Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

Kwenye kuandaa events tu uko juu
Stori za ckuiz ndefuuu mno ngachokaa
 
The beginning of the journey!

Akiwa ofisini hana mood kabisaa, kama ilivo kawaida yake siku zote hana mood ya kazi, ukisikia kufanya kazi kwa mood ya kujifosi ndo huko akasikia wenzie wakilalamikia performace review za mwaka huo. Na kulalamikia kitendo cha Pendo kuongezewa mshahara. In short mshahara uli double. Na figisu figisu ni kuwa anaongezewa mshaharaaaaa.

Da Sessy ndo analalalmika sio fair kabisaaa kuongezewaaa, wenzie wote tumepigwa unsatisfactory! Mishahara ileile mwaka wa nne huu. Itakuwa anampa bosi kipapa sio bureee. Itakuwa anampa boss kipapa lazimaaa. Mwingine akadakia atakuwa kampa nyama ya Tigo, mshahara ku double sio rahisiiii. Ikawa ndo maneno ya mkosaji. Mda wote Violla anacheza tu Zuma Deluxe hachangiii.

Ndo Malcom kumuuliza Violla mbona huchangiii? Au umeongezewa mwenzetu? Violla akajibu ofourse nimeongezewa 150,000 hahahaaaaaa! Basi wakaanza kumponda 150,000 tu ndo anataka kuzaa na uongozi kabisaaaa, jinsi gani alivo mtumwa huru. Ikikatwa kodi hilo ongezeko la 150,000 kwenye basic pay inabaki sh ngapi sasa za kumfanya yeye awe kimya badala ya kuunyambua nyambua uongozi.

Violla kama kawaida yake hakopeshiii, ila siku hio akaamua kukopesha. Wakaendelea kuchongaaa. Lau akawakumbusha wakumbuke yule Violla wanaemchokonoa akianza kuongea pale watatamani asingeongea. Ila Sessy akazidi kushupalia hilo swala la Violla kuwa mamluki, na kudiriki kumuweka kundi moja na Pendo.

Violla akaamua kunya sasa kama noma na iwe nomaaa, akapose ZUMA lake. "Lets be realistic here, hata mimi ningekuwa boss nisingewaongezea hata 10 cause hamstahili. You busy counting other peoples blessings badala ya kuangalia mjikwamue vipi. Kama Sessy umri unaenda shule huongezi, hio advanced diploma ndo umefika hapo kabisaaa, certification hujafanya, kimasters cha uzushi hunaaa, short cause ndo kabisaaa hujigusiiii, busy na mume, busy na familia, sasa boss akuongezee hela ya nini labda? Sawa you not so bright in school toa basi Chiu na Tigo kama huyo Pendo ubebwe na wanene wa humu napo hutakiiii. Lau ndo zile siku 67 za kuumwa unazimaliza na kuongeza za kwako. Usipoumwa wewe, ataumwa mkeo, ataumwa mtoto bado siku ya kuumwa House girl tu. Boss anakuvumilia sanaaaa. Siku nikiwa mimi boss naanza kuomba resignation yako. Willemi ndo sijui nianzie wapi? Mwaka wa 3 kazini you have no clue hii idara ya masoko tunafanya nini. Degree yako lazima ilikuwa ya pichu tu, huwezi kufanya hata ki project kidogo bila kusaidiwa, umezoea kubebwa bwbwa tu humu, honestly sijui uongezewe hela ya nini. We Side sawa you bright, kazi unafanya vizuri sanaaa sanaaaa, tatizo lako itikadi zako za ki CUF unaleta mpaka ofisini. Saa 10:00 kamili unaondoa bag hata boss humuagi. Jmosi kukanyaga hapa ni mwiko kwako. Kaka angu kujikomba hukuumbiwa kabisaa. Sasa ofisini ni mchanganyiko wa kazi na siasa. Kazi unafanya ila siasa zimekushindaaa kabisaaa.

Pendo mnamsema vibaya ila she earned that salary. Anakuja saa 12, anatoka saa 6 usiku. Boss hawezi kutoka bila kumuacha pendo humu, na hawezi kuja akakuta Pendo hajafika humu. Pendo hajawahi kuumwa hata siku moja tangu aanze kazi. Pendo ana masters 2, moja kaja nayo, ingine kaipata hapa hapa. Pendo anambebea boss bag akimkuta chini, anaenda kuuliza kwa boss kama kuna kazi ya ziada apewe afanye wakati huku kazi zikija tunavuta midomo kama chuchunge. Pendo huyo huyo she always goes extra miles katika kila analolifanyaaa. Mauzo yalivokuwa mabaya humu who gave a Fack? Ila Pendo hakulala mpaka akaja na ile strategy ya social media mpaka tume bounce back, bila kuambiwa kafikiria mwenyewe, katafuta solution, kaja kuuambia uongozi na hakupewa hata bonus. Nawaambia leo hii Pendo lazima atakuwa director kama sio hapa hata pengine because she has what it takes to succeed in corporate world."

Wakawa wote wamevimba sasa si kwa majibu yale. Wakamuuliza "if you so smart why are you still one of us?" Violla akawajibu because i have 100000000000000 problems, so it is pointless to solve one, ndo maana nimemuachia tu Mungu. Hata nikipata nafasi ya boss matatizo yangu yatakuwa pale pale. The difference between me and you is I have a choice but you dont! I can be boss if i decide it is what i want i have the ability to make it happen, but you cant be anything even if you want to. It is os hard to be you" Wakaangaliana na kujiuliza huyu demu vipiii? Mzimaaa kweli! Sessy akamjibu

"We dare you Violla to take boss's postion in 6 month" Violla akawauliza and if i get it what is in it for me from you guys? Lau akaanza kumjibu "I will resign, and give you my resignation on your first day in boss's job" Sessy akajibu "I will get the masters and certification same year." Willemi akadakia "I will learn all there is to know about this job. Akabakia Side hajasema kitu. Violla akamuuliza "Side bado wewe" Side akasema if you be boss madam, i will personally kiss your a.ss and every other ass in management. Violla akawaambia you all have a deal! Akatoa karatasi na peni, waandikishane, wakaandika wote wakajua Violla hatakuwa na nyimbo. Kwanza vivu la kutupwaaa, Pendo tu hamuwezi itakuwa boss?

Mchana akakumbuka ana brunch na mashoga zak nje ya mji hukooo, akatoka saa 4, Sessy akamchagizaa, aaah boss wa baadae huyo naona lunch yako leo imewahi? Hahahaaaaaaaaa! Wakacheka wote. Violla akatoka zake, kwenye lift akakutana na boss, akamuuliza vipi? "Aaah mkuu naenda kuchoma sindano hapo hospital nina sindano za masaa ujue. Boss akatingisha tu kichwa si kwa jibu lile.

Akadrive zake mpaka Jangwani Sea breeze. Kufika kule akajikuta peke yake, so akawa kakaa baharini anakunywa smoothy kama sio mda wa kazi vile. Akaja mkaka kumsalimia pale kwa bashasha nyingi, akawa anausoma mchezooo. Basi mkaka anajisemesha such a good day! Violla akawa anamjibu what is os good about it? Mkaka akaanza kuona kile kina kirefu sasa anajisemesha tu, the sun is shining bright, the wether is good, akawa kajilaza pembeni ya Violla.

Violla akawa anasoma magazine yake aliokuja nayo. Mkaka anasimulia when i was in Berlin sijui the beaches were the bomb! I wish i could take you to Berlin! Violla akamjibu tu Berlin huh! What makes you think i have never been there? Mkaka jasho likaanza kumtoka. Akahama mji akaja Carlifornia sijui nilikaa pale miaka 7. It is so amazing! Such a good place to be. Anasimulia nakwambiaaa, kasoro tu kusema alikuwa jirani yake na Snoppy! Violla akamtwanga swali, so Mr. Diaspora what have you been doing lately in Town? Like a job or something!" Makubwaaaaa! Diaspora ane akakomaaa im doing my deals, you know, im not into being employed so i have my shit rolling, trying to work things on my own! Villa anamjibu tu "Mmmmmmhhhhhhhhhhh! so you are unemployed! Okay i get it! Why did you come back anyway?" Diaspora bado anokomaa, ooh nilichoka tu kukaa kule, i missed home, nikaamua tu kurudi, i love my mom, wanted to be with my mum you know kibao. Violla akadakia "You couldnt survive there too , too bad!" Diaspora akawa kashindwa yeye sasa, sio kwa u rude huo wa bibie Violla, Akawa kabakia Kimya tu.

Wenzie walivo mtext wako ndani wana order akamuaga Diaspora, thank you for the company dear, im rolling!" Diaspora akajitutumua "Can i get your number to halla at you, at times, say hi you know" Violla akaanza zake kuondoka akmwambia "Get a job then halla at me" akitegemea jibu lake lita mrestisha in piece Diapora, ila akamkuta tu anachekaaa kwa jibu lake, akaondoka kwa mikogo.

Kufika kule akaanza kujadili na wenzie how the week has been any luck? Mwenzie akaanza i tried to make him propose but he didnt. And it is killing her, she cant wait anymore day. Mwingine akasema he met a guy, he is so nice, cant wait to meet him again on Saturday. Wakamuangalia Violla! Akajisemesha "I me a guy just right now, he is cute and all and ......" Akawa kaishia hapo. Wenzie wakamkazia macho, "And what Violla you are killing us" Violla akasita kujibu ila akamalizia " And i toasted him! I know i should have been nice. but he has no job, and he is stupid, slow thinker, i justed toasted him!" Wenzie wakaweka mikono kichwani. Yule aliesema he met a guy akadakia "My guy is also jobless but im going out with him anyway!"

Violla na mwenzie Sasha wakapaliwa kwa mpigo na juice zao, baada ya kusikia no job! Bibie Diana, mwenye jobles new guy akamwambia you never know, twende tukamtafute umpe namba, huwezi jua nini kitatokea, si kasoma lakini? Violla akajibu tu "I didnt ask him" Diana hakukata tamaa akamwambia twendeni sasa hivi itakuwa hajaondokaaa. Violla analalamika "Mus we do this?" Diana anamjibu huku wanatembea "Yes Violla, because you are getting any younger, wakawa wamefika beach, anamuuliza wapi Violla wapi mlikuwa mmekaaa. Violla akamuoneshea, Diaspora hakuwepo tenaaa, siti ikawa nyeupeeeeeee.

Wkaangaliana, Diana akavunjika moyooo, na brunch ikaishia hapo, kila mtu akaanza kurudi ofisini kwake.

ITAENDELEA KESHO SAA 5.
 
Hahahahaaaaaaaaaaaaa! Umekuwa Mange na Mzungu wake? Mimi simo kabisaa katika hii kesi mnayoichokonoa humu ndani
Hahaha kwa style hii umke wa mzungu umenishinda saa 1 asubuhi. Mange me naona anapendezaga akiwa chubby kusema za ukweli, especially usoni ila ndo mwenyewe yupo busy na diet zake khaa "size 0". Huo wito sina woyiiiii
 
Lara 1 nitakufanya kitu mbaya, I've left all my serious shit to follow this story and this is all I get? "Itaendelea kesho saa tano"?
Wenzio wana sponsor story we unaleta tishio tena ntakufanyia kitu mbaya..... Fanya usponsor kwanza mengine bidae
 
The unorthodox methods

Akiwa nyumbani anacheza game la FIFA, akasikia shemeji yake anafoka, "Mimi ndugu yako simtaki humu ndani! Ana mdomo sanaa, au jeuriii. Akapange! Jitu zee tunaka nalo la nini?" Akamsikia dada yake Tracy anamjibu mbona mama yako alikaa hapa anaumwa, nimemuuguza mpaka kanifia sikuwahi kumchoka au kumsimanga? Tena donda lile la kisukari la kukatwa mguu nimehangaika nalo mpaka mauti yake, linanukaa, linatemaaa, wewe mwenye mzazi wako hukuwahi kulifunguaaaa. Afu unataka kuniambia nini? Ndugu yangu mzimaa, ana kazi yake kwanini asikae hapa? Haami mtu hapa" Akasikia shemeji yake akifokaaa, ahameee, ndo anamjaza ujinga Vane, ugomvi wote wa Vane na mumewe ni kusikiliza maneno ya ndugu yako." Tracy akakomaa "Si ujinga wake, mama zima la miaka arobaini kwanini lizikize maneno ya kitoto cha 29? ahami humu ndani nasemaaa, napokaa mimi dada yake na yeye atakaa." Mzozo ukaendelea.

Kesho akiwa na dada yake mchana akamwambia kasikia kila kitu kuhusu kuhama. Dada yake akamwambia achana nae mpuuzi yule. Violla akamwambia sikia siku ingine wewe usibishane nae mwambie aniangalie usoni anifukuze kwake mwenyewe sio kukutuma wewe. Tracy akamuuliza "halafu akishakwambi?" Violla akmwambia amwambie tu afanye hivo yeye afu ndo itajulikana. Tracy akasema sawa kamanda kama unaona hivo ni heri sio mbaya.


Akiwa ofisini mtu akawa anasimulia, Mumewe anakuwa controlled na dada yake mpaka basi. Yaani yeye mke mtu hana hata sauti. Dada mtu yupo kwake kaolewa ila ana control kila kitu nyumbani kwao, kuanzia wanae waende shule gani, mumewe ajenge wapi, mpaka ramani ya nyumba kaitoa dada mtu. Site hesabu zote dada mtu anazijua. Mke mtu ile kutoa mawazo sebule ijengwe kawaida ila kubwa, dada mtu akatoa wazo sebule iwe ya kutumbukia kama underground kidogo. Mumemewe akawa anataka sebule ya kawaida ila dining unapanda ngazi kidogo.

Akaamua kumpa mambo mumewe mazitoo, anambembeleza wajenge sebule anayoitaka yeye, anampa mchezoo daily unconditionally, mumewe anamuitikia tu sawa baby wangu, haina wasiwasi. Siku ya kwenda site akakuta sebule imejengwa ya kudumbukia na dining ya kupanda. Roho ikamuuma mpaka basi. Sema ndo atafanyaje sasa. Ilionesha wazi alimpuuzia kabisaaaa mawazo yake. Akasua jumlaa hakukanyaga tena site. Wala hakuna aliemuomba akanyage.

Kwenye vikao vya familia bandugu dada mtu ana nguvu kuliko wanaume wa ukoo mzimaaa. Wote wanamsikilza yeye. Na asivompenda wifi mtu sasa? Kuna siku akajiloga kuchangia topic katika kikao, wacha wifi mtu amblast yeye sio familia pale, mtu wa kupita, so akae atulize mshono kama wajengezi wenzie. Tobaaaaaaaa! Akawa mdogo aje sasa.

Na what tops it all ni kitendo cha wao kuwa katika mechi na mumewe, ikilia simu ya dada mtu lazima mechi isitishwe kwanza mume aongee na dada mtu. Amejaribu kumnyima mechi baada ya simu, kununa, kulalamika hakuna kilicho saidia zaid ya kuwa hali ni ile ile, dada mtu akipiga simu hata saa 7 usiku lazima ipokelewe na akitakacho lazima kifanyikeee. Mume mtu hana sauti kabisaaaa juu ya chochote.

Na akahitimisha kwa kusema kuwa kachokaaa kabisaa na mambo hayo, yaani anangoja utokee mtanange mwingine, amwambie mume achague which is which. Kama dada au yeye. Na anaenda kufungasha na kluondoka kabisaa kiukweli ikiwa dada mtu atashinda mtiti huo.

Watu wakawa wanatoa mawazo hawezi kukuacha uondoke sababu ya dada mtu, atakupigiaje magoti sasa? Mda mwingine hawa wanaume inabidi uwafanyie suuu. Wanakupima unavojitia una busara wanazidi kukuendesha kama gari bovu sasa. Wewe uondoke watoto 2 inakuwaje hapo unafikir, lazima akili itamrudi atamblast dada mtu na kumuweka nafasi yake.

Akachangia Violla "Atashinda dada mtu" Afu basi akaishia hapo hapo pasipo kuendelea kuongeza kwanini au aje. Watu wakampuuzia mchango wake wakakubaliana amfanyie kweli dada mtu afanye kama noma na iwe nomaaaa. Sessy akamuuliza Violla umefikia wapi swala la kuchukua nafasi ya boss. Violla akamjibu bado ana warm up kwanzaaa. Wkamkumbusha deadline is 6 month! Violla akawajibu tu make it half of that time. Wakacheka woteeeee.

Akiwa bored anafanya mambo ya kawaida kutoa review ya campaign za Pendo, ikaingia whats up, toka kwa shoga ake wa kitambo sanaaa. Hi! Akamjibu tu Hi! Shoga akajieleza, i need your help dear, there is a man i love dearly nitafanya lolote kumpata. Yaani nimejitahidi imeshindikana kabisaaaa, nikakukumbuka kamanda wangu kwa ma idea huna mpinzani. Akaona it is getting interesting! Hard just the way she likes it. Pendo akaita "Viollaaaaaa!" Akainuka kumfata ofisini kwake, ila attention yote kwenye simu yake, akamjibu shoga ake "Mimina details sio kuzunguka mbuyu, umeshindwa wapi?" Huku Pendo anaongea yeye hata akili zake hazipo hapoa, akasikia tu Violla unaonaje? Sababu hakusikiza lolote akazuga naona poa tu, itakuwa nzuri sanaaaa. Pendo akabaki kumuangalia kwa mshangao. Akamwambia "Violla nimekwambia Willemi kakosea kuandika article nzima ya ile campaign na ishakuwa published na boss kaisoma sasa itakuwa nzuri vipi? Akastukaa na kuzuga zugaaaa. Akajibu tu anyway navoona tunaweza kuandika article ingine, kali zaidi itafanya ile article ya kwanza isahaulike kabisaaa. Pendo akamwambia anyway fanya kuandika hio article but kabla hujai publish ilete ni ireview.

Mmmmmhhh akaona kweli ilikuw blander sanaaa aliofanya pale kwa Pendo. Akarudi kwenye whats up yake. Ndo kumkuta shoga kajimiminaa sio kidogo sasa. "You know now im born again, nasali hili kanisa la hawa walokole, but there is this paster yaaani ananijaribu mimi, kila nikijitahidi kumtoa akilini siwezi kabisaaa. I have fallen for him and i have fallen hard! He is not married and stuborn as a bull, nimemtega wapiii, hategeki wala hata kuonesha dalili za ku noticeeee. Shoga nimeshindwa kabisaaa nifanyaje sasa." Mmmmh! Likamjia tu wazo "He is the man of Good for Christ sake!" Akasitaaa, akaendekea na kazi zake kama kawaida. Baadae ikaingia tena chat, "shoga usiniache juani, niokoe, nitakupa hata helaaa, nimekwamaaa, nakutegemea ujue" Akaamu tu kumjibu poa nitumie picha nimuone, kukulegeza hivo sio utani kajibiwa sina picha yake. Akamwambia no sweat nipe page id yake Insta au whats up Akajibiwa hayupo kote huko. Tobaaaa, Akahitimisha jpili naja huko kanisani kwenu nimuone huyo Le Pastor, Thee Man of God himself.

Jumapili ikafika akadamaka, dada yake nae akadamkaa, akawaandaa watoto uzuri tu, akawa anamwambia bora leo umeamua kwenda kanisani unisaidie hawa watoto ujue. Violla akamjibu mi neanda kanisani kwa walokole. Dada yake akadakia nini? Violla akamjibu tu naenda kwa walokole. Tracy akaanza kuwaka hivi mbona huna akili wewe, ukoo wote sisi ni waroma, bamdogo wetu alikuwa Askofu, shangazi yetu ni sista itakuwaje ukoke? Au ndo mambo ya kutafuta mume? Basi mdogo wangu sikuandami tenaaa swala la mume, usi okoke mdogo wangu. Violla akamwambia relaxxxxx, Roma ibada ya masaa 2 imenishindaa kabisaaaa, naenda kwa manati, itakuwa walokole, kuna ishu zangu nafatilia. Ogopa mimi kuwa mpagani kuliko kuokoka

(MODES ULIVOKATA HII STORY IMALIZE. MUENDELEZO SAA 2 USIKU.)
 
Back
Top Bottom