Wazungu wanajua kuwa Tanzania sasa inae Rais sahihi

Rudi katika uhalisia katazame maisha ya watanzania wakaida na hali zao kiuchumi halafu ndio useme ubora wa kiongozi huyu tuliye nae
Juzi nilikwenda kijijini kutembelea ndugu na jamaa zangu, kila unapopita wanalia hawana pesa. Mimi nikawauliza kule mjini wanapenda ndizi, kuku, mbuzi, choroko, malimao na ndimu, machungwa, bata, mahindi na hata mihogo. Ni nani anavyo nimsaidie kuvibeba kwenye gari langu bure aende akauze mjini? Kati ya wale wanaolalamika hakukuwa na mwenye hata kuku 5, wala mbuzi, wala ng'ombe, wala ndimu wala sungura waliokosa mnunuaji. Nikawauliza mnalalamika nini na kumlalamikia nani? Mbona hamna kitu cha kuuza mpate pesa?

Wao wanalalamika tu maisha magumu
 
Dunia ya leo kumdanganya mtu kwa flyover nayo yataka moyo, ajira hakuna, mishahara watumishi wanalia, biashara zinakufa bado huyu jamaa analeta porojo utawaeleza nini watanzania waliopotelewa na ndugu zao kwa ugonjwa wa corona ambao jina umebadilika ukaitwa changamoto ya upumuaji, maana ya changamoto ni kitu ambacho hua kinaweza kutatuliwa na hata kisipotatuliwa hakina madhara sana, corona sio changamoto ni tatizo na ndio maana linaacha madhara makubwa sana
Kama angekuwa amekosea kwenye kupambana na corona basi ungetuonyesha ni Rais gani alipatia kwenye kupambana na corona ambaye watu wake hawakufa kwa covid 19. Hizo ni porojo tu kwasababu hakuna aliyekuzuia usijifungie ndani, usinawe mikono, usivae barakoa, usisafiri safari zisizo za lazima.
 
Yeye kaacha kutegemea wafadhili? Juzi tu waziri wake kaenda kwa wazungu Ufaransa kuomba halafu kodi gani anakusanya wakati biashara zote kauwa au unababaishwa na matakwimu ya kupika?
Hata Marekani inakopa China kwa kazi maalum. Hata sisi kukopa kwaajili ya kazi maalum kama kumalizia reli, bwawa la umeme, na barabara kuna ubaya gani?. Zamani tulikuwa tukikopa mikopo ya kipumbavu isiyofanyakazi zilizokusudiwa wakati wa kukopa.
 
Rais Nyerere RIP alishasemaga kuwa kama mtu mwenye akili nyingi akikupa ushauri wa kijinga na wewe ukaufuata ushauri huo kama ulivyo atakudharau sana. Viongozi wengi wa Afrika walishindwa kusema NO kwa ushauri wa kijinga wenye haara nyingi kwao waliokuwa wakipewa wa wazungu. Walishindwa kusema NO kwasababu mbalimbali zikiwepo zile za:

1. Whites are always rights
2. Whites are intelligent
3. Whites knows everything
4. Whites are much better (superiors) than blacks, so you can not argue with them
5. Whites are richer than blacks, saying no to them will lead into losing their financial supports
6. Whites have military powers they can use them to sack african leaders out of power if they go against them.

Rais Magufuli anaifahamu siri hii kubwa ya wazungu. Rais Magufuli anafahamu kuwa siri kubwa ya kufanikiwa ni:
1. Kuwaamini wataalam wako
2. kuwa specious na kila mtu wa nje na ndani kwenye uchumi, afya na mipango ya taifa.
3. Kuwa siri kubwa ya maendeleo ni wananchi kulipa kodi, matumizi bora ya fedha zako na kujitegemea
4. win-win projects kutoka kwa wazungu na wenye mitaji wanaotaka kuwekeza

Inawezekana sisi wenyewe hatujui lakini wazungu weshajua miaka 5 iliyopita.
Huna akili
 
Kama mkopo gani ambao ulikopwa na haikufanya kazi iliyokusudiwa? Huyo mtu mbaya sana kazi yake ni kutukana na kukashifu viongozi wengine waliopita anajiona yeye mungu mtu na kujifanya kujua kila kitu kumbe ni mwizi kuliko hao wengine pia ni mbaguzi kwa ujumla huyo mtu wako hakupaswa kabisa kushika nafasi kubwa.
Wakati wetu sisi tulipokuwa watoto, tunapotaka kununua mpira wa miguu, jezi, filimbi au viatu vya kuchezea kwenye timu zetu za mpira tulikuwa kama timu tunakwenda kufanyakazi za vibarua kama ujenzi, kulima, kubeba, kuosha magari, nk ili tupate pesa za kununulia kama ni mpira mpya, jezi. viatu, nk
Huna akili
 
Huna akili
Real? punguza hasira nafahamu nawe ulikuwa mnufaika wa awamu zilizopita.

Tulipokuwa watoto enzi za Nyerere rip tulikuwa tukiifahamu thamani ya kujitegemea. Tulipokuwa tunahitaji mpira, viatu au jezi kwaajili ya timu yetu tuliluwa tunatafuta kazi tufanye ili tupewe hela za kununulia mpira au jezi, lakini baada ya Nyerere hata watoto walifundishwa kutegemea wahisani na wafadhili. watoto hawatafuti kazi tena ili wapate hela ya kununulia mpira wao bali wanatandika mkeka njiani kuomba hela za kununulia mpira kutoka kwa wapita njia, wenye vyombo vya usafiri na kwenda kwa matajiri kuomba hela ya kukunulia mpira, jezi, maji ya kunywa na dawa za kujichua wakati wa mechi. Vijana wanaamini kwenye kupewa sio kutafuta. Huko ndiko taifa lilikokuwa likielekea,

wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi, TRA walikuwa wanakula hiyo kodi kidogo wakiokuwa wakiikusanya. Sasa hivi thubuuuutu uone
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom