WCB Label Wanawahitaji CLOUDS MEDIA kuliko hata Wcb wanavyowahitaji Babu tale na Sallam sk

Ukweli ni kua Wasanii walioko chini ya Label ya Wcb wananyimwa Fursa kupata Promo ya Media kubwa Kama Clouds, E-fm na Eatv&radio Zinazosikika Mikoa mingi Hapa Tanzania

Ukiangalia kwa Jicho la tatu unaona kabisa Uongozi wa Wcb una Matatizo wale Mameneja ni Wachumia tumbo Macho yao yapo Kwa Diamond tu, hao Mameneja ndo Wavurugaji wakubwa wa label kila anaetoka pale Wasafi anawalalamikia jamaa, wengi wanasema Diamond hana shida ila Sallam na Tale ni Wakuda,hawataki mtu mwingine yoyote awe karibu na Mond

Diamond kabla ya kua na hawa waganga njaa alikua na mahusiano mazuri na radio za hapa bongo na hata pale alipokua wakitofatiana suluhu ilikua inatafutwa na yanaisha,.

Leo hii hana maelewano mazuri na Clouds, E-Fm na Eatv&radio, hizi ni radio zinazosikika Eneo kubwa la tanzania, hiyo Wasafi radio inasika Dar tu,

Ni Nadra sana Kumuona au kusikia msanii wa Wcb kafanya Media tour sana utawaona Times Fm ambao nao wanasikika mikoa miwili kama si mitatu hapa tanzania,.

Wanakosea sana pale wanapodhani Promo la Youtube na Insta linatosha,. Ni Watanzania wachache wanaomiliki Smartphone wenye uwezo wa kuingia uko Insta na Youtube App zinazo kula bando kama Mchwa, Na asilimia kubwa wanamiliki vitoch vyenye radio

Wasipobadilia hiyo Label itakupigwa kifo cha Mende ipate Mimba ishindwe kuendelea na Masomo
Hii ni dalili tosha kabisa kwamba ukilala,ukila,ukinya unawaza wcb tu
 
Nani mwenye maelewano mazur na media zote akafanikiwa
Usiseme hawafanyi vizuri,au kufanya kwako vizuri ni mpaka walingane au kumzidi Diamond?Unaweza sema akina Marioo,King Kiba,Jux,Barnaba,Ney wa mitego,Vanessa,Harmonize Nk hawafanyi vizuri?
Shida ni kuwa unaka kufanya kwao vizuri ni mpaka wamshinde Diamond!
Diamond tayari alikuwa ameshatengeneza fan base,lakini diamond bila maelewano na clouds na diamond akiwa na maelewano na clouds naona atasogea mbele zaidi kama atakuwa na maelewano na media nyingine!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadogo na Mshumaa!Sasa unataka harmonize awe na ngoma kubwa kuliko kwangaru wakati ni juzi tu katoka WCB?Hata diamond hana ngoma kubwa kuliko kwangaru!
Hata siku moja Media haijawahi kumuhitaji mtu kuliko yeye anavyoihitaji!Sema mnachoshindwa kuelewa ni kuwa Diamond naye pia ana Media,hivyo ni Media vs Media &Diamond!
Diamond ana ngoma nyingi hit song African beauty, kanyaga,yope remix, baba lao hizo kadogo na mshumaa sio hit song pamoja na mbio au ujui maana ya hit song?hit ni Kama iokote ya Maua sama au Muziki ya darassa.Hit song ya kiba ya mwisho ni seduce me baada ya Hapo hana ngoma yoyote hit song.
 
Mtoa mada kila mara mnaitabiria anguko la hiyo lebo lakini halifiki...kwa sasa hizo redio unazo zisema hazina nguvu yoyote na ndo maana wamepambana sana na Diamond ila wamesanda...moja ya vitu ambavyo vinasambaza sana mziki owa sasa ni boda boda na uzuri zipo nchi nzima na ndo maana kuna nyimbo nyingi watu wamezijua baada ya kuzisikia kwenye boda boda,bado kuna insta,youtube nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond ana ngoma nyingi hit song African beauty, kanyaga,yope remix, baba lao hizo kadogo na mshumaa sio hit song pamoja na mbio au ujui maana ya hit song?hit ni Kama iokote ya Maua sama au Muziki ya darassa.Hit song ya kiba ya mwisho ni seduce me baada ya Hapo hana ngoma yoyote hit song.
We ndo Maana wanakuita Lokole izo ulizotaja za Diamond ni ngoma za kawaida ni matakataka labda yopo ambayo ni idea ya mtu,.

Alafu kumbe hujui Maana ya hit Song
 
Mtoa mada kila mara mnaitabiria anguko la hiyo lebo lakini halifiki...kwa sasa hizo redio unazo zisema hazina nguvu yoyote na ndo maana wamepambana sana na Diamond ila wamesanda...moja ya vitu ambavyo vinasambaza sana mziki owa sasa ni boda boda na uzuri zipo nchi nzima na ndo maana kuna nyimbo nyingi watu wamezijua baada ya kuzisikia kwenye boda boda,bado kuna insta,youtube nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna media inayopoteza kupambana msanii, ebu lete ushaidi kua walipambana nae.
 
Ukweli ni kua Wasanii walioko chini ya Label ya Wcb wananyimwa Fursa kupata Promo ya Media kubwa Kama Clouds, E-fm na Eatv&radio Zinazosikika Mikoa mingi Hapa Tanzania

Ukiangalia kwa Jicho la tatu unaona kabisa Uongozi wa Wcb una Matatizo wale Mameneja ni Wachumia tumbo Macho yao yapo Kwa Diamond tu, hao Mameneja ndo Wavurugaji wakubwa wa label kila anaetoka pale Wasafi anawalalamikia jamaa, wengi wanasema Diamond hana shida ila Sallam na Tale ni Wakuda,hawataki mtu mwingine yoyote awe karibu na Mond

Diamond kabla ya kua na hawa waganga njaa alikua na mahusiano mazuri na radio za hapa bongo na hata pale alipokua wakitofatiana suluhu ilikua inatafutwa na yanaisha,.

Leo hii hana maelewano mazuri na Clouds, E-Fm na Eatv&radio, hizi ni radio zinazosikika Eneo kubwa la tanzania, hiyo Wasafi radio inasika Dar tu,

Ni Nadra sana Kumuona au kusikia msanii wa Wcb kafanya Media tour sana utawaona Times Fm ambao nao wanasikika mikoa miwili kama si mitatu hapa tanzania,.

Wanakosea sana pale wanapodhani Promo la Youtube na Insta linatosha,. Ni Watanzania wachache wanaomiliki Smartphone wenye uwezo wa kuingia uko Insta na Youtube App zinazo kula bando kama Mchwa, Na asilimia kubwa wanamiliki vitoch vyenye radio

Wasipobadilia hiyo Label itakupigwa kifo cha Mende ipate Mimba ishindwe kuendelea na Masomo
Kaka mpaka leo bado unafikir kizamani hivyo , Radio zenyewe hizi zilitaka kumpa chid benzi show ya elfu 50 ili wampe promo , WCB wakamatie hapo hapo mpaka tuhushimiane, kama bando linakushinda ufai kuwa mshabiki wa WCB maana ata pesa ya show huwezi kuwa nayo
 
kwa taarifa nilizopata toka clouds mleta uzi milembe panakuita...
pleas itikia wito kabla hujaharibikiwa zaidi
 
Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom