Mourinho ,sija-edit baada ya wewe kunikosoa bali niliona makosa yangu kabla ya wewe kusema
'
Pia sijatwist maneno yako wewe ndo uliyesema Cain alimwambia Mungu akikutana na watu wengine,tazama paragraph yako ya mwisho kwenye post yako
'
Lakini sehem hiyo imejirudia kwenye quote yako ya biblia kwenye posta yako uliyosema nimetwist maneno yako
'
Nashangaa kuona unasahau ulichoandika mwenyewe!
Pole sana, mbona unataka kulazimisha uelewa wako ndio uwe uelewa wa wengine?
Inawezekana kabisa waliumbwa Adam na Hawa 'tu' na wengine ni matokeo ya Evolution, ni sawa pia.
Lakini swali jepesi tu, Cain anapomwomba mungu ampunguzie adhabu ili akikutana na 'watu wengine' wasimuue kutokana na kosa lake, hawa watu wengine ni watu gani? Waliumbwa na nani? Lini? Wapi?
Mourinho ,sijui kama umenielewa
'
Unaweza ukasema kuwa binadamu alianza kuwa jiwe kisha akawa mbwa halafu binadamu
'
Sitakua na tatizo na kauli yako
'
Lakini unaposema kuwa kwa mujibu wa biblia binadamu alianzia kuwa jiwe kisha mbwa halafu akawa binadamu
'
Hapo nitakua na tatizo na kauli yako
'
Nitakua na tatizo na kauli yako kwa kuwa kwa mujibu wa biblia ni uongo,binadamu hakupitia hatua hizo
'
Ni wapi biblia inasema waliumbwa zaidi ya wawili?
'
Ni wapi nawalazimisha watu waelewe kama ninavyoelewa mimi?
'
Unapouliza Cain aliomba asikutane na watu wengine kuwa ni watu gani,kwani baada ya Caini,Adam na Hawa hawakuzaa tena?
'
Je hao hawawezi kuwa "wengine"?
Kumbe wewe ndio mwana anthropolojia? Nilimuuliza mleta mada. waweza kujibuNilikuuliza swali kutokana na hiyo post yako, hukujibu ukauliza swali jingine, nimekujibu na me naomba unijibu swali langu Mkuu.
Kumbe wewe ndio mwana anthropolojia? Nilimuuliza mleta mada. waweza kujibu
katika definition
yako ujuzi wa kujua mabaya na mema ni nini?
kwangu mimi ni utashi wa kufanya maamuzi bila kuongozwa na hisia kama
kuona njaa(senses),kutaman(emotions) nkyani kua master wa kuamua ufanye
nini saiz na usifanye nini saiz! huku ukiweka kipimo cha ubora wa hiki
ni kizuri na hiki ni kibaya.na ukishaweza kupima uzuri na ubaya nadhani
hata madhaifu ya mazuri utayaona na kujaribu kuyaboresha,that is free
thinking and being able to reason
unasema walikua bora kwa kutojua mema na mabaya kivipi wakati hawakua na
uwezo wa kubainisha hiki ni jema na hiki ni kibaya?
coz nadhan walikua wanaongozwa na emotions,na senses tu labda
unidadavulie kidogo
Mourinho ,sijui una tatizo gani,ila nimejifunza kuwa ualimu ni kipaji kikubwa na kinatakiwa kiheshimike sana,kwa maana huelewi kabisa,sijui una nini kwenye ubongo wako
'
Suala la Cain ni wewe ndo umelileta hapa sio mimi
'
Suala la "watu wengine" umelileta wewe sio mimi
'
Wewe ulisema Cain alimwomba Mungu akikutana na "watu wengine" wasimuue,mimi nikakujibu kuwa watoto waliozaliwa na Adam na Hawa hawawezi kuwa "watu wengine"?
'
Baada ya wewe na mtoa mada kuonekana kuilewa biblia tofauti,kwa maana kuwa Mungu aliumba watu zaidi ya Adam na Hawa,ndipo nikasema ni upotoshaji
'
Hapa ndipo nikakupa mfano wa binadamu kuanzia jiwe kisha mbwa halafu binadamu(isome vyema post yangu yenye mfano huu)
'
Bahati mbaya hukuuelewa mfano huo,ukafikiri nimesema wewe ndo umesema hivyo,ukweli ni kuwa niliupa mfano kukufanya ujue ni wapi sikubaliana na ninyi
'
Nadhani utakuwa umenielewa sasa!
kwa nini yahweh aliumba mti wa katikati?
Hoja yako mleta mada inaleta changamoto ila kwa mtu mwenye akili nyepesi atapepeswa na kuhadaika. Ni kweli Mungu aliwapendelea kizazi cha Adam na Hawa (ambao bila shaka ndio wana wa Israeli). Bahati mbaya hawakuwa na ufahamu wa kutambua kwamba Mungu wao aliwapenda na aliwaandaa. Sijui kwa nini aliwaandaa hao na kuwasusa wengine. Mwisho wa siku Mungu alikiri kuwa wana wa Israel hawabebeki. Kupitia Yesu Kristo, Mungu alihamishia mapenzi yake kwa mataifa (nadhani ndio wapagani).
Yesu anasema hivi katika Yohana 17: 1-12. Soma vyema.
Paulo pia anaongea na wapagani kupitia warumi kwamba, wasijishaue kwamba hawamjui Mungu. Walipewa fursa ya kuwa karibu na Mungu wakakataa. Soma Rumi 1: 18-32.
Kama haitoshi, Paulo ana siri nzito kwa waefeso kwamba mataifa ni warithi pamoja na wana wa Israeli (efeso 3: 1-13).
kila mtu anaWeza kuitumia biblia kwa manufaa yake kwa kuwa tumepewa utashi wa kuchagua mema na mabaya.
mwananthropolojia Ni kweli kuwa Yesu alilenga kuwaweka sawa watu wa israeli. Kwa ukweli wana wa Israeli tangu enzi za Musa hadi ujio wa Kristo. Shahidi ni wa haya ni maneno ya Stefano (utaniwia radhi nitaweka mwongozo tu). Mdo 7 Yote upate simulizi alilotoa Stephano mbele ya Kuhani mkuu dhidi ya ukaidi wa waisraeli.
Lakini ni Yesu huyu huyu aliyewatuma wafuasi wake akiwaambia waende ulimwenguni kote kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu...
Kadhalika ni Yesu huyu huyu kipitia Anania (Mdo 9:10-16), Paulo hakuwepo wakati Anania anapewa maagizo. Bwana anasema, Huyu (sauli) ni chombo kiteule kwangu Alichukue jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Naweza kununua hoja yako ya 'other people' lakini kusema kuwa hatuhusushwi na Kristo, na kwamba Paulo ni mwongo nakataa. Kama umeweza kuamini hoja ya other people kwa nini usiamini hoja za Paulo? Kama Petro alikabidhiwa Kanisa na Kristo, kwa nini Kristo alimwamnini wakati alimkana mara tatu? Ulitaka Paulo asiongope ili auawe mapema na kazi aliyopewa isitekelezeke?
suala la paulo lipo wazi kabisa ukisoma siku zake za mwisho mpaka kuwekwa gerezan,akiitwa mbel ya wayahudi anajifanya yeye ni myahudi anaefuata torati,akiwa na warumi anasema yeye ni wa Yesu na ni mrumi.
kwa kifupi Paulo alikua anajifanya kucheza na sheria(nadhani alikua mwanasheria),ujanjaujanja mwingi na kama Mungu anamruhusu huyo mtumishi aseme uongo ili aendelee na kazi za Mungu kuna maana gani Yesu na wanafunzi wake walipogoma kugeuza shingo zao na kusimamia imani zao mpaka dakika za mwisho?
kwani Mungu angeshindwa kuinua mtume mwingine aendelee na kazi kama Yesu alivyosema Mungu ana uwezi wa kuinua nabii hata kwenye mawe?
hakika nakwambia tusingemheshimu Yesu kama angekua kigeugeu.
hakika Paulo ni msanii
kuhus other people ushahidi wote unaonyesha hii dini haituhusu, habari zote wanajiongelea wao na sisi tunajarib kwa nguvu zote kutafta andiko litakaloonyesha sisi tunahusika kwenye hizi hadithi bila mafanikio
Nimekusoma mkuu. Hivi Mungu alishindwa nini kuwavusha wana wa israeli pale jangwani kuwapeleka nchi ya ahadi kwa muda mfupi? Kwa nini watumie miaka 40? Mungu ana njia zake za ufanyaji kazi. Kadhalika mitume wa Yesu walikuwa ni binadamu ambao wana asili yao. Kumbuka mitume walikuwa wanamshutumu Yesu mula na wenhe dhambi lakini Yesu aliwapinga. Wana hisia za kibinadamu.
Ukisoma wagalatia2;16, 19-21, Paulo anawaambia wagalatia kuwa sheria zao za torati hazitawapeleka mbinguni. Palikuwa na sintofahamu wakati Petro alipopita Galatia na kusisitizaia sheria ndipo Paulo alkpopiga tena na kuwapa huo ukweli. Kwa hiyo tukjbali tu kuwa wale ni binadamu ambao walibahatika kutumiwa n Mungu kufikisha neno lake kwa watu. Tukubali pia kuwa maandiko yana majibu kwa maswali yetu. Unataka kusema leo hii Mungu wa Israeli hajishughulishi nasi? Hata mi wakati fulani nilikuwa na maswali mengi kuhusu nafasi yetu sisi mbele ya Mungu. Majibu mengi yapo kwenye mdo na nyaraka za mitume kwa mataifa mbalimbali. Mungu kaamua kutugeukia sisi. Tusiwe kama waisrseli ambao hadi leo wanamsubiri Masiha. Waisraeli wengi ni mayahudi na si wakristo.[/QUOTE]
mmmmmmmmmmmh_hata sijaelewa...na pale nilipoelewa ninaishia kushangaa i.e iweje waisrael/wayahudi ndugu zake Yesu wamkatae mpaka sasa lakn kina yakhe kutwa kutoa mapovu mpaka kuuana.
aisee najuta kufungua hapa leo. Kama hauko vizuri kiroho unaeza kufa kabisa kiroho.
Nimekusoma mkuu. Hivi Mungu alishindwa nini kuwavusha wana wa israeli pale jangwani kuwapeleka nchi ya ahadi kwa muda mfupi? Kwa nini watumie miaka 40? Mungu ana njia zake za ufanyaji kazi. Kadhalika mitume wa Yesu walikuwa ni binadamu ambao wana asili yao. Kumbuka mitume walikuwa wanamshutumu Yesu mula na wenhe dhambi lakini Yesu aliwapinga. Wana hisia za kibinadamu.
Ukisoma wagalatia2;16, 19-21, Paulo anawaambia wagalatia kuwa sheria zao za torati hazitawapeleka mbinguni. Palikuwa na sintofahamu wakati Petro alipopita Galatia na kusisitizaia sheria ndipo Paulo alkpopiga tena na kuwapa huo ukweli. Kwa hiyo tukjbali tu kuwa wale ni binadamu ambao walibahatika kutumiwa n Mungu kufikisha neno lake kwa watu. Tukubali pia kuwa maandiko yana majibu kwa maswali yetu. Unataka kusema leo hii Mungu wa Israeli hajishughulishi nasi? Hata mi wakati fulani nilikuwa na maswali mengi kuhusu nafasi yetu sisi mbele ya Mungu. Majibu mengi yapo kwenye mdo na nyaraka za mitume kwa mataifa mbalimbali. Mungu kaamua kutugeukia sisi. Tusiwe kama waisrseli ambao hadi leo wanamsubiri Masiha. Waisraeli wengi ni mayahudi na si wakristo.