web designing inaumiza kichwa

web designing inaumiza kichwa

Mkuu Astro ninaendelea na updates zangu. Kama kawaida nilikuwa nimekuahidi kuijaza ile site full content soon. Nimemaliza sasa kwa kutumia tools sijuwi nyie mnaziitaga ni tools wakati sisi tunaziitaga ni software au program kama vile vile zilivyo program/software/tools zingine tunazotumia kila siku kama microsoft word au mozilla firefox, zote hizi ni tools/software/program.

Kwakuwa Mkuu zech naye yumo humu na ndiye alileta website yake hivi karibuni ambayo aliitengeneza from the scratch/code kwa mjibu wa yeye mwenyewe, hivyo basi nimetumia content za site yake: http://www.dsouza.co.tz kwa kutumia tools bila ku-code hata mstari mmoja. Sisemi hii ni nzuri kuliko yake la hasha, bali pamoja na kuwa nimetumia analogy (tools) na yeye alitumia digital (coding) kwa mjibu wa nyinyi, bado muonekano wake hautofautiani sana.

Mkuu zech hii ni kwa ajili ya kujifunza tu wala isikupe presha muda wowote tutaiondoa.

Nirudi kwako Mkuu Astro, nitarudi tena kuendelea kunyambuwanyambuwa maswali yako taratibu mpaka tumalizane.

NI HII HAPA: www.iyokopokomayoko.p.ht

Mkuu hii topic niliiona asubuhi ila nikashindwa kujibu kwa maana nilikuwa natumia simu ya mkononi, napata wakati mgumu kuandika maneno mengi kupitia simu. Nitajaribu kujibu maswali yako kwa lugha itakayoeleweka vizuri kwa kila mtu kwa manufaa ya wote.

1.Websites zenye poor code na hard to maintain/or modify-hapa ninamaanisha hizi (nyenzo)tools zinazofanya code generation hutengeneza kitu chenye muonekana unaoutaka lakini nyuma ya pazia [namaanisha kwenye hizo code zinazofanya hiyo tovuti yako ionekane unavyotaka huwa ni matatizo na haziweizi kusomwa na binadamu kirahisi]

Je kuna umuhimu wa Code kusomeka kwa binadamu?
Ndio umuhimu upo, pale utakapotaka kuongeza features na kukutana na hizi code zilizongumu kusomeka utapata shida sana na kama hauna uzoefu kabisa na kuandika ama kusoma codes unaweza kujaribu kufuta mstari ama neno moja na kuangusha kazi yako yote.

-Mara nyingi Hizi code zinazokuwa generated kuna neno wanaloita 'Bloated' yani zinakuwa na vitu vingi sana na kuongeza ukubwa wa tovuti yako, Kwa mfano kuna hatua ya kuhakiki kama taarifa zilizoingizwa na mtumiaji wa tovuti ni sahihi kwa mfano barua pepe,jina nk kwa kutumia code generation ya Adobe Dreamweaver unaweza ukapata mistari 15-20 wakati unaweza ukaandika mistari miwili ama mitatu na kupunguza vile vitu ambavyo havihitajiki.

-Kwa anayefahamu hizo code nini kimeandikwa anaweza kufuta vile visivyohitajika na kuongeza vile anavyotaka na kuwa huru katika kazi yake, kwa yule atakayetegemea code kuwa generated anaweza kujifunga na kupata shida sana hivyo ndio maana nilishauri mtu aanze kujifunza jinsi ya kuandika code na kuachana na njia za mkato.

2.Katika swali la pili-Nilipotaja h1,h2,p,a,images...
-Webpage yani Ukurasa wa Tovuti unaundwa na Elements (Vipengele) ambavyo ni muunganiko wa tags (vitambulisho) vinavyoelezea Web Browser (Kiperuzi cha Tovuti kama opera mini,Internet Explorer n.k) jinsi ya kuonyesha ukurasa kwa mpangilio sahihi...Kiperuzi (Web Browser) husoma hivyo vipengele na kuweza kurudisha muonekano uliosahihi (interpret/tafsiri code).

-Kuna vipengele vingi sana na Lugha inayotumika (Markup Language) ni HTML katika kuunda kurasa za tovuti. Ukurasa wa tovuti ni kama ukurasa wa kitabu ama daftari lako na umegawanyika katika sehemu kama Kichwa (head) na mwili(body).
Kichwa huwa na taarifa muhimu kuhusu ukurasa huo kwa mfano Jina La ukurasa wako na vielelezo vya taarifa za tovuti yako. Mwili (Body) huu ndio hubeba maelezo yote kama maneno picha unazotaka zisomwe na mtembeleaji wa tovuti yako.

Mfano vitambulisho hufunguliwa na kufungwa, vitambulisho vya kufungua (opening tags) huanza na namna hii <herufi moja ama zaidi> na vitambulisho vya kufungwa huadikwa kwa namna hii </herufi moja ama zaidi >

-Kwa mfano < h1 > </ h1>Ukiandika neno lolote katikati ya vitambulisho vilivyofunguliwa na kufungwa utapata kichwa cha habari kikubwa mfano < h1 >TAARIFA YA HABARI < / h1> Hiki huonekana kama maneno yaliyokolozewa kwenye kiperuzi cha tovuti. Muunganiko wa vitambulisho vya kufungua na kufunga na hilo neno huunda kipengele kimoja.

Ukitumia vitambulisho kama < h2 >,< h3 >< h4 > unamaanisha vichwa vidogo vya habari, namba inavyozidi kuongezeka ndio udogo wa kichwa cha habari (katika muonekano na hata cheo katika ukurasa)

  • Vitambulisho vingine kama < p > Hiki ni kwa ajili ya kuandika aya (paragraph)
  • < img >-Hiki hutumika kuweka picha.
  • lists hutumika kuweka orodha ya vitu katika ukurasa (kama huu unaouona hapa kwenye ukurasa wangu)
Ningependa kuoongelea sana HTML lakini itachukua sehemu kubwa sana na ninahisi kuna tutorial zimeshawekwa humu Jamiiforums kwa mfano https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/429224-html-tutorial-3.html
Ninaamini zipo nyingi sana na hata kwa kutafuta google waweza kupata maelezo zaidi.
Mfano wa HTML code ni kama hiyo hapo chini.
View attachment 108529
Kama nilivyosema vitambulisho vipo vingi sana ila si vyote utakavyohitaji kuvitumia katika kuunda tovuti yako,jaribu kuangailwa vitambulisho vilivyopo katika tovuti nyingi utakuta ni aina chache zinazotumia,

Kuviona vitambulisho na vipengele
  • tumia kiperuzi chako kufungua tovuti yoyote
  • Bofya right click(kiswahili chake sikifahamu)
  • Chagua sehemu imeandikwa view source code ama view page source (hutofautiana na viperuzi)
View attachment 108533
kwa njia hii ukiwa makini utaweza kujua ni vitambulisho vipi hutumika sana na jinsi ya kupangilia ukurasa wako.

3. Server Side Scripting Languages-hizi ni lugha (Programming Languages) zinazotumika kufanya manipulation (kucheza) na data katika upande wa server na kutuma majibu kwenye kiperuzi.

Hayo maelezo hapo juu yaweza kuchanganya kwa mtu asiye na ujuzi wa mambo ya computer.
Tuchukue mfano huu (nimejaribu kuelezea kwa njia rahisi sana na kuondoa baadhi ya maelezo ili kueleweka kiurahisi)
-Unapofungua tovuti kama Jamiiforums unatuma ombi lako kwenye kompyuta (Server) iliyobeba taarifa za Jamiiforums.
-Computer hiyo yani (Server) itatuma jibu kutokana na ombi ulilofanya kama ni kujibu topic ama kuanzisha topic mpya yenyewe itaangalia ni nini cha kukujibu, hiii yote huandikwa na wataalamu kwa kuiambia computer nini cha kufanya ombi linapotumwa.
-Lugha zinazotumika kuieeleza computer nini cha kufanya/kujibu pale ombi linapotumwa huitwa server side scripting language (Hutumika kutoa maelezo kwa upange wa computer iliyobeba taarifa za jamiiforums)
-Lugha hizi zipo nyingi sana kwa mfano PHP,ASP,JAVA-JSP,Python,Ruby, Sitoweza kuzitaja zote.

4. Adobe Photoshop-ni programu/software inayotumika kufanya mabadiliko ya muonekano wa picha/michoro.
Hii ni nyenzo muhimu sana kwa wasanifu wa website (Web Designers) kwa maana tovuti yenye muonekano mzuri huundwa na picha zenye mvuto mzuri na maumbo yanayoweza kumvutia mtembeleaji wako, kuna tools nyingine kama Gimp nayo ina uwezo mkubwa. Uwezo wa photoshop ni mkubwa sana unaweza kutengeneza picha na michoro mizuri sana wataalamu kama C6,Leh wameshaweka tutorial nyingi sana hapo nyuma kama
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...8-tujifunze-photoshop-tembocard-mockup-2.html
https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/317396-another-photoshop-tutorial.html

ambapo hata mimi niliweza kujifunza mengi kupitia kwao.

5.Search Engine Optimization-ni kufanya tovuti yako ipatikane kiurahisi katika search engine (hii ni mitandao kama Google.com/bing.com)
Jaribu kuingia Google andika neno kama Tanzania Forums, ya kwanza kutokea ni JF, hiii ina umuhimu gani?...Tovuti yako inapotokea mwanzo mwa matokeo inaongeza watembeleaji wapya wa tovuti yako, kama mimi ni mgeni katika forums na nilikuwa natafuta forum ya Tanzania kupitia google kwa namna moja ama nyingine ningejikuta nipo JF Hivyo Search engine optimization ni muhimu katika kuongeza watembeleaji katika tovuti yako.

6-Cross Browser Compatibility-Hii ni kuhakikisha tovuti yako inaonekana sawa kupitia viperuzi mbali mbali kwa mfano Internet explorer,Google chrome,Mozila etc. Usitengeneze tovuti inayoonekana kwa kiperuzi cha aina moja kwani hujui mtembeleaji wako atatumia kiperuzi gani, pale itakapotokea kiperuzi kimoja kinashindwa kuionyesha tovuti yako vizuri basi unaweza kuwa umejipotezea watembeleaji.
-Viperuzi vinavyosumbua sana ni Kama internet explorer 6-7 [hizi huwa na tabia ya kuonyesha muonekano tofauti wa tovuti ukilinganisha na viperuzi vingine vipya ila ni jukumu lako wewe designer kuhakikisha tovuti yako inaonekana vizuri]

7-Validation ya Markup-Hii ni kuhakiki kuwa HTML code zinazounda tovuti yako zipo sahihi na zinaendana na sheria zilizowekwa na mamlaka inayotoa sheria za tovuti W3C. Unashauriwa kufuatwa sheria zilizowekwa ili kuepuka matatizo kama muonekano tofauti wa tovuti kwenye kiperuzi kimoja na kingine (angalia namba 6)

8.Je nikitumia code generation tools nitaweza kufanya Search Engine Optimization,Cross Browser Compatibility na Validation Markup?
Hii inategemea na uzoefu wako na codes, kwa wale wajuzi hata akitumia code generation tool anaweza kurekebisha matatizo kama Cross Browser Compatibility na kuondoa Invalid Markup iliyotengenezwa na hizo tools bila kuharibu tovuti yake na hata kuweka Search Engine Optimization. Kama huna ujuzi na hizo code basi kufanya mambo haya itakuwa ni vigumu sana na hata kupelekea kuachana nayo kwa maana tovuti si inaonekana vizuri?, na Huu ndio mwanzo wa kazi zenye low quality.
-Utakapokuwa na ujuzi na code zako ndio utaweza kuwa na uhuru zaidi wa kufanya yote yaliyotajwa hapo juu kwenye swali.

Kwa kumaliza Mkuu japokuwa kazi yangu si web designer/web developer nina ujuzi wa kutosha kwa maana katika taaluma yangu nimeshayasomea haya mambo na kupitia juhudi zangu binafsi nikaweza kuendeleza ujuzi kwenye haya mambo, kwa sasa ninafanya kazi katika mambo tofauti lakini ninafahamu jinsi ya kutengeneza tovuti, ipi ni njia sahihi na nyenzo zipi zinafaa hasa kwa mtu anayeanza kujifunza.
Nikipata muda ninaweza kuweka tutorial hapa kuonyesha jinsi ya kutengeneza a simple attractive home page from scratch kwa kutumia HTML na CSS peke yake na kuonyesha jinsi hizo code zilivyorahisi kuziandika.

Nitakapokuwa nimekosea naomba nirekebishwe, Let us work together to Improve our society.🙂
 
Mkuu Astro ninaendelea na updates zangu. Kama kawaida nilikuwa nimekuahidi kuijaza ile site full content soon. Nimemaliza sasa kwa kutumia tools sijuwi nyie mnaziitaga ni tools wakati sisi tunaziitaga ni software au program kama vile vile zilivyo program/software/tools zingine tunazotumia kila siku kama microsoft word au mozilla firefox, zote hizi ni tools/software/program.

Kwakuwa Mkuu zech naye yumo humu na ndiye alileta website yake hivi karibuni ambayo aliitengeneza from the scratch/code kwa mjibu wa yeye mwenyewe, hivyo basi nimetumia content za site yake kwa kutumia tools bila ku-code hata mstari mmoja. Sisemi hii ni nzuri kuliko yake la hasha, bali pamoja na kuwa nimetumia analogy (tools) na yeye alitumia digital (coding) kwa mjibu wa nyinyi, bado muonekano wake hautofautiani sana.

Mkuu zech hii ni kwa ajili ya kujifunza tu wala isikupe presha muda wowote tutaiondoa.

Nirudi kwako Mkuu Astro, nitarudi tena kuendelea kunyambuwanyambuwa maswali yako taratibu mpaka tumalizane.

NI HII HAPA: [url]www.iyokopokomayoko.p.ht[/URL]

First of all, nice try, however i think you should use some dummy placeholder content and images because that information you put on that site is real information from my client, so kwanza kabisa just remove the text and images plus the names (not the design).

Now lets talk the design. First check your css code, how many lines do you have in there? now check my css style and see the huge difference in the amount of unnecessary code you have on your design, that's what Astro was talking about when he said "bloated code". Pili i think we all agree that my site is way better than yours despite the fact that you tried to duplicate it. Also try to load all the sites then disconnect the internet, can you view other pages on your version? no you can't, try mine now, exactly!, the points i'm trying to make here is, if you don't know how to write your own code, it is going to be very difficult to get your client what they want.

The requirements for that site from my client was, they needed a site that didn't require their visitors to take long to navigate their pages and they got exactly that, you can see that as long as that site is fully loaded, every page is accessible even if there's no internet connection, i don't think artisteer can help you on that unless you copy my code and change some css selectors (which you can't if you don't know how jQuery works with css selectors).

Guys, i am not trying to say that there's only one way of doing things but if you don't know how to write your own code we are always going to have bad designs in tanzania, hapa Tanzania sidhani hata kama kuna UX/UI designer, and i don't even think that terminology exists in a Tanzania's Webdesign Company's dictionary because most companies zime employ people like you who just think of shortcuts, artisteer, joomla templates, wordpress themes downloaders etc etc, if you compare Tanzania vs other East African Countries utashangaa the big difference. Angalia sites karibia 95% zote za government institutions, very ---- designs, and they all have those features mentioned in the html hell page, utaona that blinking new gif, utaona kuna visitor counter, marquee plus all those shitty stuff you don't see in good designs.

My free advice to whoever wants to be a professional designer/developer LEARN HOW TO WRITE YOUR OWN CODE or just pick another profession. I'm not bragging but i have designed for clients throughout EA and they all contact us after seeing some of our work on our site or through referrals, yes we even (once) got a request for proposal from a company in the USA, we didn't get the project but it shows that some people out there see our work and think we can do their designs. So Iyokopokomayoko remove my client's information from that site of yours, put dummy content and lets talk
 
Last edited by a moderator:
Kama alivyosema hapo chief-mkwawa, mafanikio yeyote yanahitaji jitihada na uvumilivu
USHAURI: install idm halafu pitia link zifuatazo upakue tutorials za kujifunzia HTML, CSS & PHP
Free video lectures,Free Animations, Free Lecture Notes, Free Online Tests, Free Lecture Presentations (sehemu ya coputer science)
TheNewBoston - Free Educational Video Tutorials on Computer Programming, Adobe Software, Computer Science and More! (sehemu ya video and tutorials)
Learn web design and development online free (link zinaonekana moja kwa moja)
safi sana
 
I think its about time na mimi nichangie kwenye hiii topic. Mtoa maada nakushauri uendelee kujifunza hizo code za HTML na CSS that is the right way usitake mambo marahisi na shortcut hata kidogo.

Avoid kutumia code generation tools,hizi tools zinazokuambia zinasimplify na kugenerate codes zina disadvantages nyingi utaishia kutengeneza websites zenye very poor code and very hard to maintain or modify.

HTML na CSS hazina ugumu wowote its not rocket science ni kuweka tu mpangilio wa content za web yako vizuri kwa kutumia (HTML) na kuongeza style kwa kutumia CSS. One tipe nitakayokupa usisome hizo tags zote za HTML na kuzimemorize, for a basic website utahitaji kujua Heading (h1,h2,h3...),paragraphs (p),anchor (a),images(img),lists(<ul>) n.k.
Upande wa css jistahidi kuangalia jinsi ya kuweka layout yako vizuri,font-selection na colour selection ni muhimu sana, ukiona umefika pazuri jitahidi kutumia photoshop kidogo kuongeza uzuri wa website yako na baada ya hapo hamia kwenye vitu kama javascript (unaweza kutumia JQuery which is a simple library to use) hapo utaongeza interactivity ya website yako. Ukiwa na interest zaidi unaweza kutumia server side scripting languages kama PHP,ASP.NET na kuanza kutengeneza dynamic websites na web applications.
Polepole ndio mwendo usitake kuweza kutengeneza mambo makubwa ndani ya muda mfupi take it step by step na utafika, nakushauri usizikimbie code na kutaka kurahisisha mambo, ukiwa mzoefu wa code na kuanza kutumia CMS utakuwa web designer/developer wa ukweli.

Kutengeneza website sio kazi ya kuchukua code generation tool au drag and drop kama unataka kufanya kazi professional ni lazima usome kwa bidii, unless kama unataka kutengeneza blog na website za mtaani zisizokuwa na maana kwa clients ambao wanajua wanachotaka kuna vitu vingi sana wanavyoangalia, search engine optimization,validation ya markup language unazotumia,cross browser compatibility(Internet explorer inahusika kwa sana),security (XSS,Sql Injection blah blah...). Kazi yangu sio web designer wala developer lakini haya mambo nayafahamu kiundani sana na huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.

There is no easy way kama unataka mazuri if you take my words na kuyafanyia kazi utafanikiwa kupata unachotaka.
Mkuu Astro Ahsante sana.
 
Mkuu hii topic niliiona asubuhi ila nikashindwa kujibu kwa maana nilikuwa natumia simu ya mkononi, napata wakati mgumu kuandika maneno mengi kupitia simu. Nitajaribu kujibu maswali yako kwa lugha itakayoeleweka vizuri kwa kila mtu kwa manufaa ya wote.

1.Websites zenye poor code na hard to maintain/or modify-hapa ninamaanisha hizi (nyenzo)tools zinazofanya code generation hutengeneza kitu chenye muonekana unaoutaka lakini nyuma ya pazia [namaanisha kwenye hizo code zinazofanya hiyo tovuti yako ionekane unavyotaka huwa ni matatizo na haziweizi kusomwa na binadamu kirahisi]

Je kuna umuhimu wa Code kusomeka kwa binadamu?
Ndio umuhimu upo, pale utakapotaka kuongeza features na kukutana na hizi code zilizongumu kusomeka utapata shida sana na kama hauna uzoefu kabisa na kuandika ama kusoma codes unaweza kujaribu kufuta mstari ama neno moja na kuangusha kazi yako yote.

-Mara nyingi Hizi code zinazokuwa generated kuna neno wanaloita 'Bloated' yani zinakuwa na vitu vingi sana na kuongeza ukubwa wa tovuti yako, Kwa mfano kuna hatua ya kuhakiki kama taarifa zilizoingizwa na mtumiaji wa tovuti ni sahihi kwa mfano barua pepe,jina nk kwa kutumia code generation ya Adobe Dreamweaver unaweza ukapata mistari 15-20 wakati unaweza ukaandika mistari miwili ama mitatu na kupunguza vile vitu ambavyo havihitajiki.

-Kwa anayefahamu hizo code nini kimeandikwa anaweza kufuta vile visivyohitajika na kuongeza vile anavyotaka na kuwa huru katika kazi yake, kwa yule atakayetegemea code kuwa generated anaweza kujifunga na kupata shida sana hivyo ndio maana nilishauri mtu aanze kujifunza jinsi ya kuandika code na kuachana na njia za mkato.

2.Katika swali la pili-Nilipotaja h1,h2,p,a,images...
-Webpage yani Ukurasa wa Tovuti unaundwa na Elements (Vipengele) ambavyo ni muunganiko wa tags (vitambulisho) vinavyoelezea Web Browser (Kiperuzi cha Tovuti kama opera mini,Internet Explorer n.k) jinsi ya kuonyesha ukurasa kwa mpangilio sahihi...Kiperuzi (Web Browser) husoma hivyo vipengele na kuweza kurudisha muonekano uliosahihi (interpret/tafsiri code).

-Kuna vipengele vingi sana na Lugha inayotumika (Markup Language) ni HTML katika kuunda kurasa za tovuti. Ukurasa wa tovuti ni kama ukurasa wa kitabu ama daftari lako na umegawanyika katika sehemu kama Kichwa (head) na mwili(body).
Kichwa huwa na taarifa muhimu kuhusu ukurasa huo kwa mfano Jina La ukurasa wako na vielelezo vya taarifa za tovuti yako. Mwili (Body) huu ndio hubeba maelezo yote kama maneno picha unazotaka zisomwe na mtembeleaji wa tovuti yako.

Mfano vitambulisho hufunguliwa na kufungwa, vitambulisho vya kufungua (opening tags) huanza na namna hii <herufi moja ama zaidi> na vitambulisho vya kufungwa huadikwa kwa namna hii </herufi moja ama zaidi >

-Kwa mfano < h1 > </ h1>Ukiandika neno lolote katikati ya vitambulisho vilivyofunguliwa na kufungwa utapata kichwa cha habari kikubwa mfano < h1 >TAARIFA YA HABARI < / h1> Hiki huonekana kama maneno yaliyokolozewa kwenye kiperuzi cha tovuti. Muunganiko wa vitambulisho vya kufungua na kufunga na hilo neno huunda kipengele kimoja.

Ukitumia vitambulisho kama < h2 >,< h3 >< h4 > unamaanisha vichwa vidogo vya habari, namba inavyozidi kuongezeka ndio udogo wa kichwa cha habari (katika muonekano na hata cheo katika ukurasa)

  • Vitambulisho vingine kama < p > Hiki ni kwa ajili ya kuandika aya (paragraph)
  • < img >-Hiki hutumika kuweka picha.
  • lists hutumika kuweka orodha ya vitu katika ukurasa (kama huu unaouona hapa kwenye ukurasa wangu)
Ningependa kuoongelea sana HTML lakini itachukua sehemu kubwa sana na ninahisi kuna tutorial zimeshawekwa humu Jamiiforums kwa mfano Tech, Gadgets & Science Forum
Ninaamini zipo nyingi sana na hata kwa kutafuta google waweza kupata maelezo zaidi.
Mfano wa HTML code ni kama hiyo hapo chini.
View attachment 108529
Kama nilivyosema vitambulisho vipo vingi sana ila si vyote utakavyohitaji kuvitumia katika kuunda tovuti yako,jaribu kuangailwa vitambulisho vilivyopo katika tovuti nyingi utakuta ni aina chache zinazotumia,

Kuviona vitambulisho na vipengele
  • tumia kiperuzi chako kufungua tovuti yoyote
  • Bofya right click(kiswahili chake sikifahamu)
  • Chagua sehemu imeandikwa view source code ama view page source (hutofautiana na viperuzi)
View attachment 108533
kwa njia hii ukiwa makini utaweza kujua ni vitambulisho vipi hutumika sana na jinsi ya kupangilia ukurasa wako.

3. Server Side Scripting Languages-hizi ni lugha (Programming Languages) zinazotumika kufanya manipulation (kucheza) na data katika upande wa server na kutuma majibu kwenye kiperuzi.

Hayo maelezo hapo juu yaweza kuchanganya kwa mtu asiye na ujuzi wa mambo ya computer.
Tuchukue mfano huu (nimejaribu kuelezea kwa njia rahisi sana na kuondoa baadhi ya maelezo ili kueleweka kiurahisi)
-Unapofungua tovuti kama Jamiiforums unatuma ombi lako kwenye kompyuta (Server) iliyobeba taarifa za Jamiiforums.
-Computer hiyo yani (Server) itatuma jibu kutokana na ombi ulilofanya kama ni kujibu topic ama kuanzisha topic mpya yenyewe itaangalia ni nini cha kukujibu, hiii yote huandikwa na wataalamu kwa kuiambia computer nini cha kufanya ombi linapotumwa.
-Lugha zinazotumika kuieeleza computer nini cha kufanya/kujibu pale ombi linapotumwa huitwa server side scripting language (Hutumika kutoa maelezo kwa upange wa computer iliyobeba taarifa za jamiiforums)
-Lugha hizi zipo nyingi sana kwa mfano PHP,ASP,JAVA-JSP,Python,Ruby, Sitoweza kuzitaja zote.

4. Adobe Photoshop-ni programu/software inayotumika kufanya mabadiliko ya muonekano wa picha/michoro.
Hii ni nyenzo muhimu sana kwa wasanifu wa website (Web Designers) kwa maana tovuti yenye muonekano mzuri huundwa na picha zenye mvuto mzuri na maumbo yanayoweza kumvutia mtembeleaji wako, kuna tools nyingine kama Gimp nayo ina uwezo mkubwa. Uwezo wa photoshop ni mkubwa sana unaweza kutengeneza picha na michoro mizuri sana wataalamu kama C6,Leh wameshaweka tutorial nyingi sana hapo nyuma kama
Tech, Gadgets & Science Forum
Tech, Gadgets & Science Forum

ambapo hata mimi niliweza kujifunza mengi kupitia kwao.

5.Search Engine Optimization-ni kufanya tovuti yako ipatikane kiurahisi katika search engine (hii ni mitandao kama Google.com/bing.com)
Jaribu kuingia Google andika neno kama Tanzania Forums, ya kwanza kutokea ni JF, hiii ina umuhimu gani?...Tovuti yako inapotokea mwanzo mwa matokeo inaongeza watembeleaji wapya wa tovuti yako, kama mimi ni mgeni katika forums na nilikuwa natafuta forum ya Tanzania kupitia google kwa namna moja ama nyingine ningejikuta nipo JF Hivyo Search engine optimization ni muhimu katika kuongeza watembeleaji katika tovuti yako.

6-Cross Browser Compatibility-Hii ni kuhakikisha tovuti yako inaonekana sawa kupitia viperuzi mbali mbali kwa mfano Internet explorer,Google chrome,Mozila etc. Usitengeneze tovuti inayoonekana kwa kiperuzi cha aina moja kwani hujui mtembeleaji wako atatumia kiperuzi gani, pale itakapotokea kiperuzi kimoja kinashindwa kuionyesha tovuti yako vizuri basi unaweza kuwa umejipotezea watembeleaji.
-Viperuzi vinavyosumbua sana ni Kama internet explorer 6-7 [hizi huwa na tabia ya kuonyesha muonekano tofauti wa tovuti ukilinganisha na viperuzi vingine vipya ila ni jukumu lako wewe designer kuhakikisha tovuti yako inaonekana vizuri]

7-Validation ya Markup-Hii ni kuhakiki kuwa HTML code zinazounda tovuti yako zipo sahihi na zinaendana na sheria zilizowekwa na mamlaka inayotoa sheria za tovuti W3C. Unashauriwa kufuatwa sheria zilizowekwa ili kuepuka matatizo kama muonekano tofauti wa tovuti kwenye kiperuzi kimoja na kingine (angalia namba 6)

8.Je nikitumia code generation tools nitaweza kufanya Search Engine Optimization,Cross Browser Compatibility na Validation Markup?
Hii inategemea na uzoefu wako na codes, kwa wale wajuzi hata akitumia code generation tool anaweza kurekebisha matatizo kama Cross Browser Compatibility na kuondoa Invalid Markup iliyotengenezwa na hizo tools bila kuharibu tovuti yake na hata kuweka Search Engine Optimization. Kama huna ujuzi na hizo code basi kufanya mambo haya itakuwa ni vigumu sana na hata kupelekea kuachana nayo kwa maana tovuti si inaonekana vizuri?, na Huu ndio mwanzo wa kazi zenye low quality.
-Utakapokuwa na ujuzi na code zako ndio utaweza kuwa na uhuru zaidi wa kufanya yote yaliyotajwa hapo juu kwenye swali.

Kwa kumaliza Mkuu japokuwa kazi yangu si web designer/web developer nina ujuzi wa kutosha kwa maana katika taaluma yangu nimeshayasomea haya mambo na kupitia juhudi zangu binafsi nikaweza kuendeleza ujuzi kwenye haya mambo, kwa sasa ninafanya kazi katika mambo tofauti lakini ninafahamu jinsi ya kutengeneza tovuti, ipi ni njia sahihi na nyenzo zipi zinafaa hasa kwa mtu anayeanza kujifunza.
Nikipata muda ninaweza kuweka tutorial hapa kuonyesha jinsi ya kutengeneza a simple attractive home page from scratch kwa kutumia HTML na CSS peke yake na kuonyesha jinsi hizo code zilivyorahisi kuziandika.

Nitakapokuwa nimekosea naomba nirekebishwe, Let us work together to Improve our society.🙂

Jibu zuri kabisa, Mkuu umejibu vyema bila kupaniki. Nimejifunza zaidi, ahsante sana. You have my salute.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom