Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Natanguliza kutoa onyo kwa Watanzania kuacha wivu hasa kwa wakazi wa mkoa wa Geita linapokuja suala la maendeleo.
DPP ametumia mamlaka aliyonayo kisheria na kuteleza hukumu ya utaifishaji wa bil 5.4 ambazo zilipatikana kwa biashara haramu ya upatu.
Mimi kama mkazi wa mkoa wa Geita, eneo la Bukoli niliamua kwenda Chato kuwaona jamaa zangu, jambo lililonishangaza ni shida kubwa ya upatikanaji wa maji.
Ziwa lipo karibu sana hata Km mbili hazifiki, pamoja na mtandao wa maji kuwepo kwenye makazi ya watu, maji hayatoki kwenye mabomba na hutoka kwa mgao,nyakati zingine usiku wa manane.
Hivyo basi, naomba mbunge wa Chato achangamkie fursa ya hii pesa ambayo imepatikana, aombe ipelekwe Chato ili maji yawe yanatoka wakati wote. Maana inakuwa aibu kama vile Chato ni mbali na ziwa.
N.b: Chato ni sehemu ya Tanzania. Ndio maana zilipojengwa flyover Dar wakazi wa Geita wahakumaindi.