We will never forget our school. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

We will never forget our school.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Sep 27, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Wakubwa,

  Wote tumepitia shule za msingi hapa naongelea darasa la saba (L.Y) kama tulivyozoea kuandika kwenye madaftari yetu. Baada tu ya shule za msingi kipindi hicho twasoma BURE kwa tulio wengi, tulifanya mitihani ya taifa na ndipo kipindi cha mahafali kinapokaribia, maandazi yalikuwa moto moto kuanzia mavazi, usafi maeneo ya shule, utunzi wa nyimbo, ngoma, maigizo, ngojera na risala kwa wahitimu.

  Siku ya mahafari ilikuwa open day, tulifurahi sana lakini muda wa kuagana rasmi ukifika basi tulijawa na majonzi hasa tukikumbuka upendo tuliokuwa nao kati ya walimu pamoja na wadogo zetu.

  Mimi nilimaliza shule ya msingi kijijini, lakini pia mliokuwa mijini hatukupishana sana katika dhana nzima ya sherehe ya kumaliza shule ilivyopambwa. hapa nitaongelea hasa juu ya AHADI tulizozitoka kupitia risala, maigizo, ngonjera na nyimbo, nitatoa mfano mmoja tu kwamba kuna wimbo tuliimba hivi.

  "We shall never forget our school we shall never forget you x2
  although we shall be very far away but we shall never forget you."

  Na mwingine tuliimba hivi

  "Tutamkumbuka twasemaaa (wavulana wanatangulia) kiitikio wasichana
  Na hatumsahau mwalimu wetu (Majina ya Waalimu)
  Kweli ametenda mema kwetu,
  uongozi bora - Kiitikio wa kwanza
  Kutimiza malengo - kiitikio Hatari
  Endeleza motoo babaa... (wote)

  Hizo zilikuwa siku za furaha, lakini je tumetimiza ahadi zetu tuliahidi siku hiyo?
  a) Je umesharudi shule uliyosoma na walau kuona mazingira ya ufundishaji ulivyo kwa sasa?
  b) Je umeshawahi kutoa hata 10% ya kipato chako hata cha mwezi kuchangia shule
  yako uliyosoma?
  c) Je Umeshasaidia mtoto yoyote awe yatima au asiye na uwezo kiuchumi katika shule
  uliyosoma?
  d) Umeshatoa mchango wako wowote wa kimawazo either kwa wanafunzi, kamati ya
  shule au waalimu kuendeleza shule yako uliyosoma?
  e) Umeshanunua hata dawati moja, vitabu?
  f) Ushawahi kushika chaki na kufundisha walau kwa masaa mawili (Kujitolea) kipindi cha likizo yako?

  Huoni kwa kutofanya hivi unakiuka kiapo ulichoahidi siku ya mahafali? kumbuka uliahidi "YOU WILL NEVER FORGET YOUR SCHOOL" hata kama utakuwa mbali kiasi gani.

  Fanya kitu sasa, Tunahitaji mchango wako kuwa sehemu ya mafanikio ya shule yako.
   
Loading...