Wazo la Siku: Usifurahie Adui yako aangukapo

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
Katika WAZO LA SIKU lililotangulia, tuliona umuhimu wa kuitafuta Furaha, na kuwajali wengine kama malengo muhimu sana kwa Mwaka unaoanza.

Kwavile furaha ni muhimu katika maisha yetu, kamwe tusiifurahie huzuni ya wengine hata ya Adui zetu.

Kama unavyoihitaji FURAHA, basi JALI na furaha ya mwenzako kwa MAANA HUJIONGEZEI chochote pale mwenzako anapoingia katika HUZUNI.

Hivyo basi; FURAHINI pamoja nao WAFURAHIO; LIENI pamoja nao WALIAO (Warumi‬ ‭12‬:‭15‬).

Tena, tusibague katika KUTOA BARAKA, bali; WABARIKINI wanaowaudhi (Warumi 12:14).

Zingatieni Kabisa jambo hili; BARIKINI, wala MSILAANI (Warumi 12:14)

Tena; USIFURAHI adui yako AANGUKAPO; ajikwaapo, usiache moyo wako ushangilie(Mithali 24:17)

Lakini, *Adui yako akiwa na njaa, MLISHE; akiwa na kiu, MNYWESHE; * maana ufanyapo hivyo, UTAMPALIA makaa ya moto kichwani pake (Warumi ‬ ‭12‬:‭20‬).

Kamwe; MSIMLIPE mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu WOTE (Warumi ‬ ‭12‬:‭17‬).

Lakini;
Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi MTAZAMWE na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, HAMPATI thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni (Mathayo 6:1)

KATIKA kuwapenda na KUWAJALI wengine, PENDO lisiwe na unafiki LICHUKIENI lililo ovu, mkiambatana na lililo jema (Warumi 12:9)

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima MKIWATANGULIZA wenzenu (Warumi 12‬:‭10‬)

Tumsifu Yesu Kristo
 
Hupaswi kuwa na adui, ili furaha yako ikamilike lazima usamehe, kwa hiyo huwezi kuwa na adui, ukishakuwa na adui tu, then ni halali kufurahia aangukapo.
 
Kweli kabisa ila bila Kuwezeshwa na Roho Mtakatifu mwenyewe huwezi... Tumwombe Sana atupe neema
 
Back
Top Bottom