web designing inaumiza kichwa

web designing inaumiza kichwa

Vizuri. Sasa nakushauri hata hiyo googlechrome na firefox pia na hiyo word 2010 navyo uvi-code usitumie software/program za wengine yaani googlechrome ui-code iwe imetengenezwa na wewe mwenyewe kadharika kwa firefox na word maana huko mbeleni utapata taabu sana KAMA UTAENDELEA NA HII TABIA YAKO YA KUTUMIA SOFTWARE ZA WENGINE WAKATI KU-CODE UNAJUWA.

Just because you can't code and just because you chose to take a shortcut and design using some software which still sucks (yeah because i have seen your work) don't just give people some sarcastic answers. Let this guy learn to create his own stuff, it will do him good. He chose to be different and do the right thing, let him be. Inakera sana unapomwambia eti na chrome, firefox, word atengeneze zake just because you don't want him to learn? C'mon dude show some class, there's a reason he chose to learn otherwise he could've just googled "software to create websites for me" and i am sure he would get a lot of answers from google.

If you can't contribute to his learning experience, just take some prozac and chill, you don't have to open your mouth and speak every time a post shows up on your screen, take a backseat old man and let the guy improve his craft.
 
Mkuu, mimi nilikuwa nimemjibu muuliza swali sikuwa nataka kubishana wala kujibizana na wewe. Hizo ni option nimempa kulingana na uzoefu wangu. Nimeshauri hivyo, kama ushauri wangu haumfai basi atajibu yeye isipokuwa kama wewe ni tarishi wake.

Unaposema you have seen my work, which work of mine you have seen?. Kwani mimi sijaona kazi yako? kazi yako ina kitu gani cha pekee ambacho mimi siwezi? unaweza kunionyesha website uliyotengeneza na mimi nikutengenezee? kwanini unapenda kujibizana na mimi wakati mimi sikujibizana na wewe ulipotoa mawazo yako?

Just because you can't code and just because you chose to take a shortcut and design using some software which still sucks (yeah because i have seen your work) don't just give people some sarcastic answers. Let this guy learn to create his own stuff, it will do him good. He chose to be different and do the right thing, let him be. Inakera sana unapomwambia eti na chrome, firefox, word atengeneze zake just because you don't want him to learn? C'mon dude show some class, there's a reason he chose to learn otherwise he could've just googled "software to create websites for me" and i am sure he would get a lot of answers from google.

If you can't contribute to his learning experience, just take some prozac and chill, you don't have to open your mouth and speak every time a post shows up on your screen, take a backseat old man and let the guy improve his craft.
 
I think its about time na mimi nichangie kwenye hiii topic. Mtoa maada nakushauri uendelee kujifunza hizo code za HTML na CSS that is the right way usitake mambo marahisi na shortcut hata kidogo.

Avoid kutumia code generation tools,hizi tools zinazokuambia zinasimplify na kugenerate codes zina disadvantages nyingi utaishia kutengeneza websites zenye very poor code and very hard to maintain or modify.

HTML na CSS hazina ugumu wowote its not rocket science ni kuweka tu mpangilio wa content za web yako vizuri kwa kutumia (HTML) na kuongeza style kwa kutumia CSS. One tipe nitakayokupa usisome hizo tags zote za HTML na kuzimemorize, for a basic website utahitaji kujua Heading (h1,h2,h3...),paragraphs (p),anchor (a),images(img),lists(<ul>) n.k.
Upande wa css jistahidi kuangalia jinsi ya kuweka layout yako vizuri,font-selection na colour selection ni muhimu sana, ukiona umefika pazuri jitahidi kutumia photoshop kidogo kuongeza uzuri wa website yako na baada ya hapo hamia kwenye vitu kama javascript (unaweza kutumia JQuery which is a simple library to use) hapo utaongeza interactivity ya website yako. Ukiwa na interest zaidi unaweza kutumia server side scripting languages kama PHP,ASP.NET na kuanza kutengeneza dynamic websites na web applications.
Polepole ndio mwendo usitake kuweza kutengeneza mambo makubwa ndani ya muda mfupi take it step by step na utafika, nakushauri usizikimbie code na kutaka kurahisisha mambo, ukiwa mzoefu wa code na kuanza kutumia CMS utakuwa web designer/developer wa ukweli.

Kutengeneza website sio kazi ya kuchukua code generation tool au drag and drop kama unataka kufanya kazi professional ni lazima usome kwa bidii, unless kama unataka kutengeneza blog na website za mtaani zisizokuwa na maana kwa clients ambao wanajua wanachotaka kuna vitu vingi sana wanavyoangalia, search engine optimization,validation ya markup language unazotumia,cross browser compatibility(Internet explorer inahusika kwa sana),security (XSS,Sql Injection blah blah...). Kazi yangu sio web designer wala developer lakini haya mambo nayafahamu kiundani sana na huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.

There is no easy way kama unataka mazuri if you take my words na kuyafanyia kazi utafanikiwa kupata unachotaka.
 
huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.

Couldn't agree more on that, we need to be serious with our work, we have to keep learning and perfecting our skills everyday, non-stop, that's the only secret to becoming good at anything, i look around the tanzanian webspace, i only see one company that's doing a decent job (link tanzania) ingawa most of their work somehow look the same to me, wengine wote ni utumbo mtupu, we need to get our shit together faster before we become an afterthought.
 
Mkuu,

Nimeona nikuulize maswali kulingana na ulichoandika hapa, maana kama ndiyo huu ni muda mzuri kwako Kuchangia topic hii basi kwa hakika tutajifunza mengi kwani muda wote ulikuwa hapa na huchangii wakati kumbe una mengi tu ya kuchangia.

I think its about time na mimi nichangie kwenye hiii topic.

websites zenye very poor code and very hard to maintain or modify. Unaweza kuelezea kidogo hapa ulitaka kusemaje.
Avoid kutumia code generation tools,hizi tools zinazokuambia zinasimplify na kugenerate codes zina disadvantages nyingi utaishia kutengeneza websites zenye very poor code and very hard to maintain or modify.

(h1,h2,h3...), paragraphs (p), anchor (a),images(img),lists. Unaweza kuelezea pia hapa ulikuwa unamaanisha nini? na umeshauri baadaye ajifunze photoshop, hivi photoshop ni tool au ni nini?.
for a basic website utahitaji kujua Heading (h1,h2,h3...),paragraphs (p),anchor (a),images(img),lists, muhimu sana, ukiona umefika pazuri jitahidi kutumia photoshop kidogo kuongeza uzuri wa website yako(<ul>) n.k.

kutumia server side scripting languages. Unaweza kunieleza pia ulikuwa unamanisha nini na je unaweza kuzitaja hizo server side scripting languages ZOTE?.
Ukiwa na interest zaidi unaweza kutumia server side scripting languages

Search engine optimization,validation ya markup language unazotumia,cross browser compatibility. Hapa ulikuwa unamaanisha akitumia hizi tools/softwares hatafanikiwa na mambo ya SEO na Browser compatibilities?.
Kutengeneza website sio kazi ya kuchukua code generation tool au drag and drop kama unataka kufanya kazi professional ni lazima usome kwa bidii, unless kama unataka kutengeneza blog na website za mtaani zisizokuwa na maana kwa clients ambao wanajua wanachotaka kuna vitu vingi sana wanavyoangalia, search engine optimization,validation ya markup language unazotumia,cross browser compatibility(Internet explorer inahusika kwa sana),security (XSS,Sql Injection blah blah...).

Hapa nadhani umekosea kwa sababu kama wewe siyo web designer wala developer ni ngumu kutoa ushauri wa kitaalamu kwa jambo hili, ni kama vile mtaalamu wa nyukilia akatowe mawazo ya kitaalamu kwenye masuala ya hotel management?!! hapa ataongopa tu na nadhani hili ni tatizo kubwa sana hapa Tanzania.
Kazi yangu sio web designer wala developer lakini haya mambo nayafahamu kiundani sana na huwa nashangaa kuona web designers/developers wengi wa hapa Tanzania wanavyofanya kazi zilizo na very low quality.
 
Mkuu,

Nimeona nikuulize maswali kulingana na ulichoandika hapa, maana kama ndiyo huu ni muda mzuri kwako Kuchangia topic hii basi kwa hakika tutajifunza mengi kwani muda wote ulikuwa hapa na huchangii wakati kumbe una mengi tu ya kuchangia.

Mkuu hii topic niliiona asubuhi ila nikashindwa kujibu kwa maana nilikuwa natumia simu ya mkononi, napata wakati mgumu kuandika maneno mengi kupitia simu. Nitajaribu kujibu maswali yako kwa lugha itakayoeleweka vizuri kwa kila mtu kwa manufaa ya wote.

1.Websites zenye poor code na hard to maintain/or modify-hapa ninamaanisha hizi (nyenzo)tools zinazofanya code generation hutengeneza kitu chenye muonekana unaoutaka lakini nyuma ya pazia [namaanisha kwenye hizo code zinazofanya hiyo tovuti yako ionekane unavyotaka huwa ni matatizo na haziweizi kusomwa na binadamu kirahisi]

Je kuna umuhimu wa Code kusomeka kwa binadamu?
Ndio umuhimu upo, pale utakapotaka kuongeza features na kukutana na hizi code zilizongumu kusomeka utapata shida sana na kama hauna uzoefu kabisa na kuandika ama kusoma codes unaweza kujaribu kufuta mstari ama neno moja na kuangusha kazi yako yote.

-Mara nyingi Hizi code zinazokuwa generated kuna neno wanaloita 'Bloated' yani zinakuwa na vitu vingi sana na kuongeza ukubwa wa tovuti yako, Kwa mfano kuna hatua ya kuhakiki kama taarifa zilizoingizwa na mtumiaji wa tovuti ni sahihi kwa mfano barua pepe,jina nk kwa kutumia code generation ya Adobe Dreamweaver unaweza ukapata mistari 15-20 wakati unaweza ukaandika mistari miwili ama mitatu na kupunguza vile vitu ambavyo havihitajiki.

-Kwa anayefahamu hizo code nini kimeandikwa anaweza kufuta vile visivyohitajika na kuongeza vile anavyotaka na kuwa huru katika kazi yake, kwa yule atakayetegemea code kuwa generated anaweza kujifunga na kupata shida sana hivyo ndio maana nilishauri mtu aanze kujifunza jinsi ya kuandika code na kuachana na njia za mkato.

2.Katika swali la pili-Nilipotaja h1,h2,p,a,images...
-Webpage yani Ukurasa wa Tovuti unaundwa na Elements (Vipengele) ambavyo ni muunganiko wa tags (vitambulisho) vinavyoelezea Web Browser (Kiperuzi cha Tovuti kama opera mini,Internet Explorer n.k) jinsi ya kuonyesha ukurasa kwa mpangilio sahihi...Kiperuzi (Web Browser) husoma hivyo vipengele na kuweza kurudisha muonekano uliosahihi (interpret/tafsiri code).

-Kuna vipengele vingi sana na Lugha inayotumika (Markup Language) ni HTML katika kuunda kurasa za tovuti. Ukurasa wa tovuti ni kama ukurasa wa kitabu ama daftari lako na umegawanyika katika sehemu kama Kichwa (head) na mwili(body).
Kichwa huwa na taarifa muhimu kuhusu ukurasa huo kwa mfano Jina La ukurasa wako na vielelezo vya taarifa za tovuti yako. Mwili (Body) huu ndio hubeba maelezo yote kama maneno picha unazotaka zisomwe na mtembeleaji wa tovuti yako.

Mfano vitambulisho hufunguliwa na kufungwa, vitambulisho vya kufungua (opening tags) huanza na namna hii <herufi moja ama zaidi> na vitambulisho vya kufungwa huadikwa kwa namna hii </herufi moja ama zaidi >

-Kwa mfano < h1 > </ h1>Ukiandika neno lolote katikati ya vitambulisho vilivyofunguliwa na kufungwa utapata kichwa cha habari kikubwa mfano < h1 >TAARIFA YA HABARI < / h1> Hiki huonekana kama maneno yaliyokolozewa kwenye kiperuzi cha tovuti. Muunganiko wa vitambulisho vya kufungua na kufunga na hilo neno huunda kipengele kimoja.

Ukitumia vitambulisho kama < h2 >,< h3 >< h4 > unamaanisha vichwa vidogo vya habari, namba inavyozidi kuongezeka ndio udogo wa kichwa cha habari (katika muonekano na hata cheo katika ukurasa)

  • Vitambulisho vingine kama < p > Hiki ni kwa ajili ya kuandika aya (paragraph)
  • < img >-Hiki hutumika kuweka picha.
  • lists hutumika kuweka orodha ya vitu katika ukurasa (kama huu unaouona hapa kwenye ukurasa wangu)
Ningependa kuoongelea sana HTML lakini itachukua sehemu kubwa sana na ninahisi kuna tutorial zimeshawekwa humu Jamiiforums kwa mfano https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/429224-html-tutorial-3.html
Ninaamini zipo nyingi sana na hata kwa kutafuta google waweza kupata maelezo zaidi.
Mfano wa HTML code ni kama hiyo hapo chini.
HTML-structure.jpg
Kama nilivyosema vitambulisho vipo vingi sana ila si vyote utakavyohitaji kuvitumia katika kuunda tovuti yako,jaribu kuangailwa vitambulisho vilivyopo katika tovuti nyingi utakuta ni aina chache zinazotumia,

Kuviona vitambulisho na vipengele
  • tumia kiperuzi chako kufungua tovuti yoyote
  • Bofya right click(kiswahili chake sikifahamu)
  • Chagua sehemu imeandikwa view source code ama view page source (hutofautiana na viperuzi)
Untitled-2.jpg
kwa njia hii ukiwa makini utaweza kujua ni vitambulisho vipi hutumika sana na jinsi ya kupangilia ukurasa wako.

3. Server Side Scripting Languages-hizi ni lugha (Programming Languages) zinazotumika kufanya manipulation (kucheza) na data katika upande wa server na kutuma majibu kwenye kiperuzi.

Hayo maelezo hapo juu yaweza kuchanganya kwa mtu asiye na ujuzi wa mambo ya computer.
Tuchukue mfano huu (nimejaribu kuelezea kwa njia rahisi sana na kuondoa baadhi ya maelezo ili kueleweka kiurahisi)
-Unapofungua tovuti kama Jamiiforums unatuma ombi lako kwenye kompyuta (Server) iliyobeba taarifa za Jamiiforums.
-Computer hiyo yani (Server) itatuma jibu kutokana na ombi ulilofanya kama ni kujibu topic ama kuanzisha topic mpya yenyewe itaangalia ni nini cha kukujibu, hiii yote huandikwa na wataalamu kwa kuiambia computer nini cha kufanya ombi linapotumwa.
-Lugha zinazotumika kuieeleza computer nini cha kufanya/kujibu pale ombi linapotumwa huitwa server side scripting language (Hutumika kutoa maelezo kwa upange wa computer iliyobeba taarifa za jamiiforums)
-Lugha hizi zipo nyingi sana kwa mfano PHP,ASP,JAVA-JSP,Python,Ruby, Sitoweza kuzitaja zote.

4. Adobe Photoshop-ni programu/software inayotumika kufanya mabadiliko ya muonekano wa picha/michoro.
Hii ni nyenzo muhimu sana kwa wasanifu wa website (Web Designers) kwa maana tovuti yenye muonekano mzuri huundwa na picha zenye mvuto mzuri na maumbo yanayoweza kumvutia mtembeleaji wako, kuna tools nyingine kama Gimp nayo ina uwezo mkubwa. Uwezo wa photoshop ni mkubwa sana unaweza kutengeneza picha na michoro mizuri sana wataalamu kama C6,Leh wameshaweka tutorial nyingi sana hapo nyuma kama
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...8-tujifunze-photoshop-tembocard-mockup-2.html
https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/317396-another-photoshop-tutorial.html

ambapo hata mimi niliweza kujifunza mengi kupitia kwao.

5.Search Engine Optimization-ni kufanya tovuti yako ipatikane kiurahisi katika search engine (hii ni mitandao kama Google.com/bing.com)
Jaribu kuingia Google andika neno kama Tanzania Forums, ya kwanza kutokea ni JF, hiii ina umuhimu gani?...Tovuti yako inapotokea mwanzo mwa matokeo inaongeza watembeleaji wapya wa tovuti yako, kama mimi ni mgeni katika forums na nilikuwa natafuta forum ya Tanzania kupitia google kwa namna moja ama nyingine ningejikuta nipo JF Hivyo Search engine optimization ni muhimu katika kuongeza watembeleaji katika tovuti yako.

6-Cross Browser Compatibility-Hii ni kuhakikisha tovuti yako inaonekana sawa kupitia viperuzi mbali mbali kwa mfano Internet explorer,Google chrome,Mozila etc. Usitengeneze tovuti inayoonekana kwa kiperuzi cha aina moja kwani hujui mtembeleaji wako atatumia kiperuzi gani, pale itakapotokea kiperuzi kimoja kinashindwa kuionyesha tovuti yako vizuri basi unaweza kuwa umejipotezea watembeleaji.
-Viperuzi vinavyosumbua sana ni Kama internet explorer 6-7 [hizi huwa na tabia ya kuonyesha muonekano tofauti wa tovuti ukilinganisha na viperuzi vingine vipya ila ni jukumu lako wewe designer kuhakikisha tovuti yako inaonekana vizuri]

7-Validation ya Markup-Hii ni kuhakiki kuwa HTML code zinazounda tovuti yako zipo sahihi na zinaendana na sheria zilizowekwa na mamlaka inayotoa sheria za tovuti W3C. Unashauriwa kufuatwa sheria zilizowekwa ili kuepuka matatizo kama muonekano tofauti wa tovuti kwenye kiperuzi kimoja na kingine (angalia namba 6)

8.Je nikitumia code generation tools nitaweza kufanya Search Engine Optimization,Cross Browser Compatibility na Validation Markup?
Hii inategemea na uzoefu wako na codes, kwa wale wajuzi hata akitumia code generation tool anaweza kurekebisha matatizo kama Cross Browser Compatibility na kuondoa Invalid Markup iliyotengenezwa na hizo tools bila kuharibu tovuti yake na hata kuweka Search Engine Optimization. Kama huna ujuzi na hizo code basi kufanya mambo haya itakuwa ni vigumu sana na hata kupelekea kuachana nayo kwa maana tovuti si inaonekana vizuri?, na Huu ndio mwanzo wa kazi zenye low quality.
-Utakapokuwa na ujuzi na code zako ndio utaweza kuwa na uhuru zaidi wa kufanya yote yaliyotajwa hapo juu kwenye swali.

Kwa kumaliza Mkuu japokuwa kazi yangu si web designer/web developer nina ujuzi wa kutosha kwa maana katika taaluma yangu nimeshayasomea haya mambo na kupitia juhudi zangu binafsi nikaweza kuendeleza ujuzi kwenye haya mambo, kwa sasa ninafanya kazi katika mambo tofauti lakini ninafahamu jinsi ya kutengeneza tovuti, ipi ni njia sahihi na nyenzo zipi zinafaa hasa kwa mtu anayeanza kujifunza.
Nikipata muda ninaweza kuweka tutorial hapa kuonyesha jinsi ya kutengeneza a simple attractive home page from scratch kwa kutumia HTML na CSS peke yake na kuonyesha jinsi hizo code zilivyorahisi kuziandika.

Nitakapokuwa nimekosea naomba nirekebishwe, Let us work together to Improve our society.🙂
 
View attachment 108529

View attachment 108533

Very good explanation, na umeelezea kiswahili hizi terms bila shida (ambacho si kitu rahisi). Safi sana sidhani kama kuna swali tena hapo.
 
kaka hongera sana kwa maelezo haya....umefunga mjadala...usisahau kurudi kuwapa shule vijana...
 
Kama umeshajaribu dreamweaver nakushauri ujaribu pia software nyingine inaitwa ARTISTEER utakuwa na uwezo wa kudesign sites katika:
WEB DESIGN TEMPLATES/HTML
JOOMLA TEMPLATES
WORDPRESS TEMPLATES
DRUPAL THEMES
DOTNETNUKE SKINS na
BLOGGER TEMPLATES

Vyote hivyo kwa kutumia software 1.
CODE IS POETRY.

Asante sana mkuu naifanyia kazi hiyo naona hyo itansadia xana ngoja niitafute!
 
Kimsingi mimi sipo upande wako Fadhili Paulo maana naona kama unamkatisha tamaa mshikaji. unaonekana kama hutaki ajifunze. Kama ungekuwa unatoa ushirikiano na msaada usingeweza kumwambia a code FireFox au google crome. Kwenye IT hasa Software Development tunajifunza ku appreciate kazi za watu na ku-encourage new Developers siyo kama unavyojaribu kufanya wewe. Kuhusu kazi mlizofanya wewe na Zech hapa siyo sehemu ya Mashindano lakini hata mimi nimevutiwa kutaka kujua kazi ulizofanya na nilichogundua ni alichogundua Zech. moja ya kazi yako amabayo nadhani utakuwa unaikubali zaidi amabyo hadi umeamua kuifanya sehemu ya Signature yako hapa JF ni http://maajabuyamaji.net/ Kazi nyingine ninayoijua ambayo kimsingi ilikuwa niifanye mimi ya website ya Hotel moja inaitwa nellyzinn. Hii ni Hotel amabyo ipo Mbezi na inamilikiwa na Prof.wa sheria kutoka OPEN UNIV http://nellysinn.net/. Hii nayo ni moja kati ya website mbaya(Sorry for Discouragement)... Una discourage watu usidhani hakuna watu wasiokujua kijana...we una copy templates(Siyo kitu kibaya kama we ni mtaalamu) na mwenzio anapiga from scratch acha kufanya hivyo kaka
 
Aise hata mimi sipo upande wako hata kidogo bwana Chief Lugina.
Kimsingi mimi sipo upande wako Fadhili Paulo

Mimi simkatishi tamaa, nampa namna nyingine rahisi ambayo haitamuumiza kichwa. Sijuwi ubaya wa hili upo wapi.
maana naona kama unamkatisha tamaa mshikaji.

Siyo kweli, maana hata hiyo software niliyorecoomend inahitaji ujifunze kuitumia.
unaonekana kama hutaki ajifunze.

Kumwambia hivi haina maana sina ushirikiano, ni kwamba si lazima ujuwe ku-code ndiyo utengeneza website. Ili ujuwe kutengeneza website kuna option 2:
1. Unajifunza html au
2. Unajifunza software (dreamweaver, artisteer etc).
Unataka ushirikiano gani tena zaidi ya huu?.
Kama ungekuwa unatoa ushirikiano na msaada usingeweza kumwambia a code FireFox au google crome.

Mimi nina-appreciate kazi inayofanya artisteer kwa kuwa-encourage wengine waitumie, je sijaappreciate kazi za wengine kwa style hii?
Kwenye IT hasa Software Development tunajifunza ku appreciate kazi za watu

Hujuwi tofauti ya developer na designer. Huyu mleta maada anataka kujifunza kudesign website na siyo ku-develop website, ni vitu 2 tofauti hapo ila inaonekana hujuwi kuvitofautisha.
ku-encourage new Developers siyo kama unavyojaribu kufanya wewe.

Ndiyo hii ni kazi yangu, mimi naiona ni nzuri na ninaibadili muonekano wake muda wowote nitakao, siwezi kukupa wewe utengeneze web hii kutokana na sababu zile zile zilizokufanya unyimwa kutengeneza nellysinn. Kumbe ilikuwa utengeneze wewe?! sasa ilikuwaje tena?
Kuhusu kazi mlizofanya wewe na Zech hapa siyo sehemu ya Mashindano lakini hata mimi nimevutiwa kutaka kujua kazi ulizofanya na nilichogundua ni alichogundua Zech. moja ya kazi yako amabayo nadhani utakuwa unaikubali zaidi amabyo hadi umeamua kuifanya sehemu ya Signature yako hapa JF ni http://maajabuyamaji.net/

Hapo kwenye kimsingi ilikuwa ufanye wewe ndipo penye matatizo. Hakuna zaidi ya hilo. Unaweza kueleza namna ilivyokuwa hii website kabla sijaichukuwa mimi? Sasa kwanini hukutengeneza wewe? au ndiyo wewe uliyepiga muhuri wa website kwenye sufuria nyumbani kwangu kishirikina mwezi desemba mwaka jana?. Mtafute mwenye hiyo website mwambie unataka uitengeneze wewe na akikubali nitakuachia, sawa?.
Kazi nyingine ninayoijua ambayo kimsingi ilikuwa niifanye mimi ya website ya Hotel moja inaitwa nellyzinn. Hii ni Hotel amabyo ipo Mbezi na inamilikiwa na Prof.wa sheria kutoka OPEN UNIV Home | Nelly's InnNelly's Inn. Hii nayo ni moja kati ya website mbaya(Sorry for Discouragement)

Wewe unadhani kuna watu wasiokujuwa? isitoshe mimi nipo verified kwanini nisijulikane? nikusikie tena una bwekabweka nyau weee. Na utakapokuja kujibu tena uweke na wewe website zako 2 ulizotengeneza.
... Una discourage watu usidhani hakuna watu wasiokujua kijana...we una copy templates(Siyo kitu kibaya kama we ni mtaalamu) na mwenzio anapiga from scratch acha kufanya hivyo kaka
 
yani hapo ujagusa php,java,jquery ila ukweli ni huu kuna software nyingi zinazolahisisha kazi kama dreamweaver,joomla,microsoft frontpage so tafuta

Hizo zote zinakua ngumu due to the fact that you lack the fundamentals. Mfano hauwezi kuelewa jQuery kama haujui CSS & HTML, na hauwezi kuelewa java / php kama css & html uliona usijifunze ukaamua kutumia shortcut ya dreamweaver/ joomla/ frontpage etc utaona ni vitu vigumu sana kwa sababu mind yako sio mind ya mtu anayependa kujifunza/patient hii impact yake kwenye society ni kwamba mwisho wa siku utakua unapenda pia rushwa kwa sababu rushwa ni aina nyingine ya vitu vinavyosababishwa na watu wanaopenda shortcuts.
 
Watu wanashindwa kutofautisha na kati ya web developer na designer, developer ndio anahitajika kujua code, ila designer kazi yake ni kutengeneza muonekano wa website, na kufanya ivutie kwa watazamaji. Na pia uzuri wa website sio picha, ni mpangilio wa rangi na muonekano wake, japo kuwa hata picha kama ukiweka nzuri zinavutia, na sio kila website inahitaji picha. Pia tools ni nzuri sana, kwenye web developer unahitaji kujua code na sio kuzikariri, ili hata ukitumia tool ukiziona unajua hii kazi yake ni nini na hata ukutaka kufuta unajua ufute vipi. Mimi binafsi natengeneza web kwa kutumia tools ila nikimaliza lazima code nizipitie zote kutoa na kuweka vitu navyotaka mm. So kwenye HTML jitahidi kujua key point zote vizuri. Sio lazima kila kitu ufanye wewe kuna tool za kukurahihishia.
 
Sorry, I thought like I was talking to Software Developer. Kijana naona umeamua kutoa matusi wala siyo hoja.ICT ni Progress learning kila siku tunahitaji kujifunza ili kuendana na kasi ya Technology.Hivyo tunapopata watu wa kutukosoa tunatakiwa tukubali tu hata kama mawazo yao hatuyapendi. Sikutaka kukujibu kwa sababu umeamua kutukana lakini nimeamua kukujibu coz nikiacha kama ilivyo huenda hata huko mtaani kwako ukabaki na tabia hii.

1. Kwanza umesema kuna mtu alikuja kupiga mhuri kwenye sufuria la nyumbani kwako, hii ni ajabu sana mtu aje kupiga mhuri kwenye sufuria kisa kutengeneza website. Bahati mbaya sana issues za kutengeneza website nilikuwa nafuatilia kipindi nipo UDSM na website nafanya kama Kujiburudisha tu so, kwa mwana-Technolojia kama wewe kuanza kuhisi ushirikina kwenye zama hizi ni jambo la ajabu sana and by the way hunifahamu hata naishi wapi.

2.Kuhusu Tofauti kati ya Website Designer na Developer, wewe ungekuwa umekaa kwenye hii Industry na ungejua huyu mtu alikuwa anataka website Development coz anaonekana ni mgeni kwenye haya mambo so hawezi kutofautisha. Na kwa Tanzania kama siyo Africa usitegemee kumkuta Web Designer, hapa mtu mmoja anafanya kila kitu so ki bongo bongo hatuna Designer na ndiyo maana huenda Website zako zina Design mbaya(Kwa mtazamo wangu).

3. Kuhusu kwanini sikufanya hiyo kazi, sikufanya kwa sababu zangu ambazo hazihusiani na ujuzi wangu au Malipo lakini ni sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu kwa mda huo. Na kabla hujaichukua wewe ilikuwa ni website nzuri sana na hata sijui kwa nini walikubari kubadilisha website nzuri vile na kukubali hii yako huenda ni kwa sababu either umefanya kwa malipo kiduchu au for free ili kuongeza profile(Kuwa ulishatengeneza website nyingi) lakini kimsingi hii website uliyotengeneza haina lolote kabisa(najua utabisha kwa sababu unaamini ni nzuri----Home | Nelly&#039;s InnNelly&#039;s Inn)

3.Unasema kuna option 2 ili kujifunza kutengeneza website(Hapa unakubaliana na mimi kuwa alikuwa anamaniisha wesite Development na siyo Design kama ulivyotaka kupotosha). Ambazo ni Kujifunza HTML au Softwares/Tools.
Ndugu yangu https://www.jamiiforums.com/member.php?u=53226 Option ni Moja tu unatakiwa uanze kujifunza HTML & CSS kwanza kabla ya kujifunza hizo Tools otherwise mtu anataka awe kama wewe. Nakumbuka wakati naanza Ku-Code miaka 4 iliyopita nilikatazw kabisa kutumia hizo Tools hadi nilipo Master HTML na CSS ndo nikaanza kutumia hizo Artisteer(unazotumia sasa). So hakuna cha Option hapa kama unataka kuwa website Developer lazima(rudia tena lazima) ujifunzi HTML na CSS kwanza.

4.Kuhusu watu kunijua nikweli watu wananijua na kuhusu kuwa Verified siyo issue na sija-claim even though hilo jina langu halisi. kumbuka napenda kujulikana na kujuana na watu mbalimbali so,kama unanijua ni vizuri.

MWISHO: Mimi si shindani na wewe lakini nakataa ushauri wako uliokuwa unampa mwanafunzi wa Website Developer,pia kilichopelekea kukujua ni huo ushauri wako. huwezi kutoa ushauri kama huo then ukawa unajua kufanya Website Development, kwa vyovyote vile anaetoa ushauri huo lazima awe na mapungufu kama yako. Karibu kwa matusi zaidi
 
wp.jpg
Nilitarajia utakuja na Thread ya kuuliza how to rename wp-admin page, we umekwenda kuzoa wordpress na kulitupia kavu kavu tu. Kuonesha hufuati hata terms za Wordpress umeshindwa kuacha hata ile powered by wordpress lakini ukakumbuka Designed by Fadhili Paulo. Home | Nelly&#039;s InnNelly&#039;s Inn
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom