Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuulizia matokeo ya written interview ya Workers Compensation Fund (WCF) iliyofanyika March 18.
Kwa bahati mbaya hata wao WCF hawajui watatoa lini, ukiuliza kwamba hamna pesa? Wanasema wanazo, ukiuliza hamna muda? Wanasema wanao? Ukiuliza hamna uhitaji wa watu kwasasa wanajibu wanahitaji sana? Ukiuliza kwanini sasa mnachelewa wanasema sijui kwanini.
Hili zoezi ilibidi wapewe tume ya ajira (utumishi). Hawa huwa wanajitahidi sana kuwa fair hata kama wana mapungufu yao lakini hawa WCF tunakosa imani nao.
Ikiisha wiki ijayo hawajatoa matokeo nitawaletea taarifa kuhusu nafasi za kazi zile za mwaka jana kilichotokea, nitawaeleza WCF walivyotaka kuhamisha Utumishi na kuhusu vijana wanaofanya internship pale ambao ni ndugu zao pale.
Vijana wanaofanya internship hapo WCF wapate kazi kihalali, wasipate kwa magumashi. Tutahitaji mitihani yao ya written, majina yao tunayo. Kuweni makini