Damu yangu itakufadhaisha kwasababu siku ukipumzika mawazo yako yatanikumbuka furahi leo mimi nimeenda kwa amani

Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
461
500
Basi kama ilivyo kawaida na desturi ya kibinadamu mtu mke au mume akikua hupewa mji wake naye akajitegemee kwa maana yampasa mtu ale kwa jasho na matunda ya mikono yake.

Ndivyo ilivyo kuwa kwa kijina yule aliyewashangaza wengi kwa ujasiri na weledi wake katika kipaji chake cha kushirikiana na wana kijiji wenzie na moyo wake thabiti wa kupenda kuwajuza watu mambo mengi wasiyo yajua. Mungu alimjalia ujasiri wa kutafuta habari na hadithi mbalimbali ambazo watu wa jamii yake pale kijijini hawakuwa na uwezo na uthubutu wa kuzitafuta.

Alifanya yote hayo kwa moyo akiamini asilimia kubwa ya watu wa kijiji chake ni watu wanaopenda kusikia mambo lakini huwa hawajali mpaka jambo hilo lilete madhara. Hiyo ilikuwa ni tabia na desturi ilio jengeka katika kijiji kile ambacho msingi wa jina lake (KICHAWATUWA) ulitokana na tabia ya watu na viongozi wake kutojali thamani ya kutafuta habari na hata zilipo patikana ama kwa ghafla au kwa kuletwa na majirani wenye mapenzi mema, hawakuonyesha kustuka wala kujali.

Maranyingi hatua zilichukuliwa pale tu madhara yalikuwa tayari yamekwisha kutokea. Katunene hakuipenda tabia hiyo maana moyoni aliwaza siku zote kwamba MCHELEA MWANA KULIA HULIA YEYE, hivyo alijitahidi kujaribu kuifanya jamii yake iwe ni yenye kupenda kutafuta habari na kuzitumia habari hizo kwa ustawi wa maisha ya wana kijiji kwa ujumla.

Alikuwa akiamini moyoni mwake ya kwamba mteni mkuu wa kijiji kile , alikuwa ni mtu aliyejisahau na kwamba madaraka kwake na ukuu na fahari vinayeye, akasahau kwamba hata kabla yake walikuwepo watemi wengi ambao pamoja na mambo mengine waliwahi kufanya mengi akiwemo mtemi NGOZA alieye fanikiwa kujenga ngome kuzunguka kijiji chotee cha KICHAWATUWA. Mtemi mkuu aliyejulikana kama (KANTASUNDWA) alikuwa ni mtu mwenye majivuno mtu aliye amini kwamba cheo cha utemi ni cheo milki ya familia na kama itatokea yeye hayupo basi mtoto wake au jamaa yake ya karibu itarithi kiti chake hivyo hakuna mtu angayeweza kwa namna yoyote ile kumtoa katika kiti cha enzi cha kitemi.

Mfalme (KANTASUNDWA) alikuwa mtu mashuhuri kwani alisifika kwa kugawa mvinyo kila alipoonekana, na kila alipo enda watu waliimba na kumshangilia kwa ngoma na nderemo, watu walitandika kanga ili mfalme apite juu yake na wakaimba wakisema "huyu ndiye mfalme tuliye mtaka maana hugawa pombe papo kwa hapo hakuna ahadi hakuna deni ".

Basi wimbo huo ukawa mashuhuri masikioni na midomoni mwa wana nchi wengi wa kijiji cha (KICHAWATUWA) , kiasi kwamba kila mahali ulipopita angalisikia wimbo "huyu ndiye mfalme tuliye mtaka maana hugawa pombe papo kwa hapo hakuna ahadi hakuna deni".

Watumishi wa mteni kwa maana ya wasaidizi wake katika baraza la kitemi na ushauri kwa mtemi walikuwa ni watu ambao walitumia muda mwingi kupita katika kila kona ya kijiji kuwaeleza wana kijiji ya kwamba haija wahi kutokea tangu kijiji chetu kuanzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1724 kupata mtemi mwenye roho na moyo wa kugawa pombe kama huyu mtemi KANTASUNDWA, kumbe mmekuwa ni wenye bahati bahati kuliko. Kitu hiko kilichagiza kuwaaminisha watu kwamba huyu ndiye mtemi yule tulie kuwa tukiomba kwa mizimu na mababu na sasa mizimu imejibu.

Kantasundwa hakuwahi kumuamini hata mwanae wakiume aliye julikana kama AMINI kitu kilicho mfanya mfalme ashone gunia kubwa kwakutumia ngozi za wanya na kisha kulipaka udogo juu yake, ikiwa ni kama hazina za sarafu ya kijiji ambayo yeye peke alikuwa na mamlaka ya kutumia kadiri alivyo ongozwa na maamuzi ya kitemi.

Hakupenda wanakijiji wahoji matumizi ya fedha zinazotokana na mauzo ya mazao ya mashamba ya kijiji wala zile za ushuru wa mifugo na tozo za mwaka kwa ajili ya sikukuu ya kijiji, kila aliye thubutu kunyenyua mdomo alikiona cha mtema kuni. Watu walio hoji walifungwa minyororo na kuburutwa na magari ya farasi na kupigwa viboko vya tumboni hata kufa. Mfalme aliogopeka kila alipoingia watu wali sanda wakatetema kwa hofu ya moyo wapo walio kufa kihoro wapo walio zikimbia familia na kuhamia mistuni kuokoa nafsi zao. Mfalme alitisha mpaka akapewe jina ya kwamba ni mfalme KANTANSUNDWA A.K.A NYONGO YA MAMBA.

Katika harakati za kutaka kuhakikisha wana kijiji hawa hoji chochote washauri wa baraza la kitemi na washauri watatu wa mtemi waka mshauri mteni kutunga sheria kali saana zinazo ambatana na adhabu ya kifo kama ikiwezekana zitazowafanya watu waogope kohoji mapato yatokanayo na mazao ya mashamba ya kijiji na sarafu za michango ya mifugo. Hakika mfalme aliishinda jamii hakuna jemedari yeyote wala mwanamasumbwi wala waganga mashuhuri wa jadi wala wapiga lamri wala makuhani wala kiongozi mkuu wa sungusungu wala waongoza matambiko ya kijiji wala wazee wenye hekima wala wapiga bakora wakijiji wala wafua vyuma wala wakwezi wa miti mirefu, wote walisalimu amri kwa mtemi. Ima mtemi alikuwa jemedari wa yoote.

Kijana yule aliye amini katika habari na umuhimu wake akavaa ujasiri moyoni mwake akasema kila jambo ni habari ifikapo masikioni mwa mtu. Macho huona maandishi yenye ujumbe fulani na huyabadilisha kuwa habari isimuliwayo. Kitendo cha Mtemi NYONGO YA MAMBA kukataa watu wasijadili mapato na matumizi ya kijiji chao kazi ya mikono yao wenyewe tena mashamba ya urithi wa babubu zao wenyewe, kitendo cha Mtemi kuwa uwa kwa mateso makali wanakijiji walio ama hoji au kutaka kujua habari za matumizi ya mfuko ule mnono ulio shonwa kwa ngozi za wanyama, na kunakshiwa kwa udogo wa mlima chabya pia ilikuwa ni habari. Aliamini hilo.

Kijana yule akaumia moyo akasema moyoni mwake iweje Mteni na mtawala mwenye mamlaka na nguvu zisizo mwilini mwake anatumia habari ama anazo zipata moja kwa moja kwenye mikutano yakijiji anapohojiwa na wana kijiji wenzie au habari anazo pata kutoka kwa baraza la washauri wa mtemi na anazitumia kuwa adhibu wanakijiji wenzake kwa mateso makali na kuwaua, kwanini na mimi nisitumie habari kuwa habarisha wana kijiji wenzangu kuhusu mambo mabalimbali yanayo kizunguka kijiji chetu hata kama yatamuudhi Mtemi? Hapana mm nitatumia pia habari kama njia moja wapo yakuwajuza wenzangu mambo.

Akaapa akisema nitatoa habari na habari itaniua nipo tayari kupata mateso na kuburuzwa na magari ya farasi hata kufa lakini habari itafika ama sipo lakini habari ni lazima iwe habari. Kijana yule akaendelea kutafuta habari na kuzifikisha kwajamii yote ya kijiji kwanjia mbali mbali zikiwemo za nyimbo na ngoma za asili. Watu wakaanza kuamini katika umuhimu wa habari na kupashana habari. Siku moja akiwa msituni aliwakuta watu wakijiji jirani wanakata misitu kutoka katika mipaka ya kijiji chao mbali kidogo na lango lakuingia kwenye ngome ya kijiji.

Kijana yule alikimbia kwenda mpaka kwa mtemi akapiga magoti na kuinamisha kichwa kama ilivyo kuwa desturi ya wakatu wao mtu atakapo kuongea na Mtemi ni lazima apige goti na kuinamisha kichwa chini, hapo ndipo sungusungu na walinzi wa nyumba ya Mteni humwamuru kuingia ndani kuongea na Mtemi. Kijana yule akaingia ndani akakaa kichini kwenye kiti maalum kilicho tengenezwa kwa mti mgumu wa mninga na ngozi ya punda milia kwaajili ya wageni, akaketi na kumwambia mtemi kwamba kuna watu nimewakuta huko wana kata miti kutoka kwenye mpaka wetu mbali kidogo na lango la kuingilia ngomeni naomba kuwasilisha habari na aksante.

Mfalme akashukuru na akawatuma vijana wake na magari ya farasi kwenda kuwafurusha mbali wavamizi hao. Wakaenda mbio wakatoka katika lango la mji wakawafurusha na kuwaua wavamizi kumi na mmoja. Mfalme akafurahi akasema mm ninapenda kusikia mambo kama haya sipendi kusikia habari za ajabu ajabu akamtunuku kijana yule sarafu kadhaa na jozi ya ngombe wakulimia akamshukuru kwa moyo wa ujasiri na kwa habari za haraka zilizo okoa lasirimali kutoka katika mikono ya wavamizi.

Mtemi alipendelea zaidi kusikia habari zinazo msifu na kumsujudia kutokana na nafasi yake, Lakini pia mtemi alipenda kusikia habari zihusuzo upotevu wa rasilimali za ndani ya kijiji zinazo fanywa na wavamizi kutoka nje ya kijiji lakini hakuwa tayari kumvumilia mtu yeyote awaye ama kwa namna yeyote ile kutaka kutoa habari za upotevu wa sarafu kutoka katika mfuko ule ulio shonwa kwa ngozi za wanyama kutoka kwa mtu yeyote yule wala kulitaja jina la mfalme katika maudhui isiyo yenye kulisifia. Alisema "mm ni NYONGO YA MAMBA huto baki salama ukicheza na jina langu " .

Kijana yule alipata umashuhuri mkubwa saana katika kijiji kile habari zake zikamsaidia saana wakati fulanj Mtemi kujua vijiji vya jirani vina fanya nini lakini pia aliweza kupata habari nyingi na mbalimbali kwa maana kijana yule alikuwa ni hodari wa habari na mwandishi aliye fanya kazi kwa moyo wa kujituma na mwaminifu wa kile alicho kiamini.

HAKIKA KILA MWAMINIFU HUFIA KIAPO CHA MOYO ALICHO KIAMINI.

Kama ilivyo desturi hakuna lenye mwanzo lika kosa mwisho,. Pamoja na uhodari wake wote wa kuihabarisha jamii yake na utawala wa mteni katika mambo mengi kwa maslahi yao, lakini kazi ya mikono yake badala ya kuila ikamla.

Mungu wa mbinguni akampatia Mtemi mtoto mwingjne wa kiume . Ilikuwa ni tarehe (24 ). mwezi wa (Bwana kutokushaurika aliwahi kwenda na mavi ukweni). mwaka (habari ni kuhabarishana katika yote). Ndiyo kipindi ambacho Mtemi alipata mtoto huyo wa kiume, alipozaliwa tu mfalme akampatia jina CHILIMACHIKOME. Tangu siku hiyo alipozaliwa mtoto alikuwa akilia tu alikuwa analia ala za muziki kitu ambacho kilimfanya mtemi na mama mtemi wastaajabu ni kwa nini wamepata mtoto wa aina hiyo ambaye akilia hulia ala za miziki. Kwa majira yetu haya tungesema ni ala nzuri za music wa Tewatsavenger ujulikanao kama AMINADO. Nenda kausikilize kwa mudawako.......uweze kuvuta taswira.

Mfalme na mkewe wakaamua kufanya mashauri ya siri waende kumtupa mtoto mbali huko pembezoni mwa ngome mahali karibu na njia indayo kwenye kisima kinacho hudumia kijiji kile cha mtemi NYONGO YA MAMBA. siku kadhaa zilipo pita wakasubiri mtoto amelala wakamchukua wakapanda gari ya farasi( chariot) wakaenda kumtupa huko waliko panga wao.

Kijana yule mpenda kutoa taarifa siku hiyo alikuwa msituni nje kidogo ya ukuta wa ngome ya kijiji akijaribu kutafuta taarifa husuusani za wavamizi wa rasilimali za kijiji kutoka nje , alikuwa akizunguka huku na huko akaona gari ya Mtemi inaingia mahali fulani akasogea karibu akajificha katika nyasi akaona Mtemi na mke wake wakishuka kutoka katika gari lile na kuacha kifurushi kidogo kikiwa kimefungwa nguo nyeupe. Akajipa muda akasubiri Mtemi NYONGO YA MAMBA AONDOKE.

Hata walipo fika mbali huko kiasi cha gari ile (chariot) kuto kuonekana, ndipo kijana yule akasogea kuulekea mzigo ule walio uacha akaufunua na ndipo akagundua kuna mtoto mchanga ndani yake. Ubaridi ulipo mpiga mtoto yule alistuka na kuanza kulia. Kijana yule alipigwa na bumbuwazi kusikia mtoto yule akilia ala nzuri za muziki kiasi hiki!'!!! moyoni mwake akasema na hii ni habari nita ihabarisha niendako.

Akaondoka akipiga kifua konde asiamini ni kwanini NYONGO YA MAMBA afanye unyama ule? Kitu kika mjia moyo kwamba kwasababu mtototo yule ni mchanga na kwamba hawezi kuji tetea. Basi nitaenda kwa Mtemi kumueleza akijua kwamba nimejua basi basi nitakuwa nimeokoa maisha ya mtoto yule. Kijana yule akaondoka akaenda kuaga nyumbani kwao akawaambia wazazi wake na mke wake naenda kwenye mambo yangu ya habari nitarudi nikipeleka habari.

Kijana yule alipofika kwa Mtemi NYONGO YA MAMBA akaingia na kumpasha habari zile mtemi yule. Mtemi akamuuliza "Habari hizi umesha mwambia mtu yeyote au mmoja kutoka katika jamaa yako"?

Akajibu. "Hapana mtu aliye pata habari hizi hapo kabla isipokuwa ni wewe pekee mtukufu" mfalme akaingia chumbani kwake akashauriana na mke wake akawaita mmoja kati ya walinzi wake wa kikosi cha mbele, wakanena akawaambia nitafutieni vijana hodari wa kikosi maalumu cha mbele, na wapanda farasi na wanamashua; kwa majira yetu tungesema wana maji. Akawaambia, ""Mtu huyu ni hatari kwa usalama wa na fasi yangu kama mtemi lakini ni adui mkubwa kwa usalama wa kijiji chetu naam nina mtia hatiani na kumkabidhi mikoni mwenu fanyeni mtaloweza damu yake isi mwagike katika nchi maana isije ikawa ni laana katika ardhi yetu. Sawa sawa?""

Wakajibu ""sawa mkuu na mtawala tumesikia tutatekeleza"".

Wakamchukuwa kijana yule aliyeamini katika habari kama nyenzo muhimu ya kuleta ustawi na uthubutu wa watu katika kupambana na changamoto katika kijiji chake, waka msweka katika gari la wale sungusungu wapanda farasi, wakasubiri hata ilipo fika usiku wa manane wakamuondoa wakampeleka katika bwawa la kuabudia mizimu lenye samaki wengi, waka mfunga jiwe zito kiunoni, wakaandika kwa herufi kubwa BURIANI MWANA HABARI HURU damu yako iwe juu yake aliye tupa amri na sio sisi.

Akawaambia amini nawaambia damu yangu haito nyamaza Ima enyi watembezi pia, Mimi nina kufa leo lakini kesho ni zamu yenu, Tazama mnavyo niweka humu nimeacha mke, mali, ndugu na jamaa. Hakika nina kufa nanyi mtakufa pia. Kamwambieni Mtemi, Kwa umri wake wa miaka 50 amebakiza miaka 26 ya furaha baada ya hapo ni shida na taabu. Mwambieni mm nmetangulia na yeye atakufa kama mimi, maana imeandikwa, ( MWANADAMU YEYOTE ALIYE ZALIWA NA MWANA MKE SIKU ZAKE ZA KUISHI SI NYINGI NAZO HUJAA TABU). niagieni mke na wanangu najuwa wana nitafuta hawajui nilipo mungu akipenda tutaonana baadaye. Waambieni wanakijiji wenzangu kama mambo wata yaacha yaendelee hivi kama ya livyo mimi kuuwawa kwa kazi ya mikono yangu, na watu wakaogopa kutoendelea kutafuta habari na kumwambia ukweli Mtemi, amini kuna siku wote :
Wenye maarifa;
Wenye hekima,
Wapiga lamli,
Makuhani,
Wahunzi,
Wadomi,
Na ninyi sungu sungu, woooote tuta cheza wimbo mmoja MTINDO TOFAUTI NA MAHALI PAMOJA siku moja.
Wale sungusungu wa mashuwa waka mtupa bwawani akazama na huo ukawa mwisho wake na mwisho wa habarii zake mdadisi yule (KATUNEE).

Siku iliyo fuata ndugu na jamaa na wana kijiji wapenda haki na habari huru wakamtafuta bila ya mafanikio wakamwendea mtemi, wakalalamika juu ya hilo mtemi akawaambia ni kipi bora kiwapasacho kukipigania , usalama na amani ya kijiji au maisha yenu pasi na usalam? Ondokeni mkafanye kazi maana kazi ni bora kuliko maisha ya mtu mmoja.

Wakatoka kwa ghadhabu ya maneno yale ya Mtemi. Na kijjini zika vuma habari zake watu wakanong'ona kila mahali, Mtemi akasikia habari hizo akajawa na hofu ya nguvu ya uma, akayaweka madaraka yake rehani kwa hofu yake mwenyewe, akawaita wale wakuu wa vikosi vya sungusungu wa kijiji na wale wa mstari wa mbele akawataka ushauri wa nini lakufanya kupunguza manung'uniko ya wanakijiji. Nao wakamwambia tupige marufuku watu kutokuongelea habari hizo wawapo mashambani au sehemu za kuabudia mizimu hata kwenye mikutano ya kijiji maaana jambo hili litaleta fadhaa katika kijiji chetu na kuzorotesha usalama.

Mfalme akakubaliana nao, nao wakapiga la mgambo kijiji chote kuwaambia ya kwamba yeyote Mtu mume au mke atakaye sikika akinongona juu ya habari za kijana yule au mambo mengine sawasawa na hayo ataadhibiwa viboko 12 vya tumboni hata kufa. Kila mtu akawa muoga wa nafsi yake. Watu wakaogopa kuhoji na wenye hekima na maarifa katika kijiji, woote wakawa kimya hapakuwepo na mtu mwenye kuinua kinywa chake wote wakajawa hofu ya maisha yao na mali zao.

Siku iliofuata hasubuhi watu wakatoka asubuhi na mapema kama ilivyo kawaida yao kwenda kufuata maji nje kidogo ya mbali ya ukuta wa ngome ya kijiji. Walikuwa akina mama watano na vyombo vyao vya kutekea, wakatembea umbali kidogo na hata walipo kikaribia kisima, wakasikia sauti za mtoto akilia ala saafi za muziki saafi. Wale wa mama wakasogea pahala pale lakini kabla hawaja karibia nguvu ya muziki ikazidi kiwango cha moyo kuhimiri furaha ya muziki, hivyo wakatupa ndoo nakuanza kukata viuno. Wamekata viuno.................................... kutoka asubuhi mpaka saa kumi na mbili.

Waume zao walipo ona ya kwamba mbona wake zetu hawajarudi mpaka sasa, waka kusanyana wanaume woote pale kijijini wakabeba na mashoka, mikuki na mapanga wakaenda kuwafuata huko kisimani. Walipo karibia hapo kisimani wakasikia sauti nzuri ya ala za muziki wasiweze kuvumilia pia, wakatupa mapanga na mashoka nao wakaanza kukata viuono ....................................

Watoto wao walipo ona sasa usiku umeingia, wakasema kulikoni? Huko tena ngoja tuwafuate tukashuhudie nao wakabeba mijeredi na manati wakatoka nje ya uzio wa ngome wakatembea umbali lakini walipoikaribia ile sehemu ya kisima wakasikia sauti nzuri ya ala za musiki nao wakatupa mijeredi na manati nao wakaungana kuanza kukata viuo. Waka kata viunoo........................

Vongozi wa mitaa na wajumbe wa mitaa walipoona usiku mkubwa umeingia watu wao hawarudi na kwamba kijiji kimeishiwa watu, ikabidi nao waka chukuwa mihuri na nyaraka zao wakatoka kuelekea huko pia wapate kujua ni nini kimejiri. Walipo karibia kisima nao hao wangaingia kwenye mkumbo huo wakatupa nyaraka na mihuri wakaanza kukata mauno. Wamekata wamekata.........

Wachungaji na mapadree na mashekhe na mashemasi nao walipo ona kwamba kijiji kime kuwa kimya wakaitana kwa umoja wao, wakabeba na biblia zao na qurani zao wakaenda kwa ajilii ya maombezi ya kitu kile cha watu kuhama kijiji bila kurudi kwani haija wahi kutokea hapo kabla. Wakatoka na walipo kikaribia jirani na kisima wakasikia pia ala nzuri za musiki wakatupa vitabu vyao pembeni wakavua kanzu na mishipi wengine. Wakaanza kukata mauno pamoja nao. Wakakata mauno..............................!!!!

Vyombo vya ulinzi vya kijiji kwa maana ya askari wa mashuwa na askari wa farasi na waendao kwa miguu wakajipanga wakidhania kijiji kimevamiwa na wahaini au wahujumu rasilimali kuta nje. Wakavaa kijeshi wakapanda farasi wakachukuwa na silaha zao za kivita na maguruneti, wakatoka kwa makundi wakagawana njia wakaelekea huko pia.

Vile vikosi vilipo fika pale vikasikia ala za muziki ule vyote vikaweka silaha vikatupa bunduki pembeni nakuanza kukata mauno dhidi ya muziki ule. Wamekatamaunoooo...........................

Mwisho wakajikuta kijiji kizima kime hama wameenda kucheza muziki wenye ala ileile isipokuwa mtindo (steps) tofauti. Watu wamehamia huko wakicheza mziki uleule mmoja. Hakuna wenye hekima wala, wachungaji wala wapiga ramli wala mashehe wala majasiri katika kunena wala wataua wala wakuu wa vikosi vya sungusungu wenye nguvu. Wooote wakawa huko wakicheza mdundo uleule.

Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake akiwaambia, nadhani mnaona yanayo tendeka hapa, hili ni kwa ajili ya jambo lile...... la yule mtoto wetu sasa hawa jamaa kama watarudi huko watafahamu ukweli wote nami sitakuwa nanguvu tena kwa jambo lilotendeka enendene ndani chukueni lile gunia na sarafu lote lililo shonwa kwa ngozi ambalo ndilo hazina yetu hapa, Mkalipakie kwenye chariot chukuoni na vito vyote vya thamani pakieni pia, tukimbie tuenende mbali kabla hawajarudi na hasira tusije tukafa masikini maana wakiujua ukweli hasira zao zita simama juu yangu na sinto kuwa kiongizi wao tena, maana wote watakuwa wana cheza muziki wenye kufanana na wameujuwa ukweli.

Mtemi akaondoka na hifadhi yote akatokome na mke na walinzi wake kusiko julikana hata sasa. Wanachi walipo rudi waka lala asubuhi walipo amka wakapata taarifa ya kwamba Mteni NYONGO YA MAMBA HAYUPO na makazi yapo wazi. Watu wakakusanyana katika mkutano na wale wajumbe wa mitaa kwa pamoja.

Wakaomba mkuu wa sungusungu msaidizi yule aliye bakia baada ya yule mkuu kutoroka na Mtemi, aje kwaajili ya kuongozana na wananchi kadhaa waingie ndani ya nyumba ya mtemi waangalie nini kimejiri. Ndipo walipo ingia ndani na kukuta lile gunia la hazina ya kijiji limeondoka na Mtemi. Wanachi wakalia kwa uchungu wakapiga mayowe wakazikumbuka nguvu walizo tumia kwenye mashamba ya kijiji na michango ya mifugo yao . Wakasononeka mioyo wakasema yupo wapi kijana yule mwana habari huru aliye tueleza wakati ule manufaafaa ya kutafuta na kupata habari manufaa yakupashana habari za uhakika kwa woteee yuko wapi yule...................?

Wakalia kwanini Mteni alitukataza kuhoji mambo yetu wenyewe tunayo yafanya kwa nguvu zetu wenyewe habari za watu wetu wenyewe michango ya mifugo yetu wenyewe?

Wana kiji wakalia kwa uchungu wakisema?

Eeeh mtemi umetufanyia nini hicho?!! sisi tulikuwa tuna lima kwenye mashamba ya kijiji tena juani, wewe umekaa hemani kwako kivulini, tulipalilia na kuvuna wewe ulikaa bure kula na kusaza kama kiongozi wetu, hakuna ulipo zalisha bali uli kukusanya na kutumia. Ulimuru sungusungu watupige bakora za tumbo tulipo hoji mbona huna hurumaa? Hivi umetoroka kweli na sarafu yetu? "Oweeee.. Oweee...Oweee..." vilio vilisikika.

Wakaanza kulia tena....

Viongozi wetu mliosoma kuliko sisi wanyonge mlishindwa kutumia nguvu ya hoja ya usomi wenu kumwambia Mtemi hapa ndiyo hapa sio? "Oweee... Oweee...

Enyi mapadree, mashemasi, mashekhe,na makuhani mlishindwa kutuhubiria tulisimamie hili kama haki yetu kwanin nanyi pia mlinyamaza hamkukemea. Oweee....Oweeeee....Oweeeee....

Enyi wa kuu wa sungusungu kwanini mlishindwa kumdhibiti mtu asiye na nguvu kiliko ninyi badala yake mkatuadhibu sisi kwa kutaka kuhoji mapato na matumizi ya kazi za mikono yetu na michango yetu wenyewe? Oweee....Oweee......

Enyi wazee na wenye hekima kwanini mlifunga vinywa vyenu hamkusema kitu licha ya kwamba ninyi niwashauri wazuri katika jamii? Owee.......Oweeeee........Oweee....

Watu wakawarudia wale viongozi wengine na kuwambia kwanini mlitusaliti tulio wengi na kumkumbatia mmoja katika maswala magumu na kwa nini hamkumpinga yuko wapi sasa na ninyi mko wapi sasa? Owee........Owee........

Mayowe yalisikika kila kona ya kijiji watu wakililia hazina yao kazi ya mikono yao kubebwa na Mteni NYONGO YA MAMBA.

Wale askari wakaya kumbuka maneno ya kijana yule KATUNENE mwana habari huru, mtafuta habari na mpasha habari. Waka huzinika mioyoyo wakapiga vifua kwa hasira wakafura na kukoromaa kwa dhiki kuu iliyojaa mioyoni mwao waka yakumbuka maneno ya mwisho ya kijana yule. Ya kwamba kama mtanyamaza siku moja;

"WOTE TUTA CHEZA WIMBO MMOJA LAKINI KWA MTINDO TOFAUTI NA MAHALI PAMOJA"

Wakamaliza kwakukubaliana kwamba hakutokuwa na mtu yeyote ataye kuwa kiongozi miongoni mwetu atakaye zuwiya mjadala huru katika mambo muhimu kama matumizi ya sarafu na mapato ya kijiji , hakuna mtu ataye zuwiya kwa namna yoyote ile utafutaji, upataji na utoaji wa habari katika kijiji chetu na huo ndo ukawa wimbo wao wakudumu hata sasa. Kila ulipo pita ulikuta bango:

HABARI NA MWANAHABARI HURU KWA USTAWI NA MAENDELEO.

Watoto wakaimba mashuleni hata leo.

REST IN PIECE KATUNENE.
chilemba wa mela pamputi.

Ndugu yenu.
 
Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
461
500
Umeandika gazeti sababu ulikua na muda wa kuandika gazeti! Sasa mimi sina muda wa kusoma gazeti!

Ingekua ni story iko MMU kule ningesoma, sasa kumbe jukwaa la siasa!
Wewe kazi yako ni kukosawa na ndo maana hili lika itwa the forum of the great thinker. Tusichishane mzee baba nenda kwenye udaku mzee baba
 
Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
461
500
Mm nime amua kushuka mkuu. wewe ukijua kuandika inatosha . Wenao penda kujifunza mambo watasoma sio mpaka wewe wala mm sikuandika kwaajili wewe usome. Yumkini unapungukiwa maarifa kwasababu kusoma kwako au kuto soma kwako hakuni ongezei wala kunipunguzia kitu ndugu. Heshma ni bora kuliko sadaka huwezi kujua kila kitu na ninacho kijua mm huwezi kukijuwa pia . Wala ukichangia hoja katika hbari sifaidiki kitu kama usingalivyo changia pia . Fanya unapita mazima kama unavyo zipita hoja maelfu kwa maelfu humu jukwaani na hiyo itakupunguzia udhia wa moyo bila sababu.
Em jifunze kuandika Kaka ndy niangalie ni busara gani nitumie ili nikujibu.
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,623
2,000
Basi kama ilivyo kawaida na desturi ya kibinadamu mtu mke au mume akikua hupewa mji wake naye akajitegemee kwa maana yampasa mtu ale kwa jasho na matunda ya mikono yake.

Ndivyo ilivyo kuwa kwa kijina yule aliyewashangaza wengi kwa ujasiri na weledi wake katika kipaji chake cha kushirikiana na wana kijiji wenzie na moyo wake thabiti wa kupenda kuwajuza watu mambo mengi wasiyo yajua. Mungu alimjalia ujasiri wa kutafuta habari na hadithi mbalimbali ambazo watu wa jamii yake pale kijijini hawakuwa na uwezo na uthubutu wa kuzitafuta.

Alifanya yote hayo kwa moyo akiamini asilimia kubwa ya watu wa kijiji chake ni watu wanaopenda kusikia mambo lakini huwa hawajali mpaka jambo hilo lilete madhara. Hiyo ilikuwa ni tabia na desturi ilio jengeka katika kijiji kile ambacho msingi wa jina lake (KICHAWATUWA) ulitokana na tabia ya watu na viongozi wake kutojali thamani ya kutafuta habari na hata zilipo patikana ama kwa ghafla au kwa kuletwa na majirani wenye mapenzi mema, hawakuonyesha kustuka wala kujali.

Maranyingi hatua zilichukuliwa pale tu madhara yalikuwa tayari yamekwisha kutokea. Katunene hakuipenda tabia hiyo maana moyoni aliwaza siku zote kwamba MCHELEA MWANA KULIA HULIA YEYE, hivyo alijitahidi kujaribu kuifanya jamii yake iwe ni yenye kupenda kutafuta habari na kuzitumia habari hizo kwa ustawi wa maisha ya wana kijiji kwa ujumla.

Alikuwa akiamini moyoni mwake ya kwamba mteni mkuu wa kijiji kile , alikuwa ni mtu aliyejisahau na kwamba madaraka kwake na ukuu na fahari vinayeye, akasahau kwamba hata kabla yake walikuwepo watemi wengi ambao pamoja na mambo mengine waliwahi kufanya mengi akiwemo mtemi NGOZA alieye fanikiwa kujenga ngome kuzunguka kijiji chotee cha KICHAWATUWA. Mtemi mkuu aliyejulikana kama (KANTASUNDWA) alikuwa ni mtu mwenye majivuno mtu aliye amini kwamba cheo cha utemi ni cheo milki ya familia na kama itatokea yeye hayupo basi mtoto wake au jamaa yake ya karibu itarithi kiti chake hivyo hakuna mtu angayeweza kwa namna yoyote ile kumtoa katika kiti cha enzi cha kitemi.

Mfalme (KANTASUNDWA) alikuwa mtu mashuhuri kwani alisifika kwa kugawa mvinyo kila alipoonekana, na kila alipo enda watu waliimba na kumshangilia kwa ngoma na nderemo, watu walitandika kanga ili mfalme apite juu yake na wakaimba wakisema "huyu ndiye mfalme tuliye mtaka maana hugawa pombe papo kwa hapo hakuna ahadi hakuna deni ".

Basi wimbo huo ukawa mashuhuri masikioni na midomoni mwa wana nchi wengi wa kijiji cha (KICHAWATUWA) , kiasi kwamba kila mahali ulipopita angalisikia wimbo "huyu ndiye mfalme tuliye mtaka maana hugawa pombe papo kwa hapo hakuna ahadi hakuna deni".

Watumishi wa mteni kwa maana ya wasaidizi wake katika baraza la kitemi na ushauri kwa mtemi walikuwa ni watu ambao walitumia muda mwingi kupita katika kila kona ya kijiji kuwaeleza wana kijiji ya kwamba haija wahi kutokea tangu kijiji chetu kuanzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1724 kupata mtemi mwenye roho na moyo wa kugawa pombe kama huyu mtemi KANTASUNDWA, kumbe mmekuwa ni wenye bahati bahati kuliko. Kitu hiko kilichagiza kuwaaminisha watu kwamba huyu ndiye mtemi yule tulie kuwa tukiomba kwa mizimu na mababu na sasa mizimu imejibu.

Kantasundwa hakuwahi kumuamini hata mwanae wakiume aliye julikana kama AMINI kitu kilicho mfanya mfalme ashone gunia kubwa kwakutumia ngozi za wanya na kisha kulipa udogo juu yake, ikiwa ni kama hazina za sarafu ya kijiji ambayo yeye peke alikuwa na mamlaka ya kutumia kadiri alivyo ongozwa na maamuzi ya kitemi.

Hakupenda wanakijiji wahoji matumizi ya fedha zinazotokana na mauzo ya mazao ya mashamba ya kijiji wala zile za ushuru wa mifugo na tozo za mwaka kwa ajili ya sikukuu ya kijiji, kila aliye thubutu kunyenyua mdomo alikiona cha mtema kuni. Watu walio hoji walifungwa minyororo na kuburutwa na magari ya farasi na kupigwa viboko vya tumboni hata kufa. Mfalme aliogopeka kila alipoingia watu wali sanda wakatetema kwa hofu ya moyo wapo walio kufa kihoro wapo walio zikimbia familia na kuhamia mistuni kuokoa nafsi zao. Mfalme alitisha mpaka akapewe jina ya kwamba ni mfalme KANTANSUNDWA A.K.A NYONGO YA MAMBA.

Katika harakati za kutaka kuhakikisha wana kijiji hawa hoji chochote washauri wa baraza la kitemi na washauri watatu wamtemi waka mshauri mteni kutunga sheria kali saana zinazo ambatana na adhabu ya kifo kama ikiwezekana zitazowanya watu waogope kohoji mapato yatokanayo na mazao ya mashamba ya kijiji na sarafu za michango ya mifugo. Hakika mfalme aliishinda jamii hakuna jemedari yote wala mwanamasumbi wala waganga mashuhuri wa jadi wala wapiga lamri wala makuhani wala kionzozi mkuu wa sungusungu wala waongoza matambiko ya kijiji wala wazee wenye hekima wala wapiga bakora wakijiji wala wafua vyuma wala wakwezi wa miti mirefu, wote walisalimu amri kwa mtemi. Ima mtemi alikuwa jemedari wa yoote.

Kijana yule aliye amini katika habari na umuhimu wake akavaa ujasiri moyoni mwake akasema kila jambo ni habari ifikapo masikioni mwa mtu. Macho huona maandishi yenye ujumbe fulani na huyabadilisha kuwa habari isimuliwayo. Kitendo cha Mtemi NYONGO YA MAMBA kukataa watu wasijadili mapato na matumizi ya kijiji chao kazi ya mikono yao wenyewe tena mashamba ya urithi wa babubu zao wenyewe, kitendo cha Mtemi kuwa uwa kwa mateso makali wanakijiji walio ama hoji au kutaka kujua habari za matumizi ya mfuko ule mnono ulio shonwa kwa ngozi za wanyama, na kunakshiwa kwa udogo wa mlima chabya pia ilikuwa ni habari. Aliamini hilo.

Kijana yule akaumia moyo akasema moyoni mwake iweje Mteni na mtawala mwenye mamlaka na nguvu zisizo mwilini mwake anatumia habari ama anazo zipata moja kwa moja kwenye mikutano yakijiji anapohojiwa na wana kijiji wenzie au habari anazo pata kutoka kwa baraza la washauri wa mtemi na anazitumia kuwa adhibu wanakijiji wenzake kwa mateso makali na kuwaua, kwani na mm nisitumie habari kuwa habarisha wana kijiji wenzangu kuhusu mambo mabalimbali yanayo kizunguka kijiji chetu hata kama yatamuudhi Mtemi? Hapana mm nitatumia pia habari kama njia moja wapo yakuwajuza wenzangu mambo.

Akaapa akisema nitatoa habari na habari itaniua nipo tayari kupata mateso na kuburuzwa na magari ya farasi hata kufa lakini habari itafika ama sipo lakini habari ni lazima iwe habari. Kijana yule akaendelea kutafuta habari na kuzifikisha kwajamii yote ya kijiji kwanjia mbali mbali zikiwemo za nyimbo na ngoma za asili. Watu wakaanza kuamini katika umuhimu wa habari na kupashana habari. Siku moja akiwa msituni aliwakuta watu wakijiji jirani wanakata misitu kutoka katika mipaka ya kijiji chao mbali kidogo na lango lakuingia kwenye ngome ya kijiji.

Kijana yule alikimbia kwenda mpaka kwa mtemi akapiga magoti na kuinamisha kichwa kama ilivyo kuwa desturi ya wakatu wao mtu atakapo kuongea na Mtemi ni lazima apige goti na kuinamisha kichwa chini, hapo ndipo sungusungu na walinzi wa nyumba ya Mteni humwamuru kuingia ndani kuongea na Mtemi. Kijana yule akaingia nadani akaa kichini kwenye kiti maalum kilicho tengenezwa kwa mti mgumu wa mninga na ngozi ya punda milia kwaajili ya wageni, akaketi na kumwambia mtemi kwamba kuna watu nimewakuta huko wana kata miti kutoka kwenye mpaka wetu mbali kidogo na lango la kuingilia ngomeni naomba kuwasilisha habari na aksante.

Mfalme akashukuru na akawatuma vijana wake na magari ya farasi kwenda kuwafurusha mbali wavamizi hao. Wakaenda mbio wakatoka katika lango la mji wakawafurusha na kuwaua wavamizi kumi na mmoja. Mfalme akafurahi akasema mm ninapenda kusikia mambo kama haya sipendi kusikia habari za ajabu ajabu akamtunuku kijana yule sarafu kadhaa na jozi ya ngombe wakulimia akamshukuru kwa moyo wa ujasiri na kwa habari za haraka zilizo okoa lasirimali kutoka katika mikono ya wavamizi.

Mtemi alipendelea zaidi kusikia habari zinazo msifu na kumsujudia kutokana na nafasi yake, Lakini pia mtemi alipenda kusikia habari zihusuzo upotevu wa rasilimali za ndani ya kijiji zinazo fanywa na wavamizi kutoka nje ya kijiji lakini hakuwa tayari kumvumilia mtu yeyote awaye ama kwa namna yeyote ile kutaka kutoa habari za upotevu wa sarafu kutoka katika mfuko ule ulio shonwa kwa ngozi za wanyama kutoka kwa mtu yeyote yule wala kulitaja jina la mfalme katika maudhui isiyo yenye kulisifia. Alisema "mm ni NYONGO YA MAMBA huto baki salama ukicheza na jina langu " .

Kijana yule alipata umashuhuri mkubwa saana katika kijiji kile habari zake zikamsaidia saana wakati fulanj Mtemi kujua vijiji vya jirani vina fanya nini lakini pia aliweza kupata habari nyingi na mbalimbali kwa maana kijana yule alikuwa ni hodari wa habari na mwandishi aliye fanya kazi kwa moyo wa kujituma na mwaminifu wa kile alicho kiamini.

HAKIKA KILA MWAMINIFU HUFIA KIAPO CHA MOYO ALICHO KIAMINI.

Kama ilivyo desturi hakuna lenye mwanzo lika kosa mwisho,. Pamoja na uhodari wake wote wa kuihabarisha jamii yake na utawala wa mteni katika mambo mengi kwa maslahi yao, lakini kazi ya mikono yake badala ya kuila ikamla.

Mungu wa mbinguni akampatia Mtemi mtoto mwingjne wa kiume . Ilikuwa ni tarehe (24 ). mwezi wa (Bwana kutokushaurika aliwahi kwenda na mavi ukweni). mwaka (habari ni kuhabarishana katika yote). Ndiyo kipindi ambacho Mtemi alipata mtoto huyo wa kiume, alipozaliwa tu mfalme akampatia jina CHILIMACHIKOME. Tangu siku hiyo alipozaliwa mtoto alikuwa akilia tu alikuwa analia ala za muziki kitu ambacho kilimfanya mtemi na mama mtemi wastaajabu ni kwa nini wamepata mtoto wa aina hiyo ambaye akilia hulia ala za miziki. Kwa majira yetu haya tungesema ni ala nzuri za music wa Tewatsavenger ujulikanao kama AMINADO. Nenda kausikilize kwa mudawako.......uweze kuvuta taswira.

Mfalme na mkewe wakaamua kufanya mashauri ya siri waende kumtupa mtoto mbali huko pembezoni mwa ngome mahali karibu na njia indayo kwenye kisima kinacho hudumia kijiji kile cha mtemi NYONGO YA MAMBA. siku kadhaa zilipo pita wakasubiri mtoto amelala wakamchukua wakapanda gari ya farasi( chariot) wakaenda kumtupa huko waliko panga wao.

Kijana yule mpenda kutoa taarifa siku hiyo alikuwa msituni nje kidogo ya ukuta wa ngome ya kijiji akijaribu kutafuta taarifa husuusani za wavamizi wa rasilimali za kijiji kutoka nje , alikuwa akizunguka huku na huko akaona gari ya Mtemi inaingia mahali fulani akasogea karibu akajificha katika nyasi akaona Mtemi na mke wake wakishuka kutoka katika gari lile na kuacha kifurushi kidogo kikiwa kimefungwa nguo nyeupe. Akajipa muda akasubiri Mtemi NYONGO YA MAMBA AONDOKE.

Hata walipo fika mbali huko kiasi cha gari ile (chariot) kuto kuonekana, ndipo kijana yule akasogea kuulekea mzigo ule walio uacha akaufunua na ndipo akagundua kuna mtoto mchanga ndani yake. Ubaridi ulipo mpiga mtoto yule alistuka na kuanza kulia. Kijana yule alipigwa na bumbuwazi kusikia mtoto yule akilia ala nzuri za muziki kiasi hiki!'!!! moyoni mwake akasema na hii ni habari nita ihabarisha niendako.

Akaondoka akipiga kifua konde asiamini ni kwanini NYONGO YA MAMBA afanye unyama ule? Kitu kika mjia moyo kwamba kwasababu mtototo yule ni mchanga na kwamba hawezi kuji tetea. Basi nitaenda kwa Mtemi kumueleza akijua kwamba nimejua basi basi nitakuwa nimeokoa maisha ya mtoto yule. Kijana yule akaondoka akaenda kuaga nyumbani kwao akawaambia wazazi wake na mke wake naenda kwenye mambo yangu ya habari nitarudi nikipeleka habari.

Kijana yule alipofika kwa Mtemi NYONGO YA MAMBA akaingia na kumpasha habari zile mtemi yule. Mtemi akamuuliza "Habari hizi umesha mwambia mtu yeyote au mmoja kutoka katika jamaa yako"?

Akajibu. "Hapana mtu aliye pata habari hizi hapo kabla isipokuwa ni wewe pekee mtukufu" mfalme akaingia chumbani kwake akashauriana na mke wake akawaita mmoja kati ya walinzi wake wa kikosi cha mbele, wakanena akawaambia nitafutieni vijana hodari wa kikosi maalumu cha mbele, na wapanda farasi na wanamashua; kwa majira yetu tungesema wana maji. Akawaambia, ""Mtu huyu ni hatari kwa usalama wa na fasi yangu kama mtemi lakini ni adui mkubwa kwa usalama wa kijiji chetu naam nina mtia hatiani na kumkabidhi mikoni mwenu fanyeni mtaloweza damu yake isi mwagike katika nchi maana isije ikawa ni laana katika ardhi yetu. Sawa sawa?""

Wakajibu ""sawa mkuu na mtawala tumesikia tutatekeleza"".

Wakamchukuwa kijana yule aliyeamini katika habari kama nyenzo muhimu ya kuleta ustawi na uthubutu wa watu katika kupambana na changamoto katika kijiji chake, waka msweka katika gari la wale sungusungu wapanda farasi, wakasubiri hata ilipo fika usiku wa manane wakamuondoa wakampeleka katika bwawa la kuabudia mizimu lenye samaki wengi, waka mfunga jiwe zito kiunoni, wakaandika kwa herufi kubwa BURIANI MWANA HABARI HURU damu yako iwe juu yake aliye tupa amri na sio sisi.

Akawaambia amini nawaambia damu yangu haito nyamaza Ima enyi watembezi pia, Mimi nina kufa leo lakini kesho ni zamu yenu, Tazama mnavyo niweka humu nimeacha mke, mali, ndugu na jamaa. Hakika nina kufa nanyi mtakufa pia. Kamwambieni Mtemi, Kwa umri wake wa miaka 50 amebakiza miaka 26 ya furaha baada ya hapo ni shida na taabu. Mwambieni mm nmetangulia na yeye atakufa kama mimi, maana imeandikwa, ( MWANADAMU YEYOTE ALIYE ZALIWA NA MWANA MKE SIKU ZAKE ZA KUISHI SI NYINGI NAZO HUJAA TABU). niagieni mke na wanangu najuwa wana nitafuta hawajui nilipo mungu akipenda tutaonana baadaye. Waambieni wanakijiji wenzangu kama mambo wata yaacha yaendelee hivi kama ya livyo mimi kuuwawa kwa kazi ya mikono yangu, na watu wakaogopa kutoendelea kutafuta habari na kumwambia ukweli Mtemi, amini kuna siku wote :
Wenye maarifa;
Wenye hekima,
Wapiga lamli,
Makuhani,
Wahunzi,
Wadomi,
Na ninyi sungu sungu, woooote tuta cheza wimbo mmoja MTINDO TOFAUTI NA MAHALI PAMOJA siku moja.
Wale sungusungu wa mashuwa waka mtupa bwawani akazama na huo ukawa mwisho wake na mwisho wa habarii zake mdadisi yule (KATUNEE).

Siku iliyo fuata ndugu na jamaa na wana kijiji wapenda haki na habari huru wakamtafuta bila ya mafanikio wakamwendea mtemi, wakalalamika juu ya hilo mtemi akawaambia ni kipi bora kiwapasacho kukipigania , usalama na amani ya kijiji au maisha yenu pasi na usalam? Ondokeni mkafanye kazi maana kazi ni bora kuliko maisha ya mtu mmoja.

Wakatoka kwa ghadhabu ya maneno yale ya Mtemi. Na kijjini zika vuma habari zake watu wakanong'ona kila mahali, Mtemi akasikia habari hizo akajawa na hofu ya nguvu ya uma, akayaweka madaraka yake rehani kwa hofu yake mwenyewe, akawaita wale wakuu wa vikosi vya sungusungu wa kijiji na wale wa mstari wa mbele akawataka ushauri wa nini lakufanya kupunguza manung'uniko ya wanakijiji. Nao wakamwambia tupige marufuku watu kutokuongelea habari hizo wawapo mashambani au sehemu za kuabudia mizimu hata kwenye mikutano ya kijiji maaana jambo hili litaleta fadhaa katika kijiji chetu na kuzorotesha usalama.

Mfalme akakubaliana nao, nao wakapiga la mgambo kijiji chote kuwaambia ya kwamba yeyote Mtu mume au mke atakaye sikika akinongona juu ya habari za kijana yule au mambo mengine sawasawa na hayo ataadhibiwa viboko 12 vya tumboni hata kufa. Kila mtu akawa muoga wa nafsi yake. Watu wakaogopa kuhoji na wenye hekima na maarifa katika kijiji, woote wakawa kimya hapakuwepo na mtu mwenye kuinua kinywa chake wote wakajawa hofu ya maisha yao na mali zao.

Siku iliofuata hasubuhi watu wakatoka asubuhi na mapema kama ilivyo kawaida yao kwenda kufuata maji nje kidogo ya mbali ya ukuta wa ngome ya kijiji. Walikuwa akina mama watano na vyombo vyao vya kutekea, wakatembea umbali kidogo na hata walipo kikaribia kisima, wakasikia sauti za mtoto akilia ala saafi za muziki saafi. Wale wa mama wakasogea pahala pale lakini kabla hawaja karibia nguvu ya muziki ikazidi kiwango cha moyo kuhimiri furaha ya muziki, hivyo wakatupa ndoo nakuanza kukata viuno. Wamekata viuno.................................... kutoka asubuhi mpaka saa kumi na mbili.

Waume zao walipo ona ya kwamba mbona wake zetu hawajarudi mpaka sasa, waka kusanyana wanaume woote pale kijijini wakabeba na mashoka, mikuki na mapanga wakaenda kuwafuata huko kisimani. Walipo karibia hapo kisimani wakasikia sauti nzuri ya ala za muziki wasiweze kuvumilia pia, wakatupa mapanga na mashoka nao wakaanza kukata viuono ....................................

Watoto wao walipo ona sasa usiku umeingia, wakasema kulikoni? Huko tena ngoja tuwafuate tukashuhudie nao wakabeba mijeredi na manati wakatoka nje ya uzio wa ngome wakatembea umbali lakini walipoikaribia ile sehemu ya kisima wakasikia sauti nzuri ya ala za musiki nao wakatupa mijeredi na manati nao wakaungana kuanza kukata viuo. Waka kata viunoo........................

Vongozi wa mitaa na wajumbe wa mitaa walipoona usiku mkubwa umeingia watu wao hawarudi na kwamba kijiji kimeishiwa watu, ikabidi nao waka chukuwa mihuri na nyaraka zao wakatoka kuelekea huko pia wapate kujua ni nini kimejiri. Walipo karibia kisima nao hao wangaingia kwenye mkumbo huo wakatupa nyaraka na mihuri wakaanza kukata mauno. Wamekata wamekata.........

Wachungaji na mapadree na mashekhe na mashemasi nao walipo ona kwamba kijiji kime kuwa kimya wakaitana kwa umoja wao, wakabeba na biblia zao na qurani zao wakaenda kwa ajilii ya maombezi ya kitu kile cha watu kuhama kijiji bila kurudi kwani haija wahi kutokea hapo kabla. Wakatoka na walipo kikaribia jirani na kisima wakasikia pia ala nzuri za musiki wakatupa vitabu vyao pembeni wakavua kanzu na mishipi wengine. Wakaanza kukata mauno pamoja nao. Wakakata mauno..............................!!!!

Vyombo vya ulinzi vya kijiji kwa maana ya askari wa mashuwa na askari wa farasi na waendao kwa miguu wakajipanga wakidhania kijiji kimevamiwa na wahaini au wahujumu rasilimali kuta nje. Wakavaa kijeshi wakapanda farasi wakachukuwa na silaha zao za kivita na maguruneti, wakatoka kwa makundi wakagawana njia wakaelekea huko pia.

Vile vikosi vilipo fika pale vikasikia ala za muziki ule vyote vikaweka silaha vikatupa bunduki pembeni nakuanza kukata mauno dhidi ya muziki ule. Wamekatamaunoooo...........................

Mwisho wakajikuta kijiji kizima kime hama wameenda kucheza muziki wenye ala ileile isipokuwa mtindo (steps) tofauti. Watu wamehamia huko wakicheza mziki uleule mmoja. Hakuna wenye hekima wala, wachungaji wala wapiga ramli wala mashehe wala majasiri katika kunena wala wataua wala wakuu wa vikosi vya sungusungu wenye nguvu. Wooote wakawa huko wakicheza mdundo uleule.

Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake akiwaambia, nadhani mnaona yanayo tendeka hapa, hili ni kwa ajili ya jambo lile...... la yule mtoto wetu sasa hawa jamaa kama watarudi huko watafahamu ukweli wote nami sitakuwa nanguvu tena kwa jambo lilotendeka enendene ndani chukueni lile gunia na sarafu lote lililo shonwa kwa ngozi ambalo ndilo hazina yetu hapa, Mkalipakie kwenye chariot chukuoni na vito vyote vya thamani pakieni pia, tukimbie tuenende mbali kabla hawajarudi na hasira tusije tukafa masikini maana wakiujua ukweli hasira zao zita simama juu yangu na sinto kuwa kiongizi wao tena, maana wote watakuwa wana cheza muziki wenye kufanana na wameujuwa ukweli.

Mtemi akaondoka na hifadhi yote akatokome na mke na walinzi wake kusiko julikana hata sasa. Wanachi walipo rudi waka lala asubuhi walipo amka wakapata taarifa ya kwamba Mteni NYONGO YA MAMBA HAYUPO na makazi yapo wazi. Watu wakakusanyana katika mkutano na wale wajumbe wa mitaa kwa pamoja.

Wakaomba mkuu wa sungusungu msaidizi yule aliye bakia baada ya yule mkuu kutoroka na Mtemi, aje kwaajili ya kuongozana na wananchi kadhaa waingie ndani ya nyumba ya mtemi waangalie nini kimejiri. Ndipo walipo ingia ndani na kukuta lile gunia la hazina ya kijiji limeondoka na Mtemi. Wanachi wakalia kwa uchungu wakapiga mayowe wakazikumbuka nguvu walizo tumia kwenye mashamba ya kijiji na michango ya mifugo yao . Wakasononeka mioyo wakasema yupo wapi kijana yule mwana habari huru aliye tueleza wakati ule manufaafaa ya kutafuta na kupata habari manufaa yakupashana habari za uhakika kwa woteee yuko wapi yule...................?

Wakalia kwanini Mteni alitukataza kuhoji mambo yetu wenyewe tunayo yafanya kwa nguvu zetu wenyewe habari za watu wetu wenyewe michango ya mifugo yetu wenyewe?

Wana kiji wakalia kwa uchungu wakisema?

Eeeh mtemi umetufanyia nini hicho?!! sisi tulikuwa tuna lima kwenye mashamba ya kijiji tena juani, wewe umekaa hemani kwako kivulini, tulipalilia na kuvuna wewe ulikaa bure kula na kusaza kama kiongozi wetu, hakuna ulipo zalisha bali uli kukusanya na kutumia. Ulimuru sungusungu watupige bakora za tumbo tulipo hoji mbona huna hurumaa? Hivi umetoroka kweli na sarafu yetu? "Oweeee.. Oweee...Oweee..." vilio vilisikika.

Wakaanza kulia tena....

Viongozi wetu mliosoma kuliko sisi wanyonge mlishindwa kutumia nguvu ya hoja ya usomi wenu kumwambia Mtemi hapa ndiyo hapa sio? "Oweee... Oweee...

Enyi mapadree, mashemasi, mashekhe,na makuhani mlishindwa kutuhubiria tulisimamie hili kama haki yetu kwanin nanyi pia mlinyamaza hamkukemea. Oweee....Oweeeee....Oweeeee....

Enyi wa kuu wa sungusungu kwanini mlishindwa kumdhibiti mtu asiye na nguvu kiliko ninyi badala yake mkatuadhibu sisi kwa kutaka kuhoji mapato na matumizi ya kazi za mikono yetu na michango yetu wenyewe? Oweee....Oweee......

Enyi wazee na wenye hekima kwanini mlifunga vinywa vyenu hamkusema kitu licha ya kwamba ninyi niwashauri wazuri katika jamii? Owee.......Oweeeee........Oweee....

Watu wakawarudia wale viongozi wengine na kuwambia kwanini mlitusaliti tulio wengi na kumkumbatia mmoja katika maswala magumu na kwa nini hamkumpinga yuko wapi sasa na ninyi mko wapi sasa? Owee........Owee........

Mayowe yalisikika kila kona ya kijiji watu wakililia hazina yao kazi ya mikono yao kubebwa na Mteni NYONGO YA MAMBA.

Wale askari wakaya kumbuka maneno ya kijana yule KATUNENE mwana habari huru, mtafuta habari na mpasha habari. Waka huzinika mioyoyo wakapiga vifua kwa hasira wakafura na kukoromaa kwa dhiki kuu iliyojaa mioyoni mwao waka yakumbuka maneno ya mwisho ya kijana yule. Ya kwamba kama mtanyamaza siku moja;

"WOTE TUTA CHEZA WIMBO MMOJA LAKINI KWA MTINDO TOFAUTI NA MAHALI PAMOJA"

Wakamaliza kwakukubaliana kwamba hakutokuwa na mtu yeyote ataye kuwa kiongozi miongoni mwetu atakaye zuwiya mjadala huru katika mambo muhimu kama matumizi ya sarafu na mapato ya kijiji , hakuna mtu ataye zuwiya kwa namna yoyote ile utafutaji, upataji na utoaji wa habari katika kijiji chetu na huo ndo ukawa wimbo wao wakudumu hata sasa. Kila ulipo pita ulikuta bango:

HABARI NA MWANAHABARI HURU KWA USTAWI NA MAENDELEO.

Watoto wakaimba mashuleni hata leo.

REST IN PIECE KATUNENE.
chilemba wa mela pamputi.

Ndugu yenu.
Crap
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom