kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
- Thread starter
- #21
Juzi nilikwenda kijijini kutembelea ndugu na jamaa zangu, kila unapopita wanalia hawana pesa. Mimi nikawauliza kule mjini wanapenda ndizi, kuku, mbuzi, choroko, malimao na ndimu, machungwa, bata, mahindi na hata mihogo. Ni nani anavyo nimsaidie kuvibeba kwenye gari langu bure aende akauze mjini? Kati ya wale wanaolalamika hakukuwa na mwenye hata kuku 5, wala mbuzi, wala ng'ombe, wala ndimu wala sungura waliokosa mnunuaji. Nikawauliza mnalalamika nini na kumlalamikia nani? Mbona hamna kitu cha kuuza mpate pesa?Rudi katika uhalisia katazame maisha ya watanzania wakaida na hali zao kiuchumi halafu ndio useme ubora wa kiongozi huyu tuliye nae
Wao wanalalamika tu maisha magumu