Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,450
- 12,317
Hii ni dalili tosha kabisa kwamba ukilala,ukila,ukinya unawaza wcb tuUkweli ni kua Wasanii walioko chini ya Label ya Wcb wananyimwa Fursa kupata Promo ya Media kubwa Kama Clouds, E-fm na Eatv&radio Zinazosikika Mikoa mingi Hapa Tanzania
Ukiangalia kwa Jicho la tatu unaona kabisa Uongozi wa Wcb una Matatizo wale Mameneja ni Wachumia tumbo Macho yao yapo Kwa Diamond tu, hao Mameneja ndo Wavurugaji wakubwa wa label kila anaetoka pale Wasafi anawalalamikia jamaa, wengi wanasema Diamond hana shida ila Sallam na Tale ni Wakuda,hawataki mtu mwingine yoyote awe karibu na Mond
Diamond kabla ya kua na hawa waganga njaa alikua na mahusiano mazuri na radio za hapa bongo na hata pale alipokua wakitofatiana suluhu ilikua inatafutwa na yanaisha,.
Leo hii hana maelewano mazuri na Clouds, E-Fm na Eatv&radio, hizi ni radio zinazosikika Eneo kubwa la tanzania, hiyo Wasafi radio inasika Dar tu,
Ni Nadra sana Kumuona au kusikia msanii wa Wcb kafanya Media tour sana utawaona Times Fm ambao nao wanasikika mikoa miwili kama si mitatu hapa tanzania,.
Wanakosea sana pale wanapodhani Promo la Youtube na Insta linatosha,. Ni Watanzania wachache wanaomiliki Smartphone wenye uwezo wa kuingia uko Insta na Youtube App zinazo kula bando kama Mchwa, Na asilimia kubwa wanamiliki vitoch vyenye radio
Wasipobadilia hiyo Label itakupigwa kifo cha Mende ipate Mimba ishindwe kuendelea na Masomo