume wa mtu shoga angu. Bwana wangu wa zamani. Akagunaaa kwa wivuuu ana wivu mkinga yule ni balaa! Nikamwambia hana hata kituuuu shoga angu mlinziiii. Akachekaaaa kwa dharau mking yule nae. Ila nampenda ni balaa. Nikapeleka supu Dee kijiko kinampepesusha, ikabidi sasa kumnywesha na kikombe.

Nmwambia Pendo shoga angu mmetembea lakini we si mkinga wewe, si unasikia anasema kalogwa na mpemba! Pendo akajibu, huyo Mpemba kaniwahi tuuuu nilitakiwa nimloge mwenyewe, nimmalizie mbali nisha mchelewa. Namwambia sasa si uhangaike, utembeee. Akanishushua shushuo si la nchi hii. We nawe si alikutomba sanaaa tu, mapa kukula Tigo, unaonaje ufanye hio kazi ya kwenda kushika manyanga kwa waganga, na kuvunja nazi njia panda uchi, anaweza kupona bwana wetu. Tushirikiane tunatoka wote uchi usiku si unajua misherti ya waganga, wewe unaenda njia panda kuvunja nazi mi naenda kulala makaburi kama sio kutumbukia baharini mara 7. Kwanini ubooo tusaidiane ila kuingia kwa mganga na makalio tabu hio nifanye peke yangu. Sifanyi ungese huo, kama kumuangalia ajifie hapo, wooooote tutamuangalia ajifie, msikae kabisaa kuwaza Pendo atahangaika, hakuna kitu kama hikoooo. Hahhahahaaa! Nilibaki nacheka kama mazuri. Nikapika pale mtori, na kumsimamia anywe na dawa zake, jioni nikaondoka.

Tumefika nyumbani namkuta B kajaaa tele! Sijui kaja saa ngapi na kwanini dada asinipigie simu. Nikajikausha tu, hello baby kanuna. Anajibu short short. Nikajua tayariiii kishanukaaa, na bora nilikuwa na Hudda. Akawa anaongea na Hudda, Hudda hana dogo anasimulia, uncle Dee is sick, is really sick, he is like a skeleton. Nikazidi tu kuchoka. Nikiwa sina hili wala lile, kwanza namuwaza Dee anavopigania maishaaa, nikaamua leo sitaki maneno na B. Nikamlaza Hudda chumbani kwake na kwenda chumbani kwangu kulala. Nikamuita dada na kumwambia inabidi anede kwa Dee akamuuguze yeye si nesi, nitamuongezea pesa. Kwanza dada anamuheshimu Dee mpaka basi, si ndo alieniletea, kusikia anaumwa, akasema nitafanya dada kwa moyo mmoja bila hata pesa. Nikamwambia mkewe kidogo kavurugwa, pesa nitakuwa nakupa mimi. Itabidi asubuhi uende maana hali ni mbaya sanaa. Akajiandaa saa 12 akaondoka na Hudda akaondoka.

Ugomvi ukaanza huku, dada kumbe B alimuuliza anaenda wapi, akasema ukweli. B kaniweka kiporo. Tulivobakia wawili ndo kalianzishaa, anauliza Mimi humu ndani nani? Kidogo nimjibu mngese tu kwani nani nikaamua kukaa kimya. Anagomba kwanini simshirikishi kwenye maamuzi yangu? Kwanini nimeenda kumuona bwana wangu wa zamani bila kumuaga, na kwanini nimemtoa dada bila kumwambia, namuona mngese sio, kwamba nachotaka hakina shida? Nilipata tu busara ya kunyamaza kimyaaa. Ka rap na ku hip hop hapooo mimi kimyaaa naangalia zangu chini. Akamaliza haya niletee chai. Yaani nilitumia nguvu ya ziada kumpelekea ile chai ila moyoni kwangu nakujua mwenyewe.

Akaingia ndani na kutoka na bag, naenda Mogadishuuu kikazi. Nilitakiwa ni mind na nini, ila mda huu nilipata furaha ya ajabuuu maana nitafatilia mambo ya Dee kwa ukaribu. Mpaka atoke Mogadishu leo hio. Nikapata mood ya ajabuuu, na kumfata baby Mungu akujalie ufike salamaaa, urudi salamaaa, mimi na Hudda tunakupenda na tuta kungoja. Nikaenda kumkumbatia kumbatiaaa kama si mimi, nampa mpa kiss za mateee, nikasikia kadindaaa. Hapo hapo sikawiziii. Nikatengeneza mazingira mpaka mechi ikapigwaaa.

Baada ya mechi ndo anaongea kistaarabu sasa mi bwana mambo unajiamulia tu sipendi sijui nini. Na mimi namuomba msamaha wa kinafki. Mechi moja huanzisha ingine, akajikuta anaenda airport na piki piki. Na ibakia nuktaa aachwe na ndege. Dada jioni akarudi na kunipa amendeleo. Kesho tukaenda wote. Kidogo lishe ikaanza kumpa nguvu. Nikampelekea ma alovera, glnd, trevo nampa zote kwa mpigo.

Nikaanza kuwapigia wale wataalamu wa kurogaaaa na kupulizaa wanaojua waganga mpaka wa malawi, pemba, zambia. Wanga OG. Nawaomba namba za waganga. Wananishangaaa mganga mwenye simu sio mganga tapeli, kama nataka wanipeleke. Nawaza kuloga sijawahi nitaweza uzee huu, mara mganga aniloge niwe mkewe. Roho haitakii kabisaa.

Nikaamua kumpigia shoga angu Winni anawajua wachungaji. Akanipa namba ya mchungaji, nikampigia akasema yuko busy sanaa, kwanza hanifahamu, anatoa huduma kwa watu wa kanisani kwake kwanza maana ndo kondoo wake. Navoshinda pale na Dee, nampigisha story, sivai mask kama Pendo na glopes, namuogeshaa akapata faraja sanaa, na kuanza kupata nafuuu. Anaumwa bado ila kidogo nuru ikarudi.

Tunapiga story kidogo maana dhaifu sanaa, ananiambia you were the woman for me! Na mimi namwambia I begged you ukanidhalilisha mbele ya jamii, ukaenda kuoaaa shoga angu, i was not the woman for you. Anakosa rahaaa, naona virusi ndo vinakaza mwilini. Nambadilishia topic. Utaponaa Dee, muamini Mungu. Anasema i dont know Sally! I just dont want to die. I am afraid to die. Nampa mpa moyo pale.

Ikabidi nijiongeze kwa mchungaji sasa, nikampigia na namba ingine, kwamba nataka kutoka sadaka kubwa kama 2 million in cash, ila sina mda wa kwenda kanisani kumfata. Mungu kanitendea makubwa sanaa nataka kumshukuru. Akaniuliza uko wapi nakuja sasa hivi nielekeze ulipooo. nyamaaaa! Nikamuelekeza akaja, pesa nimeziweka mezani, pembeni ya mgonjwa. Akamuona yule mgonjwa. Akamtazamaaaaaa akakaaa kimya.

Nikamchukua zile pesa na kumpa, Nikawa namsindikiza, sikumwambia muombeee wala nini, nimempa unconditional! Akaniuliza yule mumeo? Nikamwambia hapana, rafiki yangu. Akaniambia WIKI IJAYO JUMAPILI ATAFARIKI. Nilipigwa radi si radiii, shoti si shotiii ya umeme nikajikuta nimekaa chini na mkojo umenipenyaaa. Akasema usifadhaikeee Mungu anakupendaaa dada, Mungu ni mwenye nguvu. Akaanza kuondoka hivi hivi.

Nikamfata muombee basi japo safari yake iwe nyepesiii kidogo, au muombee aponee. Please! We have money, we will give you money. Mchungaji akasema it is not about the money! Na hizi pesa nimechukua sababu umesema ni sadaka, na zinatoka kwako, zingetoka kwake nisingechukua. Nikawa sielewi elewiiii, namuuliza mchungaji eeeeh?

Akaniambia VITA YAKE NI KUBWA SANA. Hata nikikwambia hutosadikiii, wala hutoniamini, ubarikiwe mama kwa sadaka yako, mi naenda. Nikamwambia mchungajiiiii can you really let a man die? Just like that? Mchungaji akasema he is willing to die. Mwambie nimuombee kama atakubali, akikubali namuombea hapa hapa right now and then. Nikamfata Dee na kumwambia mchungaji anataka kukuombea, alistukaa kama kabanwa na mlangooo, akasema NOOOOOOOO! Namuuliza kwanini we si mkirtuuu wewe, akasema we hujui, ila sitaki kuombewaaa. Pendo akawa anatizama tu ila hashangazwi na yanayo endelea. Namwambia Pendo ongea nae basi akubalii, akaniambia Sally we hujui. Huu ndo mwishooo.

Mchungaji akasema nilikwambia, sasa mimi nakwenda zangu. We endelea kuzungumza nae, akiamua vinginevyo nipigie mi nitakujaaa, ila hata jumapili yenyewe mbona mbali. Nikamwambia how can you say that pastor! Akaniambia mwenyewe anajua lakini. Na Pendo anajua ndo maana hawahangaiki. Nikawa sielewiii elewiiii kabisaa. Jioni naenda kumuaga nimpe dawa na chakula kakata kauli kabisaaa. Pendo ananiambi ataendelea vizuri nyie nendeni tu nyumbaniii.

Tukaondoka nikafika njiani nikampigia mchungaji aje afanye aafanyavo ajeee, Akasema peke yake hawezi kumuombea wanakuja kanisa zimaaa. Nikawaambia waje. Kama nilihis Pendo atagoma tusimuombee, nikawaita kina Lidya na watu woeee, kina Chriss. Kweli alianza kukataa kataaa, alivoona watu wa kijiweni wanamjia juu kwamba basi yeye ndo anataka kumuua, na wakamkazia akifa tutahakikisha atamla nyama mpaka aishe, haiwezekani mtu kakata kauli afu anamficha ndani. Paligeuka uwanja wa vitaaa. Pendo akashindwa, akasusa akaondoka, akasema akiwafia mumle nyama wenyewe.

Tukaingia na mchungaji na kanisa lake loote. Wamebeba silaha si za nchi hiii, mafuta ya mizeituniii, chumviiii, maji ya baraka, uvumbaaa, mane mane wako full, biblia zisizo na idadi. Wakaanza sasa kumuombeea. Wengine tunachungulia kwa mbali. Si alikuwa kakata kauli. Likaamka li pepo hilooo babu lao. Linaulizwa we nani? Linajibu Makata wa Makata. Waumini wenyewe walijikunyataa maana hilo ndo kubwa lao. Mchungaji akakazana mko wangapi? Anajibu tuko Jeshiiiiiiiiiiii! Mchungaji kakomaa jeshi ndo wangapi? Linajibu ALFA LELA ULELA. Manake wasio na idadi.

Anaomba anawamwagia maji, wamewasha uvumbaaa, wanachoma chumvi ya barakaa kwa fujoooo. Wanalalamika unatuoneaaaaaaa! Unatuoneaaaa! Tunamdaiiiii huyu, hatutokiiii, sababu tunamdaiiii, tuna mkataba nae. Tumempa mali za majini, sasa zamu yake kuja kututumikia ujinini. Tunamakubaliano ane, ashamaliza miaka yake ya sisi kumtumikia sasa zamu yake. Ndo watu kijiweni kubakia khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Kumbe utajiri wa Dee utajiri wa majiniii na kugawa maishaaa? Looh!

Mchungaji anagombana nao, huyu si wenu, huyu ni wakristo alibatizwa kwa damu ya Yesu iliomwagika Calvary, hamna mamlaka nae, nabatilishaaa mikataba yote mlioongia nae, naifuta kwa damu ya Yesu, chumvi hii ikamfutie roho zote za mauti, roho za mapoozo, roho ya vifo, na akapate uzimwa katia bwana wetu yesu kristo, kwa malaka niliopewa na mbingu na kwa malaka niliopewa na Mungu baba aliejuuu nawa amuru mtokeeeeeeee na mchukue kila kilicho chenu katika maisha ya huyu Deus! Iliandikwa vyote nitakavyo vifungulia duniani vimefunguliwa Mbinguni naenda kumfungu Deus kwenye mikataba yote ya kipepo, kiibili, kishetaniii, kichawiii, kamajini na kinguvu za gizaaa, naenda kumweka huruuuu kwa Jina la Yesu lie hai..........!

Mchungaji aliombaaa aliombaaaaa, wale wadogo wote wakaondoka likabakia kubwa lao sasa ndo bishii hatari. Limekomalia tunamdaiii tunamdaiii, mi nimetumwa nirudi ane, siwezi kurudi bila yeye. Mchungaji anakomaa huna mamlakaaa katika jina la Yesu! Huendi nae kokote. Anaombaaaa Holyghost fireee, linaungua linapiga ukungaaa, Japo alikuwa amekondeana ila Dee alishikwa na watu 15 na aliwashinda nguvu. Walijitutumua kumshika asijiumizeee. Tumeombaaa tumeombaaa maana Dee akawa anapigania roho yake.

Jini linalamika, alikuja Congo, kutaka utajiri kwa mganga, akapewa masharti, akakubali, na utajiri kapewa kwanini tunataka kuleta dhulumaaa. Anakomaa mkataba ufatwe. Mchungaji anapamba nalo hauna mamlakaaaaa katika Jina la Yesu kakombolewa na damu ya Yesu. Pambana pambanaaa, akalifungia kuzimu sasa. Dee akazimia sasa. Flat kabisaaaa. Masaa 10. Haikuwa kazi ndogo.

Akazindukaa, akaambiwa leta kila kitu chao tuchome motooo, kikibakia tu amekiwshaa, vyoteee ulivopewa na mgangaaa. Akatoa aple chungu uvunguni, hirizi, usinga, kumbe mjinga alikuwa mshirikina sio kidogooo. Mwanga mwanga kweliii mpaka kuwa na chungu sio mwanga mtoto huyo. Akaulizwa mara 100 ndo vyote hivi? Akasema ndio. Wakamwagia mafuta ya mzeituni na kuviwashaa moto. Akaambiwa sasa mali zao zitaanza kurudi moja moja. zilipotokeaaa. Na wakaondoka nae kwenda kanisani maana Pendo nae haaminiki kabisaaa.

Wenyewe hsawaa mimi niliewahi kuwa mwanamke wa Dee, nikawa sikosi maji ya baraka, chumvi ya baraka, kwenye pochi mda wote. Sjiamini amini. Na mimi na familia nzima nikaanza kusali huko kwa mchungaji. Dee akawa anaishi kwa mchungaji kabisaaa. Na ndani ya huo mwezi gari zake 4 semi trella ziendazo Kongo zilipata ajali, mali zikapotea potea porini huko. Bank wakawa wanamjia juu rejesho wanatak kuuza nyumba zake. Vingine anauza mwenyewe apate mtaji, mtaji unakataa. Alianza kufilisika hivi hivi tunamtizamaa. Mchungaji akasema vitaondoka vyoteeeeeeeeeeeee, siku senti yao ya mwisho ikiisha Dee ndo atakuwa huru, hawaachagi kitu wale. Atabaki kama siku aliokuwa anaenda kwa mganga kuomba utajiri ndo watakuwa wamemalizana nae. Akazane na maombi. Pendo alirudi kwao Makete, watu wakawa wanasema kaanza kuumwa mambo yao na Dee yanamgeuka na yeye pia.

Mtoto wao akachukuliwa na Chriss mpaka baba yake apone vizuri. Maana bado Afya ya mwili ilianza kurudi ila bado kichwa chake hakikuwa vizuriiii. Bado walikuwa wanapambana nae, mali za watu mchezooo. Afu watu wenyewe majini. Bado maruwe ruwe yalikuwa yanamtokeaa. Mnaweza kuwa mmekaa hivi akaanza kuona watu. Nyumba aliokuwa anakaa Pendo ndo ilikuwa ya kwanza kuuzwa. Sasa tukashangaa mbona ghafla hivo? Ndo kufatilia bank, kumbe alianza kufilisika mda tu, maana alifeli kurejesha mdaa sanaaa. Ikawa kimakosa sijui ndo kichawi nyumba haikuwapo kwenye orodha ya kupigwa mnada, waliofeli nae nyumba zao zishauzwa kitambooo sanaaa miaka mi 2 iliopita. Ndolast month wamegundua hiko kitu.

Niliskitika sanaaa, ila B akawa amekaa miezi mi 2 Mogadishu akasema anakuja tuonge maonezi serious makubwaaa. Nikashangaaa makubwa mbona yanafululizanaaa.

ITAENDELEA
 
DOOOOOOOOOOOOOOOH!
DIIIIIIIIH
DAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAH
DEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
DUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUH!
 
Back
Top Bottom