Baada ya kujifunza jinsi tunavyoweza ku-gawa kurasa yetu, sasa bado hatua chache tu, ili tuweze kumaliza kabisa kipengele hiki.
Tunafahamu kuwa, website yetu imekusanya mafaili mbali mbali ya taarifa. Mafaili yote ndani ya website yetu yanatakiwa kuonekana kwa mtumiaji kupitia file moja ambalo awali tulikuwa tunaliita file maalum na sasa tunaliita Web page au kurasa mtandao.
Baada ya kuona jinsi tunavyoweza kuandaa kurasa yetu, sasa moja kwa moja tuanze kuangalia ni namna gani tunaweza ku-display mafaili yaliyobaki kwenye kurasa mtandao (webpage yetu).
Katika darasa la leo tutaanza na jinsi ya ku-display Picha kwenye WebPage yetu.
Picha kwenye Web Page
Kama tulivyojifunza tangu awali, kila kitu kinachoongezwa kwenye web page ni element, picha pia ni element. Element zote huundwa na tag, tag inayotumika kuunda element ya picha ni <img>.
Tofauti na element nyingi ambazo tumeshajifunza mpaka sasa, element ya picha ni element pekee, ni aina ya element inayoundwa na Tag awali peke yake, yenyewe hujitosheleza bila tag tamati.
Ukifahamu element hii tayari utakuwa umefahamu jinsi ya kutumia mafile ya picha kwenye website yako.
Matumizi ya element ya picha
Element ya picha <img> , japokuwa haihitaji tag tamati ili kukamilika, element hii haiwezi kukamilika bila kuwa na kipambizo chazo.
Kipambizo chanzo ni kipambizo cha anuani kinachoisaidia element kufahamu sehemu ambayo picha ipo. Unapotaka kuweka picha kwenye Web Page unatumia <img> , Unakuwa umetengeneza element ya picha, lakini picha hiyo haitaweza kuonekana na kufanya element isikamilike bila kuongeza kipambizo ambacho kitaisaidia element kujua picha inayotakiwa ku-display.
Kipambizo (Attribute)
Kipambizo kinachotumika kukamilisha element ya picha ni kipambizo chanzo src, Kama tulivyojifunza kuhusu vipambizo, kipambizo hiki hufanya kazi ya kuipa element anuani ya picha unayotaka kuitumia/unayotaka ionekane kwenye element. Kipambizo hiki hutumika kama ifatavyo:-
src= "anuani".
Vitu vidogo vidogo kama hivi huwa vinafanya baadhi ya watu waone kuwa HTML ngumu kwasababu tu ya kukariri. Ngoja nikuchambulie kidogo kipambizo hiki ili uelewe na sio umeze.
Src ni kifupi cha neno source ambalo kwa maneno matamu ya Kiswahili linamaanisha chanzo, kwa hiyo kuandika src= "" ni sawa na kuandika source= "" au kusema chanzo= "".
Ndani ya funga semi na fungua semi unaweka chanzo chako(anuani). Kama picha yako umeiweka sehemu moja na web page yako, kwenye chanzo weka jina la picha tu likiwa na extension.
Ninaposema weka jina la picha likiwa na extension namaanisha kuwa, Mafaili ya picha yamegawanyika katika makundi tofauti tofauti. Kuna aina za picha ambazo ni jpeg, zingine ni png pia kuna gif, sasa unapoandika jina la picha kwenye anuani ni lazima uweke jina la picha likiwa na extension kulingana na picha husika na usipofanya hivyo picha yako haitaonekana.
Mfano: Kama picha yako inaitwa "bango" anuani yako utaiita bango.jpg au kama picha yako ni gif basi utasema bango.gif
Element ya picha ya kuongeza kwenye web page yetu tutaitengeneza kwa kufata hatua zifatazo.
1. Ongeza element ya picha
<img>
2. Ongeza kipambizo anuani kwenye element, src= "bango.jpg"
<img src= "bango.jpg" >
Wooooh! Ni hatua mbili tu za kufata unapotaka picha yako ionekane kwenye web page, rahisi sanaaa
Note: Hakikisha picha yako ipo sehemu moja na web page yako.
Tuishie hapa kwa leo, kwenye somo lijalo tutaangalia jinsi tunavyoweza kuongeza vipambizo zaidi kwenye element yetu, ili kuipa picha sifa na muonekano tunaotaka.