A-Z Rich Mavoko kuondoka WCB - Mchawi Babu Tale na Sallam

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Kuna mambo mengi yamejificha juu ya Mavoko kuondoka wasafi, tuachane na propaganda za udini kama wengi walivyokuwa wanaaminishwa.

Mtakumbuka wakati Mavoko anasaini WCB alikuwa katika ubora wake kiasi cha kuanza kushindanishwa na Diamond Platnumz. Hilo suala lilikuwa likimnyima usingizi Diamond na kuhofia kushushwa. Ili kuweza kummaliza Mavoko ilitakiwa asainiwe WCB, kweli waliweza kumshawishi na kumpa mkataba wa miaka 10.

Kimbembe kikaanza pale Wasafi Rich Mavoko hakuwa tena yule wa 'Pacha wangu' bali kila alichotaka kufanya alikuwa anabanwa na mkataba, akabaki kuwa mpenzi mtazamaji.

Kila mmoja anamjua Mavoko kuwa ni mtunzi mzuri sana, ana nyimbo kibao za kutoa lakini ataanzia wapi masikini kutoa! Mkataba ulikuwa mchungu sana kwake, hata kolabo nazo zikawa shida na kukatishwa tamaa.

Diamond ni mbaya ndio lakini wabaya zaidi ni Babu Talent(Babu Tale) na Sallam. Hawa wanamnyenyekea sana Diamond wapate kula yao. Ilifika wakati mpaka Mavoko alivyowasikilizisha nyimbo zake, kama waliipenda nyimbo hawa wanyonyaji walitoa uamuzi kuwa hapa akikaa Diamond hii ngoma itakuwa noma. Wimbo kama Baila kapokwa mtoto wa Moro.

Nyimbo ambazo wasanii wa WCB walipeleka kwenye menejimenti na hawa wanyonyaji kujua kuwa zitakuwa hit songs lazima walishinikiza Diamond awepo. Wimbo kama Kokoro ilibid iwe Mavoko na Davido, Kwang'waru ilibidi asimame Konde Boy na Davido ila menejimenti ikasema hapa piga ua lazima akae Mond.

Mavoko alikuwa na jina kubwa Wasafi lakini mifukoni hana mavumba goto limekata, asilimia kubwa ilikuwa inaingia WCB. Kaondoka mnyonge hana kitu huku Babu Talent na Sallam wakitokwa mashavu.

Pale mwenye sauti kidogo kati ya wasanii ni Konde Boy kipenzi cha Mond, wengine hawana namna ndio maana unaona kama Vany Boy kajenga kastudio kake, huyu alishapigwa biti ukizingua tunakurudisha Tip Top connection.

Kichekesho ni Mbosso, huyu pesa yake inaenda kwa Fella mnyonyaji kwa makubaliano kwamba Fella ilitakiwa aue kundi la Mkubwa na wanae maana walishaanza kuwa tishio na likivunjika basi WCB wamtwae Baba Moza, ila akawachomolea ndio wakadondokea kwa Mbosso.

Mavoko soon atakuwa juu kama yote, subiri Boss Ruge apone muone, NASEMA subiri Boss Ruge afanikiwe kupona muone kampeni za kumkabidhi Mavoko kiti cha ufalme zitakavyo-damshi.

Nimewapa habari kama yote.

Mbona mnapata shida sana nyie wakina Soudy?
 
Attachments

  • VID-20180721-WA0012.mp4
    505.9 KB · Views: 93
Alafu hiii mada imekaa kinafki kwasababu mavoko alisaini WCB wakati ana hali mbaya kimuziki na baada ya kuna WCB ndio akaanza na nyimbo ya imebaki story nayo ikahit, ikaja KOKORO ndio uspime tena kamshirikisha Diamond sasa kama diamond alikuwa ananyimwa usingizi na mavoko aliwezaje kumruhusu kutoa ngoma kali kama kokoro, ?

Mavoko kujitoa wcb ndio atapotea kabisa wait and see
 
Yaani hapo kwenye hali mbaya naomba niongezee "Sana"
 
Nikiangalia wimbo wa Kwangwaru naona jinsi Diamond alivyomharibia wimbo Hamonizer.
Hayo ya kundi kuhujumiana tuwaachie wao
 
Alafu hiii mada imekaa kinafki kwasababu mavoko alisaini WCB wakati ana hali mbaya kimuziki na baada ya kuna WCB ndio akaanza na nyimbo ya imebaki story nayo ikahit, ikaja KOKORO ndio uspime tena kamshirikisha Diamond sasa kama diamond alikuwa ananyimwa usingizi na mavoko aliwezaje kumruhusu kutoa ngoma kali kama kokoro, ?

Mavoko kujitoa wcb ndio atapotea kabisa wait and see
Imebaki story aliufanya kwa tud thomas ilikuwa hit song kipind anataka kuachia ule wimbo ndipo harakat za kuingia wasafi zilikuwa zinaanza ndipo tud na wasafi walikubaliana kuingiza vionjo vya wasafi ktk wimbo wa mavoko kifupi wimbo kwa asilimia kubwa umefanya na tud.
 
Hao hao haswa Sallam kamfanta Doamond awe kituko.. kisa asikae na mwanamke mwenye akili nae yaani wao wakakosa kupiga pesa zile za pembeni..

Eeeeh

Zari aliwaogopeshaaaaa

Diamond nae kawa zobaaaa.. vikiki upupwu anazidi kupoteza mashabiki wa kutumia pesa kwake..
 
Lakini yote kwa yote nafasi ambazo diamond aliwekwa alizitendea haki.je kuna alipoharibu?
 
Imebaki story aliufanya kwa tud thomas ilikuwa hit song kipind anataka kuachia ule wimbo ndipo harakat za kuingia wasafi zilikuwa zinaanza ndipo tud na wasafi walikubaliana kuingiza vionjo vya wasafi ktk wimbo wa mavoko kifupi wimbo kwa asilimia kubwa umefanya na tud.
Acha uongo,imebaki story imefanywa kwa tuddy kipindi kile tuddy alikuwa sound injinia wa bendi ya diamondi.tuddy kafanya na I miss u pia kafanya my number one remix.rich kasaidiwa sana na diamond.kitu msichojua diamond anasauti ya mwisho na maamuzi ya mwisho pale wasafi hao mameneja hawapindui kwa diamond.
Akina mchomvu wanampotosha sana rich pia rich havumiliki kama baraka da prince
 
Soma vizur nilichoandika umeelewa au umekurupuka?
 
Mtakumbuka wakati Mavoko anasaini WCB alikuwa katika ubora wake kiasi cha kuanza kushindanishwa na Diamond Platnumz. Hilo suala lilikuwa likimnyima usingizi Diamond na kuhofia kushushwa. Ili kuweza kummaliza Mavoko ilitakiwa asainiwe WCB, kweli waliweza kumshawishi na kumpa mkataba wa miaka 10.
Hayo mengine sina haja ya kujadili lakini hilo hapo juu ni uongo usio na maana yoyote!!

Ni kweli Rich Mavoko ni mkali lakini Rich Mavoko alienda WCB wakati ameshaanza kupotea!! Aliposainiwa na Kaka Empire, watu walitarajia huenda labda angerudi yule Mavoko wa zamani, lakini wapi!!!!

Msipende kujisahaulisha haya mambo! Mavoko ambae alitabiriwa kuchukua nafasi ya Diamond ni wa enzi za Marry Me:

Back
Top Bottom