Nguvu ya msamaha

noney

noney

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Messages
202
Likes
271
Points
80
noney

noney

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2015
202 271 80
Hii nimeitoa kwa mshana Jr.
Imenigusa na kuona ni share tena na kuongezea machache.

Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake.

Jr

""

Msamaha ni kile kitendo cha kumwachilia mtu na kosa alilokukosea kwa namna ambayo hata ukikumbuka kosa alilokukosewa haiamshi hisia hasi maana unajua ulishamsamehe huyo mtu.

Msamaha unakupa fursa ya kumpa mtu aliyokukosea nafasi nyingine.

Moja ya vitu ambavyo vinachochea uchungu katika maisha yetu baada ya kukosewa ni kuwaza na kufikiri sana juu ya kosa na kwazo na kutokuwa tayari kuelewa kwanini mtu alikufanya alichokufanya.

Kuna wakati watu wanaweza kukufanyia mambo magumu sana kwa sababu wamekamatwa na roho nyingine.

Yesu akilitambua hili akiwa pale msalabani aliwaombea rehema wale watu waliyo mtesa na kumsulubisha kwa kumwambia baba Yake, “Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.”

Yesu alitangaza huu msamaha akiwa kama mwanadamu au Mwana wa Adamu.

Kama Yesu aliweza, uwe na uhakika, hata mimi na wewe tunaweza.

Usikubali kusukumwa na roho ya kulipa kisasi maana kisasi mwisho wake ni maumivu zaidi.

Maandiko yanatufundisha:

Warumi 12: 17 – 21.

17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Unapokosewa kunakuwa na msukumo unaotokana na hasira na maumivu ya kukosewa ya kulipa kisasi.

Usikubali kufanya vitu kwa msukumo wa hasira na maumivu yatokanayo na kosa ulilokosewa au kwazo.

Ukitendewa baya, usilipize kwa wewe kumtendea huyo mtu baya vilevile.

Hakikisha kwa upande wako kuwa unaishi kwa namna ambayo haitazua maswali kwa watu kuwa kwanini unawafanyia vitu hivyo wengine.

Kukosewa na kuumizwa sio sababu nzuri ya kutosha ya kuwatendea watu mambo magumu.

Jitahidi wewe kwa upande wako kuishi kwa amani na watu wote.

UWE NA MWANZO MZURI WA MWAKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,431
Likes
124,788
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,431 124,788 280

Forum statistics

Threads 1,250,502
Members 481,371
Posts 29,735,841