We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

kazi ipo! Ila take my word watawala roho zao zinawasuta na matumbo yanawauma na wanaona aibu kwa Watz sasa hivi
 
Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu, naomba kwanza nijibainishe wazi, mimi sio mshabiki wa Chadema wala sishabii fuja, bali ni mtetezi wa haki.
polisi wetu wanatakiwa kufanya kazi sio tuu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, bali pia kwa kutumia common sense. Kwa kilichotokea Arusha, ni polisi imejidhalilisha na sasa naana kum doubt uwezo wa Kamanda Mwema. Enzi za Mahita, hata kwa kumtazama tuu usoni, alionekana empy, lakini ukimtaza Mwema, he has substance, jana nilimshangaa sana alivyotetea vijana wake!.

Njolay akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Alhamisi moja mwaka 1995, vingozi wa kimila wa Kimasai, Ma Algwanani, waliamuru Morani wao, wachome moto ofisi ya CCM na Nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji fulani huko Ngaramtoni, huku wao wakisimamia na ofisi na nyumba ya mwenyekiti wa kijiji zikachomwa.

Ijumaa, Defender ya polisi ikawasomba hao wazee wanne na kusweka polisi Arusha walalala ndani Ijumaa hiyo, Jumamosi na Jumapili,
Jumatatu asubuhi, imji wa Arusha ukavamiwa na Morani wa Kimasai toka pande zote, wameshika shime, ngao na mikuki, wamajipaka yale marangi yao makundu na midomoni kama wamekunwa damu mbichi, hawaongei lolote zaidi ya kuhema kwa mingurumo.

Moja kwa moja mpaka ofisini kwa Njolay pale Regional Bldg. Viongozi wao huku wakizungumza kwa Lugha ya Kimasai, walimuamuru, wanawataka wale Ma Lagwanan wao wanne waachiliwe pale saa hiyo hiyo vinginevyo wataigeuza Arusha nzima dimbwi la Damu within no time!.
Njolay akawashauri, wamsubiri, aitishe kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama, wakajadiliana, Njolay akaishauri kama, wazee wa Kimasai, waachiliwe, Mkuu wa polisi akagoma, kuwa wale ni wahalifu hawawezi kuachiwa, Njolay akaondoka in person mpaka kituo kikuu cha polisi na kuamuru wazee waachiwe, atajibu mbele ya safari, wazee wale waliachiwa, na Wamasai wakarejea nao umasaini.

Hawa si ni walikuwa wahalifu kabisa tena wametenda jinai ya wazi mbele ya kadamnasi ya watu, walifanywa nini?. Huyo Mbowe na wafuasi wake wangeachiwa kuandamana kwa amani mpaka pale uwanjani, huku wakisindikizwa na polisi just ku guarantee usalama, wangepata athari gani?.

Amini nakuambia, hakuna cha habari za inteligensia wala nini, bali baada ya IGP kutangaza wameyazuia maandamano, Chadema waliokataa kutii, polisi wakaamua kuwaonyesha nani zaidi ili kuwakomoa!. Mbele ya jumuiya ya kimataifa hao vijana wa Mwema, wanamuiaibisha nani?, wanawakomoa Chadema, ama wanautia najisi mji wa Arusha ambao ndio kitovu cha utalii?. Hivi hao polisi wana akili timamu kweli?.

Kama Njoolay alipoasses situation aliamua kuwaachia wale wazee wa Kimasai, huyo Andengenya alishindwa nini kua asses?. Lengo la kumshikilia mtu ni kujiridhisha asipotee, people of no fixed abode, unamjua kabisa Godbless Lema ni Mbunge wa Arusha, Mbowe na Slaa ni viongozi wa Chadema, hivi kweli polisi walikuwa na haja ya kuwashikilia usiku kucha kwa kuhofia watatoroka!. Walitakiwa wakishaandika maelezo waawachie na kuwaambia siku ya kuja mahakamani.

Risasi za moto ni kwa wahalifu ama wanaotaka kutoroka, kwanini risasi za moto zinatumika kuwasambaza waandamaji ili hali rubber bullets zipo?.

Kama rais Kikwete atalipongeza jeshi la polisi kwa kazi mzuri iliyofanyika Arusha, sio siri, sitamshangaa, ila nitaamini kuwa kumbe ni kweli, uwezo wake wa kiakili ni ule wa GPA ya below 2.0!.

Pasco!
Tatizo limesababishwa na pande zote mbili na hili sijalifumbia macho lkn kuwapa polisi walioko underground lawama wakiwa na wao walikuwa wanajihami kupoteza maisha yao vile vile si busara.Kwanini Mh. Dr Slaa ktk hali tata kama hiyo aliamua kuingiza watu wenye hasira mtaani na kibaya zaidi kwenda kituo cha polisi kutaka kutumia nguvu kuwatoa wenzao hivi kama wangefanya mkutano baadae wakaenda kuwatoa kwa njia zinazokubalika kiutaratibu kusingeepusha haya yaliyotokea.Mara nyingine matakwa na matamanio ya kutimiza malengo yao wanasiasa yanakwanza utumikaji wa busara ktk kufanikisha hio na yanatoa mwanya kwa udhaifu wa maamuzi kuchukua mkondo na kilichotokea Arusha kimesababishwa na hili.
 
We are a land of laws, rules, and regulations. This is an example of disgruntled politicians, using their rhetorical prowess to push the public to the limit and argue them to disobey the law.

Kama polisi walisema maandamano hakuna, kwanini muandamane?

Inalilahi waina lillah rajiun (Hakika sisi ni wa Allah, na kwake tutarejea)

Polisi hawana madaraka MADARAKA YA KUTOA KUKATAZA MAANDAMANO. Wanaarifiwa ili KUTOA askari wa KULINDA USALAMA wakati wa maandamano ILI KUSIWE NA UVUNJIFU WA AMANI. KWA HAPA wewe unaota. This land is not my land mimi nimpangaji kwa walioteka nchi kwa mabavu.

We are not a land, we are people of a county a robbed country. We have laws, rules, and regulations of this nation which are abused by a clique.

This incident is an example of determined politicians, using their prowess to educate the public politely at their will without disobeying the law of thye land.

This incident is an example of mislead police force, using their guns to kill unarmed members of the public at their masters instructions to people who are excersing their constitutional rights (the law of the land).
 
Pasco!
Tatizo limesababishwa na pande zote mbili na hili sijalifumbia macho lkn kuwapa polisi walioko underground lawama wakiwa na wao walikuwa wanajihami kupoteza maisha yao vile vile si busara.Kwanini Mh. Dr Slaa ktk hali tata kama hiyo aliamua kuingiza watu wenye hasira mtaani na kibaya zaidi kwenda kituo cha polisi kutaka kutumia nguvu kuwatoa wenzao hivi kama wangefanya mkutano baadae wakaenda kuwatoa kwa njia zinazokubalika kiutaratibu kusingeepusha haya yaliyotokea.Mara nyingine matakwa na matamanio ya kutimiza malengo yao wanasiasa yanakwanza utumikaji wa busara ktk kufanikisha hio na yanatoa mwanya kwa udhaifu wa maamuzi kuchukua mkondo na kilichotokea Arusha kimesababishwa na hili.
Nakubaliana na wewe.
 
Pasco!
Tatizo limesababishwa na pande zote mbili na hili sijalifumbia macho lkn kuwapa polisi walioko underground lawama wakiwa na wao walikuwa wanajihami kupoteza maisha yao vile vile si busara.Kwanini Mh. Dr Slaa ktk hali tata kama hiyo aliamua kuingiza watu wenye hasira mtaani na kibaya zaidi kwenda kituo cha polisi kutaka kutumia nguvu kuwatoa wenzao hivi kama wangefanya mkutano baadae wakaenda kuwatoa kwa njia zinazokubalika kiutaratibu kusingeepusha haya yaliyotokea.Mara nyingine matakwa na matamanio ya kutimiza malengo yao wanasiasa yanakwanza utumikaji wa busara ktk kufanikisha hio na yanatoa mwanya kwa udhaifu wa maamuzi kuchukua mkondo na kilichotokea Arusha kimesababishwa na hili.

No body not even a child will circum to stupidity as you argue. Ndugu yako ananyanyaswa ati wewe unatulia tu unasubiri malaika wakuongoze busara mahali ambapo haipo. Malaika walishachoka na nchi hii. Wadhaifu huwaoni wanatumia askari wenye silaha za moto. Wakuu wa polisi na mabwana zao wangekuwa na busara wasingejiingiza kwenye maji yaliyotulia juu wakati chini yanakwenda kasi.

Umenikera sijui unaishi nchi gani
 
kazi ipo! Ila take my word watawala roho zao zinawasuta na matumbo yanawauma na wanaona aibu kwa Watz sasa hivi

Hakuna watawala Tanzania. Kuna viongozi waliochaguliwa kwa kura halali na asilimia nyingi tu kuliko upinzani.

Aibu? Hao viongozi wa Chadema wanajuwa aibu ni nini?

Kwanza tazama yao, wanayoyafanya. Wanathubutu mpaka kuchukuwa wake za watu kupiga nao kampeni, halafu ndio useme kuhusu aibu.

Kuna aibu zaidi ya Daktari wa kanoni kuvunja sheria za kanoni?

Kama padiri mwenye udaktari wa kanoni kaweza vunja sheria za kanoni, ni nini kitamzuwia kuvunja sheria za polisi?
 
Naona Halmashauri yako ya ubongo haina ushirikiano.Unatumia sana personal attack kuliko hoja.

Kuna hoja hapa? Raia wanaofata tu waambiwalo na viongozi wao, hata kama si jema, wameuliwa. Halafu unataka hoja? Hoja ya nini? Ya kuwafufua? Ni nini zaidi kilichowafanya hawa viongozi wa chadema wasifate amri za polisi?

Jee, hawakujuwa kukaidi amri ya polisi ni kuvunja amani na kutafuta shari na polisi?

Hoja, kuna hoja gani ya kugombea utakacho kwa kutoa roho za wengine?

Hoja? Kuna hoja ipi iliowafanya waandamane?

Kisa, labda ni kusimika misalaba? Crusade?
 
Bila maumivu hakuna matibabu simple logic

Wanaodharau amri halali wataumizwa baada watatibiwa
 
I beg Independent lawyers who are interested for our nation to consider the issue without delay! Our courts,our police force,our rulers have turned against the public. Its pity to relate Arusha event as political,its a national vice and our rulers are to brought to law and bet them kept behind bars! Gents n ladies,our nation is under arrest,our blood and human intelligence is the only power we remain with. Africa now rises to democratic dictortorship,this will remain my indelible thread ever posted at the expense of my prophecy!
 
Pasco!
Tatizo limesababishwa na pande zote mbili na hili sijalifumbia macho lkn kuwapa polisi walioko underground lawama wakiwa na wao walikuwa wanajihami kupoteza maisha yao vile vile si busara.

Mawazo ya namna hii yanashangaza; yumkini wewe unaweza kuona mtu aliyeshika manati na aliyeshika SMG kuwa wako sawa wanapotunishiana misuli. Yule mwenye SMG akimtungua jamaa na kumuua wewe unaweza kabisa kusema "makosa yalifanywa na wote wawili". Aidha hutaki kuangalia the gravity of the situation na hutaki kutambua the moral culpability aliyonayo mwenye SMG na silaha nyiingine nzito. Hii inanishangaza. Angalau basi polisi wangeokota hata kabastola kamoja toka kwa waandamanaji kusema kuwa walikuwa "wanajihami"! Wanajihami kwa watu ambao hata mawe hawakubeba zaidi ya sauti zao. Give me a F$@#%NG break!
 
No body not even a child will circum to stupidity as you argue. Ndugu yako ananyanyaswa ati wewe unatulia tu unasubiri malaika wakuongoze busara mahali ambapo haipo. Malaika walishachoka na nchi hii. Wadhaifu huwaoni wanatumia askari wenye silaha za moto. Wakuu wa polisi na mabwana zao wangekuwa na busara wasingejiingiza kwenye maji yaliyotulia juu wakati chini yanakwenda kasi.

Umenikera sijui unaishi nchi gani
Mimibaba!
wewe endelea kukereka hivyo hivyo na kuniita majina yote uyapendayo na sijui kama hayo maandamano yaliyoleta madhara yalikuondolea hilo kero? wakati kama tungejiepusha nayo tusingekaa leo hii hapa kujadili upoteaji wa maisha yao hao unaowaita ndugu zetu, wakati hata thamani ya maisha yao watu kama wewe huyathamini.Mimi binafsi hiyo serikali unayoisema imenitesa na kuyafanya maisha yangu kipindi fulani kuwa dhalili lakini je kuandamana maandamano yaliyojaa fujo na mauaji ndiyo suluhisho la kutokomeza udhalimu wa viongozi wa serikali dhidi yetu?
 
Mawazo ya namna hii yanashangaza; yumkini wewe unaweza kuona mtu aliyeshika manati na aliyeshika SMG kuwa wako sawa wanapotunishiana misuli. Yule mwenye SMG akimtungua jamaa na kumuua wewe unaweza kabisa kusema "makosa yalifanywa na wote wawili". Aidha hutaki kuangalia the gravity of the situation na hutaki kutambua the moral culpability aliyonayo mwenye SMG na silaha nyiingine nzito. Hii inanishangaza. Angalau basi polisi wangeokota hata kabastola kamoja toka kwa waandamanaji kusema kuwa walikuwa "wanajihami"! Wanajihami kwa watu ambao hata mawe hawakubeba zaidi ya sauti zao. Give me a F$@#%NG break!
Mzee Mwanakijiji!
Mfano wako hauendani na uhalisia wa kile kilichotokea kwenye tukio mjini Arusha.Vyanzo vyote vya habari vimeainisha Polisi kuzidiwa nguvu na Raia ambao unawaita wabeba manati.Swali la msingi la kujiuliza Idadi ya wabeba manati ilikuwa wangapi hadi kupelekea kuwazidi nguvu idadi ya waliobeba SMG? unapozidiwa nguvu na wenye manati wakati una SMG ,hivi hiyo SMG inakusaidia nini?Hoja ya msingi ni kwamba kama kweli wenye manati imetokea kuwazidi nguvu waliokuwa na SMG,Mabomu ya machozi,magari ya maji ya kuwasha basi hayumkiniki kwamba nguvu ya hali ya juu ilitumika kuzidi nguvu polisi wenye SMG na vitendea kazi vingine kama nilivyoanisha, kwa maana nyingine kulikuwa na fujo na uvunjwaji wa Amani kulikopelekea kupoteza maisha ya watu.Na kama kuna Polisi aliyeuawa kwa kuchomwa visu, je manati yamekuwa kisu au maneno ya waandamanaji kama ulivyoanisha imekuwa silaha yenye ncha kali ya kusababisha Multiple stabing wound kwa marehemu Polisi?
Tusiwe tunatoa nafasi kwa vitendo kama hivi chini ya kivuli cha kupambana na serikali wakati maisha ya watu yanapotea bila ya kuleta athari chanya kwa serikali au kwa wanasiasa waliosababisha.Tumeona unapousimamia utaratibu na kuufuata popote pale udhalimu unatokomea mfano halisi Chadema hao hao waliposimama kidete Mwanza na Kigoma kwa njia za kufuata taratibu na kuzisimamia zisipotoshwe wameweza kufanikisha bila ya maandamano wala mauaji.Hakuna njia ya mkato za kuleta mabadiliko bali ni kujipanga na kuweka mikakati ya kuleta mabadiliko bila ya umwagaji wa damu na upoteaji wa maisha ya watu.Yaliyotokea Arusha kila upande uliohusika una hisa yake juu ya hilo na Haya ni kulaniwa na siyakupewa nafasi.Nakuelewa Mzee Mwanakijiji ni muumini mtiifu wa maandamano na mara nyingi umekuwa muhamasishaji wa hilo lkn ktk hili la Arusha kama lengo lilikuwa ni kukutana,kuhabarishana ,kuongea na wapiga kura,kudai haki,kupanga mikakati ya kuleta mabadiliko hivi mkutano usingetimiza lengo husika hadi maandamano ambayo matokeo yake ni ngeu,uharibifu wa mali na upoteaji wa maisha ya watu.Teteeni maandamano ya Arusha lkn kulikuwa na ajenda nyingine zaidi ya ukutanaji wa watu kwa ajili ya kujadili jambo litakaloleta mabadiliko na kama ajenda ilikuwa ni kukutana na kujadili mabadiliko basi fursa ya kufanya mkutano ilikuwepo.Tuendelee kujifunika blanketi tukidhani wote hatujui kilichofunikwa na hilo blanketi.
 
Mwaihojo, japo nakubaliana wa wewe, lakini wanasiasa mahiri ulimwenguni kote, walipambana. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, inapiganiwa. Mandela aliandamana, Martin Luther King pia aliandamana, kina Kenyetta waliandamana, na wote hao walipigwa mabomu ya machozi na kuishia jela, ikiwepo loss of life, lakini mwisho wa siku, ukombozi utapatikana.

Hata Mungu alikuwa na uwezo wa kumkingia mwanaye Yesu Kristu na mateso yale, aliweza kuleta ukombozi bila kupitia mateso, lakini alimuacha ili kutoa somo kwa ulimwengu kuwa ukombozi, unakuja kwa njia ya mateso wakati wingine hadi kifo ili waliobaki waponywe.
Kwa kupigwa kwake, sisi tuluiponywa, ndivyo hivyo kwa kupigwa wana Chadema, Tanzania itaponywa!.

Aluta Continua!.

Pamoja na mapungufu tuliyonayo kama taifa lakini suala la uchaguzi wa Umeya wa Arusha halikufikia bado kwenye level ya liwalo na liwe, kwa namna yeyote kitendo cha kuwaamuru vijana kwenda kupambana na polisi kinaonyesha upeo wa maamuzi ya kukurupuka na yasiyozingatia mustakabali wa vijana wale.

Ukizingatia pia kuwa wananchi wa Tanzania ni waoga sana wa vurugu, na kwa miaka mingi sasa baada ya mfumo wa vyama vingi suala la amani ya nchi hii bado limekuwa ni turufu ya kisiasa ya CCM ikitambua kuwa majority ya Watanzania kwao amani ni muhimu kuliko mambo mengine yeyote, lililotokea Arusha linaweza likainufaisha zaidi CCM kisiasa kuliko Chadema, hivyo hizi approach japo ni valid lakini ukizitumia kwa kukurupuka bila ya kuzingatia mazingira na wakati zinaweza kuwa kikwazo cha kufikia lengo/mafanikio yaliyotarajiwa.
 
Mzee Mwanakijiji!
Mfano wako hauendani na uhalisia wa kile kilichotokea kwenye tukio mjini Arusha.Vyanzo vyote vya habari vimeainisha Polisi kuzidiwa nguvu na Raia ambao unawaita wabeba manati.

Naomba utoe mfano wa chanzo kimoja huru cha habari kilichoanisha kuwa Polisi walizidiwa "nguvu na raia". Naomba uweke kimoja tu na walizidiwa nguvu kabla ya kujaribu kuvunja maandamano au baada ya jaribio la kijinga la kuvunja maandamano halali?





Swali la msingi la kujiuliza Idadi ya wabeba manati ilikuwa wangapi hadi kupelekea kuwazidi nguvu idadi ya waliobeba SMG?

Swali hili linaweza kuwa na hekima kidogo lakini ukiliangalia halizingatii ukweli. Watu 100 wenye manati wanalinganishwa vipi na mtu mmoja mwenye SMG? Je askari mia moja wenye SMG unaweza kulinganisha na wananchi 100 ambao hawana silaha?
unapozidiwa nguvu na wenye manati wakati una SMG ,hivi hiyo SMG inakusaidia nini?

Tatizo ni kuwa hawa wananchi hawakuwa hata na manati! Hakuna aliyekamatwa na kisu wala fimbo. Walikuwa mikono mitupu. Now u tell me kuna ulinganifu gani kati ya mikono mitupu na SMG, magari ya maji ya upupu, bastola, mabuti, virungu n.k? Really? Yaani unalinganisha wananchi wasio na silaha ya yote na jeshi la Polisi lenye udhaifu wa muda mrefu na silaha bwelele?

Hoja ya msingi ni kwamba kama kweli wenye manati imetokea kuwazidi nguvu waliokuwa na SMG

hapana hii si hoja ya msingi; kwani hakukuwepo na wenye manati! walikuwwepo watu wenye mikono mitupu. Sasa hiyo ni hoja ya msingi..

,
Mabomu ya machozi,magari ya maji ya kuwasha basi hayumkiniki kwamba nguvu ya hali ya juu ilitumika kuzidi nguvu polisi wenye SMG na vitendea kazi vingine kama nilivyoanisha,

Yaani silaha zote hizo na unaniambia walizidiwa nguvu? Really, wangezidiwa nguvu maandamano yangefika mwisho. Polisi hawakuzidiwa nguvu bali waliwazidi nguvu wananchi wasio na silaha na kusababisha mauaji. Thats is a fact.


kwa maana nyingine kulikuwa na fujo na uvunjwaji wa Amani kulikopelekea kupoteza maisha ya watu.

Nice try. Hakukuwa na fujo yoyote kabla ya jeshi la polisi lenye mwelekeo wa udhalimu lilipoamua kuingilia maandamano yaliyokuwa yanasonga mbele. Haki ya kulinda uhai unaita mtu yeyote anayeshambuliwa kujitetea hata ukishambuliwa na Polisi. Wananchi walikuwa wanaandamana vizuri tu hadi pale POlisi walipoona maandamano kweli yanafanikiwa wakaamua kuingilia kati. Hakuna vurugu yoyote kabla ya polisi kuingilia kati.
Na kama kuna Polisi aliyeuawa kwa kuchomwa visu, je manati yamekuwa kisu au maneno ya waandamanaji kama ulivyoanisha imekuwa silaha yenye ncha kali ya kusababisha Multiple stabing wound kwa marehemu Polisi?

msisitizo wa neno lako ni "kama".

Tusiwe tunatoa nafasi kwa vitendo kama hivi chini ya kivuli cha kupambana na serikali wakati maisha ya watu yanapotea bila ya kuleta athari chanya kwa serikali au kwa wanasiasa waliosababisha.

Nadhani ungetazama kinyume chake. Tusiruhusu watawala kutumia nguvu dhidi ya raia pale ambapo njia nyingine zingeweza kutumika. Tusiruhusu kwa kisingizio cha kuwaridhisha wanasiasa wa chama tawala Jeshi la POlisi linavunja haki za msingi za kiraia. Hiili tusiliruhusu.

Tumeona unapousimamia utaratibu na kuufuata popote pale udhalimu unatokomea mfano halisi Chadema hao hao waliposimama kidete Mwanza na Kigoma kwa njia za kufuata taratibu na kuzisimamia zisipotoshwe wameweza kufanikisha bila ya maandamano wala mauaji.

Unachosahau ni kuwa huko kote POlisi hawakujipeleka kimbelembele kuzuia wananchi kufanya kazi zao za kisiasa. Huko kote jeshi la POlisi halikusitisha shughuli za Chadema kinyemela kama walivyofanya Arusha.

Hakuna njia ya mkato za kuleta mabadiliko bali ni kujipanga na kuweka mikakati ya kuleta mabadiliko bila ya umwagaji wa damu na upoteaji wa maisha ya watu.

Hapana, kuna wakati wananchi wanapokosa imani na vyombo vyao vya dola wana haki ya kuwakataa watawala wao kwa njia mbalimbali za kiraia. Haki hii haiwezi kuondolewa kwa vitisho. Nyerere mwenyewe alisema vizuri kabis akuwa wananchii wanapokosa imani na serikali yao na serikali hiyo inapokuwa ya kibabe dhidi yao, basi wananchi wana haki ya kuiondoa serikali hiyo kwa nguvu. Lakini kabla ya kufika huko wananchi wana haki ya kuipinga serikali hiyo na kuikataa pale inapotishia haki zao za msingi. Hii ndiyo falsafa iliyosababisha tuunge mkono ANC, FRELIMO, n.k. Ni muhimu kuelewa dhana hii ya kisiasa.

Serikali haiwezikuwa juu ya wananchi wake na viongozi wake hawawezi kutenda with impunity kwa sababu ni "serikali". Ni lazima kutambua kuwa haki ya kutawala inatoka kwa wananchi sasa serikali can not hold its citizens hostage or in contempt as it seems the Tanzanian government is doing now.



Yaliyotokea Arusha kila upande uliohusika una hisa yake juu ya hilo na Haya ni kulaniwa na siyakupewa nafasi.

Hapana, tatizo ur trying to create a moral equivalency kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wasio na silaha. You can not find that.

Nakuelewa Mzee Mwanakijiji ni muumini mtiifu wa maandamano na mara nyingi umekuwa muhamasishaji wa hilo

Usianze kunisingizia katika hilo; mimi ni muumini wa demokrasia na njia za kidemokrasia za kuwatumia ujumbe watawala. NInaamini kuwa hoja ndiyo njia ya kwanza kabisa ya kuwashawishi watawala. Lakini watawala wasiosikia la pili ni kuwapinga hadharani kwa njia halali za kiraia na kidemokrasia. Hizi ni njia za kisiasa, siyo makosa kama unavyoashiria. I'm proud to support the cause of democracy.

lkn ktk hili la Arusha kama lengo lilikuwa ni kukutana,kuhabarishana ,kuongea na wapiga kura,kudai haki,kupanga mikakati ya kuleta mabadiliko hivi mkutano usingetimiza lengo husika hadi maandamano ambayo matokeo yake ni ngeu,uharibifu wa mali na upoteaji wa maisha ya watu.

Lengo la maandamano lilikuwa kuipinga Serikali mkoani Arusha. Hayo mengine naona umekuja nayo tu. Maandamano yalikuwa ni ya kupinga serikali.

Teteeni maandamano ya Arusha lkn kulikuwa na ajenda nyingine zaidi ya ukutanaji wa watu kwa ajili ya kujadili jambo litakaloleta mabadiliko na kama ajenda ilikuwa ni kukutana na kujadili mabadiliko basi fursa ya kufanya mkutano ilikuwepo.Tuendelee kujifunika blanketi tukidhani wote hatujui kilichofunikwa na hilo blanketi.

ajenda ilikuwa kupinga vitendo vya kuingilia uchaguzi wa meya wa Arusha na kupigwa kwa mbunge wa Arusha mjini. usisahau hilo.
 
163893_475471016155_687191155_6563333_7552055_n.jpg

There was no justification whatsoever of the brutal use of force against innocent and unarmed demonstrators in Arusha on January 5th, 2011 which lead to the killing reportedly of 2 civilians and injuring a score of other demonstrators. What happened in Arusha is inexcusable and indefensible.

We have to understand that you can not have a political opposition without actual opposition. It is like having a car but denied the right to drive it while others things are all constant. What the Tanzanian government shown through its police force yesterday is an ability and willingness to thwart any strong dissent when that is dissent is paired with other means of civil disobedience such as the demonstrations.

What I still don’t understand is the fact that if there was anytime the government could have used force was the time when people were waiting for results after the much contested elections last year. During that time the political situation in Tanzania was dramatically transformed and there was a credible fear that things could have gone out of hand. But the police and other security organs remained calm, composed and restrained. They did not use force in Arusha, Mwanza, or Mbeya and when they did in fact use force it was restrained and in a relative measure to the political opposition of the time.

That was not so in Arusha yesterday. The demonstrators wanted to demonstrated going to an open space area for a political rally. It was purely a political event charged with political rhetoric. I for one expected that the police force will be there to ensure a peaceful demonstrations and safety of other non-involved people. The demonstrations was well organized and there was nothing whatsoever that signaled trouble before the main event day. None whatsoever.

But abusing their authority the police force decided to cancel the demonstrations and by doing so assaulting the right of individuals to assemble and the right of citizens to air the political grievances. This was indeed an assault on democracy and the principles that govern it.

The deaths of the two individuals can not go unrecognized. Once again our country has seen blood in the hands of the State. We have seen this during the Mwembechai killings, we have seen it in Pemba and it has happened before elsewhere (in other incidents). The police force in Tanzania has this proclivity to use brutal force against citizens not just in such political settings but as we all know during civil issues. It looks like the police force is not well trained in understanding and dealing with the modern world of political plurality and the dynamism of political dissent.

I believe Mr. Said Mwema the current IGP has lost the credibility to lead this force at this juncture of our history. And so has Mr. Andengenye the current Regional Police Commander of Arusha. These two individual bear full responsibility for what happened in Arusha yesterday and they must be sacked immediately. The individual police officers who obeyed an illegal order knowing fully that obeying an illegal order is not a criminal defense they have to be brought to justice and pay the price of the illegal killings of Tanzanians.

As we continue to forge ahead with the cause of democracy and as we continue pushing for the new constitution before 2015 we stand together with all political activists in the country as well as the human rights activists who have come out to condemn the brutal attack on civilians who were protesting their government. I urge Chadema to call for A Day of Mourning to remember our comrades and to show solidarity with each other at this time.

We have to take a stand, for in the presence of evil there is no neutrality.

My friends, if we don’t stand together to oppose the rise of political tyranny in our country then we will surely see our country falling into tyranny. We can choose to stand together or they will find a way to silence us individually. Whatever they (the government, ruling party and their puppets) do we can not retreat or surrender for a brighter future for Tanzania under new people centered Constitution is possible. Yes, a new Tanzania without CCM at the helm of power is coming we just have to hasten it.

By. M. M. Mwanakijiji (BGM).

Actually and in real situation there is similarity of these killings to the one instituted legal actions against Mr. Zombe in 2005/6; with the facts that the gap between them is that, Mr. Zombe did under secrecy and Mr. Null IGP did it publicly; so wonder if our legal system is of such double standard when it comes to human rights.
 
Back
Top Bottom