We Dada kama umo humu asante sana

We Dada kama umo humu asante sana

Mu-sir

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
3,621
Reaction score
1,643
Ni muda umepita nilikuja Benki kwenu kutoa Pesa kwa Western union (Hata hivyo sikufanikiwa) ukaniomba kitambulisho ikabidi nikupe Passport yangu. Leo nilitakiwa ku submitt Passport yangu ubalozini kwa ajili ya visa ndio Nahamaki kumbe sina Passport na sijui ilipo. Nimetafuta sana ndani ya nyumba na ndani ya gari na kuuliza watu mbali mbali bila mafanikio.

Nimechanganyikiwa hadi kidogo nipate ajali barabarani. Mara nikakumbuka kuwa mara ya mwisho niliitoa kule Benki.... na kukupa wewe kama kitambulisho. ikabidi nije huku nikiwa nakumbuka akilini kuwa niliichukua kutoka kwako na kurudi nayo. Hivyo nilikuja ili tu kupata uhakika kuwa niliichukua kwako. Wakati nimefika nakutana na suprise ya passport yangu hadi nashindwa kuelezea shukrani zangu.

Nakushukuru kwa kuchukua na kuitunza Hati hiyo na nakueleza kuwa maneno ya shukrani bado nayaumba ili nije nikushukuru. Labda siku moja nitakununulia Dinner pale....

Ubarikiwe sana sana sana.
 
...labda hayumo humu, kampe lunch au dinner kwa kumshukuru kwa usamaria mwema.
 
Aaah jamani.......si ulinishukuru ya kutosha.......sasa mpaka huku......
Ukienda huko unakokwenda uniletee pafyumu..........

We mdada umetoka lini Arusha? Haya nitakuletea usijali kama ni wewe.
 
Aaah jamani.......si ulinishukuru ya kutosha.......sasa mpaka huku......
Ukienda huko unakokwenda uniletee pafyumu..........

Sabuni ya rungu inakutosha.

Cha ajabu nina passport imebakisha mwezi mmoja iishe muda wake na haija wahi kugongwa muhuri hata mmoja.
 
Sabuni ya rungu inakutosha.

Cha ajabu nina passport imebakisha mwezi mmoja iishe muda wake na haija wahi kugongwa muhuri hata mmoja.

Wee nae........twende Kigali ukaisafishe.......ni aibu sana kurenew passport plain..........uliomba ya nini sasa........?.......miaka kumi hata boda moja hujavuka........?.......acha hizo bana..........
 
Nilimshukuru na nilimpa kifuta jasho lakini nikilinganisha na umuhimu ule naona haijatosha shukrani ile ndo mana nimeandika hapa.

una yako mengi si bure,
Funguka mzee!
 
ungesahau wallet yenye mpunga ndo ungejua kama kweli ni mwema au la....
 
Back
Top Bottom